ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 21, 2011

MVUA DAR ZALETA MAAFA NA KUUA SITA!

JIJI la Dar es Salaam na vitongaji vyake, limekumbwa na maafa ya vifo vya watu sita mpaka sasa akiwamo mmoja aliyepigwa na radi, uharibifu wa miundombinu huku mamia ya watu wakikosa makazi, kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia jana.Wakazi wa eneo la Tandale wakitaabika.
Mvua hizo zilisababisha tatizo kubwa la usafiri kutokana na barabara kujaa maji, kuezua nyumba na kuua watu sita na kuacha maelfu ya wakazi wa jiji hilo bila makazi baada ya nyumba zao kuezuliwa mapaa.

Mvua ilianza kunyesha mnamo saa 9:00 alfajiri ikiambatana na radi na ngurumo nzito na kusababisha kukatika mara kwa mara kwa umeme katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaal.

Nyumba zikiwa zimezingirwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam jana.

Mmoja ya wakazi akipima maji ili kuona uwezekano wa kwenda kuwasaidia watu waliozingirwa na maji.

Baadhi ya wakazi wakiwa sintofahamu baada ya kushuhudia mafuriko yaliochokuwa maisha ya wapendwa watatu.

Baadhi ya waokoaji wakiwa na vifaa vya kazi tayari kuokoa maisha ya wakazi wa mabondeni.
Picha na Michuzi JR.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.