WAGOMBEA Ubunge wa majimbo ya Sumve na Kwimba kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM) wamechukua fomu za tume ya uchaguzi baada ya kukamilisha mashariti yote na kanuni za uchaguzi. Hata hivyo mgombea wa Chadema wilayani kwimba jimbo la Sumve Milton Rugimbana amezuiwa na Afisa wa tume ya uchaguzi wilayani Kwimba Kalala selemani kwa kushindwa kukamilisha kanuni za uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa mgombea huyo amezuiwa kutokana na kutokuwa na barua ya utambulisho wa chama chake hivyo kumtaka kufika na barua hiyo kwanza ili aweze kuchukua fomu kama ambavyo kanuni za uchaguzi zinaagiza.
MGOMBEA WA CCM JIMBO LA KWIMBA SHANIF MANSOOR AKIPOKEA FOMU YA UBUNGE TOKA KWA AFISA UCHAGUZI WA KWIMBA KALALA SELEMANI.
MGOMBEA WA CCM JIMBO LA SUMVE RICHARD NDASA AKIPOKEA FOMU YA UBUNGE TOKA KWA AFISA UCHAGUZI WA KWIMBA KALALA SELEMANI.
“Mapaka sasa wameshafika wagombea wengi, na wamechukua fomu lakini mgombea wa Chadema katika jimbo la Sumve nilirudisha na kumzuia kuchukua fomu kutokana na kukiuka masharti ya uchaguzi kwa kukosa utambulisho wa chama chake” alieleza.
Amewataja wagombea ambao mpaka sasa wamekwisha chukua fomu za kuwania ubunge katika jimbo la Kwimba ni Shanif Mansoor (CCM), Bujiku Yusufu (UDP), Ligwa Samwel Ndalawah(CUF) pamoja na mke wa mtoto wa hayati baba wa taifa Leticia Nyerere.
Kwa jimbo la Sumve ambao wamechukua fomu za tume ya taifa ya uchaguzi kuwania ubunge katika jimbo hilo, ni Richard Mganga Ndasa (CCM), Julius Samamba (CUF) ambapo mgombea wa Chadema Militon Rutabana alizuiliwa kuchukua fomu.
Hata hivyo wagombea wa CCM kwa majimbo yote mawili ya Sumve na Kwimba walichukua fomu leo kwa pamoja huku wakisindikizwa na wanachama wa CCM.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.