ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 18, 2023

"UHURU NDIYE ALIFANYA RAILA KUTOCHAGULIWA" PASTA EZEKIEL ASEMA

Pasta maarufu Ezekiel Odero (kushoto) amesema Raila Odinga (kulia) alipoteza uchaguzi wa urais mwaka jana kwa kujihusisha na aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta.

Odero alisema Wakenya hawakumtaka Uhuru na hivyo kisu chao kikapita na kumkata Raila kwa sababu alikuwa rafikiye. Amemuonya Rais William Ruto kuwa waliomshabikia na kumchagua bado watamgeuka na kumwangusha.

“Hawa hawakupendi, ni kwa sababu hawakumpenda Kenyatta na wewe ulijitenga na yeye na hivyo wakakuona kama chaguo. Lakini si eti wanakupenda, hawa watu hawakupendi,” alisema Odero. Odero ametabiri kuwa hivi karibuni Rais Ruto atapokea upinzani mkali kutoka kwa wananchi.

“Rais niskie, hawakupendi. Usipowapa kile wanataka, wembe ni ule ule,” mhubiri huyo alimwambia Rais. Alisimulia kuwa wapiga kura huwachagua viongozi ila huwa wanakataa wapinzani kwenye debe na ndipo wengine kuibuka washindi.

“Walimkataa Moi, wakamchagua Kibaki. Kisha wakamkataa Kibaki tena, 2013 walichagua Uhuruto . . . kisha wakawakataa tena. Mimi Rais Ruto nakwambia wafanyia kazi kwa moyo mmoja lakini usidhani wanakupenda,” aliongeza. 

MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUANGUKIWA NA JIWE JIJINI MWANZA WAKATI AKITEKELEZA ADHABU

 Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwinuko iliyoko Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Glory Faustine (14) amefariki huku mwingine, Emmanuel Lyatuu (13) akivunjika mguu wa kulia baada ya kudondokewa na jiwe wakitekeleza adhabu ya kuchimba kifusi.

Akizungumza jana Machi 17, 2023 Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema wanafunzi hao ni kati ya wanafunzi 30 waliokuwa wamepewa adhabu ya kusomba kifusi kama adhabu ya kuzungumza Kiswahili shuleni hapo. Pia alisema jeshi hilo linamshikilia Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mwalu Baluya (51) na Mwalimu wa zamu, Theonest Malosha (35) kwa tuhuma za kufanya uzembe uliosababisha madhara kwa wanafunzi hao.

Thursday, March 16, 2023

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA AFRIKA KUSINI CYRIL RAMAPHOSA KATIKA KATIKA ZIARA YAKE YA KISERIKALI PRETORIA.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa mara baada ya kuwasili katika Majengo ya (Union Buildings), Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 16 Machi, 2023.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa wakati wakielekea kwenye Viwanja vya mapokezi ya Viongozi vilivyopo katika Ofisi za Majengo ya (Union Buildings), Pretoria nchini Afrika Kusini wakati wa ziara yake tarehe 16 Machi, 2023.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa katika viwanja vya Mapokezi ya Viongozi vilivyopo kwenye Majengo ya (Union Buildings), Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 16 Machi, 2023.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mapokezi ya Viongozi vilivyopo kwenye Majengo ya (Union Buildings), Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 16 Machi, 2023.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa wakati akimuonesha Majengo mbalimbali ya Mji wa Pretoria katika Ziara yake ya Kiserikali nchini Afrika Kusini tarehe 16 Machi, 2023.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuanza mazungumzo Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 16 Machi, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa yaliyofanyika katika Ofisi za Majengo ya Muungano, Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 16 Machi, 2023.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa wakati wakishuhudia utiaji saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi mbili, Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 16 Machi, 2023.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivalishwa Nishani ya Heshima kutoka kwa mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuzungumza na Wanahabari katika ziara yake ya Kiserikali, Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 16 Machi, 2023.

NAIBU KATIBU MKUU FEDHA AZIPONGEZA TIRA NA BENKI YA CRDB UANZISHWAJI WA AKAUNTI YA DHAMA YA BIMA

Dar es Salaam 16 Machi 2023 – Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Bima (TIRA), pamoja na Benki ya CRDB kwa kutekeleza mchakato wa uanzishwaji wa Akaunti ya Dhamana ya Bima (Trust Account).

Mafuru ametoa pongezi hizo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya utekelezaji wa akaunti hiyo kwa Wakurugenzi Watendaji na Maafisa Wakuu wa Fedha wa makampuni ya bima nchini yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.

Mafuru amesema uanzishwaji wa Akaunti hiyo ya Dhamana ya Bima ni hatua nzuri ambayo itasaidia kuimarisha usimamizi wa sekta ya bima kuendana na matakwa ya kisheria na udhibiti yaliyowekwa na TIRA.
Akielezea changamoto za hapo awali, Mafuru amesema utaratibu uliokuwa ukitumika mwanzoni katika usimamizi wa dhamana ya bima haukuwa mzuri jambo ambalo lilipelekea TIRA kushindwa kusimamia vizuri amana hizo pindi ziliporejeshwa kwa makampuni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) baada ya kuiva.

Amesema kuwa kampuni nyingi za bima zilikuwa zikitumia fedha za amana ya Akiba katika matumizi mengine, pasipo kupata idhini ya TIRA hivyo kupelekea kuingia katika changamoto ya ukwasi, na wakati mwengine kushindwa kulipa fidia kwa wateja kutokana na fedha kuwekezwa katika miradi mingine.

Mafuru alibainisha kuwa uamuzi wa kufungua Akaunti ya Dhamana ya Bima katika benki za biashara ni mwarobaini wa changamoto hiyo, kwani sasa TIRA itaweza kusimamia moja kwa moja fedha hizo za amana za akiba, jambo ambalo si tu litaimarisha usimamizi, bali pia kuboresha maendeleo ya sekta ya fedha.
“Niwapongeze Benki ya CRDB kwa kuwa benki ya kwanza kuungana na TIRA katika uanzishwaji wa Akaunti ya Dhamana ya Akiba. Lakini nimevutiwa na namna ambavyo mmeona kuna umuhimu wa kuandaa mafunzo haya ambayo yanalenga kuwajengea uelewa makampuni ya bima juu ya uendeshaji wa akaunti hiyo,” amesema Mafuru.

Aidha, Mafuru alimtaka Kamishina wa TIRA kuhakikisha kampuni zote za bima zinafuata sheria kwa kuweka dhamana ya amana. Alisema kwa kufanya hivyo kutasaidia kuchochea mafanikio ya sekta ndogo ya bima kama ilivyoanishwa katika Mpango wa Taifa wa miaka 10 wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Nchini ‘Financial Sector Development Master Plan’.
Akizungumza katika warsha hiyo, Kamishina wa Mamlaka ya Bima, Dkt. Baghayo Saqware amesema chimbuko la Akaunti hiyo ya Dhamana ya Bima ni Kanuni ya Bima ya mwaka 2009 inayozitaka Kampuni za Bima kuweka Amana za Usalama angalau asilimia 50 ya kiwango cha chini cha mtaji halisi wa kampuni husika ya bima.

Dkt. Saqware amesema mwaka jana Mamlaka kwa kushirikiana Chama cha Watoa Huduma za Bima (ATI), walikubaliana kuandaa Mwongozo wa Uwekazaji wa Usimamizi wa Ukwasi ambao pia ulielekeza uanzishwaji wa Akaunti ya Dhamana ya Akiba kupitia benki za biashara ili kuondokana na tatizo la changamoto ya kimtaji au kushindwa kulipa fidia za madai ya wateja wake.
“Mfumo unaokwenda kutumika katika akaunti hii mbali na kuboresha usimamizi, lakini pia ni rafiki na unaleta uwazi zaidi kwa wadau kwa maana ya kampuni za bima. Makampuni yataweza kupata taarifa ya dhamana kwa wakati, na kufanya uwekezaji kulingana na makubaliano na Mamlaka,” aliongezea Dkt. Saqware.

Akitoa taarifa za utendaji wa sekta ya bima, Dkt. Saqware alimjulisha Naibu Katibu Mkuu kuwa sekta hiyo imeendelea kukua kulinganisha na miaka iliyopita. Amesema mwaka jana mauzo ya bima yaliongezeka kwa asilimia 25 kufikia Shilingi Trilioni 1.146 kulinganisha na mauzo ya 2021. Aidha, alibainisha kuwa malengo ya mwaka huu ni kufikia Shilingi Trilioni 1.5.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid ameishukuru TIRA kwa kuipa fursa ya kushiriki katika uanzishwaji wa Akaunti ya Dhamana ya Bima. Nsekela alipongeza uamuzi wa uanzishwaji wa akaunti hiyo na kusisitiza kuwa inachukua jukumu muhimu katika kukuza uwazi zaidi na uwajibikaji katika sekta ya bima, na kuwa itakwenda kusaidia pia kujenga imani kwa wadau wa sekta hiyo.

Nsekela Akaunti ya Dhamana ya Bima iliyofunguliwa Benki ya CRDB imezingatia kwa asilimia mia moja mapendekezo ya TIRA na wadau wa sekta ya bima, huku akibainisha kuwa akaunti hiyo imeunganishwa na mifumo ya kidijitali itakayosaidia katika usimamizi na utoaji wa taarifa kwa Mamlaka na kampuni za bima.
“Kwa kuzingatia kuwa fedha hizi pia zimekuwa zikitumika kwa uwekezaji wa makampuni, Benki yetu imejipanga kikamilifu katika kutoa ushauri na usaidizi wa uwekezaji kupitia Idara yetu ya Hazina na Masoko ya Mitaji,” amesema Nsekela.

Nsekela alimuhakikishia Naibu Katibu Mkuu kuwa Benki ya CRDB itaendelea kushirikiana na TIRA na wadau wa sekta ya bima kusaidia Kuboresha sekta hiyo. Nsekela alisema Benki hiyo imekuwa kinara katika utoaji wa huduma za bima kupitia mfumo wa BancAssuarance, huku akibainisha kuwa imekuwa ikitoa huduma hizo katika matawi yake, CRDB Wakala, na kidijitali kupitia SimBanking.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru (katikati), Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Baghayo Saqware (kulia), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB na TIRA walioshirika katika mchakato wa uanzishaji wa Akaunti ya Dhamana ya Bima wakati wa hafla ya mafunzo ya uendeshaji wa akaunti hiyo iliyoandaliwa na Benki ya CRDB na TIRA.

KAMA KUNA KAMPUNI YA BIMA INAKUZUNGUSHA HAITAKI KUKULIPA HILI HAPA SULUHISHO.

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Zipo changamoto nyingi ambazo jamii imekuwa ikikumbana nazo wakati wa kudai fidia za bima mbalimbali, iwe chombo cha moto cha usafiri, bima ya nyumba, kampuni, bima ya afya au hata pengine pale mtu kutoka ndani ya jamii anapotumikia kazi au ajira yake kwa uaminifu na ikafika wakati wa ulipwaji kukazuka changamoto katika udai wa fidia.

Kupitia maonesho ya WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI iliyofanyika katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, Jembe Fm inadhuru katika banda la Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima ambapo inapata maelezo kwa kina. Sasa basi kama unachangamoto ya kupunjwa fidia, kutoridhika na kiwango cha fidia, kucheleweshewa malipo, kukataliwa madai yote, huu ni wasaa wako wa utatuzi.

Wednesday, March 15, 2023

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan awasili Jijini Pretoria kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku moja nchini Afrika Kusini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Waterkloof Air Force Base Pretoria kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya Kiserikali nchini Afrika Kusini tarehe 15 Machi, 2023.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Maua kutoka kwa Mtoto Malaika Adam Issara mara baada ya kuwasili Jijini Pretoria kwa ajili ya ziara ya Kiserikali nchini Afrika Kusini tarehe 15 Machi, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiimba pamoja na baadhi ya Watanzania wanaoishi Pretoria nchini Afrika Kusini (Diaspora) mara baada ya kuwasili nchini humo tarehe 15 Machi, 2023.

DC MOYO MARUFUKU KUWAWEKEA VIJITI WATOTO WA KIKE.

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi kuacha mara moja tabia ya kuwawekea vijiti watoto wao

Na Fredy Mgunda, Iringa.

MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amewataka wanawake kuacha tabia ya kuwawekea vijiti vya uzazi wa mpango watoto mwenye umri wa chini ya miaka 18 kufanya hivyo sawa na ukatili wa kijinsia.

Akizungumza wakati mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Litula, Moyo aliwataka wanawake kuacha mara moja tabia kuwawekea vijiti watoto wadogo kwa kuwa hawajui madhara yake.

Moyo alisema tabia ya kuwawekea vijiti watoto wakiwa na umri mdogo kutasababisha waanze kufanya mapenzi katika umri huo bila kuwa na woga wowote ule.

Alisema kuwa ataanzisha msako maalumu kwa kila shule ili kubaini wanafunzi wangapi wamewekewa vijiti na ni nani kawawekea vijiti hivyo na hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Aidha Moyo aliwataka wazazi wa wilaya hiyo kuwafundisha watoto amaadili mema ambayo yatawasaidia watoto walelewe katika misingi inavyotakiwa.

Moyo alimazia kwa kusema kuwa kuwawekea vijiti watoto kunawakinga na mimba pekee yake vipi kuhusu magonjwa mengine kama vile ukimwi,kisonono,na mengine yanayotokana na ngono zembe

Kwa upande wao wazazi wa watoto hao walikiri kufanya jambo hilo la kuwawekea vijiti vya uzazi watoto wao ili kuwaepusha na mimba za utotoni ambazo zimekuwa zikikatisha ndoto za maisha yao mapema.

GODBLESS LEMA 'BODABODA WAKISTUKA WATAKUJA KUNISHUKURU'

 NA ALBERT GSENGO/MWANZA

Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kanda ya kaskazini Godbless Lema kazingumza na mtangazaji Alice Stephen 'Queen Chichi' katika kipindi cha Kazi na Ngoma ya Jembe Fm na kurejea kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kuhusu bodaboda nchini. Pamoja na hayo amezungumzia pia utawala wa Serikali ya awamu ya sita unaoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ......

Monday, March 13, 2023

SADC: MAKATIBU WAKUU WA SADC WAKUTANA KINSHASA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye ni Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC ngazi ya Makatibu Wakuu akiwa katika meza ya Tanzania wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa SADC unaofanyika Kinshasa, Jamhui ya Kidemokrasia ya Congo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mtangamano wa Kikanda wa DRC ambaye ni Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu, Balozi Songhu Kayumba akisoma hotuba ya ufunguzi ya kikao hicho.
 Wajumbe wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wanaoshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC, ngazi ya Makatibu Wakuu unaofanyika Kinshasa, Jamhui ya Kidemokrasia ya Congo.

Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ( SADC) umefunguliwa leo tarehe 13 March 2023 jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambapo ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina  Shaaban.

Wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Makatibu Wakuu, Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mtangamano wa Kikanda wa DRC, Balozi Songhu Kayumba alisisitiza umuhimu wa wajumbe kushiriki kikamilifu kwa kutoa maoni yatakayolenga kufanikisha utekelezaji wa agenda  zitakazojadiliwa.

Makatibu Wakuu wanajadili agenda mbalimbali ambazo ni pamoja na hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Maamuzi ya Wakuu wa Nchi na Serikali waliyotoa katika Mikutano iliyopita.

Tanzania inashiriki kikamilifu kwenye Mkutano huo na imejipanga kusukuma utekelezaji wa agenda ilizoziibua au kuziunga mkono katika mikutano iliyopita.

 Agenda hizo ni pamoja na: ujenzi wa sanamu la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambalo litasimikwa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU); Tafsiri ya Nyaraka muhimu za SADC katika lugha ya Kiswahili ambayo ni hatua muhimu ya utekelezaji wa matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye Jumuiya; Mpango wa Kanda wa Ununuzi wa Pamoja wa Bidhaa za Afya unaoratibiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD); na Mkakati wa pamoja wa Kanda wa Kusimamia Sekta ya Mbolea.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena L. Tax (Mb) anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri  utakaofanyika kuanzia tarehe 18 hadi 20 Machi 2023 baada ya Mkutano wa Makatibu Wakuu kukamilika.

MSOWOYA AWAFUNDA WASICHANA KIDATO CHA SITA KATIKA MAHAFARI YA TYSS - MBALAMAZIWA SEKONDARI

Dkt Tumaini Msowoya akizungumza na wanafunzi wa kidato cha sita na pembeni ni Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbalamaziwa, Sister Revina Kilai
Dkt Tumaini Msowoya akizungumza na wanafunzi wa kidato cha sita na pembeni ni Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbalamaziwa, Sister Revina Kilai
Dkt Tumaini Msowoya akifurahia jambo na wanafunzi wa kidato cha sita Shule ya Sekondari ya Mbalamaziwa.

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Iringa Dkt Tumaini Msowoya amewaasa wasichana wa kidato cha sita  kuwekeza katika bidii, utii na kumcha Mungu kama ngao yao ya mafanikio.

Dkt Msowoya alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafari ya kidini ya TYSS,  kwa wanafunzi wa kike wa kidato cha sita katika  Shule ya Sekondari ya Mbalamaziwa, Wilayani Mufindi, Mkoani Iringa.

"Hata ukifaulu kwa alama za juu sana kama sio mtii, humchi Mungu bidii yako ni bure tu," amesema.

Mjumbe huyo wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Iringa pia aliwapongeza walimu na viongozi wa Kanisa la Roman Katholiki kwa kuwafundisha wanafunzi hao katika msingi wa maadili kiasi cha kuwafanya wajitambue.

Awali, Paroko wa Patokia ya Nyakipamba, Padre Kizito Fungo aliwaasa wahitimu hao kumtanguliza Mungu katika kila jambo.

Nae Makam Mkuu wa Shule ya Sekondari ya  Mbaramaziwa, Sister Revina Kilai amesema wanafunzi hao wameandaliwa vizuri tayari kwa kukabiliana na mitihani.

RC MONGELLA AZITAKA TAASISI MBALIMBALI KUHAKIKISHA KUNAKUWEPO NA UWIANO WA KIJINSIA MAHALA PA KAZI.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongella amezitaka taasisi mbalimbali kuhakikisha kunakuwepo na uwiano sawa wa jinsia kati ya wanaume na wanawake ili kuwepo kwa usawa mahala pa kazi. Ameyasema hayo jijini Arusha wakati akizungumza na wadau mbalimbali wa Benki ya CRDB walipokutana katika chakula cha jioni  kusherehekea siku ya wanawake duniani, iliyofanyika jana jijini humo.

Mongella alisema, hakuna agenda ya maendeleo inayoweza kufikiwa bila kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanawake na kuweza kupatiwa ufumbuzi kwani wanawake ni jeshi kubwa na wana mchango mkubwa sana katika jamii.

"Naipongeza sana benki ya CRDB kwa namna ambavyo imejitahidi kukumbatia usawa wa kijinsia na kuweza kuwajengea uwezo wa kuwezesha wafanyakazi wa kike kwani nameambiwa asilimia 47 ya wanawake ni wafanyakazi wa benki hii huku wanaume wakiwa ni asilimia 53 na juhudi zaidi zinaendelea za kuongeza idadi ya wanawake ni mfano mzuri wa kuigwa na taasisi zingine. "amesema Mongela.
Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile amesema, kumekuwepo na ongezeko  la asilimia 3 la idadi ya wanawake katika benki hiyo tofauti na miaka ya nyuma na kuweza kuleta dhana nzima ya usawa wa kijinsia mahala  pa kazi.
 
Alisema benki hiyo ina programu ya kuwajengea uwezo wanawake katika ngazi ya kati ambapo wanawake mia moja wanashiriki katika programu hiyo huku lengo kuu ni kufikia idadi ya zaidi ya wanawake mia mbili ili kuleta usawa wa kijinsia.

"Kupitia kitengo cha biashara benki imeweza kufikia wanawake wadogo na wa kati kwa kutoa kiasi cha shs 67.3 bilioni hadi desemba 2022 ambapo jumla ya wanawake 3,122 wameweza kufikiwa katika mikoa yote Tanzania."amesema Bruce.

Aidha amesema kuwa, benki hiyo imeendelea kusisitiza jitihada zake katika maswala ya kijinsia na kukumbatia usawa katika jamii kwa ujumla ili kuondokana na changamoto ya kupigania usawa mahala pa kazi penye uwiano.
Kwa upande mwingine watoa mada mbalimbali walipata fursa ya kuchangia na kutoa wito kwa Wanawake nchini kujiamini na kuangalia fursa mbalimbali zilizopo na kuweza kuzichangamkia kwakua wao wanamchango mkubwa sana katika jamii kwa kuinua pato la taifa.

”Mwanamke ana uwezo mkubwa sana wa kuleta mabadiliko  katika jamii endapo atatumia fursa zilizopo kujikwamua kiuchumi bila kujali  nafasi hiyo inamhusu yeye au lah. alisema mchangia mada, Faraja Nyalandu.

Aliongeza kuwa, katika nyakati hizi za sayansi na teknolojia kila mmoja wetu anapaswa kwenda na mabadiliko yaliyopo sambamba na kuwa wabunifu katika maswala mbalimbali na kuwa kinara wa kuweza kutoa ajira kwa wanawake wengine.

Kwa upande wake Mshauri wa maswala ya ukimwi katika hospitali ya Olturumeti, Dk Consolata Swea akizungumza katika jukwaa hilo aliwataka wazazi wote kwa pamoja kuhakikisha wanasimamia malezi ya watoto wao kwani kwa.sasa hivi maadili yameporomoka kwa kiwango  kikubwa sana.

Aidha aliwataka wazazi kuwa marafiki wa watoto wao ili waweze kuwa wawazi katika kuelezea yale yote wanayofanyia na ndugu kwani kadri unavyokuwa karibu na mtoto ndivyo wanakuwa wawazi katika kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili.

"Kila mmoja anajua ukatili wanaofanyiwa watoto wetu na wanaofanya hivyo ni ndugu wenyewe wa familia na nawaomba sana msiwaamini ndugu kamwe wanapofika na wakati mwingine kulala na watoto kwani hao hao ndio wanawageuka."amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha ICT kutoka benki ya CRDB, Mwanaisha Kejo alisema kuwa,wanawake wana uwezo mkubwa wa kuyasemea maswala mbalimbali sambamba na kuendesha mabenki hivyo wanatakiwa  kujiongeza zaidi  na kufika viwango  vya juu zaidi.

Benki ya CRDB imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mwanamke haachwi nyuma, na kila mwaka imekuwa ikiunngana na wadau wengi Duniani katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimisha kila ifikapo machi 8 ya kila mwaka.