ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 23, 2014

WAZIRI MKUU PINDA ATEMBELEA UJENZI WA UPANUZI WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWANZA LEO

Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda (katikati), Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Charles Tizeba (kulia mbele), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Dkt Anthon Dialo (kulia kwa Pinda) wakiwa tayari wamevalia vifaa tayari kutembelea eneo la mradi wa ujenzi wa jengo la kuongozea ndege lililopo kilimani jirani na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwanza.
Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda (wa pili kushoto), Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Charles Tizeba (wapili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Dkt Anthon Dialo (katikati), Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Amina Masenza, wakati Pinda wakieleza jambo wakati alipotembelea eneo la mradi wa ujenzi wa jengo la kuongozea ndege lililopo kilimani jirani na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwanza.
Watu wa Kazi za ujenzi wa jengo hilo.
Kutoka kilimani.
Mwonekano wa uwanja wa ndege wa Mwanza.
Ndege ya Air Tanzania ikituwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwanza
Waziri Mkuu Pinda akipata maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Wizara wa Uchukuzi Dk Tibeza kilimani lilipo jengo la kuongozea ndege alipotembelea leo jijini Mwanza wengine ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Dkt Anthon Dialo (wa tatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto mbele) wakiangalia uwanja wa ndege ambao kwa sasa uko kwenye upanuzi. 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilemela Zuberi Mbyana akiwa na Mkandarasi mshauri raia wa Zimbabwe.
Shehena ya changalawe zikiwa zikisubiria kuwekwa kwenye Mtambo wa kisasa kabisa wa kuchanganyia lami ya uwanja wa ndege wa Mwanza.
Mtambo wa kisasa wa kuchanganyia lami 
Waziri Mkuu Pinda akipata maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Wizara wa Uchukuzi Dk Tibeza wakiangalia mtambo wa kisasa jana jijini Mwanza wengine ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Dkt Anthon Dialo (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto mbele) na kulia ni Mkandarasi wa ujenzi wa uwanja akitoa maelezo.
ulinzi umeimalishwa eneo alilotembela Waziri Mkuu Pinda.
Waziri Mkuu Pinda akipata maelezo ya Mkandarasi kwenye eneo linaloongezwa la urefu wa mita 400 la kurukia ndege kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwanza jana
Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa ujenzi wa uwanja wa ndege na viongozi wengine.

KIKONGWE WA MIAKA 76 AAMUA KUJITENGENEZEA JENEZA LAKE MWENYEWE KWA SABABU YA UGUMU WA MAISHA.

Bi Scholastika Mhagama akiwa katika mlango wa nyumba yake.
 ---------------------
Na Oswald Ngonyani wa demashonews - Peramiho.
Wahenga walisema Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni;Jamii inazidi kujawa na chuki na ukatili ndani yake, imekuwa kawaida siku hizi kusikia fulani kamuua fulani kwa kisa kisichokuwa na maana.

Maalbino wanakatwa viungo vyao kwa visingizio vya kupata utajiri kwa watu wasiokuwa na huruma, watoto wadogo wananyimwa haki zao na kuwekwa ndani ya maboksi na wengine kuishi maisha yao katika uvungu za kitanda yote haya ni mambo ya kutisha yanayotendeka katika jamii zetu.

Hali imekuwa tete amani na upendo vinazidi kuyeyuka kama barafu, watu hawana utu tena, wamejivika ngozi za kondoo wakati mioyo yao ni ya Simba, hakuna tena roho ya huruma kwa wanadamu wa dunia ya leo.
Choo cha bibi Scholastika Mhagama
Wakati haya yote yanaendelea kutendeka katika jamii zetu ni kama vile tunazidi kuugeuza ulimwengu tunaoishi kuwa ‘Uwanja wa dhambi’ ulimwengu wa kutojaliana  tena, wanadamu wamebadilika na kuwa kama wanyama na tena hata zaidi ya mnyama.

Katika hali isiyo ya kawaida Bibi mmoja ambaye ni mlemavu wa miguu na mzee sana anayeishi peke yake katika kibanda ambacho kwake ni kama gereza ambalo hataweza kutoka tena maisha yake yote, amejikuta akifanya kitu kisicho cha kawaida kwa binadamu wa kawaida.
Jeneza la bibi likitolewa ndani kwake na wanachama wa Kombination Camp.
Namzungumzia Bibi Scholastica Mhagama mwenye umri unaokadiriwa kufikia (76), ambaye ni mlemavu wa miguu anayejongea kwa kutambaa ambaye anaishi peke yake katika kibanda chake katika kijiji cha Lundusi mtaa wa Linga huko Peramiho Songea mkoani Ruvuma. Ni jambo la kusikitisha sana kwa bi kizee kama huyu kuishi peke yake akiwa hana msaada wa kueleweka kutoka kwa jamii inayomzunguka.

Bibi huyu anayeishi kwa uchungu na majonzi amekata tamaa kabisa ya maisha hali iliyomfanya aamue kuchonga jeneza lake mwenyewe akijiandaa kufa siku yoyote.Bibi huyu anaishi na jeneza hilo chumbani kwake.

“Maisha yangu ni magumu sana, naishi kama mnyama, sipendwi na ndugu zangu wala na jamii inayonizunguka. Wamenichoka sina raha natamani hata Mungu anichukue sasa hivi ili nikapumzike, nasali kwa sala zote natubu na kujuta kila siku lakini wala Mungu hanichukui, sijui kwanini” Anasema Bi Scholastica Mhagama kwa uchungu.
 Jeneza la Bi Scholastika Mhagama

Akielezea historia ya maisha yake Bi Scholastika anasema alizaliwa akiwa na miguu yote lakini alipata bahati mbaya ya kugongwa na nyoka alipokuwa darasa la pili hali iliyomfanya kukatwa mguu ili kuepusha madhara mengine kama vile kifo. Hivyo maisha yake yalibadilika na tangu hapo akawa mlemavu.

 Hali hiyo ya ulemavu lakini pia uzee alionao vimemfanya ashindwe kujihudumia kwa lolote zaidi ya kupika tu. Hata hivyo anakosa mahitaji muhimu kama vile maji na chakula hali inayomfanya alale na njaa kwa baadhi ya siku.

Kwa hali aliyo nayo ni wazi kuwa Bi Scholastika anahitaji baiskeli ya miguu mitatu (wheel chair) ambaye itamwezesha  kutembea  kwa kuwa hivi sasa anatambaa na kupata maumivu makali kutokana na nyama iliyobakia kwenye nyonga baada ya kukatwa mguu.

Bi Scholastika anazidi kueleza kuwa kuna watu waliwahi kufika kumuandikisha jina lake na kumuingiza katika orodha ya watu wanaostahili kupata msaada lakini anasikia misaada inafika kwa jina lake lakini yeye mwenyewe hajawahi kuipata.

Vipi kuhusu Sera ya Wazee?
Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 inaweka bayana kuwa suala la uzee na kuzeeka limekuwa lenye umuhimu mkubwa ambapo karne ya ishirini imeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya wazee.

Kwa kurejelea takwimu zilizopo ni kwamba, ifikapo mwaka 2050 idadi ya wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 nchini hapa itaongezeka na kufikia wazee milioni 8.3 (Sawa na asilimia 10 ya watanzania wote)

Kama hiyo haitoshi, Taarifa ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 1999 inaeleza kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wazee duniani na kwamba ongezeko hilo linaonekana zaidi katika nchi zinazoendelea (Tanzania ikiwepo) ambapo viwango vya ongezeko hilo havilingani na uwezo wa rasilimali zilizopo za kuwahudumia.

Rasilimali hizo zinajikita zaidi katika Nyanja za msingi katika makuzi ya binadamu yoyote zikiwemo Nyanja za afya, lishe na huduma nyingine za msingi zisizoweza kuepukwa na binadamu yeyote.

HAPPY BIRTHDAY MWANALIBENEKE MC BARAKA


Namshukru mwenyezi mungu kunifikisha siku hii ya leo Jumamosi Aug 23 nikiwa naadhimisha siku ya kuzaliwa kwangu
Namshukuru Mungu kwa kunipa nguvu na ujasili wa kupambana na misukosuko ya hapa na pale hakika yeye ndiye muweza wa kila jambo mpaka mie kufika hapa nilipo.
Natoa shukrani kubwa kwa wadau,ndugu na marafiki pamoja na wanalibeneke wanao endelea kuniunga mkono.
HAPPY BIRTHDAY TO ME!


G SENGO BLOG INAUNGANA NAWE KATIKA SIKU HII MUHIMU KWAKO MWANALIBENEKE IKIKUTAKIA HERI, FANAKA NA BARAKA ZOTE. MUNGU AKUPE NGUVU NA AZIDI KUKUBARIKI.

MASAI SAFARI BENDI KUZINDUA ALBUM AUGUST 30

Na Mwandishi Wetu
 BENDI ya Masai Safari ya jijini Dar es salaam inatarajia kuzindua albam yake ya kwanza kabisa watakayozindua siku ya August 30 katika ukumbi wa raunch time ya jijini akizungumzia uzinduzi wa albam hiyo rais wa bendi hiyo Fransic Mwaisela amesema kwamba siku hiyo watasindikizwa na bendi mbalimbali wakiongozwa na bendi ya Extra bongo inayo ongozwa na Ali Choki

Alizitaja nyimbo zilizomo katika albam hiyo ni sita itakayozinduliwa siku hiyo ikiwa nyimbo ambayo iliyobeba albam ni akuna kama baba ya pili ni njia panda,mikono ni kazi,ndoa ni mpango wa mungu,usiwasikilize wambeya,kilio changu nyimbo hizo ndio zitakazokuwa katika albam hiyo itakayo zinduliwa mwishoni mwa mwezi huu

Aliongeza kwa kutaja wasanii wengine watakaokuwepo siku hiyo ni Omari Tego,Maua Tego pamoja na wasanii mbalimbali wa bondo flefa watakaosindikiza uzinduzi uho

Bendi hiyo kwa sasa ipo kwenye mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kutoa burudani kabambe siku ya uzinduzi wa albam ya bendi hiyo