Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwinuko iliyoko Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Glory Faustine (14) amefariki huku mwingine, Emmanuel Lyatuu (13) akivunjika mguu wa kulia baada ya kudondokewa na jiwe wakitekeleza adhabu ya kuchimba kifusi.
Akizungumza jana Machi 17, 2023 Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema wanafunzi hao ni kati ya wanafunzi 30 waliokuwa wamepewa adhabu ya kusomba kifusi kama adhabu ya kuzungumza Kiswahili shuleni hapo. Pia alisema jeshi hilo linamshikilia Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mwalu Baluya (51) na Mwalimu wa zamu, Theonest Malosha (35) kwa tuhuma za kufanya uzembe uliosababisha madhara kwa wanafunzi hao.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.