ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 8, 2022

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI AKAGUA MAENDELEO UJENZI WA MV MWANZA


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara ametembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Meli ya “MV Mwanza Hapa Kazi Tu” wenye gharama ya shilingi bilioni 89, ni mradi wa ujenzi ambao unatekelezwa na kampuni ya ujenzi ya GAS ENTEC wakishirikiana na KANG NAM kutoka Korea Kusini pamoja na SUMA JKT kutoka Tanzania.

MV Mwanza Hapa Kazi tu, itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200, mizigo tani 400, magari makubwa 3 na magari madogo 20, huku ikiwa na urefu wa mita 92 (sawa na pungufu kidogo ya ukubwa wa uwanja wa mpira wa miguu). Meli hii itakuwa mbadala wa meli ya MV Bukoba ambayo miaka 25 iliyopita ilizama na kupoteza maisha ya Watanzania wengi. Katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2015 Rais wa Awamu ya Tano, Hayati, Dkt John Pombe Magufuli aliwaahidi wananchi wa kanda ya ziwa kuwa atajenga meli kubwa kuwaenzi waliokufa kwenye ajali hiyo lakini pia kuimarisha usafirishaji upande huo wa Tanzania kwani kuna fursa nyingi za biashara.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.