ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 12, 2012

ALEX FERGUSON AOMBEA JAMBO LA KIJINGA LITOKEE DHIDI YA JIRANI ZAO MANCHESTER CITY

Mwali bado kafichwa kwa sababu mwenye dau kubwa bado hajajulikana, japokuwa ni kati ya wababe wawili wa Manchester - Manchester City na Manchester United.Timu hizi mbili zina pointi 86, lakini City wana mabao mengi manane kuliko United.
Kwa kuzingatia hayo, mechi muhimu zaidi kesho Jumapili ni ile inayozikutanisha Manchester City na Queen Park Rangers (QPR), mchezo unaofanyika Etihad, nyumbani kwa City mbele ya washabiki wake. Mechi nyingine inayotia wadau matumbo joto ni ile ya Manchester United na Sunderland, United safari hii wakichezea ugenini.

Ili City watwae ubingwa wanatakiwa kuwa na matokeo kama ya United au mazuri zaidi. Kwa kifupi ni kwamba, City wakishinda kuna uwezekano mkubwa wa kutangazwa wafalme wa soka wa England.

Ni katika hali hiyo Kocha Mkuu wa Manchester United, Sir Alex Ferguson anasema wao wanaombea litokee jambo la 'kijinga' dhidi ya jirani zao (Manchester City) ili wanyakue tonge mdomoni mwao.

Lakini ikumbukwe kwamba vijana hao wa Roberto Mancini katika msimu wote wamepoteza pointi mbili tu katika uwanja wao huo wa Etihad, yaani wameshinda mechi zote isipokuwa mbili tu walizotoka sare. Ndiyo maana washabiki wao wengi wana matumaini makubwa ya kutwaa ubingwa walioupata mara ya mwisho mwaka 1968.

Wanachotegemea dhidi ya QPR ni ushindi tu. QPR wananolewa na kocha wa zamani wa City, Mark Hughes aliyetupiwa virago Desemba 2009 baada ya kushinda mechi mbili tu kati ya 11 City walizocheza mfululizo. Kocha huyo pia ameichezea United na Ferguson anamtegemea 'amsaidie kuiangamiza City'. Kwa ujumla timu mbili hizi za Manchester zinatarajiwa kuibuka na ushindi kwenye mechi zao hizi za mwisho.

MWANZA KWANZA YAMTEKA KALA JEREMIAH

Kala Jeremiah(L) katika flash na mwenyekiti wa Mwanza kwanza Philbert Kabago(R).
Katika hatua nyingine Umoja wa wasanii na watu wa Mwanza (Mwanza kwanza) umefanikiwa kuziteka hisia na hatimaye kumwingiza kundini msanii wa hip hop nchini kinara aliyetikisa BSS, Kala Jeremiah.

Akizungumza na blogu hii Kala Jeremiah amzitaja kwa kifupi sababu za kujiunga na Umoja huo kuwa kwanza ni sifa yakuwa mzawa wa moja ya vitaa vya jiji hilo la miamba, pili akiamini kuwa Umoja ni nguvu amefurahishwa na kuvutiwa na misingi iliyopo ndani ya umoja huo sanjari na msimamo pamoja na mshikamano uliopo.

Mwanza kwanza imeendelea kuteka fani mbalimbali kama vile Waigiza filamu, Watayarishaji wa muziki, Ma-Dj, Watangazaji, Waimbaji Muziki wa injili na Muziki wa kizazi kipya akiwemo Dudu Baya, Sajna, Sisar Madini na wengine wengi.

'KWETU PAZURI'

Flash nikiwa na watoto wa familia ya Paulo Lugwecha ambaye ni mwenyekiti wakiji cha Imalamate kilichopo tarafa ya Ngasamo wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Ramani ya kijiji cha Ngasamo..

Picha za ukutani ofisi ya mtendaji wa kijiji.

'TUNATUPIAMO' Hivi tangu uzaliwe umeshawahi kuweka maoni kwenye kisanduku hiki? Au unahofia kwamba mfunguaji kisanduku ndiye mlengwa...?

Ligi ya Uingereza imeteka hadi vijiji vyetu..

Hifadhi ya fagio kwenye kaya kijijini..upo hapo...!
Pozi la raha toka kazini, hapa ni kusubiri msosi tu...

Umerudi toka kazini huna hata mia babake unahitaji nguvu ya Jesus....

Wadau wakikosha mikono kujipatia maakuli katika hotelini kubwa kuliko zote kijijini hapa.

Dhabahu iliyosakwa imepatikana...

MASUMBWI- "R.I.P RACHEL MWILIGA"

Kampuni ya BigRight Promotion kupitia kwa mkurugenzi wake Ibrahim Kamwe imepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mhariri wa Michezo wa gazeti la Mtanzania, Rachel Mwiligwa kilichotokea jana (Mei 11 mwaka huu).

Kwa niaba ya mabondia, makocha na mapromota wa masumbwi nchini tunawataka familia ya Rachel na Kampuni ya New habari wawe wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba.
Tunatoa POLE! -
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU RACHEL PEPONI - "ameeein"

TANZANIA DMV KUCHUANA NA ETHIOPIA KUNDI (B)

Na Abou Shatry
Katika mchezo wa lingi ya 2011 Diaspora World Cup zinazoendelea katika viwanja vya Hyattsville na Germantown jijini Maryland Nchini Marekani, timu ya Tanzania DMV watachuwana vikali na timu ya Ethiopia Leo hii Jumamosi May 12, 2012 mida ya 12:PM (Mchana wa saa sita) katika kiwanja cha Greencastle, kiliopo Burtonsville, Maryland
TANZANIA DVN

ETHIOPIA
Kundi (B) Timu ya wa Ethiopia katika mchezo wa awali walifungwa bao 3-0 na timu ya Malawi ndani ya uwanja cha Greencastle, Burtonsville, Maryland, ambao leo watajianda vikali ili kutaka kurudisha nguvu zao kwa mchezo waliopoteza dhiti ya timu hiyo ya Malawi, ambao leo hii timu ya Malawi watapambana vikali na timu ya Armenia mida ya saa 1:PM Mchana wa leo, kwa mechi ya kwanza timu ya Armenia waliwabamiza Nigeria bao 4-1 katika mchezo wa awali.

Pia timu ya waTanzania DMV katika mchezo wa kwanza siku ya Jumapili ya April 29,2012 walifanikiwa kuwabamiza timu ya Ghana bao 3-2 ndani ya uwanja wa SoccerPlex Stadium uliopo Ager Road Hyattsville Maryland.

Kama kawaida yao timu ya waTanzania DMV inawaomba Watanzania wote ushirikiano wenu wa kila hali ili kuipa changamoto timu ya Watanzania DMV, mnaombwa pia kufika mapema mida ya saa 11:AM kuzowea mazingira kabla ya mchezo huo kuanza. 
Adress ya mchezo utakaochezwa leo hii ni Fairland Field 3928 Greencastle Rd. Burtonsville, Maryland 20866 Habari na http://swahilivilla.blogspot.com/

Friday, May 11, 2012

PPF YAIPIGA JEKI MWAUWASA SACCOS MIL 900

Meneja wa mfuko wa Mashirika ya Umma (PPF) Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 900, Vedastus Pilla, Mwenyekiti wa chama cha kuweka na kukopa cha Mamlaka ya Maji safi na majitaka, jijini Mwanza (MWAUWASA Saccos) kwa ajili ya mkopo wa chama hicho jana. Kulia ni Meneja wa saccos hiyo, Tungaraza Njugu Clement pamoja na wafanyakazi wa PPF na wanachama wa MWAUWASA.

Mkopo huo umetolewa na PPF kwa Mwauwasa Saccos ni moja ya huduma zinazotolewa na PPF na wanachama wake ili kuwawezesha kiuchumi na kuwaondolea ugumu wa maisha unaotokana na kukosa kipato cha kutosha na pia kuwaandaa waweze kuwa na maisha bora wawapo katika ajira na mara baada ya kustaafu.


"Huu ni mpango mahususi wa PPF katika kuboresha maisha ya wanachama wake, mpaka sasa PPF imekwishatoa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 40 kwa vyama vya kuweka na kukopa 36 kwa nchi nzima , na lengo la utoaji wa mikopo hiyo ni kuwawezesha wanachama wa PPF katika ujenzi wa nyumba, kulipa gharama za elimu, kujiendeleza katika kilimo, kujiendeleza kibiashara na kuwa na ufugaji bora”, alisema Meshack Bandawe (Pichani).


Naye Mwenyekiti wa Mwauwasa Saccos, Vedastus Pilla (Pichani) ameushukuru uongozi wa PPF kwa uamuzi iliouchukua ya kuiweza Mwauwasa Saccos ili iweze kuimarika kiuchumi na kuwawezesha wanachama wake kupata maisha bora.

Meneja wa MWAUWASA Saccos, akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa mfuko wa PPF pamoja na wanachama wa chama hicho cha kuweka na kukopa cha Mamlaka ya Maji safi na majitaka jijini Mwanza, muda mfupi baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi milioni 900 za mkopo kwa wanachama wa saccos hiyo leo.

MADIWANI CCM,CHADEMA WAMKATAA DC HENJEWELE

Na Shomari Binda Tarime

 Siku moja baada ya kuteuliwa kwa wakuu wa Wilaya Madiwani wa Halimashauri ya Wilaya ya Tarime wamemkataa Mkuu wa Wilaya ya Tarime na kumuomba Rais Jakaya Kikwete aweze kumuondoa katika Wilaya hiyo na kumpangia Wilaya nyingine ya kufanyia kazi baada ya kushindwa kudhititi usalama wa Raia na mali zao na kufanya ukaidi kila anaposhauriwa.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele (mwenye suti kulia) wakati akimpa maelezo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu kuhusu eneo linalotarajiwa kujengwa soko kubwa la kisasa katika mji wa Sirari mkoani Mara.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuhailishwa kwa kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kifanyike katika ukumbi wa mikutano wa Halimashauri hiyo,Madiwani hao walidai kuwa DC Henjewele akiwa kama Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ameshindwa kudhibiti matukio ya mauajia ambapo hivi karibuni katika mgodi wa Nyamongo na Tarime Mjini lakini Mekaa kimya.

 Kiongozi wa upinzani katika Baraza la madiwani wa Halimashauri hiyo Ndesi Charles wa kata ya Turwa (CHADEMA) alisema wameamua kwa kauli moja kutokufanya kikao cha Baraza la Madiwa kutokana na DC huyo kuigeuza Halimashauri ya Tarime kama Taasisi yake na kusema kuwa hawataendesha vikao vya Baraza hilo mpaka hapo mkuu wa Mkoa atakapokuja na kuondoka na DC huyo.

Ndesi amesema kuwa wameshangazwa na uteuzi uliofanyika jana wa ma DC na Henjewele kuendelea kubakishwa katika Halimashauri hiyo licha ya taarifa ya kulalamikiwa na Wananchi pamoja na Madiwani kwa kushindwa kuzingatia utawala bora na kuendelea kukumbatiwa. "Madiwani wote tumeamua kwa pamoja kugomea kufanya kikao hicho ambacho kilikuwa na ajenda ya kupitia taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) lakini tumeshindwa kufanya na hatutafanya mpaka hapo DC Henjewele atakapoondolewa katika Wilaya ya Tarime,"alisema Ndesi.

Alisema DC Henjewele kwa sasa anafanya biashara zake na amewekeza katika mgodi wa Nyamongo na kushindwa kufatilia kelo za Wananchi na kufikia hatua ya kuzuia wawekezaji waliopo kuatika mgodi huo wa ABG kukataa kulipia karo za wanafunzi kama ilivyo katika makaubaliano na mgodi huo.

 Diwani wa kata ya Nyamaraga Antony Manga (CCM) alisema suala la DC huyo lilishaongelewa katika vikao vya chama lakini ameshindwa kuwa msikivu katika masuala ya msingi anayolalamikiwa na Wananchi pamoja na Madiwani hivyo nao wameamua kwa pamoja kumkataa na sio chaguo sahihi kwa Tarime katika dhana nzima ya kuhalakisha maendeleo.

Amesema kumekuwa na kero mbalimbali zinazomuhusu ikiwemo kutokusikiliza kuondolewa kwa kizuizi cha Nkende kata ya Sirari ambacho kimekuwa kikwazo kikubwa kwa wafanyabiashara kufanya shughuli zao za kimaendeleo kutokana na kuwepo kwa kizuizi hicho na kudai kuwa kizuizi cha Kirumi kinatosha.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Tarime na Diwani wa kata ya Sirari Amos Sagara amesema kutokufanyika kwa kikao hicho cha kawaida cha Baraza la Madiwani ni baada ya kutokea kwa marumbano ya madiwani wote kabvla ya kikao wakitaka kutokufanyika kwa kikao hicho mpaka hapo atakapokuja mkuu wa Mkoa ili aweze kuondoka na DC huyo kutokana na madai yao mbalimbali juu yake.

Alisema baada ya maluymbano hayo kuzidi aliamua kuhitisha kikao cha ndani na Madiwani wote na kupitisha azimio moja la kutokufanyika kwa kikao hicho mpaka hapo watakapowasiliana na Mkuu wa Mkoa ili kushiriki katika kikao cha pamoja na Madiwani hao ili kuweza kufikia muafaka wa yale yanayozungumzwa.

Akiongea kwa njia ya simu na BINDA NEWS Henjewele alisema yale yote yanayolalamikiwa na Madiwani hao si ya kweli na kama wanataarifa za kimaandishi wanapaswa waziwasilishe na si kuongea mambo ambayo hayana ukweli na kudai kuwa huenda wanazo sababu zao nyingine.

Alisema kuwa hali ya kiusalama katika Wilaya ya Tarime ni nzuri na hayo wanayo yaongea na kufikia hatua ya kugomea kikao juu yangu si ya kweli na kuendele kusisistiza kama wanao ushahidi juu ya hayo yote waweze kuyatolea taarifa kwa njia zinazo stahili.

Thursday, May 10, 2012

TWIGA STARS YAIBUGIZA ROCK CITY QUEEN 5-0

Mchezo baina ya timu ya taifa ya wanawake Tanzania (Twiga Stars) na kombaini ya timu ya wanawake Mwanza (Rock City Queens) umekatika kwenye dakika ya 58 mara baada ya mvua kubwa kunyesha katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza na hali ya uwanja kuwa tete.

Kabla ya mechi hiyo kuvunjika Twiga Stars ilikuwa ikiongoza kwa bao 5-0.

Twiga Stars iko kwenye mazoezi ya kujiandaa na mashindano ya Afrika dhidi ya Nigeria ambapo Jumamosi (Mei 12 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya mpira wa miguu kwa wanawake ya Zimbabwe.

HONDA YAZINDUA TAWI LAKE MWANZA

Mkuu wa wilaya Nyamagana Said Amanzi akizindua tawi jipya la Kampuni ya Quality Motors Limited mkoani Mwanza, kampuni inayo jihusisha na usambazaji na uuzaji wa pikipiki, majenereta, na vifaa mbalimbali vya kampuni ya Honda nchini Tanzania.

Mkuu wa wilaya Nyamagana Said Amanzi akijaribu ubora wa moja kati ya mali zilizopo kwenye tawi hilo jipya huku akishuhudiwa na wadau wa karibu wa kampuni hiyo.

Ufunguzi wa tawi hilo utakuwa na manufaa mengi kwa wakazi wa kanda ya ziwa kwani wataondokana na adha ya nishati ya umeme ambayo imekuwa kikwazo kikubwa katika utendaji kazi wao wa kila siku hali inayosababisha kuingia katika gharama za ziada zinazokwamisha maendeleo kutokana na kipato chao duni, ikumbukwe kuwa wakazi wengi hususani wa visiwani hutumia majenereta kama chanzo cha nishati ya umeme kwa viwanda vya usagaji na ukoboaji nafaka, umeme wa majumbani maduka ya kuchaji simu, karakana za uchoeleaji na kadhalika.
Uzinduzi wa tawi hilo umekuja wakati muafaka ambapo usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda ukiendelea kuwa tegemeo kwa wakazi wengi wa mikoa ya kanda ya ziwa kutokana na tozo nafuu la nauli, hali inayo wafanya wananchi wengi kuufanya usafiri huo kuwa kimbilio lao

Mteja wa kwanza katika duka la Honda Mwanza bw. Vicent Hariah kutoka kampuni ya African Wheels and Tyres LTD akikabidhiwa pikipiki yake mara baada ya kuinunua.

Wateja wakipata maelezo toka kwa wahudumu na wadau wa Tawi la Honda Mwanza lililopo katika barabara ya Kenyeta karibu na tawi la Benki ya Posta.
Honda 'Best quality at Chinese price'

Honda at Quality Motors, Nyerere road Mwanza.

Sudhir Bargaonkar ni meneja masoko wa Kampuni ya Quality Motors Limited akimtembeza mgeni rasmi kwenye karakana ya tawi hilo jipya lililozinduliwa.

Wakitoka kwenye karakana ambapo pia katika duka hili spea mbalimbali za Honda iwe ni jenereta au pikipiki zitauzwa.

Picha ya kumbukumku... Hadi kufikia mwezi march 2012 halmashauri ya jiji la Mwanza ilikuwa na madereva wa pikipiki za biashara zaidi ya 6,000 wanaotambulika nao wamekuwa wakiongezeka siku baada ya siku.

OBAMA AUNGA MKONO NDOA ZA JINSIA MOJA

video platform video management video solutions video player Rais Barack Obama amesema kwamba watu wa jinsia moja wawe na haki ya kuoana.
 
Bwana Obama amesema daima amekuwa mgumu kukubali kwamba wanaume na wanawake wenye uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja nchini Marekani watendewe haki na jamii kwa kutambua uhusiano huo, lakini amekuwa akipitia kile anachokiita mabadiliko ya kimtazamo kuhusu suala la ndoa za jinsia moja.

Kwa kauli hii Obama anakuwa rais wa kwanza wa Marekani kuunga mkono ndoa za jinsia moja, suala ambalo limeleta mgawanyiko miongoni mwa raia wa Marekani. Kumekuwa na maoni tofauti miongoni mwa Wamarekani kuhusu kuunga mkono ndoa za aina hii.

Rais Obama anasema amejadili suala hilo na familia, marafiki na majirani kwa muda mrefu na kutilia maanani wafanyakazi wenzake na askari ambao wamejikita katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja.

Hatimaye amekuja na hitimisho kwamba ndoa zilizozoeleka hazikidhi matarajio ya wote.


Ni moja kati ya ndoa za mashoga iliyofungwa Jumamosi ya Oktoba 17, mwaka 2011, kati ya Bw Daniel Chege Gichia (39) na Charles Ngengi (40), jijini London
Mpinzani wake katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu, Mitt Romney, wa chama cha Republican amesema bado anabakia kupinga ndoa za watu wa jinsia moja.


Amesema wakati akiunga mkono ndoa ambazo hazijatambuliwa kisheria, kwa maoni yake, suala la ndoa za kawaida ni jambo lingine tofauti na hizo ndoa za jinsia moja.

Kauli ya Bwana Obama, imekuja siku moja baada ya jimbo la North Carolina kupitisha mabadiliko ya katiba ya jimbo hilo, yanayofafanua kuwa ndoa ni muungano tu kati ya mwanaume na mwanamke.

WAKUU WA WILAYA WAPYA 70 NA VITUO VYAO

1. Novatus Makunga - Hai
2. Mboni M. Mgaza - Mkinga
3. Hanifa M. Selungu - Sikonge
4. Christine S. Mndeme - Hanang
5. Shaibu I. Ndemanga - Mwanga
6. Chrispin T. Meela - Rungwe
7. Dr. Nasoro Ali Hamidi - Lindi
8. Farida S. Mgomi - Masasi
9. Jeremba D. Munasa - Arumeru
10. Majid Hemed Mwanga - Lushoto
11 Mrisho Gambo - Korogwe
12. Elias C. J. Tarimo - Kilosa
13. Alfred E. Msovella - Kiteto
14. Dkt. Leticia M. Warioba - Iringa
15. Dkt. Michael Yunia Kadeghe - Mbozi
16. Mrs. Karen Yunus - Sengerema
17. Hassan E. Masala - Kilombero
18. Bituni A. Msangi - Nzega
19. Ephraem Mfingi Mmbaga - Liwale
20. Antony J. Mtaka - Mvomero
21. Herman Clement Kapufi - Same
22. Magareth Esther Malenga - Kyela
23. Chande Bakari Nalicho - Tunduru
24. Fatuma H. Toufiq - Manyoni
25. Seleman Liwowa - Kilindi
26. Josephine R. Matiro - Makete
27. Gerald J. Guninita - Kilolo
28. Senyi S. Ngaga - Mbinga
29. Mary Tesha - Ukerewe
30. Rodrick Mpogolo - Chato
31. Christopher Magala - Newala
32. Paza T. Mwamlima - Mpanda
33. Richard Mbeho - Biharamulo
34. Jacqueline Liana - Magu
35. Joshua Mirumbe - Bunda
36. Constantine J. Kanyasu - Ngara
37. Yahya E. Nawanda - Iramba
38. Ulega H. Abadallah - Kilwa
39. Paul Mzindakaya - Busega (mpya)
40. Festo Kiswaga - Nanyumbu
41. Wilman Kapenjama Ndile - Mtwara
42. Joseph Joseph Mkirikiti - Songea
43. Ponsiano Nyami - Tandahimba
44. Elibariki Immanuel Kingu K- isarawe
45. Suleiman O. Kumchaya - Tabora
46. Dkt. Charles O. F. Mlingwa - Siha
47. Manju Msambya - Ikungi (mpya)
48. Omar S. Kwaangw’ - Kondoa
49. Venance M. Mwamoto - Kibondo
50. Benson Mpesya - Kahama
51. Daudi Felix Ntibenda - Karatu
52. Ramadhani A. Maneno - Kigoma
53. Sauda S. Mtondoo - Rufiji
54. Gulamhusein Kifu - Mbarali
55. Esterina Kilasi - Wanging’ombe (mpya)
56. Subira Mgalu - Muheza
57. Martha Umbula - Kongwa
58. Rosemary Kirigini - Meatu
59. Agness Hokororo - Ruangwa
60. Regina Chonjo - Nachingwea
61. Ahmed R. Kipozi - Bagamoyo
62. Wilson Elisha Nkhambaku - Kishapu
63. Amani K. Mwenegoha - Bukombe
64. Hafsa M. Mtasiwa - Pangani
65. Rosemary Staki Senyamule - Ileje
66. Selemani Mzee Selemani - Kwimba
67. Lt. Col. Ngemela E. Lubinga - Mlele (mpya)
68. Iddi Kimanta - Nkasi
69. Muhingo Rweyemamu - Handeni
70. Lucy Mayenga - Uyui
OFISI YA WAZIRI MKUU,
DAR ES SALAAM.
9 MEI 2012

LOWASA AMPONGEZA KIDUNDA AKIWA DUBAI

KATIBU wa shirikisho la ngumi za Ridhaa nchini BFT Makore Mashaga pamoja na makocha na viongozi wa BFT kwa pamoja wamempongeza bondia Selemani kidunda kwa kuteuliwa kushiriki mashindano ya Olimpiki yanayotarajia kufanyika hivi karibuni akizungumza katika hafla hiyo ya kumpongeza na kumtia moyo kuendelea na mazoezi kwa ajili ya michunano ya olipiki inayokuja karibuni.

Aidha Makamu mwenyeki wa BFT Michael Changalawe amemshukuru Waziri Mkuu Mstaafu Eduward Lowasa kwa kumpatia Kidunda Dola 100 baada ya kukutana Dubai wakati wanarudi Tanzania kambi ya ngumi inaingia kambini leo hii tarehe 10 katika uwanja wa ndani wa taifa kwa ajili ya mazoezi zaidi.

Mbali na mashindano hayo timu hiyo imeomba wafadhili mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya kuipa sapoti kampeni hiyo ambapo wanatarajia kwenda botswana kwa ajili ya kuweka kambi ya bondia Kidunda na wengine kupima Viwango vyao.

Timu hiyo inakabiliwa na uhaba wa fedha hivyo wametoa wito kwa watu binafsi, mashirika pamoja na makampuni kujitokeza kusaidia mchezo wa masumbwi ili uweze kusonga mbele.

Kwa sasa kambi hiyo itakuwa na mabondia kumi kila uzito.
Na:Super D Boxing Coach

Wednesday, May 9, 2012

UKIKOSA SYRIA INTERNATIONAL EXHIBITION IN MWANZA USIJEKUJILAUMU MWANAWANE......!!!

Maonesho ya utamaduni na bidhaa za watu wa nchi ya Syria yanaendelea katika ukumbi mkubwa wa Gold Crest Hotel jengo la PPF barabara ya Kenyeta jijini Mwanza.

Bidhaa mbalimbali mapambo ukutani zinapatikana kwenye maonesho ambazo pia waweza kujinunulia. 

Perfumes na marashi mbalimbali yenye thamani yanapatikana hapa tena utanunua kwa vipimo. 

Suti kali rangi zote pia zipo. 

Mdau akionyesha pasi ya muundo wa kipekee yenye uwezo wa kunyosha nguo yenye kitambaa aina yeyote bila usumbufu hata vile vitambaa vyenye kuchagua pasi (hauhitaji kwenda dry creaner) inauzwa sh 65,000/= tu! 

Kushoto ni maboksi ya pasi zinazouzwa kwenye maonesho hayo ya Syria na kulia ni fagio/dekio maalum lisilotumia umeme lenye uwezo wa kufyonza uchafu aina zote, unakamua kwa kuvuta kishikio maalum 'hauhitaji kupinda mugongo mwanawane....' 

Akinadada wakijichagulia bangili, pochi, shanga, mikufu ya asili, hereni na mapambo ya ukutani ndani ya maonyesho haya. 

Vitendea kazi vyote vya jikoni, vikatio, vimenyeo na kadhalika. 

Hadi pipi... vitafunwa vyauzwa kwa kilogramu. 

Makobazi kwa wanaume yenye ubora wa hali ya juu bei poa. 

Sendoz nzuri kwa wanawake... 

Katika banda hili wadau wa Mwanza wakijinunulia poket na wengine wakanunua pochi. 

Mchuuzi katika pozi la kuwasikiliza wateja. 

Haya wale wa maharusi shela zinauzwa kwenye maonesho haya ya utamaduni wa watu wa Syria. 

Mavazi muntashar' kwa wanawake.

Soksi 'pure cotton' kwa watoto na watu wazima. 

Ushawahi ona sabuni za kuogea zinazotokana na malighafi ya miti asili na asali? 

Shanga, mikanda, bangili na na na na nanini...''' 

Maonesho ya wazi ya utamaduni wa Syria, yalioanza tarehe 1/05/2012 yanategemewa kufungwa rasmi tarehe 14/05/2012. Pliz' usije jilaumu kwamba sijakustua kwamba kuna mambo mazuri yanaendelea Mwanza.