ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 24, 2024

YANGA YATINGA ROBO FAINALI KIBABE

 


Wananchi wanaandika historia ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kishindo kufuatia ushindi wa 4-0 dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria kwenye hatua ya makundi.

FT: Young Africans ðŸ‡¹ðŸ‡¿ 4-0 ðŸ‡©ðŸ‡¿ CR Belouizdad
⚽️ Mudathir Yahya 43’
⚽️ Aziz Ki 46’
⚽️ Kennedy Musonda 48’
⚽ Joseph Guede 84’

MSIMAMO KUNDI D
1. ðŸ‡ªðŸ‡¬ Al Ahly ——— 9
2. ðŸ‡¹ðŸ‡¿ Yanga Sc ——— 8
3. ðŸ‡©ðŸ‡¿ CR Belouizdad ———5
4. ðŸ‡¬ðŸ‡­ Medeama ———4

Yanga SC imefuzu moja kwa moja kwa kuwa mbabe wa ‘head to head’ kati yake na CR Belouizdad, kwa maana hata kama Belouizdad atashinda mechi ya mwisho hawezi kufuzu.

Itakumbukwa mechi ya kwanza Yanga ilipoteza 3-0 kabla ya kushinda 4-0 kwenye mchezo wa marudiano.

Thursday, February 22, 2024

MICHUANO YA KIBAFA VIJANA CUP YAACHA GUMZO WADAU WAMPA HEKO MBUNGE KOKA

 NA VICTOR MASANGU, PWANI FEBRUARI 22


HALMASHAURI ya Kibaha mji mkoani Pwani katika kukuza sekta ya mchezo wa soka imetenga eneo lenye ukumbwa wa hekari 40 katika eneo la mintamba lengo ikiwa ni kujenga uwanja mkubwa  wa kisasa ambao utatumika katika michuano mbali mbali ya kitaifa na kimataifa.


Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha mji Mhe.Mussa Ndomba wakati wa halfa ya  kufunga rasmi mashindano  ya Kibafa Vijana Cup chini ya umri wa miaka 25 yaliyofanyika kwenye dimba la Mwendapole.

INSERT..1 TV MHE. MUSSA NDOMBA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA KIBAHA MJI.

Kwa upande wake Katibu wa mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Said Mbecha amebainisha kwamba wameweza kusapoti mashindano hayo kwa kuchangia zaidi ya shilingi milioni 6.

INSERT..2 TV SAID MBECHA KATIBU WA MBUNGE JIMBO LA KIBAHA MJINI


Kwa Upande wake Makamu mwenyekiti wa chama cha soka Mkoa wa Pwani (COREFA) Mohamed Lacha hakusita kumpongeza Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini kwa kuamua kudhamini michuano hiyo kwa asilimia mia moja.


INSERT..3 TV MOHAMED MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA PWANI(COREFA)

Naye Mratibu wa Mashindano hayo Walter Mwemezi  amebainisha kwamba  lengo lao kubwa ni kuinua na kukuza mchezo wa soka hasa kwa vijana


INSERT..4 TV WALTER MWEMEZI MENEJA WA MASHINDANO 


Mashindano  ya Kibafa Vijana Cup iliyodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji Silivestry Koka imetamatika kwa timu ya Chestmocker kuwa mabingwa,na kuzawadiwa milioni moja,Umwerani mshindi wa pili na kupata laki tano na TP Pwani mshindi wa tatu na  kupata seti ya jezi.

JEH NI KOSA KUMPA PASSWORD YAKO MKE AU MUME?

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Je! Unafahamu kutoweka nywila (password) kwenye simu yako ni kosa kisheria na unaweza kwenda jela ama kulipa faini? na vipi kuhusu kutoa nywila kwa mpenzi wako au mtu mwingine yeyote? Ungana na Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Imelda Salum, ambaye ameambatana na Afisa Mawasiliano TCRA Makao Makuu, Robin Ulikaye pamoja naye Afisa Masoko TCRA Benadetha Mathayo wakifunguka mengi zaidi kupitia kipindi cha Drive Mix ya 93.7 Jembe Fm Mwanza.

COREFA KIBAFA YAMFAGILIA MBUNGE KOKA KUSAPOTI MASHINDANO YA KIBAFA VIJANA CUP

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 

Uongozi wa chama cha soka Mkoa wa Pwani (COREFA) pamoja na chama cha soka Wilaya ya Kibaha (KIBAFA) umempongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa kuamua kujitoa kwa hali na mali   kusapoti sekta ya michezo hasa kwa vijana.

Akizungungumza wakati wa halfa ya kufunga rasmi mashindano ya Kibafa Vijana Cup chini ya umri wa miaka 25,Makamu Mwenyekiti wa Corefa Mohamed Lacha alisema kwamba mbunge Koka ameweza kusapoti michuano hiyo kwa asilimia mia moja.

Lacha alisema kwamba amefarijika sana kuona sapoti kubwa ambayo ameweza kuitoa mbunge huyo kwa lengo la kuweza kufanikisha mashindano hayo ya vijana yaweze kufanyika na kwamba yamefanikiwa.

"Kwa kweli mimi kwa nafasi yangu kama Makamu mwenyekiti wa Corefa nipende kwa dhati kabisa kumshukuru Mbunge wa Jimbo la kibaha kwa kutoa fedha kwa ajili ya kudhamini mashindano haya,"alisema Lacha
Kadhalika aliongeza kuwa kauli mbiu yao kubwa ni kwamba  mpira lazima uchezwe katika Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa mchezo wa soka.

"Tunashukuru mashindano haya yamemalizika salama na timu zote zimeweza kupatiwa zawadi zao ambazo zimetolewa na mdhamini mkuu ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka,"alifafanua Lacha.

Kwa upande wake .mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya chama cha soka Wilaya ya Kibaha (KIBAFA) Jeremia Komba alisema kwamba Mbunge huyo amekuwa mstari wa mbele katika kushiriki kikamilifu katika kusaidia sekta ya michezo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Kibaha Mussa Ndomba aliwataka viongozi wa vyama soka kuendelea kumpa sapoti Mbunge huyo kwani ameweza kutumia zaidi ya milioni sita katika kudhamini michuano hiyo.

Pia na sisi kama halmashauri tumejipanga vilivyo katika kutenga maeneo ya viwanja kwa michezo ili kuweza kutoa fursa zaidi ya vijana kupata ajira kupitia michezo.

Nao baadhi ya wachezaji na wadau wa mchezo wa kabumbu walisema jambo ambalo amelifanya Mbunge Koka la kudhamini michuano hiyo kwa asilimia 100 linatia moyo katika nyanja ya kukuza mchezo wa soka  hasa kwa vijana.

Waliongeza kuwa kitendo ambacho amekifanya Mbunge Koka cha kuziwezesha timu 16 kwa kuzipatia jezi  pamoja na mipira ikiwemo na kutoa zawadi kwa washindi watatu kimewapa faraja sana katika medani ya soka.

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amekuwa ni nguzo kubwa ya kuwasaidia vijana katika kuibua na kukuza vipaji walivyonavyo ambapo safari hii amekuwa mdhamini mkuu wa michuano ya Kibafa vijana Cup kwa asilimia mia moja.

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MGODI WA BARRICK NORTH MARA, YAVUTIWA KWA KUENDESHWA KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, David Mathayo David, akizungumza wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo katika mgodi wa Barrick North Mara (kushoto) ni Naibu Waziri wa Madini,Mh.Stephen Kiruswa na (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mtanda.

Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imetembelea Mgodi wa dhahabu wa North Mara uliopo wilayani Tarime na kutoa ushauri wa kuboresha sekta ya madini ili iweze kuwanufaisha wananchi na taifa kwa ujumla. Pia ilipongeza kampuni hiyo kwa kufanya uwekezaji mkubwa wenye tija na ufanikishaji wa miradi ya kijamii kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) sambamba na kuendeleza mahusiano na wananchi wanaoishi kwenye maeneo yanayozunguka mgodi.

Ziara ya Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake, Mh. David Mathayo David. Awali wajumbe wa Kamati hiyo walipata maelezo kuhusu shughuli za uendeshaji wa mgodi huo kabla ya kutembelea sehemu mbalimbali, ikiwemo eneo la majitaka, kinu cha kuchenjua dhahabu na baadhi ya miradi ya kijamii iliyotekelezwa kutokana na fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) katika vijiji vilivyo jirani na mgodi wa North Mara.

Baadhi ya miradi hiyo ni Shule ya sekondari Matongo, mradi mkubwa wa maji wa Nyangoto na ule wa kilimo biashara unaoendeshwa na vijana katika kijiji cha Matongo.

Akiongea kwa niaba ya kamati baada ya kumaliza ziara hiyo, Dk.David Mathayo alisema “Kwa muda mfupi mmebadilisha mazingira ya mgodi huu. Mnatunza mazingira vizuri, wabunge wamefurahi - na kwa niaba yao ninawapongeza, endeleeni kuwa watunzaji wazuri wa mazingira kwa usalama wa wananchi wetu.”
Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Melkiory Ngido (katikati) akitoa ufafanuzi katika kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea mgodi wa Barrick North Mara ,(kushoto) ni Meneja wa mgodi wa North Mara, Apolinary Lyambiko,(kulia) ni Meneja wa Mahusiano ya Jamii wa mgodi huo Francis Uhandi.
--
Pia Kamati hiyo iliipongeza Barrick kwa kuendelea kuwa mfano mzuri katika ulipaji wa kodi mbalimbali serikalini, pamoja na utoaji wa mabilioni ya fedha za kugharimia utekelezaji wa miradi ya kijamii kupitia mpango wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

“Kwenye kampuni kubwa za kibiashara ninyi [Barrick] mnaongoza kwa kulipa kodi na kutoa gawio kwa Serikali,” Mathayo alisema katika sehemu ya hotuba yake ya kuhitimisha ziara hiyo.

Kamati hiyo pia ilieleza kuridhishwa na jinsi Kampuni ya Barrick Gold inavyotekeleza Sheria ya ‘Local Content’ na hivyo kuwezesha Watanzania wengi wakiwemo wazawa wanaoishi jirani na migodi yake kunufaika na uwekezaji wake kupitia biashara na ajira, miongoni mwa mambo mengine.
Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiangalia utunzaji wa mazingira walipofanya ziara ya kikazi katika mgodi wa Barrick North Mara jana.
---
Nao baadhi ya Wabunge wa kamati hiyo walipongeza Barrick kwa kuendelea kuleta mapinduzi kupitia uwekezaji mkubwa wa sekta ya madini nchini na walishauri mgodi uangalie uwezekano wa kuwasaidia wachimbaji wadogo ili wajikwamue kiuchumi kwa kuwapatia baadhi ya maeneo wachimbaji hao.

Akiongea wakati wa ziara hiyo, Naibu Waziri wa Madini, Mh.steven Kiruswa ,alitoa wito kwa wadau waliopo kwenye sekta ya madini kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa na Serikali ikiwemo kanuni inayohusiana na mgawanyo wa fedha za Uwajibikaji kwa jamii (CSR) na ushirikishwaji wa wazawa wa Tanzania katika shughuli za Mnyororo wa madini (Local content).

‘’Pamoja na changamoto tulizozisikia kutoka kwa viongozi wa wananchi wa eneo hili linalozunguka mgodi, natoa pongezi kwa kampuni ya Barrick kwa uendeshaji migodi yake nchini kwa weredi, uwazi na kuchangia pato la Taifa kupitia kodi, sambamba na kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia miradi inayotekelezwa kwa fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR).
Baadhi ya wabunge kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakifuatilia maelezo kutoka kwa watendaji wa Barrick wakati walipotembelea mgodi wa North Mara
Diwani wa kata ya Nyamwaka, Mwita Marwa Magige akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini katika mgodi wa Barrick North Mara
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakikagua mradi wa kilimo biashara ulioanzishwa na mgodi wa Barrick North Mara kwa ajili ya kuwawezesha wananchi wanaoishi jirani na mgodi huo katika kijiji cha Matongo.
---
Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Melkiory Ngido, aliwashukuru wajumbe wa kamati hiyo kwa kutembelea mgodi huo na kuahidi kuwa maoni na ushauri uliotolewa na wajumbe yatafanyiwa kazi “Barrick siku zote tutahakikisha tunaendesha shughuli zetu kwa uwazi na kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na Serikali”,alisisitiza.

Awali akitoa maelezo kuhusiana na shughuli za kampuni, Melkiory Ngido ,alisema Barrick kupitia migodi yake ya North Mara na Bulyanhulu imewekeza hapa Tanzania shilingi zaidi ya trilioni sita, na kwamba kati ya kiasi hicho, Serikali imepokea trilioni tatu ambazo zimelipwa kwa mifumo wa kodi na gawio tangu mwaka 2019 ilipokabidhiwa na kuanza kuendesha migodi hiyo kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.

Kuhusu mgodi wa North Mara, Ngido alisema: “Huu mgodi ulitakiwa kuisha [kufika kikomo] mwaka 2026 lakini kwa juhudi za uwekezaji na za kitaalamu utaenda hadi miaka 15 ijayo - utafika hadi mwaka 2039.”

Ngido, alisema Barrick kupitia mpango wake ujulikanao kama The Barrick-Twiga Future Forward Education Programme, imetoa Dola za Kimarekani milioni 30 sawa na shilingi takriban bilioni 70 kwa ajili ya kusaidia uboreshaji wa miundombinu ya shule za sekondari za juu upande wa mabweni na madawati, miongoni mwa mambo mengine katika maeneo mbalimbali nchini.

“Mradi huu upo chini ya TAMISEMI na sisi kama Twiga na Barrick tunafurahi kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ili watoto wote waende A level (high school) na wasome katika mazingira rafiki,” alisema, Ngido.

Kamati hiyo ya Bunge pia ilielezwa kuwa asilimia 96 ya wafanyakazi takriban 3,000 wa Mgodi wa North Mara ni Watanzania, na kwamba juhudi za kuongeza idadi ya wafanyakazi wanawake zinaendelea.

Wakati huo huo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeiagiza Serikali ya mkoa kumaliza tatizo la uvamizi katika mgodi wa North Mara unaofanywa na makundi ya watu (intruders) mara kwa mara kwa lengo la kuiba mawe yenye dhahabu.

“Uwekezaji huu ulindwe, hivi mpaka watu wanabeba mapanga na kuvamia mgodi, vyombo vyetu [vya ulinzi na usalama] vinakuwa wapi, vyombo visaidie kutatua tatizo hili (uvamizi mgodini) kwa sababu tunajirudisha nyuma wenyewe na tunaharibu taswira ya nchi yetu kwa wawekezaji,” alionya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mathayo.

Kwa upande mwingine, Kamati hiyo imeagiza Serikali ngazi ya wilaya na mkoa kumaliza malalamiko ya wananchi kuhusu mchakato unaotumika katika uthaminishaji wa ardhi inayohitajika kwa ajili ya upanuzi wa shughuli za mgodi wa North Mara.

Baadhi ya viongozi waliofuatana na Kamati hiyo katika ziara hiyo ni Naibu Waziri wa Madini, Dkt Steven Kiruswa, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mohamed Mtanda, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele, Madiwani na Wenyeviti wa vijiji kutoka Kata tano zenye vijiji 11 vilivyo jirani na mgodi wa Noth Mara.

Migodi ya dhahabu ya North Mara na Bulyanhulu inaendeshwa na Kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.

Wednesday, February 21, 2024

RAMADHANI BROTHERS KUTOKA TANZANIA WATWAA TAJI LA 'AMERICA GOT TALENT'


Wanasarakasi wawili kutoka Tanzania kwa jina Ramadhan Brothers wameibuka washindi katika mashindano ya American Got Talent kitengo cha fantacy league.


Wawili hao wanaoshirikisha Fadhili Ramadhan na Ibrahim Jobu, walishinda taji hilo Jumatatu usiku.


Waliwashinda wapinzani wao wakuu Pack Drumline, V. Unbeatable, Sainted na Musa Motha.

‘Tunaamini Maisha yetu yanabadilika kuanzia wakati huo’, Ramadhan alinukuliwa na jarida la US Today akisema. ‘’Ushindi huu una maana kubwa kwetu, tuna furaha sana isio na kifani’’.


Kwa mujibu wa US Today, ushindi huo wa tuzo ya AGT ni safari ya miaka miwili ya vijana hao wawili.


Ramadhani Brothers walipanga kufanya majaribio ya "AGT" Msimu wa 17, lakini Jobu hakuweza kupata visa yake ya kusafiri kwa wakati.


Kwa muda, wawili hao walionekana kwenye mfululizo kadhaa wa "Got Talent", ikijumuisha "Australia's Got Talent," "Got Talent España" na "Românii au talent," ambayo ilianzisha jukwaa lao la kwanza la "AGT" Msimu wa 18.


Katika shindano hilo Ramadhani Brothers waliwashangaza waamuzi kwa onyesho linalohusisha mwanasarakasi mmoja kusawazisha uzito wa mwili wa mwenzake kichwani huku wakipita seti tofauti.


Hatahivyo licha ya kuingia fainali kama wahitimu wakuu, walipoteza kwa mshindi wa Msimu wa 18 Adrian Stoica & Hurricane.

KATIBU CCM KIBAHA MJI ATEMA CHECHE KWA VIONGOZI WANAOLALAMIKA KWA NJIA YA MITANDAO

 


NA VICTOR MASANGU/KIBAHA 

Viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) wametakiwa kuachana kabisa  na tabia ya kulalamika kwa kutumia mitandao ya kijamii na badala yake wanatakiwa kuzingatia vikao halali vya kikanuni au kumtafuta muhusika ili kupata ufumbuzi.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa chama cha mapinduzi  (CCM) Wilaya ya Kibaha Mjini Issack Kalleiya wakati wa kikao kazi kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Wilaya na kuwakutanisha madiwani wa kata zote 14 za  Kibaha Mjini na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa.

Katibu huyo alisema kuwa viongozi wanapaswa kutimiza wajibu wake ipasavyo kwa kufuata maelekezo ya chama kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa na sio vinginevyo kulalamika kwenye mitandao ya kijamii.


Katibu huyo   alisema kwamba  viongozi CCM  wanatakiwa wajiweke tayari kwa uchaguzi na kuacha kulalamika kwa watu ambapo jambo hilo limekua linashika kasi kwa baadhi ya viongozi kutoa siri za vikao na kuwapa watu ambao hawahusiki.

Katibu wa CCM amesisitiza kuwa kwa sasa Wilaya ya Kibaha Mjini ina jambo kubwa la Uchaguzi ww Udiwani Kata ua Msangani hivyo amewataka wote kujiweka tayari kwa kushiriki katika Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Machi 20,2024.
Aidha, Katibu Kalleiya amewataka Madiwani pamoja na wenyeviti wa Serikali za Mitaa kushiriki katika Uchaguzi wa Udiwani Kata ya Msangani pindi watakapohitajika ikiwemo kusaidia kunadi Chama wakati wa kampeni na kutafuta kura kwa wananchi ili CCM ishinde kwa kishindo.

Katibu Wa CCM amesema, wote wanatakiwa wawe tayari ambapo ratiba ya uchukuaji na urudishani wa fomu za Uchaguzi unaanza tarehe 21/02/2024 hadi 23/01/2024.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha na Diwani wa Kata ya Sofu Mhe. Mussa Ndomba amepokea maelekzo hayo kwa kuahidi kushirikiana na Chama katika Uchaguzi huu mdogo wa marudio ili kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo.

Pia, amesema maelekezo yote yaliyotolewa watayafanyia kazi na kwa sasa watakuwa wanakaa vikao pamoja katika ya madiwani na wenyeviti wa Serikali za Mitaa sambamba na Mkurugenzi ili kujadili masuala mbalimbali na kuweza kutatua changamoto zilizopo katika mitaa yao.

Kikao hicho kilitoka na kauli moja ya CCM Moja KIbaha Moja ambapo wote Madiwani na Wenyeviti walikubali kushirikiana katika kukijenga Chama, kusimamia na kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Tuesday, February 20, 2024

SEMA NA TANGA WAKOSHWA NA UWEKEZAJI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA-BOMBO WAHAIDI KUWA MABALOZI

 

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo akizungumza wakati wa ziara ya Kundi la Sema na Tanga mara baada kumaliza ziara hiyo yenye lengo la kuona uwekezaji uliofanywa na Rais Samia Suluhu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt Frank Shega na kulia ni Mwenyekiti wa Sema na Tanga 

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Frank Shega akizungumza wakati wa ziara hiyo ya Kundi la Sema na Tanga kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo 

Na Oscar Assenga, TANGA

Kundi la Sema na Tanga leo wamefanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo huku wakifurahishwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uwekezaji na kuimarisha huduma za Afya hapa nchini na kuhaidi kuwa mabalozi wa kuisemea vizuri.

Wametembelea na wamejionea uwekezaji mkubwa uliofanyika katika kitengo cha dharura (EMD), kitengo cha uangalizi maalumu (ICU), Kitendo cha radiolojia (CT-scan), Kitengo cha uangalizi maalumu kwa watoto wachanga (NICU), Wodi ya upasuaji, Kitengo cha kusafisha figo (Dialysis Unit)

Akizungumza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Japhet Simeo alisema kwamba kundi hilo ambalo ni wadau wa maendeleo walialikwa ili kuweza kuona huduma nzuri ambazo zinatolewa katika Hospitali hiyo na wamethibitisha kuwa uwekezaji ni mkubwa sana na wengi wao walikuwa na picha tofauti na waliyokuwa nayo awali na hawakuamini kama Hospitali hiyo ingeweza kuwa na vifaa kama hivyo na watu wanatibiwa na kupona.

“Ambao waliokuwa na hisia za zamani kwa sasa zitafutika maana wengine wanaamini yale mambo ya miaka 10 iliyopita bado, kwa hiyo Sema na Tanga wanaenda kufuta hayo mambo kwenye fikra za wananchi na tunaamini mtakuwa mabalozi wazuri wa kulisemea hili”Alisema

Hata hivyo alisema hivi sasa wanaendelea kuboresha huduma huku akiishukuru ofisi ya Mkuu wa Mkoa ilivyosimamia kuhakikisha rasimali zinazoletwa zinasimamiwa kikamilifu akianza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba na Katibu Tawala Pili Mnyema namna wanavyompa ushirikiano mkubwa na hivyo kufanya kazi kwa kujiamini

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Kundi la Sema na Tanga alisema wana haja ya kuja kukuunga mkono kama wadau wa maendeleo kutembelea kutokana kujionea maboresho ya huduma yaliyosaidia kuondoa makelele yaliyokuwa yakisikika.

Alisema wametembelea wameona maboresho makubwa ,vifaa mbalimbali, nyenzo nzuri za kisasa.“Tuwaheshimu madaktari na wauguzi hapa nchini na tuache kuingiza siasa kwenye mambo ya kitaalamu maana tutakuwa tunawavunja moyo kama kuna mtu atawahujumu sisi tupo tayari kuwasemea na kusimamia na nyie”Alisema

“Tunamshukuru Waziri Ummy kwa kuteletea Mganga Mfawidhi Mpya Dkt Frank Shega na zile kelele zilizokuwepo kwa sasa hazipo zimeondoka ameonyesha waledi mkubwa, tutakutetea kwa kazi yako nzuri unayoifanya bila kupepesa macho”Alisema

KATIBU WA CCM KIBAHA MJI AWAHIMIZA WANACHAMA KUGOMBEA UDIWANI KATA YA MSANGANI


VICTOR MASANGU,KIBAHA


Katibu wa Chama cha malinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Issack Kalleiya kuchangamkia fursa ya kujitokeza kwa wingi katika kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya udiwani wa kata ya Msangani ambayo ipo wazi kwa sasa.


 Katibu huyo aliwahimiza wanachama wote ambao wana sifa za kugombea kujitokeza bila woga kwa lengo la kuweza kuziba nafasi hiyo ya diwani ambayo ipo wazi kutokana na aliyekuwa diwani wa kata hiyo kufariki dunia hivi karibuni.


Katibu  Kalleiya aliyasema hayo  wakati akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata Msangani kuwa uchukuaji wa fomu ndani ya Chama utaanza tarehe 21/02/2024 hadi 23/02/2024 ambapo wanachama wote wenye sifa za kugombea watatakiwa kuchukua fomu na kurudisha ndani ya muda uliopangwa.

Amesema, Ofisi ya CCM Wilaya itakuwepo katika kuhakikisha kila mwanachama aliyechukua fomu anapata nafasi ya kuirudisha ili kusije kutokea malalamiko ya wagombea kukuta Ofisi za Kata zimefungwa.

Kalleiya alisema kwamba  zoezi hilo lonapaswa lifanyike kwa uweledi na kusisitika kuwa  hatopependa kusikia mwanachama yoyote ameshindwa kuchukua fomu yq Ugombea, bali kila mwenye sifa achukue ila maamuzi ya nani anafaa yatakuwa ni maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Kata.

Pia, Katibu wa CCM amesisitiza kuhusu uundwaji wa Kamati za Ushindi katika kila Tawi na Mashina ili kuhakilisha Chama Cha Mapinduzi kinashinda nafasi hiyo kwa mara nyingine tena.
Akizungumzia suala la daftari la wapiga kura, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini Ndg Mwl. Mwajuma Nyamka amesmea uchaguzi huu mdogo ni ww kujaza nafasi baada ya Diwani wa Kata ya Msangani kufariki ila kiutaratibu wale ambao walipiga kura katika Uchaguzi wa mwaka 2020 ndiyo wanapaswa kupiga kura.

Akifafanua zaidi, Mwenyekiti amesema kwa wale ambao wametimiza umri wa kupiga kura na hawakuwepo katika daftari la wapiga kura la mwaka 2020 hawataruhusiwa kushiriki Uchaguzi huu. 

Aidha, Kamati ya Siasa Wilaya iliweza kufanya ziara katika Matawi kila mmoja akiwa mlezi wa tawi na kusikiliza mawazo na ushauri wa wanachama ili kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo na kipi kifanyike na kuweza kupata ushindi wa kishindo.

Tume ya Uchaguzi nchini imetangaza tarehe ya Uchaguzi wa kujaza nafasi za Udiwani nchini ambapo Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 20/03/2024.

Monday, February 19, 2024

KWA MARA YA KWANZA MAFUNDI WAJENZI NCHINI WAKUTANA KUUNDA CHAMA CHAO WATUMA SALAMU KWA SERIKALI

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Semina imeendeshwa Jumapili hii jijini Mwanza! Shukrani kwa Mafundi zaidi ya 1200 walioshiriki

KOKA ATIMIZA AHADI YAKE AKABIDHI ZAWADI KWA MABINGWA MICHUANO YA KIBAFA VIJANA CUP


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka ametekeleza ahadi yake kwa vitendo kwa kutoa  fedha na vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 1.7 kwa ajili ya kukabidhiwa  washindi watakashinda katika michuano ya  kombe la Kibafa  Vijana Cup wenye umri  chini ya miaka 25.

Michuano hiyo ya fainali ambayo ilikuwa inasubiliwa kwa hamu na shauku kubwa na mashabiki wa soka  inatarajiwa kulindima Februari 21  mwaka huu   kwenye uwanja wa Mwendapole mjini kibaha.

Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Mbunge katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini  Method Mselewa wakati wa halfa fupi iliyofanyika katika ofisi za Mbunge na kuhudhuliwa na viongozi wa Kibafa na wadau wa soka.

Katibu Mselewa alibainisha  kwamba  wakati wa mashindano yananza Mbunge aliahidi kuwa mdhamini mkuu wa michuano hiyo na kutoa vifaa mbali mbali kwa ajili ya timu zishiriki.
Mselewa alibainisha kwamba ofisi ya mbunge imeweza kukabidhi zawadi mbali mbali ikiwemo fedha taslimu kiasi cha  shilingi milioni 1 kwa ajili ya timu itakayoibuka kuwa bingwa.

"Mbunge aliahidii kutoa zawadi kwa mshindi wa kwanza mpaka wa tatu na leo tumekabidhi zawadi hizo kwa viongozi wa Kibafa ambapo milioni moja kwa mshindi wa kwanza laki tano mshindi pili na mshindi  wa tatu zawadi ya jezi,"alisema Mselewa.

Aidha aliongeza kuwa mbunge aliamua kusapoti michuano hiyo kwa lengo la kuweza kukuza na kuibua vipaji kwa vijana wa jimbo lake ikiwa pia ni utekelezaji wa ilani ya chama.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kibafa David Mramba amempongeza Kwa dhati kwa kuweza kusapoti mashindano hayo pamoja na kutoa jezi na vifaa Ili kufanikisha ligi hiyo ya vijana.

Pia alifafanua kwamba katika ligi hiyo Mbunge aliweza kutoa  jezi 16 pamoja na  mipira 20  kwa   timu zote 16 ambazo zimeshiriki katika michuano hiyo.

Naye meneja wa mashindano hayo Walter Mwemezi alisema alimpongeza Mbunge huyo kwa kuweza kufanikisha ahadi yake kwa vitendo kwa kutoa zawadi kwa timu zitakazoshinda.

Pia aliongeza kuwa mashindano hayo yameweza kupewa sapoti kubwa na mbunge kuanzia mwanzo na amekuwa mstari wa mbele katika kukuza sekta ya michezo.


Kivumbi cha fainali za  michuanoo hiyo ambayo ilizishirikisha timu 16 za Jimbo la la Kibaha mjini kinatarajiwa kufikia tamati yake Februari 21 mwaka huu katika viwanja vya mwendapole ambapo itazikutanishw timu ya Umwerani watamenyana na Chestmocker.

QATAR CHARITY YATOA MSAADA TANI 90 KWA WANANCHI WA HANANG'

 

Na Mwandishi Wetu.

Ubalozi wa Qatar Tanzania kwa kushirikiana na Tasisi ya Qatar Charity, kwa niaba ya Serikali ya Qatar, imewasilisha misaada muhimu ya kibinadamu kwa waathirika wa Maporomoko ya Udongo yaliyotokea Hanang mkoani Manyara. 

Shehena ya misaada hiyo iliyotolewa leo tarehe 18 Februari 2024 kwa kutumia ndege mbili za mizigo kutoka Qatar inalenga kugusa maisha ya wananchi wa Hanang walioathirika na maafa hayo ambayo madhara yake yalikuwa makubwa. 

Serikali ya Qatar imetoa kwa ukarimu misaada hiyo ya kibinadamu inayojumuisha chakula kikavu katika vifungashio 1,440 (Dry food basket), chakula kilicho tayari kuliwa katika vifungashio 3,024 (Ready to Eat canned food) na vifaa vya usafi wa wanawake jumla 4,200 (women’s dignity kit) na hivyo kufanya jumla ya tani 90 za shehena. 

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amesema kuwa Serikali imepokea kwa moyo wa upendo misaada hiyo itakayoleta faraja kwa Waathirika na kuahidi kufikishwa kwa Walengwa kama ilivyokusudiwa. 

Vilevile Mhe. Nderiananga ameeleza kuwa Serikali inatambua mchango wa wadau wote ikiwemo wananchi, sekta binafsi, asasi za kiraia na kidini, mashirika ya kimataifa na umoja wa mataifa kwa ushiriki wao katika kusaidia wananchi walioathirika na maporomoko ya tope katika wilaya ya Hanang' 

Akipokea Misaada hiyo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Queen Cuthbert Sendiga ameishukuru Serikali ya Qatar kupitia Qatar Charity kwa misaada hiyo ya kibinadamu ambayo itakwenda kuwasaidia wananchi wa Hanang kurejea kwenye hali yao ya Kawaida.

Aidha, Mhe Mkuu wa Mkoa amesema kuwa kupatikana kwa Misaada hiyo ni matokeo ya mahusiano mazuri ya nchi ya Tanzania na nchi za jirani ambayo yameimarishwa na serikali ya awamu ya sita Chini Rais  Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ndege ya mizigo iliyosheheni misaada hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Manyara akishuka kwenye ndege hiyo mara baada ya kufanya makabidhiano ya msaada.
Viongozi waliohudhuria hafla hiyo fupi iliyofanyika katika uwanja wa ndege wa KIA.