ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 2, 2019

CCM NJOMBE YAMPONGEZA LOWASA


Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Kimepinga Vikali Taarifa Zinazosambaa Mitandaoni na Mabishano ya Baadhi ya Wanasiasa Wanaomtuhumu Aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowasa Kurejea CCM Kuwa Amemkimbia Tundu Lissu Aliyetangaza Kuwa Endapo Chama Chake Kitampa Ridhaa ya Kugombea Urais Mwaka 2020 Basi Atagombea.

Mwaka 2015 Edward Lowasa Baada ya Jina Lake Kukatwa Kwenye Harakati za Kutaka Kugombea Urais Kupitia CCM Alitimkia CHADEMA Na Kuhudumu Katika Chama Hicho Kwa Kipindi Cha Takribani Miaka Mitatu Sasa na Hatmaye Jana Ametangaza Kurejea Kwenye Chama Chake Cha CCM.

TAARIFA ZAIDI NA AMIRI KILAGALILA

Friday, March 1, 2019

TCRA YAWA MFANO KATIKA MKUTANO WA TAASISI ZA MAWASILIANO AFRIKA AFRAT



TANZANIA kama ilivyo nchi nyengine duniani, imeshuhudia ukuaji wa sekta ya mawasiliano ambayo imechangia katika kuboresha maisha ya wananchi kijamii na kiuchumi sambamba na pato la taifa.

Ukuaji wa sekta hii umechangiwa na kuwepo kwa sera, sheria kanuni na mfumo mzuri wa utoaji leseni za huduma za mawasiliano.

Sekta hii inachangia katika uchumi moja kwa moja na kwa kupitia sekta ya elimu, afya, kilimo, biashara, ajira, mabenki, utalii, uwekezaji na sekta nyingine zote kama nyenzo ya uwezeshaji katika kuongeza ufanisi wa utendaji kupitia jamii habari.

Tarehe 28 Februari 2019 jiji la Mwanza linakuwa wenyeji wa mkutano wa Baraza la Uongozi la Mawasiliano kutoka Chuo cha Raslimali Watu kwa Maendeleo ya Afrika (AFRALTI) kilichopo Jijini Nairobi nchini Kenya.  ambapo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella leo anafungua mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania, Isack Kamwelwe.

Huu ni mkutano unaojumuisha nchi za mbalimbali kutoka Afrika Mashariki na Kusini ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, Zimbabwe, Msumbiji, Lesotho na Burundi. wa Mkoa wa Mwanza John Mongella anamwakilisha Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi  kama mgeni rasmi wa mkutano huo.

Fuatilia video kujua yapi yaliyojiri.

MWILI WA RUGE WAWASILI NCHINI UKITOKEA AFRIKA KUSINI.




Mwili wa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group, Ndugu Ruge Mutahaba umewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ukitokea Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu. Ambapo msafara umeanza kutoka Airport mpaka Lugalo.

Thursday, February 28, 2019

TAMKO LA WANAHABARI MWANZA KWA JESHI LA POLISI.


WAZIRI wa mambo ya ndani Kangi Lugola na mkuu wa jeshi la polisi nchini Simon Sirro wameombwa kutoa maagizo kwa jeshi la polisi nchini kutambua uwepo wa waandishi wa habari wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao kutokana na kukithiri kwa vitendo vya jeshi hilo kuwakamata waandishi wa habari pindi  wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kikazi.

Ombi hilo limetolewa jijini Mwanza na Chama cha waandishi wa habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania [OJADACT] kwa kushirikiana na klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Mwanza [MPC] kufuatia tukio la kukamatwa waandishi wawili wa habari wakati wakitekeleza majukumu yao  katika kituo cha polisi Nyakato mkoani Mwanza.

Picha: WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezungumza na Wafanyabiashara wa Kati na wadogo wa Karikoo kwenye ukumbi wa Anatouglo jijini Dar Es salaam.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza kaika kikao cha wafanyabiashara wa kati na wadogo alichokiitisha, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa  Anatouglo jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza kaika kikao cha wafanyabiashara wa kati na wadogo alichokiitisha, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa  Anatouglo jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019
Baadhi ya wafanyabiashara wa kati na wadogo wa Kariakoo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Anatouglo jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019

Wednesday, February 27, 2019

RUGE AMTOA MACHOZI MKUU WALIYE SOMA NAYE SHULE MOJA.


MKUU wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema kuwa baada ya kupokea taarifa za msiba wa Ruge Mutahaba usiku wa jana hakuweza kupata usingizi kwa kuweweseka.

Mongella amesimulia mazito ya ukaribu wake na marehemu Ruge alioanzia shuleni hadi nyumbani kwa wazazi.

WAKATI HUO HUO.

Familia imeamua kwamba Ruge Mutahaba atakwenda kuzikwa nyumbani kwao huko Bukoba siku ya Jumatatu, siku ya Jumapili mwili utasafirishwa kwenda Bukoba.

Afya ya Ruge Mutahaba ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group (CMG) ilianza kutetereka katikati mwa 2018, na Juni mwaka huo alikwenda India kwa ajili ya matibabu na alirejea nchini Agosti 21, 2018.

Baada ya muda kidogo hakuonekana, Oktoba 2018 alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu, amekaa huko hadi alipofariki.

Ruge Mutahaba amefariki siku ya jana nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu ya figo. Ruge alizaliwa mwaka 1970, Brooklyn nchini Marekani, atakumbukwa zaidi kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya muziki nchini.

Monday, February 25, 2019

REPSSI YAENDELEA NA KAMPENI KUTOKOMEZA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI

Mkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala akiongea na vijana kijiweni kuhusu athali za mimba.

Mkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala akiongea na vijana kijiweni kuhusu athali za mimba
Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala 

Mwandishi wetu, Pwani.

Shirika linalojihusisha na masuala ya kijamii na kisaikolojia kwa watoto (REPPSI) limeendelea kufanya kampeni ya kutokomeza tatizo la ndoa na mimba za utotoni mkoani Pwani.

Kampeni hiyo inafanyika ili kuhakikisha watoto wa kike wanatimiza ndoto zao za kielimu ili kushiriki katika mkakati wa Serikali wa Tanzania ya viwanda.

Akizungumza na wakazi wa Kibiti Mkoani Pwani, Mkurugenzi Mkazi wa REPSI Tanzania, Edwick Mapalala alisema tatizo la mimba na ndoa za utotoni bado kubwa na kwamba linahitaji jitihada za pamoja kupambana nalo.

“Mfano ni hizi kampeni za kutoa elimu na kuihamasisha jamii kumthamini mtoto wa kike zinasaidia kwa hiyo kama tutaendelea nazo jamii itaelewa, watoto watatimiza ndoto zao,” alisema.

Mapalala alisema katika kampeni hizo wanazoshirikiana na Shirika la Pasada linalojihusisha na masuala ya Ukimwi chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Pwani, vijana hasa madereva bodaboda wamefikishiwa elimu kuhusu thamani ya mtoto wa kike.

Baadhi ya viongozi wa vijiji na kata walikiri kuwa ndoa za utotoni ni changamoto kubwa lakini wanaendelea kupambana nayo.

Mratibu wa Elimu Kata ya Salala, Wilayani Kibiti Erasmus Assenga alisema kwa mwaka huu tu wanafunzi wawili wa Sekondari katika kata hiyo wameacha masomo kwa mimba.

“Kwa hiyo kampeni hii ni muhimu kwa sababu watoto wa kike wenyewe wanafikishiwa elimu, jamii hasa wanaume wanaelezwa na wanajua umuhimu wa kuwathamini,” alisisitiza.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Pasada Ester Mbwana alisema anaamini kuwa baada ya kampeni hizo kutakuwa na mafanikio makubwa kwa sababu, jamii inaelewa na imekubali kusaidia katika ulinzi wa mtoto.

MAHAKAMA YASOGEZA MBELE KESI YA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE


Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe leo imewapandisha kizimbani kwa mara ya pili  watuhumiwa watatu wa mauaji ya watoto watatu wa familia moja wa kijiji cha Ikando kata ya kichiwa wilayani Njombe.

Watuhumiwa hao ni Pamoja na JOEL JOSEPH NZIKU,NASSON ALFREDO KADUMA  na ALPHONCE EDWARD DANDA Ambao Wanakabiliwa na Mashtaka ya Kuwaua Watoto Hao Kijijini Humo.

Watoto hao ni pamoja na Godliver Nziku, Gasper Nziku na  Giriad Nziku ambao ni watoto wa familia moja huku ikielezwa kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa la kuwaua januari 20 mwaka huu

Hakimu mkazi mkoa wa Njombe Magdalena Ntandu Ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 11 mwezi machi mwaka huu mpaka itakapotajwa tena huku watuhumiwa wakirejeshwa rumande.

kesi hiyo kwa mara ya kwanza ilitajwa mnamo tarehe 12 mwezi wa pili 2019 mbele ya mahakama na wakili mwandamizi wa serikali Ahmed Seif.

Sunday, February 24, 2019

SALAMU ZA POLE KUFUATIA AJALI ILIYOUA WATU 19 SONGWE

 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus E. Mwangela akitoa salamu za pole kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa ndugu, jamaa na marafiki wa wafiwa, kufuatia ajali ya gari iliyosababisha vifo 19. 
 Ndugu, jamaa na marafiki wa wafiwa, kufuatia ajali ya gari iliyosababisha vifo 19 wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus E. Mwangela akitoa salamu za pole.
 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus E. Mwangela akikagua majeneza kabla hayajakabidhiwa kwa wafiwa, kufuatia ajali ya gari iliyosababisha vifo 19.
Sehemu ya Majeneza 19 yaliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe kufuatia ajali iliyohusisha magari matatu, mkoa pia umewezesha usafiri wa miili ya marehemu hao.
MKUU wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus E. Mwangela anatoa salamu za pole kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa ndugu, jamaa na marafiki wa wafiwa, kufuatia ajali ya gari iliyosababisha vifo 19 ikiwa wanaume ni 15 na wanawake wanne.
Brig. Jen. (Mst) Mwangela amesema kutokana na ajali hiyo iliyotokea usiku eneo la Senjele Wilayani Mbozi ikihusisha magari matatu yaliyokuwa yakielekea Mbeya kugongana, serikali Mkoani Songwe imetoa majeneza 19 pamoja na usafiri kwa ajili ya kuhifadhi miili ya marehemu.
“Rais Magufuli amenituma niwape pole na ametuelekeza kama Mkoa kusimamia Mamlaka za Usalama barabarani kufanya uchunguzi na hatua zinazo stahili kuchukuliwa, pia ameelekeza tujipange vizuri kukabiliana na matukio ya ajali za barabarani”, amesema Brig. Jen. (Mst) Mwangela.
Brig. Jen. (Mst) Mwangela amesema chanzo cha ajali hiyo kimetokana na gari la abiria aina ya coaster kugongwa na gari la mizigo lililokuwa nyuma yake kisha coaster kugonga gari la mizigo lililo kuwa mbele yake na kupelekea gari la abiria kubanwa katikati ya magari mawili ya mizigo.
Aidha ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, kuweka utaratibu maalumu wa magari kupita kwa kupokezana katika maeneo yote yenye miteremko mikali, kuwepo ukaguzi wa magari kabla hayajaanza kushuka au kupanda mlima pamoja na kuweka ulinzi wa maeneo hayo.
“Mungu ametupa akili za kufanya kazi na akili hizi tuzitumie kuzuia ajali ndani ya Mkoa wa Songwe, hivyo nawasihi watumiaji wote wa vyombo vya moto kuhakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani ili kuweza kuepuka ajali kama hizi”, amesisitiza Brig. Jen. (Mst) Mwangela.
Mapema jana Brig. Jen. (Mst) Mwangela amefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songwe ambapo miili ya marehemu ilikuwa imehifadhiwa ili kuwafariji wafiwa waliofika kutambua miili ya ndugu zao.