ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Showing posts with label KUMBUKUMBU. Show all posts
Showing posts with label KUMBUKUMBU. Show all posts

Monday, October 14, 2019

KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA MWALIMU JK NYERERE MKOANI LINDI.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli anahudhuria maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na Wiki ya Vijana Kitaifa katika Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi

Sunday, June 16, 2019

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA NI MIAKA 43 SASA MACHOZI YASIYOFUTIKA KWA WANA WA AFRIKA KUSINI.

Safari ya Mwaka 2016 ya Mwanahabari/Blogger kutoka Jembe Fm Gsengo ilimfikisha hapa mbele ya kaburi la kijana Hector Pietersen.
Afrika Kusini inaadhimisha miaka 43 sasa tangu maandamano ya wanafunzi wa Soweto, walipopinga ubaguzi wa rangi katika elimu kwa kulazimishwa kusomeshwa kwa lugha ya Ki-Afrikaan.
Afrikaans ni lugha inayotumika huko Magharibi mwa Ujerumani na kabila dogo la nchi hiyo na ilitambulishwa hapa Afrika na makaburu kwa makusudi ya kuwachanganya waafrika wakibaki kuwa watumwa ikasambaa sehemu za Afrika ya kusini na Namibia.

Lugha hiyo haikuwa na msaada kwa wahitimu zaidi ya kuwachanganya pindi wanapo hitaji kwenda kwenye masomo ya juu au pindi wanapo ajiriwa wakashindwa kupenya kwenye nafasi za juu za uongozi na kubakia kuwa watumwa.

Mamia ya wanafunzi walifariki katika vurugu zilizojiri wakati serikali ya ukoloni ya wazungu makaburu ilipotumia nguvu kupita kiasi, kujaribu kuzima maandamano hayo.
Maandamano hayo yalikuwa kama mwanzo wa kuelekea hatua za kumalizwa kwa utawala wa makaburu wa Afrika Kusini.
Luis ni mwelekezi anayejitolea kwa watalii wanaodhuru eneo hili la kaburi la Hector Pieterson anasimuliwa kilichotokea. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA 
(SAUTI ITAWAJIA HIVI PUNDE)
Ujumbe aliouandika mama wa kijana aliyebeba mwili wa kijana Hector Pieterson katika harakati za kumuokoa baada ya kupigwa risasi na polisi. Ujumbe unasomeka "Mbuyisa ni au alikuwa kijana wangu (kwa sababu alitoweka baada ya tukio hilo na hajulikani aliko mpaka sasa) akiendelea kusema ...... "Lakini si Shujaa. Kwenye utamaduni wetu kumbeba Hector siyo tukio la kishujaa, lilikuwa ni jukumu lake kama kaka. Kama angemuacha pale chini na mtu mwingine angemshuhudia akiuruka au kuukanyaga mwili wa marehemu Hector, asingestahili kuishi hapa"  ujumbe wa Ma'Makhubu.
Kila kilichopo hapa kina maana yake:-  Ukuta wa mawe yaliyopangwa ukimaanisha umoja wa watoto walioungana kwenye maandamano hayo kupinga ubaguzi, maji yanayotiririka yanaashiria machozi ya huzuni yaliyomwagika siku ya tukio toka kwa wazazi, watoto na taifa kwa ujumla, urefu unaopishana wa mawe unamaanisha umri wa watoto waliouawa, mianya katikati ya mawe inamaanisha taarifa zilizo potea au kufichwa hadi leo na kubaki bila ufafanuzi kama nani aliyemuua Pieterson na kadhalika, sakafu nyekundu ni damu iliyo mwagika, mawe ndani ya maji yanaashiria silaha pekee walizotumia watoto kujilinda dhidi ya polisi siku ya tukio.
Gsengo mbele ya picha ya mwili wa kijana Hector Pieterson uliobebwa na mwanafunzi mwenzake aitwaye Mbuyisa baada ya kupigwa risasi na polisi. Hii ndiyo picha iliyoibua hamasa na hasira kubwa na kuufanya ulimwengu kulaani ukatili uliokuwa ukiendelezwa na utawala wa makaburu enzi za ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
a

Marehemu Hector Pieterson alizaliwa mnamo mwaka 1963 na June 1976 alikuwa ni mmoja kati ya mamia ya watoto waliouawa naye amewekwa kwenye historia kwani ni mmoja ya vijana wadogo waliouawa na makaburu na risasi ya kwanza ilimuua kijana huyo  akiwa na umri mdogo miaka 12 tu.
Pichani juu mwili wake ukiwa umebebwa na mwanafunzi mwenzake aitwaye Mbuyisa Makhubu baada ya kupigwa risasi huku dada yake akiwa naye anakimbia jirani kutafuta msaada.
Maji haya yanayotiririka mbele ya kaburi la Hector Pieterson yanaashiria machozi ya wazazi watoto na taifa juu ya tukio hilo la mauaji ya mamia ya watoto lililotokea mnamo tarehe 16 June 1976.

Jiwe hili lilitumika ngao kujikinga na risasi za mitutu ya bunduki za polisi kwenye maandamano ya watoto mnamo mwaka 1976.

a

Barabara hii ndiyo iliyo tumika kwa maandamano ya mwaka 1976 ikiwa ndiyo kiunganishi cha maeneo ya mji wa Soweto nchini Afrika Kusini.



Pembeni hatua chache kutoka eneo lilipo kaburi kuna Jumba hili la makumbusho la Hector Peterson, Humo ndani kunavielelezo vyote vya yale yaliyotokea kwa njia ya picha, video na baadhi ya mabaki ya nguo, silaha na baadhi ya nyezo walizotumia watoto hao kujikinga wakati wa vurugu zilizotokea zilizotumika kwenye tukio hilo lenye kumbukumbu yenye simanzi.


The Hector Pieterson Museum is a large museum located in Orlando West, Soweto, South Africa, two blocks away from where Hector Pieterson was shot and killed. Jumba hili lilipewa jina la marehemu kijana huyo kama heshima kwake.

Thursday, April 19, 2018

HISTORIA ISIYOFUTIKA WORLD CUP DHIDI YA SOKA LA DRC (ZAIRE)


 Uhuni haukuanza leo upo tangu enzi za wajomba, tena kipindi hicho kulikuwa na wababe kweli #UndavaUndava na uzinguaji #Gangwe Best time wasting tactic?
#SportsRipoti .
.
.
Timu ya Taifa ya Demokrasia ya Kongo (DRC) iliyokuwa Zaire zamani kwa mara ya kwanza ilijitokeza katika fainali za Kombe la Dunia mnamo mwaka  1974 ikiijulikana Zaire.

Vilevile ilikuwa ni timu wa kwanza kutoka ukanda wa Sahara barani Afrika kushiriki fainali za michuano ya Kombe la Dunia.
.

Pamoja na kusukuma kandanda safi na la kuvutia dhidi ya  Scotland na Brazil, timu hiyo katika michezo mitatu tu ya fainali hizo walikung'utwa jumla ya magoli 0-14. .

Way back Thursday #WBT aka #TBT

PIA CHEKI VIDEO YA CHINI ILIYOIGIZA TUKIO LA HASIRA KATIKA FREE KIK

Wednesday, April 11, 2018

HUYU NDIYE #EDWARD_MORINGE_SOKOINE SHUJAA WA WANYONGE MZALENDO WA TANGANYIKA, ADUI WA WAHUJUMU UCHUMI NA WATENDAJI WAZEMBE Tangu 1/8/1938 -12/4/1984

HUYU NDIYE #EDWARD_MORINGE_SOKOINE SHUJAA WA WANYONGE MZALENDO WA TANGANYIKA, ADUI WA WAHUJUMU UCHUMI NA WATENDAJI WAZEMBE Tangu 1/8/1938 -12/4/1984
.
. "Ole wao wale wanaotumia nafasi zao za umma na serikali, kuiba, kuhujumu uchumi, kupokea rushwa, maana salama yao ni kudra za Mwenyezi Mungu labda nisiwajue"

Hayo ni maneno aliyowahi kuyatamka hayati kaka na mzalendo wa taifa hili shujaa Moringe Sokoine, wakati akilihutubia kwenye mkutano kikao cha NEC mjini Dodoma 12/04/1984, wakati huo vita ya kupambana na suala la uzembe makazini, ulangunguzi, rushwa na biashara ya magendo, enzi hizo taifa lilikuwa la moto kila sehemu ilikuwa moto, mpaka #WALANGUZI wakamchukia...... lakini mpaka leo kauli yake inaishi, inatumika, inaamsha hali ya uzalendo na maadili ya taifa hasa wakati huu ambapo wanasiasa na serikali kwa ujumla wanaishi kinyume na misingi mikuu ya taifa hili, misingi mikuu ya chama chao na msingi mkuu wa uwajibikaji wa serikali, ingawa Rais #JPM kanyoosha watu si mchezo.
.
.
Leo  tunakumbuka, kifo cha mpendwa wetu huyo kwa yale mazuri aliyoifanyia Tanganyika kwa ujumla wake, lakini pindi tunakumbuka kumbukumbu hii tujiulize je? Je viongozi wetu wanaishi kimatendo kama hayati  Sokoine? 
.
#Tafakari @jembefm

Saturday, April 7, 2018

JEMBE FM, METDO NA WADAU WAKE WAMUENZI KARUME KWA KUTEMBELEA NA KUTOA CHAKULA KWA KITUO CHA KULEA WAZEE BUKUMBI.

Leo ni Tarehe 7 April 2018, tunaadhimisha Kumbukumbu ya Kifo Cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar Abeid Aman Karume @Jembefm 93.7 kupitia kipindi chake cha muziki wa Injili yaani #JembeGospel kwa Kushirikiana na wanamuziki wa muziki huo, Wachungaji wa makanisa kadhaa ya Kipentekoste pamoja na METDO, wameitumia siku hii muhimu ya #KarumeDay kwa kuwatembelea ndugu zetu wa kituo cha Wazee wasiojiweza kilichopo Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza na kutoa mahitaji mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 'First Lady' Mama Janeth Magufuli.

Vilevile kuipa thamani Kazi ya utumishi uliotukuka na Kuuenzi Upendo na Msisitizo wa Mshikamano aliokuwa nao Hayati Mzee Karume.

Mshikamano ulipo baina ya Tanzania na Zanzibar umeendelea kudumu sasa yapata miaka 46. 

Ni takribani miaka miwili sasa imepita tangu Mama Janeth Magufuli alipodhuru kwenye kituo hicho (mwezi March 7 mwaka 2016) ambapo aliteuliwa rasmi kuwa Mama Mlezi Mkuu wa Kituo hicho  baada ya kuhamasisha mashirika mbalimbali, watu binafsi na taasisi za kifedha kutoa michango ya vitu mbalimbali vilivyofikia thamani ya shilingi milioni 54 na kukiwezesha kituo hicho kwa chakula, malazi na mavazi.

Hivyo mpango huu umekuja kama sehemu ya kuitikia wito wa Fist lady. 

CC:- #JembeGospel @nzwallajr @gsengo @jembenijembe







PICHA ZAIDI ZAJA.................

Wednesday, March 29, 2017

MIAKA 11 TANGU FATHER NELLY AFARIKI: JCB AKUMBUSHIA KIFO KILIVYOKUWA NA PENGOLAKE KWENYE HIP HOP.


African song: X Plastaz - Ushanta (Maasai hip hop) 

 @Regrann from @bongofive - Miaka 11 tangu Father Nelly afariki: JCB akumbushia kifo cha kilivyokuwa na pengo lake kwenye hip hop ________________________________________ Leo ni miaka 11 tangu kifo cha rapper wa kundi la Xplastaz, Father Nelly. Rapper huyo alifariki baada ya kuchomwa kisu March 29, 2006 jijini Arusha. 

Jumatano hii, nimezungumza na rapper @JCBWatengwa aliyekuwa rafiki yake wa karibu ambaye anatukumbusha jinsi kifo cha Nelly kilivyotokea.

 “Mahali anapokaa kulikuwa na ugomvi kati ya jirani yake na rafiki yake sasa akaenda kama kuingilia kwamba ‘ebana inakuaje’ basi yule jamaa ambaye ndiye muuaji akamuambia Father Nelly ‘na wewe unataka sio’ akamchoma visu vingi sana pale pale bana. 

Kumchoma visu jamaa akakimbia watu wakamkimbiza Father Nelly Mount Meru hospitali akakaa siku ya kwanza, siku ya pili ndio siku kama ya leo akafariki kwa maumivu makali sana,” amekumbushia JCB. 

JCB amesema Father Nelly ni mmoja wa watu walioanza kurap mapema zaidi huko Arusha kuanzia mwaka 1992/93 akiwa na umri mdogo kabisa. 

“Watu wa Arusha watakuwa wanammiss sana sababu wao [Xplastaz] ndio walikuwa wa kwanza kuipeleka game ya Arusha Dar es Salaam huko, kuipeleka nje ya Tanzania. Nadhani Xplastaz na Mr 2 ndio waliweza kuwa watu wa kwanza kwenda kurap nje ya Tanzania,” anasema JCB. 

 JCB anasema Arusha haitokuja kumsahau rapper huyo na kwamba miaka ya nyuma siku kama ya leo kulikuwepo na desturi ya kufanya kongamano la kumkumbuka, kitu ambacho kimepotea kwa sasa. 

JCB aliwahi kuandika wimbo maalum wa kumkumbuka rapper huyo pamoja na watu wengine waliotangulia mbele ya haki.

Friday, October 14, 2016

MAMBO YA ZIADA AMBAYO HUKUWAHI KUDHANI JUU YA MWL. JULIUS KAMBARAGE NYERERE.


Hivi unajua pale Butiama chakula cha mwisho alichovuna Mwl. Jk. Nyerere enzi za uhai wake bado kipo hadi sasa (miaka 17) na kimebaki kama kumbukumbu..............!? 


Jeh hivi unajua pamoja na baba wa Taifa kumiliki gari hakuwahi wala hakuthubutu kujifunza kuendesha gari....................................................................................................!?


Basi kijana aliyekuwa chipukizi wa mwisho kumvisha scarf kwenye mapokezi wilayani Bunda Enzi za utawala wake baada ya kung'atuka na kubakia kama Mwenyekiti wa CCM kijana Lawrenti Alphonce maarufu Jicho' atakwenda kusimulia mengi ikiwa ni pamoja na story ya....................................................................................


@prince_arn @mansourjumanne @gsengo #Mchepuko na mikito mikali ya djscopion #NyerereDAyDriveMIXspecial


BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

ZITTO: NYERERE WANGU ALIKUWA HIVI

Mwaka 1984 nilianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kigoma, katika mji wa Kigoma. Nakumbuka kupelekwa Shule siku ya kwanza na mama yangu mzazi Bi Shida Salum (Mungu amrehemu) nikiwa sina viatu yaani pekupeku wala begi la mkononi, nilikuwa nimebeba mfuko wa nailoni. Nakumbuka usiku wa kuamkia siku ya kwanza kwenda shule, sikulala kwa furaha na hamu ya kuwa msomi, nilijisikia fahari kuanza shule japokuwa sikuwa na kitu chochote cha zaida zaidi ya kaptula ya shule na shati liloshonwa kwa kitambaa cha sanda. Pia nilianza shule nikiwa nimechelewa kwa mwaka mmoja maana wenzangu walianza wakiwa na miaka 7. Mwaka 1983 nilipopelekwa shule mkono wangu haukuweza kushika sikio upande wa pili, ambacho kilikuwa kipimo cha kuandikishwa darasa la kwanza.
Hali ya maisha wakati huo ilikuwa mbaya sana. Nakumbuka kwenda shuleni nikiwa sina kitu tumboni au siku nzima nilikunywa uji usio na sukari. Uji wenyewe ulikuwa ni wa unga wa njano uliotokana na mahindi ya njano ambayo tuliambiwa nchi yetu ililetewa kama msaada kutoka nchini marekani.
Shule yetu kama zilivyokuwa shule nyingi za wakati huo hatukuwa na madawati ya kutosha na vyumba vya madarasa vilikuwa vichache sana. Ilikuwa ni kawaida kwa wadogo (darasa la kwanza mpaka la tatu) kusomea chini ya mwembe na kukaa juu ya matofali. Hali hiyo ilipelekea kaptura yangu ya shule kuwekwa viraka vingi maana ilikuwa inachanika mara kwa mara. Nyakati nyingine ilibidi kwenda shuleni na shati likiwa halijakauka hasa siku za alhamis, siku ya usafi na iwapo nikiwa zamu ya mchana kwani nilikuwa nina shati moja tu tena lililotokana na kitambaa cha sanda.

Kwa dhahiri, watoto wa masikini na matajiri tulikuwa shule moja, darasa moja hata wote kukaa kwenye matofali. Watoto watawala na watawaliwa tulicheza mpira pamoja, kuruka dana na hata kuruka kamba. Hatukujisikia wanyonge kwa sababu hatuna viatu au kuvaa kaptura zenye viraka na mashati ya sanda. Kamwe sikumbuki kudharauliwa shuleni sababu ya uduni wa maisha yangu. Heshima ilitokana na uwezo wako darasani na kupitia hilo nilipata marafiki wa kutoka madaraja yote ya maisha. Nakumbuka mtoto wa Mkurugenzi wa Maendeleo Mkoa wa Kigoma ndugu Daniel Masanja ndiye alikuwa rafiki yangu wa karibu na kwa kuwa sikuwa na hata pesa ya kununua bajia wakati wa mapumziko, yeye alikuwa ananinunulia.

Huko baadaye, ada yangu ya kidato cha kwanza ililipwa na Mzee Sebastian Kasomi ambaye mwanaye Kasomi Mabula alikuwa rafiki yangu mkubwa mara alipohamia shuleni kwetu akitokea mjini Shinyanga. Mzee Kasomi alikuwa Mkuu wa idara ya Kodi ya Mapato mkoani Kigoma.

Licha ya uduni wa maisha watoto wengi tuliishi kwa matumaini makubwa sana. Mwalimu wetu Mkuu ndg. Daniel Andulile alikuwa mkali sana kwa watoto wote bila kujali daraja la maisha la wazazi wao. Alikuwa anatucharaza viboko kwa makosa na utundu bila ubaguzi. Alisisitiza sana kusoma kwa bidii ili kujenga Taifa. Dhana hii ya kujenga Taifa iliingizwa kwenye akili zetu na sisi kumeza bila kujali maana yake. Wakati mwingine tulikuwa tunarudi nyumbani huku tukijadili kitoto kuwa tunajenga Taifa. Kila siku mwendo wa kilometa Sita kwenda na kurudi shuleni.

Elimu hii isiyo ya kibaguzi sasa najua ilitokana na sera za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Jitihada zangu darasani ndio ziilikuwa kipimo cha utu wangu na sio uwezo wa kiuchumi wa wazazi wangu.. Elimu iliyompa fursa sawa za kuendelea na kusonga mbele mtoto aliyekuwa kigoma, kantalamba au Dar es salaam. Elimu iliyokuza ndoto, kuinua ari na kujenga matumaini ya kila mtoto wa kitanzania. Elimu iliyovunja na kusambaratisha matabaka ya kiuchumi na dhamana. Elimu iliyojenga uzalendo na hamasa ya kutumikia taifa letu kwa misingi ya haki, uadilifu na upendo.

Sikuwahi kukutana na Mwalimu Nyerere isipokuwa niliwahi kumwona akiwa ndani ya gari nikiwa nimepanga mstari barabarani alipofanya ziara mkoani kwetu mwaka 1987 nikiwa darasa la nne. Lakini nilikuwa kama ninaishi naye kutokana na namna nilivyotaka kuwa kama yeye. Nikiwa darasa la pili nakumbuka katika mkebe wangu ( mathematical set) mkuu kuu niliweka picha ya kukatwa kutoka kwenye gazeti ya Mwalimu na Kawawa. Na nilijisikia fahari kuwa na picha zao, mara zote nilipokuwa nafungua mkebe kutoa kalamu nilijisemea kimoyomoyo, “siku moja nitakuwa kama wewe”

Licha ya maisha magumu tuliyokuwa tunaishi, maisha ya kupanga mawe kwenye mstari wa kununua mahitaji muhimu kama sukari, sabuni na mafuta kutoka duka la ushirika, maisha ya kushindia uji wa yanga na kutembea mwendo mrefu kwenda shuleni, niliishi kwa imani kubwa kuwa mimi na watoto wengine tupo sawa. Usawa katika kupata elimu, usawa katika kucheza na usawa katika ndoto na matumaini. Nimemaliza elimu ya Chuo Kikuu, ndoto niliyoruhusiwa kuwa nayo kwa sababu ya sera za Ujamaa, za Mwalimu Nyerere.

Ujamaa haukuwa katika usawa wa elimu tu ambapo kila mtoto alipata elimu bure na bora katika Shule za umma bila ubaguzi bali pia namna jamii iliishi. Mtoto alikuwa analelewa na jamii nzima. Ukifanya makosa mtaani mzazi yeyote anakuadhibu ili kukurekebisha. Ukifanya jambo jema, mzazi yeyote anakupongeza.

Mwaka 1985 mwezi Novemba nilipokuwa natoka shuleni, karibia na Benki ya Taifa ya Biashara Tawi la Obed Katikaza, nilikutana na Mama Colleta Furugunya tuliyekuwa tunaishi mtaa mmoja na nikimwita bibi Colleta. Aliponiuliza matokeo yangu ya mtihani wa kumaliza muhula wa pili wa darasa la pili kwa kujiamini nikampa karatasi yangu ya matokeo. Nilikuwa nimeshika nafasi ya tatu darasani nyuma ya Ramadhan Kalukula na Haki Manyaga. Bibi Colleta alinishika mkono mpaka duka la Viatu, Bora Shoes na kuninunulia jozi yangu ya kwanza ya viatu. Viatu vile viliitwa Asante Salim, aliyekuwa Waziri Mkuu wa mwisho wa Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa anajaribu kubadili hali mbaya iliyokuwepo. Hivyo ndivyo nilivyopata viatu vyangu vya kwanza vya shule. Shukrani kwa sera nzuri ya ujamaa, mshikamano na upendo.

Wednesday, May 20, 2015

MISA YA KUWAOMBEA WALIOPOTEZA MAISHA AJALI YA MV BUKOBA KUFANYIKA KESHO KATIKA KANISA LA RC NYAKAHOJA MWANZA

MISA ya kuwaombea watu waliopoteza maisha katika ajali ya meli ya Mv Bukoba iliyotokea mnamo tarehe 21 Mei 1996 na kuua mamia ya watu na mali zao inatarajiwa kufanyika kesho alhamisi ya tarehe 21 Mei 2015 katika kanisa la Mtakatifu Francis Nyakahoja jijini Mwanza.

Mwanamitindo wa kimataifa anaye ipeperusha vyema bendera ya Tanzania Flaviana Matata ni mmoja kati ya watu waliopoteza wazazi na ndugu kupitia ajali hiyo, hivyo kupitia Foundation yake amewajumuisha marafiki zake kushiriki ibada hiyo ikiwa ni pamoja na kufanya matukio kadhaa ya kijamii likiwemo suala la kuzikumbusha Mamlaka husika kuzingatia sheria za usafiri majini.

Katika ibada hiyo Flaviana atajumuika na wanamuziki mahiri muziki wa Bongo Fleva kama Mwana FA, Fid Q, Ay, Damian Soul, One Inclidible na mshindi wa Big Brother Africa Idrisa Sultan.

ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA RATIBA KAMILI.

Wednesday, May 13, 2015

WABUNGE MH,MBATIA NA MH,MREMA WAKUTANA KATIKA IBADA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU BABA ASKOFU STEPHANO MOSHI.

Mbunge wa kuteuliwa na rais,Jmaes Mbatia akizungumza jambo na mbunge wa jimbo la Vunjo ,Agustino Mrema mara baada ya kukutana kwa mara ya kwanza jimboni humo katika ibada ya kumbukumbu ya askofu wa kwanza wa KKKT dayosisi ya Kaskazini iliyofanyika mwishoni mwa wiki/
Kanisala la KKKT ,Usharika wa Mamba Kotelailokofanyika ibada hiyo
Mbunge Mbatia akiingia kanisani humo.
Ujenzi wa taasisi ya saratani ya Bishop Moshiunaofanyika kando ya Usharika huo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bishop Moshi wakiwa katika ibada hiyo.
Viongozi mbalimbali wa dini pia walikuwepo.
Mbunge Mrema akiwa ameketi na mbunge mwenzake Mbatia wakifuatilia ibada hiyo.
Askofu mstaafu Dkt Martin Shao akizungumza wakati wa ibada hiyo.
BabaAskofu Dkt Fredrick Shoo akiongoza ibada hiyo ya kumbukumbu ya miaka 29 ya kifo cha aliyekuwa askofu wa kwanza wa KKKT dayosisi ya Kaskazini,Stephano Moshi.
Askofu mstaafu Dkt Erasto Kweka akimzungumzia marehemu Baba Askofu Stephano Moshi jinsi alivyo mfahamu.
Baba Askofu Dkt Shoo akitoa hotuba yake .
Ikafika wakati wa kuchangia ujenzi wa taasisi ya saratani ya Bishop Moshi na aliyealikwamwanzo alikuwa ni Mbunge wa jimbo hilo Dkt  Mrema .
Dkt Mrema akimtizama mkewe Rose Mrema wakati akitoa pesa kwa ajili ya mchango wa harambee ya kuchangia taasisi hiyo ambapo alitoa kiasi cha sh 500,000.
Baadae ikafika zamu ya Mbatia ambaye alipata nafasi ya kuzungumzakido huku akieleza kuwa tayari amekwisha changia kiasi cha Sh Mil 10 kwa ajili ya shule ya sekondari ya Bishop Moshi na pia alitoa kiasi cha sh Mil 2 kwa ajii ya ujenzi wa taasisi hiyo.
Baba Askofu ,Dkt Shoo akimhukuru Mbatia kwa mchango anaoendelea kutoa kwa kanisa.
Baba Askofu Dkt Shoo akizindua rasmi jengo la kuweka kumbukumbu za Askofu wa Kwanza wa KKKT dayosisi ya Kaskazini Stephano Moshi.
Baba Askofu Dkt Shoo akiingia katika jengo hilo.
Baba Askofu Dkt Shoo akitia saini katika kitabu cha kumbukumbu.
Baba Askofu,Dkt Shoo akiweka shada la maua katika kaburi la askofu wa kwanza wa KKKT dayosisi ya Kaskazini na kufanya maombi katika kaburi hilo.
Mbunge wa kuteuliwa na rais,James Mbatia akitia saini katika kitabu cha kumbukumbu ya askofu wa kwanza wa KKKT dayosisi ya Kaslazini mStephano Moshi .
Mbunge wa kuteuliwa ,James Mbatia akiweka shada la mauakatika kaburi la Askofu wa kwanza wa KKKT dayosisi ya kasakzini ,hayati Stephano Moshi.
Maaskofu wastaafu ,Dkt Erasto Kweka na Dkt Martini Shao wakiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kumbu kumbu ya asakofo wa kwanza wa KKKT ,Stephano Moshi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kasakazini.