ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 11, 2012

MADIWANI CCM,CHADEMA WAMKATAA DC HENJEWELE

Na Shomari Binda Tarime

 Siku moja baada ya kuteuliwa kwa wakuu wa Wilaya Madiwani wa Halimashauri ya Wilaya ya Tarime wamemkataa Mkuu wa Wilaya ya Tarime na kumuomba Rais Jakaya Kikwete aweze kumuondoa katika Wilaya hiyo na kumpangia Wilaya nyingine ya kufanyia kazi baada ya kushindwa kudhititi usalama wa Raia na mali zao na kufanya ukaidi kila anaposhauriwa.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele (mwenye suti kulia) wakati akimpa maelezo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu kuhusu eneo linalotarajiwa kujengwa soko kubwa la kisasa katika mji wa Sirari mkoani Mara.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuhailishwa kwa kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kifanyike katika ukumbi wa mikutano wa Halimashauri hiyo,Madiwani hao walidai kuwa DC Henjewele akiwa kama Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ameshindwa kudhibiti matukio ya mauajia ambapo hivi karibuni katika mgodi wa Nyamongo na Tarime Mjini lakini Mekaa kimya.

 Kiongozi wa upinzani katika Baraza la madiwani wa Halimashauri hiyo Ndesi Charles wa kata ya Turwa (CHADEMA) alisema wameamua kwa kauli moja kutokufanya kikao cha Baraza la Madiwa kutokana na DC huyo kuigeuza Halimashauri ya Tarime kama Taasisi yake na kusema kuwa hawataendesha vikao vya Baraza hilo mpaka hapo mkuu wa Mkoa atakapokuja na kuondoka na DC huyo.

Ndesi amesema kuwa wameshangazwa na uteuzi uliofanyika jana wa ma DC na Henjewele kuendelea kubakishwa katika Halimashauri hiyo licha ya taarifa ya kulalamikiwa na Wananchi pamoja na Madiwani kwa kushindwa kuzingatia utawala bora na kuendelea kukumbatiwa. "Madiwani wote tumeamua kwa pamoja kugomea kufanya kikao hicho ambacho kilikuwa na ajenda ya kupitia taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) lakini tumeshindwa kufanya na hatutafanya mpaka hapo DC Henjewele atakapoondolewa katika Wilaya ya Tarime,"alisema Ndesi.

Alisema DC Henjewele kwa sasa anafanya biashara zake na amewekeza katika mgodi wa Nyamongo na kushindwa kufatilia kelo za Wananchi na kufikia hatua ya kuzuia wawekezaji waliopo kuatika mgodi huo wa ABG kukataa kulipia karo za wanafunzi kama ilivyo katika makaubaliano na mgodi huo.

 Diwani wa kata ya Nyamaraga Antony Manga (CCM) alisema suala la DC huyo lilishaongelewa katika vikao vya chama lakini ameshindwa kuwa msikivu katika masuala ya msingi anayolalamikiwa na Wananchi pamoja na Madiwani hivyo nao wameamua kwa pamoja kumkataa na sio chaguo sahihi kwa Tarime katika dhana nzima ya kuhalakisha maendeleo.

Amesema kumekuwa na kero mbalimbali zinazomuhusu ikiwemo kutokusikiliza kuondolewa kwa kizuizi cha Nkende kata ya Sirari ambacho kimekuwa kikwazo kikubwa kwa wafanyabiashara kufanya shughuli zao za kimaendeleo kutokana na kuwepo kwa kizuizi hicho na kudai kuwa kizuizi cha Kirumi kinatosha.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Tarime na Diwani wa kata ya Sirari Amos Sagara amesema kutokufanyika kwa kikao hicho cha kawaida cha Baraza la Madiwani ni baada ya kutokea kwa marumbano ya madiwani wote kabvla ya kikao wakitaka kutokufanyika kwa kikao hicho mpaka hapo atakapokuja mkuu wa Mkoa ili aweze kuondoka na DC huyo kutokana na madai yao mbalimbali juu yake.

Alisema baada ya maluymbano hayo kuzidi aliamua kuhitisha kikao cha ndani na Madiwani wote na kupitisha azimio moja la kutokufanyika kwa kikao hicho mpaka hapo watakapowasiliana na Mkuu wa Mkoa ili kushiriki katika kikao cha pamoja na Madiwani hao ili kuweza kufikia muafaka wa yale yanayozungumzwa.

Akiongea kwa njia ya simu na BINDA NEWS Henjewele alisema yale yote yanayolalamikiwa na Madiwani hao si ya kweli na kama wanataarifa za kimaandishi wanapaswa waziwasilishe na si kuongea mambo ambayo hayana ukweli na kudai kuwa huenda wanazo sababu zao nyingine.

Alisema kuwa hali ya kiusalama katika Wilaya ya Tarime ni nzuri na hayo wanayo yaongea na kufikia hatua ya kugomea kikao juu yangu si ya kweli na kuendele kusisistiza kama wanao ushahidi juu ya hayo yote waweze kuyatolea taarifa kwa njia zinazo stahili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.