Saturday, December 24, 2011
ELIMU
Eti viongozi wanatuhamasisha kuchangia elimu, huku wakikandia kuhusu jinsi tunavyochangia maharusi mamilioni... Ulikuwa Hujui sanaa imeanzia juu....!!
Chekshia hivi majuzi tumesheherekea miaka 50 ya UHURU kwa bilioni 4 safi sanaaa, wakati zingeenda kwenye madawati na ujenzi wa madarasa suala la wanafunzi kukaaa chini mashuleni lingekuwa ndoto. Lakini mmh tuna muda mrefu sana labda tukisheherekea tena miaka 200 ya uhuru kwa maumivu.
Tamasha kubwa la muziki wa Injili linalotambulika kwa jina la ‘Gospel Festival’, limepangwa kufanyika siku ya Boxing Day (Desemba 26/2011) kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Mwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa F&G Promotions, Fabian Fanuel, alisema kuwa, Tamasha hilo la msisimko na laaina yake litahusisha kwaya, bendi na waimbaji binafsi kutoka maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa na nje ya kanda ya ziwa.
Fanuel alizitaja baadhi ya Kwaya shiriki kuwa ni pamoja na Kwaya ya EAGT Msumbiji, Nyakato Moravian za Mwanza, Kwaya ya Mapambano kutoka Geita, AIC Ushirombo kutoka Ushirombo, Chipukizi ya Baptist Misungwi, T.A.G Vijana choir Geita, Ufunuo P.A.G choir, A.I.C Nyakato choir, Vijana Choir Nyakato, Tumaini Anglikan Igoma, Jerusalem choir, C.A.G Unguja, Imani Baptist choir Buhongwa, Revival Mission Band, Grace Wagana, Christina G. Vitta kuoka Kwimba, Tumaini KKKT Igoma choir, AIC Muungano choir, Mtakatifu Mkwasa RC choir Nyakato na Mwanza Gospel.
“Washiriki wengine ni Jerusalem Band na Glory Band zote kutoka Mwanza, pamoja na Kwaya nyingine kadha wa kadha kutoka katika madhehebu mbalimbali hapa Kanda ya Ziwa ambao watapewa tafu na waimbaji maarufu kama Tumsifu Rufutu aliyeimba 'Mwambie Farao', Danie Safari wote kutoka Dar es salaam” alisema Fanuel ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha radio Living Water FM, Mwanza.
Fanuel alisema kuwa Tamasha hilo litafanyika sambamba na uzinduzi wa Kampuni hiyo F&G Promotions iliyojikita zaidi kwenye uandaaji wa matamasha ya aina mbalimbali kama vile maigizo, vichekesho pamoja na muziki wa aina mbalimbali kama vile, Muziki wa Injili, Muziki wa kizazi kipya, na Muziki wa Dansi.
Aidha, Fanuel aliwaomba wakazi wote wa Kanda ya Ziwa kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia vipaji vya uimbaji kutoka ukanda wao, ambapo pia siku hiyo kampuni hiyo sambamba na kutambulisha wadau wake itatoa vyeti maalum kutambua mchango wa waimbaji, Redio mbalimbali pamoja na watumishi wa Mungu.
Tamasha la ‘Gospel Festival’ litakalokuwa likifanyika mara moja kwa mwaka, limelenga 'Kuamsha ari ya kiroho kwa watanzania kufanya kazi kwa imani na kutokata tamaa'
Thursday, December 22, 2011
HABARI
MH Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mizengo Pinda Akiongea kuhusu mchakato wa kutafuta katiba na Baraka Baraka kutoka Urban Pulse Creative.
Wednesday, December 21, 2011
AFYA
Wanasayansi wanasema mahitaji ya usingizi kwa watu yana uhusiano na jeni zao yaani genes. Usingizi
Wamegundua kuwa watu wenye aina ya jeni iitwayo ABCC9 wanahitaji takriban dakika thelathini za ziada za usingizi kila usiku kuliko wale wasiokuwa nayo. Utafiti uliofanywa ulilenga bara la Ulaya na kugundua kuwa humusi ya watu wana aina hiyo ya jeni.
Wanasayansi hao wa Ujerumani na Uingereza wamesema matokeo hayo ni muhimu kwasababu ukosefu wa usingizi unahusishwa na matatizo mengi ya kiafya, kama vile maradhi ya unene na moyo.
Viongozi wa kisiasa, kuanzia mtawala wa zamani wa Ufaransa Napoleon hadi aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Margaret Thatcher walikuwa na sifa ya kuweza kufanya kazi zao bila matatizo licha ya kulala muda wa saa nne au tano tu kila usiku.
Lakini kwa wengine akiwemo mwanafizikia Albert Einstein hata muda wa saa 10 wa usingizi haukumtosha.
Sasa wanasayansi wanasema tofauti hizi katika mahitaji yetu ya usingizi yanaweza kuelezeka kwa kutazama muundo wa jeni zetu.
Walichambua chembe chembe za asidi nasaba DNA kutoka watu 10,000 kote barani Ulaya- na kuzilinganisha na mitindo yao ya kulala.
Walifikia kauli kwamba watu walio na aina ya jeni iitwayo ABCC9 wanahitaji muda wa nusu saa zaidi usingizini ikilinganishwa na wale wasio na aina hiyo ya jeni. Mtu mmoja kati ya kila watu watano barani Ulaya wanaaminika kuwa na jeni hiyo ya usingizi mwingi.
'STOP' Hakuna njia.
Akijilaza tu.. Twafa!
Picha kwa hisani ya PGS ISAAC
nI kWa mARa yA kWANzA mWANZA kUPENdEzA USIKOSE!!!!
Tuesday, December 20, 2011
ELIMU
Hivi Serikali imelala usingizi gani huo mzito hadi wamiliki wa vituo vya mafuta wanapata kiburi kugoma kutoa huduma hiyo?
Kwa migomo kama hii ya mara kwa mara inawezekana Serikali yetu Tz imewekwa mfukoni na Atajiri wachache wa Mafuta?....!!!
Rais Jakaya Halfani Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda mbona hatuoni makali yenu? Ngeleja Upo wapi hadi uji wa mgonjwa unamwagiwa mchanga…..?!!!!...!!!
TAFAKARI CHUKUWA HATUA KABLA KENGELE HAIJA LIA….Konng….kONNg’’’!!!!!