ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 21, 2010

HII HAPA RATIBA YA ZIARA YA RAIS KIKWETE KWA AJILI YA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU 2010 MKOANI MWANZA.

RAIS JAKAYA M.KIKWETE KATIKA MOJA YA MIKUTANO YAKE.

RATIBA NDIYO HII.


Friday, August 20, 2010

MWANANCHI WILAYANI TARIME AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI .

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya ASP Costatine Massawe amesema kuwa tume imeundwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi ambapo amekiri kuwa marehemu James ameuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi huko Kinesi wilayani Rorya mkoani Mara.




JAMES JOSEPH ALIYEUAWA NA ASKARI.

ASP Massawe amesema kuwa ,James aliuawa kwa kupigwa risasi na askari kwa madai ya kuthubutu kumnyan’ganya silaha ya Bunduki moja kati ya polisi waliomweka chini ya ulinzi wilayani Rorya Mkoa wa Mara tukio lililotokea marehemu akiwa katika nyumba ya wageni iitwayo Silent Inn Bar and Guest house mnamo agosti 12 saa 11 jioni ambapo siku iliyofuata ya agosti 13 alifikishwa katika hosptali ya Wilaya na kufanyiwa uchunguzi ili apate kuzikwa ambapo hakuzikwa hadi leo hii.

“Nimepokea simu nyingi toka kwa watu mbali mbali wakiuliza ni risasi ngapi zilizoua lakini mimi kwa sasa siwezi kuzungumzia swala hilo kwani tayari tume nimeisha anza uchunguzi tangu jana na tayari baba wa marehemu ameshatoa maelezo mimi nasuburi tume ikamilishe uchunguzi wake. Tume hiyo inahusisha wanasheria pamoja ofisi ya polisi makao makuu na ikikamilika mwanasheria wa Serikali atatoa taarifa na taratibu nyingine zitafanyika” alisema.

Hatua zote hizi zinzfanyika IKIWA leo ni siku ya 8 mwili wa marehemu James Joseph Mag’ancha (25) bado ukiaendela kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hosptali ya wilaya mjini Tarime kufutia familia ya marehemu kutoridhika na uchungunzi uliofanywa awali.

Hata hivyo uchunguzi mwingine ulifanyika upya agosti 17 katika chumba cha kuhifadhia maiti mbele ya baba mzazi wa marehemu, mama mdogo, daktari pamoja na ASP Massawe ambapo bado wazazi hawakuridhika kufatia mabishano juu ya matundu ya risasi ambapo kamanda alidai ni matundu mawili, lakini baba mzazi alisema ni zaidi ya mawili hivyo hali hiyo ikapelekea kuundwa upya kwa tume huru ya kipolisi iliyoanza rasmi uchunguzi juzi agosti 18.

Baba mzazi wa Marehemu, mzee Joseph Mag’ancha aliwambia waandishi wa habari juzi kuwa hatamzika marehemu mpaka atakopofika kijana wake mkubwa ambaye ni mwanajeshi aishie Dar es salaam ili kusaidiana nae kuhakikisha kuwa uchunguzi unafanyika kwa haki.

Maga’ncha amesema kuwa mwanae hakuwahi kuingia katika jeshi lolote kama inavyodaiwa kuwa aliwahi kuingia JKT, vile vile alikanusha mwanae huyo kuwa na upungufu wa akili kama ilivyodaiwa ambapo amesema kuwa mwanae alikuwa na akili timamu na siku zote alikuwa akifanya biashara ndogondogo (machinga) na kipindi chote alikuwa akiishi Jijini Dar es salaam.

Mauti hayo yamemkuta kijana James kipindi ambapo baba mzazi alimwita toka jijini Dar es salaam kuja kujenga kaburi la mama yake mzazi pamoja na bibi yake mzaa mama yake, ambapo siku ya kutiko tayari alikuwa amekwisha nunua matofari ,mchanga pamoja na simenti na kuongeza kuwa marehemu ameacha mke na watoto wawili.

BREAKING NEWS:DREVA TAX AUAWA JIJINI MWANZA. TUNAOMBA RADHI KWA PICHA ZILIZOPO KATIKA HABARI HII:

POLISI WAKIFANYA TATHMINI USIKU WA TUKIO.

DREVA TAX MAARUFU WA MAENEO YA VILLA NA KISS CLUB JIJINI MWANZA AITWAE KAROLI (UMRI KATI YA 30-35 KABILA MUHAYA), MWENYE GARI TOYOTA PREMIO LENYE NAMBA ZA USAJILI T406BCX AMEUAWA KIKATILI NA MTU ASIYEJULIKANA KWA KUCHOMWA KISU SHINGONI NA BAADHI YA MAENEO KICHWANI.
KAROLI DREVA TAX ALIYEUAWA.

TUKIO LILILOTOKEA 19/8/2010 MAJIRA YA SAA 5:30 USIKU, KATIKA BARABARA YA MAKONGORO MTAA WA FURAHISHA KIRUMBA JIJINI MWANZA JIRANI KABISA NA KANISA LA KKKT MAKONGORO.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MWANZA M B.JANDWA.

KAIMU KAMANDA WA JESHI LA POLISI MWANZA AFANDE MGETA B.JANDWA AMETHIBITISHA KUTOKEA KWA TUKIO HILO LA MAUAJI AKIONGEZA KUWA GARI ALILOKUWA AKIENDESHA MAREHEMU LIPO KITUO CHA POLISI LIKIMSUBIRI MMILIKI WAKE AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA.
POLISI WAKICHUKUWA VIELELEZO.

BLOGU YAKO KATIKA UCHUNGUZI:
KWA MUJIBU WA MADREVA WALIO KUWEPO ENEO LA MAEGESHO FURAHISHA WANADAI KUWA MFANYAMAUAJI HAYO KABLA YA KUPATA USAFIRI HUO WA MAREHEMU INASEMEKANA KUWA HAKUPEWA HUDUMA YA USAFIRI NA BAADHI YA WAENDESHA PIKIPIKI NA HATA MATAXDREVA WA ENEO LA CLUB HIZO ZILIZOKO FURAHISHA KIRUMBA AMBAO WOTE WALIMKATALIA KWA MUONEKANO WAKE WA SHAKASHAKA, LAKINI HATIMAYE AKAPATA USAFIRI WA DREVA KAROLI AMBAYE BAADAE ALIKUTWA KAUAWA KWA KISU AMBACHO KILIOKOTWA NA POLISI MITA 20 TOKA ENEO LA TUKIO.

DAMU ZILIZOTAPAKAA ENEO LA TUKIO.

USIKU HUO MTUHUMIWA ALITOKOMEA KUSIKOJULIKANA DAKIKA CHACHE BAADA YA KUFANYA MAUAJI HAYO, JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA UCHUNGUZI NA HATUA ZA KUMSAKA MUUAJI.

MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU.

Thursday, August 19, 2010

CHECHE LARUDI TENA MTAANI.

Salaam, kama tulivyoahidi hatimaye kijarida chenu mkipendacho ambacho bila ya shaka mmekikosa kwa karibu mwaka mzima kimetoka tena kuelekea Uchaguzi Mkuu. Tunatarajia kuendelea kukitoa kila wiki tena na tunawakaribisha kuendelea kukisambaza kwa wengi zaidi!

Mhariri

Frederick M. Katulanda
Mwananchi Newspapers,
Mwananchi Communications Limited,
Lake Zone Bureau,
Mwanza, TANZANIA.
Tell: +255 28 2540939.
Fax: +255 28 2540939.
Cell: +255 784 642620,
Alternative: +255 713 642620
+255 754 642620
E-mail: fkatulanda@yahoo.com
Web: www.mwananchi.co.tz

MKENYA ALIYEMWUUZA ALBINO ATANDIKWA MVUA 17 NA FAINI JUU.

Baada ya kukiri kosa, Mahakama ya mkoa wa Mwanza nchini Tanzania imemhukumu Nathan Mutei (PIC-KUSHOTO) ambaye ni raia wa Kenya anayedaiwa kutaka kumwuuza albino kifungo cha miaka 17 gerezani na kutozwa faini ya zaidi ya shilingi milioni 80.

Polisi wamesema walimkamata Mutei alipojaribu kumwuuza mwenzake kutoka Kenya ambaye ni albino kwa kiwango cha sh milioni 400.

Mutei, mwenye umri wa miaka 28, alikamtwa nje kidogo ya mkoa wa Mwanza.

Katika harakati hizo za kumkamata, ziliyotangazwa rasmi siku ya Jumanne, polisi walijiweka katika nafasi ya wafanyabiashara wanaonunua viungo vya albino.


Kamanda polisi wa mkoa wa Mwanza, Simon Siro, amesema kuwa Bw Mutei alimlaghai Bw Mkwama (PIC-KULIA) mwenye umri wa miaka 20, kuwa atapata kazi Tanzania kama msaidizi wa dereva la lori.

Hapa nchini viungo vya maalbino vimekuwa vikitumiwa na waganga wa kienyeji kutengeneza dawa wanazowaambia wateja wao zitawasaidia kuwa matajiri au kuwa na afya njema.

Idadi kadhaa ya maalbino wameuawa, na mauaji hayo yameenea mpaka nchi jirani ya Burundi. Albino huyo, Robinson Mkwama, atasindikizwa kurudi nyumbani kwao nchini Kenya na ulinzi polisi.

MTUHUMIWA NGUVUNI.

Serikali ya Tanzania imeahidi kuwasaka wanaouza viungo vya albino, na wengi wamehukumiwa kifo kufuatia mauaji hayo.

Wednesday, August 18, 2010

JEH! MKOMBOZI WAKO WA MSIMU ANA NAFASI TENA?

TUKIANGALIA NYUMA KATIKA UANAHARAKATI DHIDI YA RUSHWA KATIKA MIAKA MITATU ILIYOPITA TUNAONA KUWA UTAMADUNI WA RUSHWA BADO UNAZIDIKUENEA DUNIANI KOTE (RUSHWA INAZIDI KUONGEZEKA). LAKINI PIA TUNAONA MIJADALA LUNINGANI, RADIONI, VIJIWENI KWENYE YETU MASKANI, HATA MTANDAONI, MJADALA UNAOKUWA JUU YA NINI KINACHOWEZA KUFANYWA KUZUIA RUSHWA, KUTANGAZA UWAZI NA KUONGEZA MAJADILIANO YA KIJAMII.

YOTE HAYA YAMEFANYIKA MBONA KAMA HALI IKO VILE VILE NA INAONGEZEKA? JEH! RUSWA INALINDWA NA TEKNOLOJIA AU TUNAIPENDAAAAAAAaaaaaaaaaaaa?

Tuesday, August 17, 2010

UBUNGE KWIMBA, SUMVE, CCM YA CHUKUA FOMU KWA KISHINDO. MGOMBEA WA CHADEMA AZUILIWA KUCHUKUWA FOMU.

WAGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA KWIMBA (SHANIF MANSOOR) ALIYENYOOSHA FOMU JUU WA PILI KUTOKA KUSHOTO PAMOJA NA MGOMBEA UBUNGE WA SUMVE RICHARD NDASSA HUKU MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA KWIMBA PETER NG'INGI (KATIKATI YAO) AKIWASHUHUDIA.

WAGOMBEA Ubunge wa majimbo ya Sumve na Kwimba kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM) wamechukua fomu za tume ya uchaguzi baada ya kukamilisha mashariti yote na kanuni za uchaguzi. Hata hivyo mgombea wa Chadema wilayani kwimba jimbo la Sumve Milton Rugimbana amezuiwa na Afisa wa tume ya uchaguzi wilayani Kwimba Kalala selemani kwa kushindwa kukamilisha kanuni za uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa mgombea huyo amezuiwa kutokana na kutokuwa na barua ya utambulisho wa chama chake hivyo kumtaka kufika na barua hiyo kwanza ili aweze kuchukua fomu kama ambavyo kanuni za uchaguzi zinaagiza.


MGOMBEA WA CCM JIMBO LA KWIMBA SHANIF MANSOOR AKIPOKEA FOMU YA UBUNGE TOKA KWA AFISA UCHAGUZI WA KWIMBA KALALA SELEMANI.

MGOMBEA WA CCM JIMBO LA SUMVE RICHARD NDASA AKIPOKEA FOMU YA UBUNGE TOKA KWA AFISA UCHAGUZI WA KWIMBA KALALA SELEMANI.

“Mapaka sasa wameshafika wagombea wengi, na wamechukua fomu lakini mgombea wa Chadema katika jimbo la Sumve nilirudisha na kumzuia kuchukua fomu kutokana na kukiuka masharti ya uchaguzi kwa kukosa utambulisho wa chama chake” alieleza.

Amewataja wagombea ambao mpaka sasa wamekwisha chukua fomu za kuwania ubunge katika jimbo la Kwimba ni Shanif Mansoor (CCM), Bujiku Yusufu (UDP), Ligwa Samwel Ndalawah(CUF) pamoja na mke wa mtoto wa hayati baba wa taifa Leticia Nyerere.

Kwa jimbo la Sumve ambao wamechukua fomu za tume ya taifa ya uchaguzi kuwania ubunge katika jimbo hilo, ni Richard Mganga Ndasa (CCM), Julius Samamba (CUF) ambapo mgombea wa Chadema Militon Rutabana alizuiliwa kuchukua fomu.

Hata hivyo wagombea wa CCM kwa majimbo yote mawili ya Sumve na Kwimba walichukua fomu leo kwa pamoja huku wakisindikizwa na wanachama wa CCM.

TUME YA UCHAGUZI YAKATAA KUTOA FOMU YA KUGOMBEA URAIS KWA CHAMA CHA SAU.

Tume ya uchaguzi Zanzibar imekataa kutoa fomu za kuwania urais wa Zanzibar kwa chama cha SAU kutokana na kujitokeza wagombea wawili wanaowania nafasi hiyo kupitia chama kimoja.

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Salim Kasim amesema wagombea hao waliojitokeza kuchukua fomu ni Haji Ramadhani Haji barua yake iliwasilishwa Ogasti 12 na Haji Musa Kitole barua yake iliwasilishwa Agosti 13.

Amesema kwa mujibu wa sheria za uchaguzi kila chama kitalazimika kuteuwa mgombea mmoja kushiriki katika uchaguzi huo, hivyo tume imeshindwa kutoa fomu kwa wagombea wa urais kupitia chama hicho.

Hata hivyo mkurugenzi huyo amesema fomu hizo zinaweza kutolewa kwa chama hicho endapo kitawasilisha barua ya kufuta jina moja kati ya wagombea hao wawili

Haji Mussa Kitole na Haji Ramadhan Haji wote kutoka chama cha SAU wakiwa na barua tofauti wakati kitole akiwa na barua ya Mwenyekiti, Ramdhan alikuja na barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho wote wakidai kupitishwa na chama chao.

Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Zanzibar, Salim Kassim Ali aliwaambia waandishi wa habari kwamba haiwezekani kutolewa fomu mbili kwa chama kimoja kwa kuwa sheria za uchaguzi zimeeleza mgombea mmoja kutoka chama husika ndie anayepaswa kupewa fomu na sio zaidi ya hapo.

Hata hivyo wagombea hao walikuwa na maoni tofauti huku kila mmoja akijitetea kwamba ameteuliwa kihalali na chama chake na kutaka mwenzake arudi katika chama ili kupata ridhaa ya mkutano mkuu ambao ndio wenye maamuzi ya mwisho.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Khatib Mwinyichande aliwataka wagombea wote waliopewa fomu za urais kutimiza masharti yaliowekwa katika ujazaji wa fomu hizo ikiwa pamoja na kurejesha kabla ya Agosti 30 mwaka huu zikiambianishwa na dhamana wa shilingi millioni mbili na wadhamini wasiopungua 200 katika mikoa mitano ya Unguja na Pemba.

'QUICK FOOT WEAR' SHOP LA SWAGA' ROCK CITY!!!

NOW DAYZ WASHKAJI 'WANASHAIN ILE MBAYA'. JIJINI MWANZA NG'AA KISASA NA DUKA LA VIATU LA FOOT WEAR.

DUKA LINAPATIKANA BARABARA YA LUMUMBA KARIBU NA SWEET CONNER BAR, UCHOCHORO WA GALAX PHARMACY DUKA LA 3.

VITU VYA UKWELI NI QUICK FOOT WEAR TU!.

SWAG....ON ILE ILE!!

KARIBU 'QUICK FOOT WEAR' UPATE KITU KITAKACHO KUFAA TAMANI YA ROHO YAKO.

MDAU USHINDWE MWENYEWE!

MA T SHIRT.

SHOES ON LINE.

SHOES ON LINE TWO.

UKIFIKA NDANI YA QUICK FOOT WEAR UTAKUBALI MWENYEWE.

Monday, August 16, 2010

KIRUMBA MWANZA JUU KWA JUU!!

WACHA LEO TUSAFIRI NAMUNA HII..
MAKAZI YA WATU.

'KIRUMBA RESSORT' MAHALA PA MISOSIz YA UKWELI YA ASILI.

KIRUMBA SOKONI.

NINYIME UGALI... NIKUNYIME MBOGA!!!!

MBUNGE WA TARIME ALIYEMALIZA MUDA WAKE KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA CHARLES MWERA (KULIA) AKIPOKEA KADI YAKE RASMI YA KUJIUNGA NA CHAMA CHA CUF TOKA KWA NAIBU MKUU WA CUF JUMA DUNI HAJI, BAADA YA KIHAMA CHAMA CHA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO NCHINI (CHADEMA) JANA JIJINI DAR ES SALAAM.

KIUKWELI SIASA ZA MIAKA YA SASA MIE SIZIELEWI.....

UN YAHIMIZA MISAADA ZAIDI KWA PAKISTAN.

HAYA NDIYO MAKAZI MAPYA.

Wiki mbili baada ya mafuriko kuanza nchini Pakistan, bado kuna idadi kubwa ya watu ambao bado wanahamishwa kutoka maeneo yenye hatari.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon, amesihi dunia kuzidisha usaidizi wake kwa nchi ya Pakistan iliyoathirika vibaya kutokana na mafuriko hayo.

Akizungumza baada ya kukutana na rais wa Pakistan na makamu wake, Ban amesema Pakistan imesimama bega kwa bega na dunia nzima katika operesheni za wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa mataifa na kwamba dunia nzima lazima isaidia nchi hiyo.

Ameelezea ziara yake nchini humo kuwa ni ya kuvunja moyo kwake na kwa ujumbe wake.


''Sitawahi kusahau uharibifu na mateso niliyoshuhudia hii leo. Nimetembelea maeneo mengi ambayo yamepitia majanga ya kiasili kote duniani, lakini hakuna kinachokaribia nilichoshuhudia'', bw. Ban amesema baada ya kuzuru maeneo yaliyoathirika vibaya. Amesema kuwa kiwango cha janga hilo ni kubwa mno, na watu wengi, katika maeneo mengi wanahitaji msaada.


TIZAMA VIDEO YANAYOJIRI PAKISTAN.

Shirika la Umoja la Mataifa limetoa ombi la dharura la dola nusu billioni kwa nchi ya Pakistan.

Takriban mtu mmoja kati ya kumi ameathirika moja kwa njia moja au nyingine. Huenda , watu millioni ishirini, ambayo ni humusi ya watu nchini Pakistan wameathiriwa na mafuriko hayo.

Zaidi ya watu 1500 wamefariki dunia kufuatia mafuriko hayo.


KWA HISANI YA BBC SWAHILI.