ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, December 13, 2022

BIBI HARUSI ASHANGAZA KUVALIA GAUNI JEUSI KWENYE HARUSI YAKE.

Bibi harusi kutoka Nigeria kwa sasa anavuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha zake za harusi kusambaa mtandaoni.


Dasplang Rinset Lisa aliamua kubadilisha tamaduni ya kuvalia gauni jeupe kwenye harusi na kuvaa gauni jeusi.


 Katika picha hizo, bibi harusi huyo aliyetambulika kwa jina la Dasplang Rinset Lisa, aliamua kubadilisha tamaduni ya kuvalia gauni jeupe kwenye harusi na kuvaa gauni jeusi na alionekana kupendeza ndani yake.


Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Lisa alifichua kwamba watu wengi walimuuliza maswali mengi kuhusu kwa nini aliamua kuvaa nguo nyeusi siku ya harusi yake.

 

“Nilipata maswali mengi kuhusu kwa nini nilichagua kuvaa gauni jeusi kwenye harusi yangu.

Sawa nina majibu mengi ya maswali, hili nitaandika baadaye, lakini kwa sasa kuna mtu yeyote anaweza kuniambia kwa nini atapendelea gauni jeupe na kwa nini asipende rangi nyingine yoyote ya mavazi?” alimaka.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.