ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 11, 2012

PPF YAIPIGA JEKI MWAUWASA SACCOS MIL 900

Meneja wa mfuko wa Mashirika ya Umma (PPF) Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 900, Vedastus Pilla, Mwenyekiti wa chama cha kuweka na kukopa cha Mamlaka ya Maji safi na majitaka, jijini Mwanza (MWAUWASA Saccos) kwa ajili ya mkopo wa chama hicho jana. Kulia ni Meneja wa saccos hiyo, Tungaraza Njugu Clement pamoja na wafanyakazi wa PPF na wanachama wa MWAUWASA.

Mkopo huo umetolewa na PPF kwa Mwauwasa Saccos ni moja ya huduma zinazotolewa na PPF na wanachama wake ili kuwawezesha kiuchumi na kuwaondolea ugumu wa maisha unaotokana na kukosa kipato cha kutosha na pia kuwaandaa waweze kuwa na maisha bora wawapo katika ajira na mara baada ya kustaafu.


"Huu ni mpango mahususi wa PPF katika kuboresha maisha ya wanachama wake, mpaka sasa PPF imekwishatoa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 40 kwa vyama vya kuweka na kukopa 36 kwa nchi nzima , na lengo la utoaji wa mikopo hiyo ni kuwawezesha wanachama wa PPF katika ujenzi wa nyumba, kulipa gharama za elimu, kujiendeleza katika kilimo, kujiendeleza kibiashara na kuwa na ufugaji bora”, alisema Meshack Bandawe (Pichani).


Naye Mwenyekiti wa Mwauwasa Saccos, Vedastus Pilla (Pichani) ameushukuru uongozi wa PPF kwa uamuzi iliouchukua ya kuiweza Mwauwasa Saccos ili iweze kuimarika kiuchumi na kuwawezesha wanachama wake kupata maisha bora.

Meneja wa MWAUWASA Saccos, akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa mfuko wa PPF pamoja na wanachama wa chama hicho cha kuweka na kukopa cha Mamlaka ya Maji safi na majitaka jijini Mwanza, muda mfupi baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi milioni 900 za mkopo kwa wanachama wa saccos hiyo leo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.