Saturday, December 17, 2022
JUMLA YA VIJANA 300 KUNUFAIKA NA MRADI WA IMARIKA KIJANA MKOANI IRINGA.
Friday, December 16, 2022
UKEREWE HAIJAWAHI KUWA NA HOSPITALI YENYE ICU
NA ALBERT G. SENGO/UKEREWE
Halmashauri ya wilaya ya ukerewe mkoani mwanza imefanikiwa kuokoa shilingi millioni 74 kwenye mradi wa ujenzi wa Jengo la wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum(ICU)katika Hospitali ya BWISYA iliyopo kwenye kisiwa cha Ukara wilayani humo. Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo DOKTA ALEX SIBONA amesema kuwa fedha hizo ni kati ya shilingi millioni 251 zilizotolewa na serikali kuu kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi huo. Ujenzi wa mradi wa ICU katika hospitali ya BWISYA umefikia hatua za mwisho kukamilika ambapo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ukerewe EMMANUEL SHELEMBI amewaasa wananchi kuendelea kuunga mkono Jitihada za serikali ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Wilaya ya ukerewe kwa sasa haina huduma ya ICU na Hospitali ya BWISYA inatarajiwa kuwa ya kwanza kutoa huduma hiyo.MKENYA AISHIYE MAREKANI AKUTWA AMEFARIKI CHUMBANI KWAKE.
Usiku wa Jumamosi ya Desemba 10, Kevin Odero alikuwa nyumbani kwa wazazi wake huko Connecticut, Marekani, na dada yake mdogo alipokata roho ghafla. Kulingana na dadake, mwili wa Kevin tayari ulikuwa umebadilika na kuwa rangi ya zambarau polisi walipofika.
Wakati huo babake kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 alikuwa amesafiri hadi Kenya na kuwaacha, bila kujua kwamba mauti yangelimfika mwanawe mpendwa.
Dadake Kevin Elizabeth Odero alimwambia Hillary Lisimba wa TUKO.co.ke kwmaba dada yao aligundua mwili wa kaka yao ingawaje kwa kuchelewa.
Kwa mujibu wake, mwili wa kijana huyo ulikuwa tayari umegeuka zambarau na juhudi za kupigia simu ya 911 ya huduma za dharura kuja kumkimbiza hospitalini hazikuzaa matunda.
“Walijaribu kumuamsha lakini maafisa wa afya walithibitisha kuwa tayari alikuwa amefarik dunia, ndiposa polisi walipochukua maiti ili kufanya uchunguzi,” alieleza.
Elizabeth alifichua kuwa marehemu alikuwa na umri wa miaka 20, alizaliwa na kukulia Nairobi lakini alijiunga na familia yake Marekani mnamo 2020.
Wakati wa kifo chake, alikuwa amemaliza tu diploma yake ya shule ya upili na alikuwa akifanya kazi ya muda huko Amazon.
Mojawapo ya mipango ya Kevin kwa mwaka ujao ilikuwa kujiunga na chuo cha ufundi mwezi Januari na kuendelea na kozi ya ufundi wa mabomba.
"Mwili wake ulichukuliwa na polisi jana na kwa sasa umelazwa katika makafani moja huko Massachusetts," alisema Elizabeth.
Familia yake kwa sasa inajaribu kuchangisha dola 18,000 (KSh 2.2 milioni) ili kuwezesha mwili wake kurejeshwa nchini Kenya kwa mazishi.
Katika michakato mtandaoni iliyolenga kusaidia kuchangisha fedha, Kevin alisifiwa kama "mwana mpendwa wa Joseph Odero na kaka wa Virginia wa New Haven Connecticut na Adrian Amani."
"Tafadhali mkumbuke Joseph na binti yake katika maombi na ujisikie huru kuwaambia marafiki wengine na kuwaongeza kwenye kikundi," sehemu ya chapisho hilo ilisema.
Elizabeth alifichua kwamba familia hiyo itaandaa misa ya wafu Desemba 23 kisha mwili utasafirishwa hadi nchini Kenya kwa mazishi.
MREMBO HUYU ANASIKITIKA KUKOSA MPENZI WA KUMUOA.
Kisura ambaye ni mama wa mtoto mmoja, Ayishatu Adams ametangaza mitandaoni kwamba anatafuta mume wa kumuoa.
Katika video ya kusikitisha kwenye TikTok, mwanafunzi anayesomea uuguzi alifichua kuwa atakuwa na umri wa miaka 35 mnamo 2023 na bado hana mchumba.
Ayishatu alilalamika kwamba wanaume wanaomrushia ndoano huhepa baadaye kwani hawataki kuchukua majukumu ya kumlea mtoto wake.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 34 alifichua kwamba jambo hilo linamtia huzuni.
"Nitakuwa na umri wa miaka 35 mwakani na bado sijaolewa kwa sababu nina mtoto. Mwanaume yeyote anayekuja kwangu anasema hawezi kujukumikia kisicho chake."
Haya ni baadhi ya maoni ya watu kuhusiana na kilio cha kidosho huyo;
Abbati SK alisema: "Hao wanaume kamwe hakupendi wala kukuthamini ndiyo maana wanakuhepa. Mtu sahihi atakuja na atakuthamini."
Abubakari Rahinat683 alisema: ''Mwanamume sahihi na mcha-Mungu atakupata na hakuna haraka maishani. Mwenyezi Mungu anapanga zawadi maalum kwa ajili yako."
korkor_1992 alisema: ''Zingatia sana kumlea mtoto wako kwani yeye ndiye mtu pekee ambaye atakuwepo kwa ajili yako kila wakati." zee-money alisema: "Usifadhaike wanaume wote unaokutana nao sio wako Mungu atakutendea haki."
BENKI YA CRDB, IFC ZAKUBALIANA MAENEO SITA YA USHIRIKIANO.
Tuesday, December 13, 2022
BIBI HARUSI ASHANGAZA KUVALIA GAUNI JEUSI KWENYE HARUSI YAKE.
Bibi harusi kutoka Nigeria kwa sasa anavuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha zake za harusi kusambaa mtandaoni.
Dasplang
Rinset Lisa aliamua kubadilisha tamaduni ya kuvalia gauni jeupe kwenye harusi
na kuvaa gauni jeusi.
Katika picha hizo, bibi harusi huyo
aliyetambulika kwa jina la Dasplang Rinset Lisa, aliamua kubadilisha tamaduni
ya kuvalia gauni jeupe kwenye harusi na kuvaa gauni jeusi na alionekana
kupendeza ndani yake.
Kupitia
ukurasa wake wa Facebook, Lisa alifichua kwamba watu wengi walimuuliza maswali
mengi kuhusu kwa nini aliamua kuvaa nguo nyeusi siku ya harusi yake.
“Nilipata
maswali mengi kuhusu kwa nini nilichagua kuvaa gauni jeusi kwenye harusi yangu.
Sawa nina
majibu mengi ya maswali, hili nitaandika baadaye, lakini kwa sasa kuna mtu
yeyote anaweza kuniambia kwa nini atapendelea gauni jeupe na kwa nini asipende
rangi nyingine yoyote ya mavazi?” alimaka.
TALIA: WANAWAKE WATATU WAUAWA KWA RISASI KATIKA MGAHAWA
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo aliingia katika mgahawa uliopo Jijini Rome na kufyatua risasi ambazo pia zilijeruhi wengine wanne huku mmoja akiwa kwenye hali mbaya kiafya
Mtuhumiwa ambaye ana umri wa miaka 57, amekamatwa baada ya kuzidiwa nguvu na raia waliopambana kumdhibiti
Mmoja kati
ya waliouawa ni Nicoletta Golisano, huyu ni rafiki wa Waziri Mkuu wa Italia,
Giorgia Meloni.
Monday, December 12, 2022
TMDA YAWAPIGA MSASA WAKAGUZI WA DAWA NA VIFAA TIBA MKONI IRINGA.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kuwajengea
uwezo wataalamu wa ukaguzi wa dawa na vifaa tiba katika Halmashauri zote za
Mkoa wa Iringa kwa lengo la kuboresha ufanisi wa kazi wawapo kazini ili kulinda
afya za watumiaji wad awa na vifaa tiba.
Akizungumza wakati wa kufungua
mafunzo hayo kaimu katibu tawala mkoa wa Iringa,Elias luvanda alisema kuwa ni
kielelezo tosha kuwa wakaguzi ngazi ya Halmashauri mnathamini mchango wa TMDA
katika kuwapa elimu kuhusu namna bora ya kutekeleza majukumu na kulinda Afya za wananchi ili waweze kushiriki
kikamilifu katika ujenzi wa taifa letu la Tanzania.
Luvanda alisema kuwa Mamlaka ya
Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Afya, yenye
jukumu la kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa Dawa, Vifaa Tiba na
Vitendanishi na Taasisi hiyo imeundwa chini ya sheria ya Dawa na Vifaa Tiba
sura 219.
Alisema
kuwa majukumu yanayofanywa na TMDA na yale yaliyokasimishwa kwenu, lengo lake
ni lilelile la kulinda afya ya jamii kwa kuzuia athari zinazoweza kujitokeza
kutokana na matumizi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi.
“Kwa
kutambua jukumu zito la TMDA, Serikali iliona ni vema kukasimu baadhi ya
madaraka na majukumu yao kwa Halmashauri kwa lengo la kusogeza karibu na
wananchi huduma za udhibiti wa ubora na usalama wa dawa, vifaa tiba na
vitendanishi”alisema Luvanda
Luvanda aliwataka watendaji wote
kufanya kazi kwa kutoa taarifa zilizo sahihi kwa wakati unatakiwa ili
kurahisisha utendaji wa taasisi hiyo hivyo Mwongozo wa Kukasimu Madaraka na
Majukumu umebainisha wazi kuwa taarifa za utendaji kazi za robo mwaka na
taarifa za ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa kazi za udhibiti wa ubora,
usalama na ufanisi wa bidhaa zinazodhibitiwa katika soko zinatakiwa kuandaliwa
na kutumwa TMDA kupitia viongozi wa ngazi ya Halmashauri.
“Ni mategemeo yangu kwamba mafunzo haya yatatoa
maelekezo ya namna ya kuboresha utendaji kazi wenu, na kuondoa changamoto
zinazojitokeza mara kwa mara kuwa, wakaguzi wa Halmashauri wanatumia nguvu
nyingi nyakati za kaguzi ambazo husababishwa na kutokutoa elimu kwa wateja
(wafanyabiashara) Hivyo kukinzana na utaratibu wa ukaguzi wa TMDA ambao
umejikita zaidi katika kuelimisha na kuwezesha” alisema Luvanda.
Alimalizia kwa kusema kuwa Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa itafanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa maagizo na makubaliano
yatakayowekwa ili kuhakikisha wananchi wanahakikishiwa upatikanaji wa bidhaa
bora na salama.
Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka
ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kanda ya kati
Sonia Mkumbwa alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea ujuzi wakaguzi
ili waweze kufanya kazi ya ukaguzi kwa kuzingatia sheria.
Mkubwa alisema kuwa wakaguzi
watatekeleza kazi zao kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo kama zilivyotolewa
na TMDA kama vile Kufanya ukaguzi wa maeneo yanayohusika na utunzaji,
uuzaji na usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi, Kufanya ufuatiliaji
na kutoa taarifa za ubora na usalama wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika
soko.
Aliongeza kuwa wakaguzi watatakiwa kuchukua sampuli za bidhaa
zinazodhibitiwa kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara pale inapohitajika na kufanya ufuatiliaji wa madhara/matukio yanayohisiwa
kusababishwa na matumizi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi.
Mkumbwa
alisema kuwa wakaguzi wanatakiwa kufanya uhakiki wa bidhaa zisizofaa kwa
matumizi kabla ya uteketezaji kwa kujaza fomu ya uhakiki (Kiambatisho Na.7)
baada ya mawasiliano na Ofisi ya Kanda ya TMDA na kusimamia zoezi la kuteketeza
bidhaa ambazo hazifai kwa matumizi baada ya uhakiki na kisha kujaza fomu ya
uteketezaji (Kiambatisho Na. 8) na kuiwasilisha ofisi ya Kanda ya TMDA kwa
ajili ya kuandaa cheti cha uteketezaji.
Alimazia kwa kuwasema kuwa kila
Halmashauri itaandaa na kuwasilisha taarifa za utendaji kazi kwenye Ofisi za
TMDA za Kanda na kuwasilisha nakala kwa
Katibu Tawala wa Mkoa ambazo ni taarifa ya utendaji ya robo
mwaka na taarifa
ya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa kazi za udhibiti wa ubora, usalama
na ufanisi wa bidhaa katika soko.