ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 8, 2010

SAMAKI MKUNJE ANGALI MCHANGA'

SHULE YA WATOTO WADOGO (CHEKECHEA) HUKO UMASAINI KANDA YA KASKAZINI, SHULE IKIPATIKANAINA KIJIJI KWETU.

VITA DHIDI YA VIFO VYA AKINA MAMA NA WATOTO WAKATI WA KUJIFUNGUA.

NI MKAKATI WA KUPIGANA VITA KUPINGA VIFO DHIDI YA AKINA MAMA NA WATOTO WAKATI WA KUJIFUNGUA. TUKIO LA UELIMISHAJI, UPASHAJI HABARI NA UCHANGIAJI VIFAA LILIFANYIKA LEO PALE KITUO CHA KLINIKI NYAMAGANA MKOANI MWANZA.

MPANGO HUU UNASAFIRI KATIKA NCHI ZA KENYA, TANZANIA NA RWANDA, KABLA YA KUHUDHURIA MKUTANO WA AFRICAN UNION SUMMIT UTAKAO FANYIKA UGANDA AMBAPO WAKUU MBALIMBALI WA MASHIRIKA YA AFYA DUNIANI NA VIONGOZI WA NCHI WATADHURU KUJADILI MPANGO KABAMBE WA KUDHIBITI VIFO VYA AKINAMAMA NA WATOTO WAKATI WA KUJIFUNGUA.

SHUHUDA MAMA 'PAULINA SAMSON' (MWENYE WATOTO SABA) ALIKUWA AKIPATA PRESHA WAKATI WA UJAUZITO NA KIPINDI CHA KUJIFUNGUA. ALIKUWA HANA UTARATIBU WA KUHUDHURIA KLINIKI KUPIMA AFYA NA KUPATA USHAURI LAKINI MARA BAADA YA KUANZA KUHUDHURIA , ANA AFYA BORA NA AMEPATA ELIMU YA UZAZI WA MPANGO.

MAMA MREJUNA, MAMA MWENYE WATOTO WANNE AMEKUWA AKITUMIA KANUNI NA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO BAADA YA KUPATA ELIMU, SASA AMEFUNGA UZAZI NA MAISHA YANAENDELEA VIZURI RAHA MUSTAREHE. HIVYO ANAWASHAURI AKINAMAMA WENZAKE WENYE IMANI POTOFU JUU YA HUDUMA YA KUFUNGA UZAZI , KUJIUNGA NA HUDUMA HIYO KWANI HAINA MADHARA KIAFYA KAMA WENGI WANAVYODHANI.

MGANGA MKUU WA MKOA WA MWANZA AKIPIGA SAINI KUPINGA VIFO DHIDI YA AKINA MAMA NA WATOTO WAKATI WA KUJIFUNGUA.

WANANCHI WALIOGUSWA NA KAMPENI HIYO.

DR NA MANESI.

SEHEMU YETU KWA WALE WA SAINI ZA DOLE GUMBA.

Wednesday, July 7, 2010

"JAMANI BULAH! BULAAAAAAA! ON THE 1N'2."

KUTOKANA NA UFANISI WAKE KATIKA KAZI, UTENDAJI MAHIRI USIO NA MASIKHARA, UPIGAJI NGOMA KALIKALI ZA SASA HATA ZA ZAMANI TOKA MATAIFA YOTE, JAMAA AMEKUWA AKIPATA MIALIKO HAPA NCHINI ILE MBAYA......................................................... ............................................................................................................... HUYU NI DJ BULAH WA CLOUDS FM!
BIG UP!

HAPA NA KULE.

MDAU WA BLOG HII MM0JA ALINIOMBA NIMPATIE PIC ZA JAPO NYUMBA AU MAZINGIRA YA MIANZINI ARUSHA, CHUKUWA HII INGAWA SIKUWEZA KUINASA FRESH KUTOKANA NA SPEED YA GARI.

ENEO LA PEMBENI KUPANDISHA SANAWARI MJINI ARUSHA.

KWA NINI MKOA WA ARUSHA ULINYANG'ANYWA HADHI YA JIJI!? WAKATI NIKIWA NA HILO KICHWANI, NIMESHUHUDIA KATIKATI YA MJI BARABARA NYINGI MBOVU, DUH! NA VIKAO VYOTE VILE MJENGONI!? . KIUKWELI SUALA LA MIUNDO MBINU NALIONA LIPO VINYWANI MWA WATAWALA WETU NA SIYO KATIKA UTEKELEZAJI.

WAKATI JIJI LA MWANZA LIKITUNUKIWA TUZO YA 5 MFULULIZO KATIKA SUALA LA USAFI MIJI MINGINE NCHINI TANZANIA KWA KWASI INALIENDELEZA SUALA LA USAFI. PICHANI BUSTANI INAYOPENDZESHA MANDARI MJI WA MOSHI, MKOANI KILIMANJARO. MEKUU.. MWAMBIE MASAWEE MAMBO YOTE TAREHE 10 'LA LIGA' FIESTA.

WANANCHI KATIKA UTAFUTAJI SEHEMU FULANI TANZANIA.

Tuesday, July 6, 2010

FIESTA jipanguse ..2010 MWANZA ndiyo MWISHO.

JIJI LA MWANZA MAHALA AMBAPO WAKAZI WAKE WAMEPEWA DHAMANA YA KUHITIMISHA MAADHIMISHO YA FIESTA 2010.

*FIESTA 2010*
Tamasha la kumi la burudani na michezo na sanaa nchini Tanzania, linalojulikana zaidi kwa jina la Fiesta limewadia, msimu unaanza tarehe 7 mwezi Julai ambapo utakuwa ni msisimko wa burudani kwa mwezi mzima, huku wasanii wakitembelea baadhi ya mikoa ya Tanzania yenye msisimko wa sanaa kujumuika na mashabiki wa sanaa, na kuonesha kazi zao.

Kwa mwaka huu wa 2010, Fiesta imepewa msemo wa Jipanguse, ikiwa na mlengo wa kuhamasisha vijana, kuachana na tabia ya kulalamika kuhusiana na matatizo wanayokutana nayo katika maisha yao ya kila siku, na badala yake wachukulie matatizo hayo kama ni sawa na kuanguka, wajipanguse na kuendelea na safari ya maisha..

Kauli mbiu hii inamsisitiza kijana wa kitanzania kuachana na habari za kuhubiri matatizo yake huku akiomba msaada wa kuyatatua wakati akitumainiwa kama mjenzi wa Taifa, kupitia burudani kijana anaelimishwa kuhubiri jinsi ya kuutumia ujana wake kukabiliana na ugumu wa Taifa akiwa kama nguzo ya Taifa.


Mikoa nane ya Tanzania itajipangusa kiburudani na tamasha hili ambalo hufanyika mara moja tu kila mwaka huku mwaka huu mikoa ya Arusha na Moshi ikitarajia kupata ugenni kutoka Burundi ambapo mwanamuziki anayesifika kwa tungo za mahaba mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya, anayejulikana kwa jina la Kidumu, anatarajiwa kufanya maonesho mawili makali na kulipa tamasha hili mtazamo mtofauti mwaka huu.

Katika kuanzia, tarehe 7.07.2010 katika viwanja vya Jamhuri mjini Morogoro, kuanzia saa nne asubuhi patakuwa na mambo, yakiwemo yale ya mbio za mikokoteni, kukimbia na magunia, mbio za baiskeli za walemavu na za kawaida na baada ya hapo, wanamuziki mahiri wanaoiendesha fani ya muziki wa kizazi kipya nchini watatarajiwa kupanda jukwaani kuonesha sanaa yao kwa mashabiki wa muziki wa mkoa huo.

Hii itakuwa ni kabla ya kuelekea katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambapo matamasha ya mikoa hii yatafanyika tarehe 9 na 10.

Tamasha hilo litazunguka katika mikoa 8 ambayo ni Morogoro, Arusha, Moshi, Dodoma, Tanga, Dar es Salaam, Zanzibar, Musoma na Mwanza.

Ratiba kamili inasema, baada ya Morogoro tarehe 7, tarehe 9 ni Matongee Club Arusha na tarehe 10, kazi itakuwa mkoani Kilimanjaro, wilaya ya Moshi katika ukumbi wa La Liga.

Baada ya hapo Ijumaa ya tarehe 16 Julai, kazi itakuwa Royal Village ambapo wasanii hawa watafanya onesho kali la usiku na kisha kesho yake, yaani mchana wa tarehe 17 Julai, uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma tamasha litafanyika kwa ajili ya familia.

Tarehe 24 Julai, safari ya kuelekea mkoani Tanga uwanja wa mkwakwani na kama ilivyokuwa katika ufunguzi, mashindano mbali mbali, na kisha burudani kwa wakazi wa mkoa wa Tanga.

Mwisho wa mwezi sasa, ndipo tamasha kubwa kwa ajili ya mji mkubwa, huku msanii wa kimataifa na uwakilishi wa kutosha wa Afrika Mashariki utaonekana. Jiji la Dar es Salaam na vitogoji vywake litajipangusa na kuwa safi na kisha litajitupa katika ama Viwanja vya Leaders au vya Posta Kijitonyama, mtafahamishwa zaidi kuhusiana na hili kadri tunavyoendelea.

Baada ya hapo safari ya kuelekea visiwani Zanzibar itaanza na huko burudani itaangushwa pembezoni mwa bustani ya Forodhani, ndani ya ukumbi wa Ngome Kongwe. Wakazi wa Zanzibar wataipata burudani hii kwa masaa yasiyozidi saba, na kisha wasanii watarudi Dar es Salaam kujiandaa na safari ya Musoma.

Huko Tamasha litafanyika Musoma Hotel siku ya Ijumaa ya tarehe 6, na msanii mwenyeji wa huko atakuwa ni Beatrice Moses, mwana Hip Hop ambaye ni zao la shindano la Bongo Star Search 2009.

Tamasha litafungwa mkoani Mwanza, ambapo tarehe 7 mwezi wa nane, ndani ya ukumbi wa Yatch, kutakuwa na patashika nguo kuchanika, na kisha kujipangusa na burudani hii ya muziki, na siiku inayofuata, kazi itamalizikia CCM kirumba ambapo mashindano ya michezo na burudani ya muziki vitaunguruma.

Tamasha la mwaka huu linakuja likiwa na wasanii wapatao 30 ambao ni Diamond, Belle 9, Hussein Machozi, Baby J, Offside Trick, Chege& Temba, Shaa, Juma Nature, Dully Sykes, Barnaba, Amini, Linah, Godzilla, Joh Makini, Roma, Kiki Wa Pili, Young Dee, Fid Q, Mwana Fa, Mataaluma, JCB, Tip Top, Mwasiti, Pina na Beatrice.

Fiesta Jipanguse ya 2010, inakujia kwa hisani kubwa ya Serengeti Breweries Limited, Precision Air, Prime Time Promotions, Kitangoma Magazine, Mradi wa kuzuia Malaria wa Zinduka, na Clouds FM.

Monday, July 5, 2010

PATI LA KUFUFUKA MTU LAFUATA MARA BAADA YA HARUSI YA Q.

MARA BAADA YA NDOA TAKATIFU KTK KANISA LA ANGLICAN NYAMANORO JIJINI MWANZA, SHEREHE YA KUKATA NA SHOKA NDIYO ILOFUATA NAYO ILIFANYIKA UKUMBI WA BOT PASIANSI.

ALIYE NA MACHO AAMBIWI TAZAMA, ILA USITIZAME SAAAAAAANA USIJE UKAZAMA.

Rrrrrraaah! MAHARUSI WAKIIADHIBU KEKI IKIYOUMBWA DIZAINI KAMA KINANDA HIVI.

NILISHE NIKULISHE.

MIMINA MIMINA! SASA NI WAKATI WA SHAMPEIN.

NASAHA TOKA KWA MAMA WA BI HARUSI.

NASAHA TOKA KWA BABA WA BWANA HARUSI.

CHEKSHIA' KULIA MTANGAZAJI MAHIRI TOKA RADIO FREE AFRIKA 'MAMAA RAHABU FRED' (SHEM) AKIWA NA SHOSTIAKE.

NIMEONA MWANGA.

MKALI NANI? SI KATIKA HIP HOP PEKEE BALI HATA TWISTI. EH BANA q. KUMBE ANAYAWEZA HAYA MAGOMAMOTOMOTO. TEHEEE!

MUZIKI MUZIKIIII!! MIE NA BI HARUSI AKA SHEM. NAFASI KAMA HIZI NI KWA RUKSA MAALUM, TENA UNAPEWA NA RISITI. ALAA!.

MPAKA ASUBUHI - MUZIKI NA BURUDANIZ KWA WOTE BILA MALIPO.

NI KUBANJUKA NA SUTUMUKA.

AFRIKA DAY NDANI YA JAPAN NYUMBANI KWA HIROSHI.

Jioni ya J2(jana) Mjapani mmoja mwenye mapenzi makubwa na waafrika aliwaalika nyumbani kwake. Huyu ni Hiroshi Ikeuchi ambaye anazifahamu sana nchi za Afrika ya Mashariki, mtaa kwa mtaa.

Kwahakika ilikuwa hafla nzuri sana iliyowajumuisha washiriki kutoka mataifa ya Tanzania, Uganda, Botswana na zambia na karibu wote walikuwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali vikuu hapa Japani isipokuwa wachache kama mirindimo...

wananchi walikuwa bize kwenye chakula...

sijui nianzie wapi? (Mirindimo)Wacha nishughulike na hiki kwanza....hai tebo...

Ilikuwa jioni njema watu walikunywa , kula na kuzungumza na kubadilishana taarifa .

Shibe inapunguzwa kwa tizi, baada ya shibe mazoezi ya Kung-fu. Rafiki kutoka Botswana akifuata maelekezo ya mwalimu Hiroshi. Nyuma yake ni jamaa kutoka Zambia.
PICHA NA TAARIFA AMENITUMIA MIRINDIMO.

Sunday, July 4, 2010

HARUSI YA Q. LIVE KANISANI ASUBUHI YA LEO.

NYUSO ZA FURAHA DUNIANI HIZI HAPA.
eeeh bana dah! MWENYE WIVU ASITULETEE MAMBO YA AJABU, PLIZZ - AJIPANGUSEEEE'''''' Rrrrrraaah!

MCHUNGAJI WA KANISA LA ANGLICAN NYAMANORO MWANZA, REV. NESTORY MUHETA AKIENDESHA IBADA YA NDOA HIYO.

MAHARUSI WAKILISHWA NENO.

BWANA HARUSI NICOLOUS OWITTI (Q) AKIMVISHA PETE BI. SONIA IBRAHIM.

NAE BI HARUSI AKIKAMILISHA HILOO.. JAMBO JEMA KWA BWANA HARUSI.

SASA SI WAWILI TENA, BALI NI MWILI MMOJA!! KWAYA YA NYAMANORO IKITUMBUIZA WIMBO MAALUM KWA MAHARUSI.

MAHARUSI NA WAPAMBE WAKITOKA KANISANI.

Rrrrrrraaah! MIE NA MAHARUSI.

MAMA MO RECORDS (KUSHOTO) KATIKATI MAHARUSI NA KULIA KABISA AMESIMAMA MDOGO WAKE BWANA HARUSI.

GARI LA MAFUTA LAANGAMIZA 220 KONGO.

Zaidi ya watu 220 wanahofiwa kufa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Watu hao wameangamia baada ya lori moja lilobeba mafuta kuanguka na kuwaka moto katika kijiji cha Sange, mashariki mwa nchi hiyo.
Inaarifiwa kuwa watu hao walikuwa wakijaribu kuchota mafuta kutoka lori hilo, lilokuwa limepinduka, baada ya dereva wake kushindwa kulidhibiti.
Baadhi ya waliokufa walikuwa wakichota mafuta yaliyokuwa yakivuja, lakini walinaswa ndani ya majengo, ikiwa ni pamoja na ukumbi wa sinema.
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa waliungana katika jitihada za kuokoa waliojeruhiwa.
Walioshuhudia wanasema moto uliangamiza idadi kubwa ya nyumba.


"Watu walijaribu kukimbia, lakini walinaswa na moto huo mkali uliowaangamiza na kuwa majivu," Tondo Sahizira, 28, alilieleza shirika la habari la AFP.
Ajali hiyo ilitokea Ijumaa jioni eneo la Sange, yapata kilometa 70 kusini mwa mji wa Bukavu, Kivu Kusini.
Gari hilo lililokuwa likisafiri kutoka Tanzania, lilipinduka na mafuta kuanza kuvuja.
"Mafuta yalianza kuvuja, lakini badala ya watu kukimbia, walianza kuchota mafutal," alisema Bw Sahizira.
"Dakika chache baadaye kulikuwa na mlipuko, miale ya moto ilifumuka na kusambaa kwa kasi."
Nyumba kadhaa zilizoezekwa nyasi ziliwaka moto, vile vile ukumbi uliokuwa ukitumika kuonyesha mechi za Kombe la Dunia.
Madnodje Mounoubai, msemaji wa jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa, alisema idadi ya vifo huenda ikaongezeka.

HABARI KWA HISANI YA BBC Swahili.

HARUSI YA Q. MWENZAKO TAYARI NINA CARD.

PRODUCER Q. WA MO.RECORDS, LEO NDO SIKU YAKE ANAFUNGA NDOA.
JINA LA LAKE KAMILI NI NICOLAUS OWITTI NA MKEWE MTARAJIWA ANAITWA SONIA IBRAHIM.
TAFATHALI FIKA NA KADI HII..