ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 8, 2022

BREAKING NEWS: RAIS AFANYABMABADILIKO KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi Januari 8,2022 amefanya mabadiliko Madogo katika Baraza la Mawaziri, Makatibu Wakuu, Manaibu Makatibu Wakuu.


Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Akitangaza mabadiliko hayo leo Jumamosi Januari 8, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Rais amefanya mabadiliko ya muundo katika wizara tatu.


Rais Samia amefanya mabadiliko hayo ikiwa anatimiza ahadi yake ya kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.


Ofisi ya Rais Ikulu
Waziri wa Nchi Kazi Maalum – Kapeni Geroge Mkuchika

Waziri wa Utumishi – Jenista Mhagama

Naibu Waziri Utumishi – Deogratius John Ndejembi


TAMISEMI

Waziri – Innocent Bashungwa

Naibu Waziri – David Silinde

Naibu Waziri – Dugange


Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira

Waziri – Suleimani Jafo

Naibu Waziri – Hamis Hamis


Wizara ya Kazi Ajira

Waziri – Ndalichako

Naibu Waziri – Patrobas Katambi


Wizara ya Fedha

Waziri – Mwigulu Mwigulu
Naibu Waziri – Chande


Wizara ya Ulinzi

Waziri – Stergomena Tax


Wizara ya Sheria na Katiba
Waziri –  George Simbachawene
Naibu Waziri – Godfrey Mizengo Mizengo Pinda


Wizara ya Kilimo
Waziri – Hussein Bashe
Naibu Waziri – Anthony Mavunde


Wizara ya Uvuvi
Waziri – Mashimba Ndaki
Naibu Waziri – Abdallah Hamisi Ulega


Wizara ya Ardhi
Waziri – Angelina Mabula
Naibu Waziri – Ridhiwani Kikwete


Wizara ya Mambo ya Ndani

Waziri  – Mhandisi Hamad Masauni
Naibu Waziri – Sagini Jumanne Abdallah


Wizara ya Mambo ya Nje
Waziri – Liberata Mulamula
Naibu Waziri – Mbaruku


Wizara ya Maliasili
Waziri – Dkt. Damas Ndumbaro
Naibu Waziri – Mary Masanja


Wizara ya Nishati
Waziri – January Makamba
Naibu Waziri – Steven Byabato


Wizara ya Madini
Waziri – Dkt. Dotto Biteko
Naibu Waziri – Kiluswa


Ujenzi
Makame Mbarawa
Atupele Mwakibete
Godtlfrey Kasekenya


Viwanda
Kijaji
Kigahe


Wizara ya Afya
Ummy Mwalimu
Ole Mollel


Wizara ya Elimu
Mkenda
Kipanga


Maendeleo ya jamii
Gwajima dorothy
Mwanaidi Hamis


Wizara ya Maji
Jumaa aweso
Mahundi


Wizara ya Utamaduni
Mchengerwa
Gekul

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI AKAGUA MAENDELEO UJENZI WA MV MWANZA


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara ametembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Meli ya “MV Mwanza Hapa Kazi Tu” wenye gharama ya shilingi bilioni 89, ni mradi wa ujenzi ambao unatekelezwa na kampuni ya ujenzi ya GAS ENTEC wakishirikiana na KANG NAM kutoka Korea Kusini pamoja na SUMA JKT kutoka Tanzania.

MV Mwanza Hapa Kazi tu, itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200, mizigo tani 400, magari makubwa 3 na magari madogo 20, huku ikiwa na urefu wa mita 92 (sawa na pungufu kidogo ya ukubwa wa uwanja wa mpira wa miguu). Meli hii itakuwa mbadala wa meli ya MV Bukoba ambayo miaka 25 iliyopita ilizama na kupoteza maisha ya Watanzania wengi. Katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2015 Rais wa Awamu ya Tano, Hayati, Dkt John Pombe Magufuli aliwaahidi wananchi wa kanda ya ziwa kuwa atajenga meli kubwa kuwaenzi waliokufa kwenye ajali hiyo lakini pia kuimarisha usafirishaji upande huo wa Tanzania kwani kuna fursa nyingi za biashara.

BABU AJIUA KWA KUJINYONGA UGWETO SHINYANGA

 

Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Magesa Mahona anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 60 na 65 mkazi wa mtaa wa Ugweto manispaa ya Shinyanga amefariki dunia kwa kujinyonga katika nyumba yake majira ya usiku.

Mwili wa marehemu uligunduliwa na familia yake leo asubuhi Jumamosi Januari  8,2022 baada ya kukutwa ukining’inia. Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, ACP George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Thursday, January 6, 2022

Breaking : SPIKA JOB NDUGAI AJIUZULU

 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo ndani ya Bunge leo Alhamisi, Januri 6, 2022 kutokana na fukuto la kisiasa linaoendelea kufuatia kauli yake aliyoitoa kuhusu Rais Samia Suluhu kukopa Tsh trilioni 1.3. 

Ifuatayo ni barua yake ya kujiuzulu.

MBUNGE KENYA AFUKUZWA KWA KUGAWA PEREMENDE BUNGENI.

 




Mbunge wa Kenya siku ya Jumatano alifurushwa kikaoni kwa siku moja baada ya kupatikana akifawanya peremende kwa wenzake wakati mjadala ulipokuwa ukiendelea.


Fatuma Gedi alisema "viwango vya sukari vilikuwa vimeshuka" baada ya kushiriki kikao kirefu.


Alikuwa ametuhumiwa na mbunge mwenzake Ndindi Nyoro kwamba alikuwa akigawanya pesa ndani ya ukimbi wa bunge.


Bw Nyoro aliombwa kuthibitisha madai yake ya hongo na kuzuiliwa kuhudhuria vikao kwa siku mbili baada ya kukosa kufanya hivyo.


Bi Gedi alizuiliwa kuhudhuria kikao kimoja kwa kosa la kugawanya bungeni.


Wabunge waliidhinisha marekebisho kadhaa katika mswada wa vyama vya siasa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu


Tazama kilichotokea wakati wabunge walipotoa madai ya hongo:

LUSINDE AMTAKA SPIKA NDUGAI AJIUZULU LEO.

 

Mbunge wa Jimbo la Mvumi Mkoa wa Dodoma (CCM), Livingstone Lusinde amemtaka Spika wa Bunge Job Ndugai kujiuzulu kabla siku ya leo kuisha.


Akizungumza hii leo Januari 6, 2022 Lusinde amesema anamtaka Ndugai kuchukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kwa kupitia video nzima ya hotuba Spika Ndugai aliyoitoa hivi karibuni kwenye mkutano wa Wagogo wa Kikundi kinachofahamika kama Wanyausi.


“Napenda kusisitiza hilo na namtaka leoleo kabla ya siku kuisha awe amejiuzulu kwasababu haiwezekani mtu unaomba msamaha kwa kujitetea.. msamaha hauombwi hivyo kwa kuanza kukanusha kosa ilibidi aongee maneno machache tu” amesema


Lusinde amesema mikopo aliyoizungumzia Spika Ndugai anayokopa Rais hatumii na familia yake bali hutumika nchi nzima kwenye kuboresha miradi ya maendeleo.


Aidha amesema ikiwa itapita siku ya leo Spika atazidi kuweka msuguano usio na sababu kwakuwa vikao vya Kamati ya Bunge vinatarajia kuanza hivyo si vema kuanza vikao hivyo kukiwa na mgogoro.


“Na kwakuwa hajachukua hatua siku zote ndo maana nimemtaka leo mimi kama mdogo wake atoke na kuchukua hatua mapema kwakuwa vikao vya Bunge muda si mrefu vitaanza”amesema


Pia amesema kitendo cha Ndugai kujiuzulu ni kuwaletea heshima viongozi wa Mkoa wa Dodoma na itasaidia viongozi wa mkoa huo kutokuchukiwa na Rais.


Lusinde amesema kama Ndugai hatajiuzulu mpaka kesho Ijumaa, atakusanya wazee maarufu wa Mkoa wa Dodoma kwenda nyumbani kwake kumuomba ajiuzulu.

UJENZI BARABARA NJIA NNE KUANZIA MBEYA.

 


Msongamano wa  magari katika barabara kuu ya Tanzania na Zambia (Tanzam) umetafutiwa ufumbuzi kufuatia kuanza kwa utekelezaji wa ujenzi wa barabara za njia nne kutoka Igawa Wilayani Mbarali mpaka Mji wa Tunduma Mkoa wa Songwe.


Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Januari 6, 2021 Naibu Spika na Mbunge wa Jimbo la Mbeya, Dk Tulia Ackson amesema kuwa  kwa sasa tayari upembuzi yakinifu umeshafanywa kinachosubiria ni utekelezaji wa mradi wa barabara njia nne katika barabara kuu ya Tanzania na Zambia.


''Tayari fedha za mradi tumepata kwa ufadhili wa benki ya dunia na miundombinu hiyo ikikamilila itaondoa hadha ya msongamano wa magari na kuchochea shughuli za kiuchumi''amesema.


Dk Tulia amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imewekeza katika miradi mbalimbali ambapo katika Jiji hilo wameweza kuboresha miundombinu korofi ambapo baada ya kupokea Sh2 bilioni.


''Wakati mradi huo wa njia nne ukiwa unaanza utekelezaji na barabara za jiji zimeboreshwa katika maeneo ambayo yalikuwa yakisababisha msongamano wa magari kwa kuboresha barabara za michepuko ''amesema.


Dereva wa magari ya mizigo, Salim Ally amesema kuwa endapo Serikali ikaharakisha ujenzi wa miundombinu ya barabara nne itakuwa na mchango mkubwa katika shughuli za kiuchumi na kwamba msongamo wa magari umekuwa changamoto kubwa kwao.


'' Kwa sisi Madereva wa masafa marefu foleni kwetu ni changamoto kwani tunapaswa kuwahi Tunduma kupanga foleni kwa ajili ya kulipia vibali mbalimbali mpakani sasa unakuta kuna wakati tunatumia muda mwingi kukaa njiani'amesema.


Ameishauri Serikali kupitia Wizara husika kuharakisha mradi huo ili uweze kuleta tija kwao na taifa kwa ujumla kwani Sekta ya usafirishaji imekuwa na mchango mkubwa katika kuchangia pato la Taifa.

MBUNGE MSAMBATAVANGU : VIJANA TENGENEZENI VIKUNDI VYA KIUCHUMI

 


Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Jesca Msambatavangu amefanya mazungumzo binafsi na wajumbe wa baraza la vijana la wilaya ya Iringa Mjini chini ya Mwenyekiti wake Ndg Salvatory Ngerera

Katika mazungumzo hayo, Mbunge alijielekeza kuwaasa wajumbe wa baraza hilo kuchukua hatua za kuunda vikundi vya kiuchumi ili wawe sehemu ya kunufaika na fedha zinazotolewa na serikali ya chama chao.


 Mheshimiwa mbunge amechukua hatua hiyo baada ya kuona muitikio wa vijana katika kuunda vikundi hivyo ni mdogo sana, ili hali vikundi hivyo vinathibitika kuwa msaada wa kweli kwa vijana kujikwamua na kujiendeleza kiuchumi.


Mheshimiwa mbunge ametoa rai  kwa vijana hao kuwa ifakapo mwezi wa tano, atakapokuwa na ziara yake ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo, moja ya mambo ya msingi atakayoyafanya ni kivifuatilia vikundi hivyo vitakavyokuwa vimeundwa na atachukua hatua za kuvisaidia na kuviendeleza kwa jitihada zake binafsi.


Pamoja na mambo mengine, mheshimiwa mbunge pia alizungumzia shughuli zote za maendeleo zinazoendelea katika jimbo la Iringa Mjini na kuwataka wajumbe wa baraza hilo kuwa mabalozi wa mambo mazuri yanayofanywa nae pamoja na madiwani wote kwa kushirikiana na serikali ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Rais Samia Suluhu Hassan

Wednesday, January 5, 2022

DONDOO TANO (5) ZA KUJIKINGA NA UTI


 1: HAKIKISHA UNAKOJOA/JISAFISHE KILA BAADA YA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA

Utasaidia kuondoa bakteria na vijidudu vingine vya magonjwa ambavyo vinaweza kuwa viliingia kwenye mrija wa mkojo wakati unashiriki tendo la ndoa

2: JISAFISHE KUTOKA MBELE KWENDA NYUMA (Frontal to back wiping) kila baada ya haja kubwa na ndogo.Itasaidia kuzuia uingiaji wa bakteria ndani ya mrija wa mkojo kupitia uke.Utakuwa unajikinga pia na magonjwa hasa UTI ambao umekuwa ugonjwa sugu siku za hivi karibuni.

3: WAKATI WA HAJA NDOGO UNAPASWA KUWA UMETULIA (Relaxed),mara nyingi kujisaidia huku umesimama au umejikunja kwa namna yoyote ile hubana misuli ya kibofu cha mkojo hivyo kusababisha kiasi fulani cha mkojo kibaki ndani.Hii husababisha athari kwenye kibofu cha mkojo pamoja na magonjwa hasa UTI.Wakati wa haja ndogo,jitahidi uchuchumae au ukae (kama choo ni cha kukaa).

4: HAKIKISHA MKOJO WOTE UNAISHA

Pia hakikisha huutunzi mkojo kwa muda mrefu.Unapofanya hivi wadudu hasa bakteria huzaliana kwa wingi sana.Unajiweka kwenye hatari ya kuugua magonjwa mengi hasa UTI. 

5: Baada ya kufanya mambo haya,hakikisha unavaa NGUO ZA NDANI zilizotengenezwa kwa pamba 100% pia uvae nguo zilizokauka ambazo hazikubani sana.Husaidia hewa inayopatikana kwenye uke na kibofu cha mkojo iwe imekauka. 

Nguo mbichi,zinazobana pamoja na nguo za ndani zilizotengenezwa kwa nylon au material yoyote ambayo SIYO ya pamba hutunza hewa yenye unyevu.Hali hii huchochea uzalianaji wa wadudu hasa bakteria hivyo kukufanya uwe unaugua mara kwa mara magonjwa mbalimbali hasa UTI.