Na Victor Masangu,Kibaha
Wananchi wa mitaa mitatu ya Saeni,Zogowale na Jonung"ha iliyopo kata ya Misugusugu ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya kufuata huduma ya afya kwa umbari mrefu wameondokana na adha hiyo baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa zahanati.
Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wakati wa halfa ya uzinduzi wa zahanati ya Saeni ambayo imehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali,viongozi waCcm,Dini,pamoja na wananchi kutoka maeneo mbali mbali.
Koka alibainisha kwamba kumalizika wa mradi wa ujenzi huo kutaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kutaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuwaboreshea zaidi wananchi kupata huduma ya matibabu kwa urahisi zaidi.
Aidha alisema kwamba hapo awali wananchi wa kata ya misugusugu walikuwa wanapata shida ya kutembea umbari mrefu hivyo akaamua kushirikiana na wananchi kwa pamoja ili kuwaunga mkono.
Koka aliongeza kuwa kabla ya kuanza mradi huo alichangia kiasi cha shilingi milioni 6.5 kwa ajili ya kununua mifuko ya saruji kwa ajili ya kuweza kuanza ujenzi huo wa ujenzi wa zahanati.
"Mara ya kwanza nilitoa milioni tano lakini awamu ya nilichangia tena kiasi cha shilingi milioni 1.5 lengo ikiwa ni kuanza mradi huo wa ujenzi wa zahanati hiyo ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi.
Koka alibainisha lengo lake kubwa ni kuwatumikia wananchi wake hivyo atahakikisha kuwa ataendelea kuboresha zaidi huduma ya afya ili wananchi waweze kuondokana na kero ambazo wamekuwa wakizipata.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa halmashauri ya mji Kibaha Peter Nsanya alibainisha kuwa ujenzi huo mpaka kukamilika umegharimu kiasi cha shilingi milioni 181.
Alibainisha kuwa mradi wa ujenzi huo utaweza kusaidia zaidi hasa kwa Upande kwa huduma za mama na mtoto ambao walikuwa wanapata shida ya kwenda Hadi eneo la mlandizi.
Naye Diwani wa kata ya Misugusugu Upendo Ngonyani amemshjkuru Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kwa kutekeleza ilani kwa vitendo kwa kuchangia fedha ambazo zilisaidia katika mradi wa ujenzi huo wa zahanati.