Friday, October 18, 2024
WAHUDUMU WA AFYA KIBAHA MJI WAFANIKIWA KUIBUA WAGONJWA WAPYA 113
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
HARMONIZE ATOBOA SIRI MAHABA YAKE NA KAJALA -USIKU WA BURUDANI SIKU YA MWALIMU DUNIANI BUKOMBE
NA ALBERT GSENGO / BUKOMBE
HATIFUNGANI YA KIJANI YA TANGA UWASA YAORODHESHWA LUXEMBOURG.
Rasmi, Hatifungani ya Kijani ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) yaorodheshwa katika Soko la Hisa la nchini Luxembourg.
Thursday, October 17, 2024
Wednesday, October 16, 2024
RAIS RUTO KUMTEUWA MAKAMU WA RAIS MPYA IWAPO SENETI ITAIDHINISHA KUBANDULIWA KWA GACHAGUA
Rais William Ruto anatarajiwa kumteua naibu rais mpya iwapo Bunge la Seneti litaendelea na hatua ya kumtimua Rigathi Gachagua. Picha: Rigathi Gachagua/William Ruto.
Kuondolewa kwa Rigathi Gachagua ofisini kutakuwa ni tukio la kihistoria, kwani itakuwa mara ya kwanza kwa naibu rais aliye madarakani kukabiliwa na mashtaka ya kutokuwa na imani naye katika historia ya Kenya.
Tumaini la mwisho la Gachagua kuokoa wadhifa wake ni nini? Hatima ya Naibu Rais sasa iko mashakani huku Seneti ikitarajiwa kuanza kujadili mashtaka yake Jumatano, Oktoba 16, na uamuzi wa mwisho ukitarajiwa kufanywa Alhamisi jioni, Oktoba 17.
Matokeo ya mchakato wa kuondolewa kwake yanategemea ikiwa theluthi mbili ya maseneta watapiga kura kumuondoa ofisini.
Akizungumza na NTV, Wakili wa Mahakama Kuu Steve Ogolla alisema kuwa hatima ya Gachagua sasa iko mikononi mwa Seneti, kufuatia mahakama kukataa kusimamisha Seneti kuendelea na mjadala wa mashtaka ya kutokuwa na imani naye.
"Hii ilikuwa nafasi yake ya mwisho kusimamisha mchakato huu na hakufanikiwa. Ukweli ni kwamba hatima yake sasa iko mikononi mwa Seneti. Lakini, naamini pia amejiandaa kwa Seneti, tumeona amewasilisha majibu yake kwa hoja hiyo," Ogolla alisema.
Ni nini kitafuata ikiwa Gachagua ataondolewa na Seneti? Kuondolewa kwa Gachagua kutoka ofisini kunaweza kuacha pengo kubwa ndani ya serikali ya Kenya Kwanza, na kumlazimu mkuu wa nchi kuteua naibu rais mpya kufikia Ijumaa, Oktoba 18. "Kinachoweza kutokea baada ya kuondolewa ni kwamba rais anaweza kuteua mrithi wa Gachagua haraka.
Lakini kifungu cha 149 bado kinahitaji kuwa mgombea huyo apitishwe na Bunge la Kitaifa ndani ya muda wa siku 60, lakini wanaweza kufanya hivyo haraka," Ogolla aliongeza.
UANDIKISHAJI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA WAFIKIA 45% NCHINI - WAZIRI MCHENGERWA
Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana Oktoba 15, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza kwa lengo la kufikisha elimu na hamasa kwa Wananchi juu ya umuhimu wa kujiandikisha.
Mhe. Mchengerwa amewataka wananchi wenye sifa na wanaokidhi vigezo vya kugombea wajitokeze kuchukua fomu kuanzia Oktoba 26, 2024 mpaka Novemba 1, 2024 ili waweze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa serikali za Mitaa na Vijiji.
Vilele Waziri Mchengerwa amewataka wasimamizi wa uchaguzi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, kanuni, miongozo pamoja na maelekezo ya usimamizi wa uchaguzi.
"Maelekezo yangu kwa wasimamizi wa uchaguzi kuzingatia kanuni viapo na kutekeleza majukumu kwa mujibu wa viapo vyao". Amesisitiza Mhe. Mchengerwa.
Aidha Mhe. Mchengerwa amewataka Viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa kutoa elimu kwa wanachama wao juu ya kujiandikisha na kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Zoezi la kujiandikisha katika daftari la makazi limeanza rasmi Oktoba 11, 2024 mpaka Oktoba 20, 2024 ambapo kila Mwananchi mwenye sifa na vigezo anatakiwa kujiandikisha katika eneo analoishi ili aweze kushiriki zoezi la Uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Tuesday, October 15, 2024
MAFIA BOXING PROMOTION WAUNGA MKONO KAMPENI YA RAIS DKT SAMIA SULUHU YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA
Monday, October 14, 2024
RAIS SAMIA APOKEA MWENGE WA UHURU KWENYE KILELE CHA MAADHIMISHO MBIO ZA MWENGE WA UHURU MWANZA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wakati akihitimisha Kilele cha Mbio za Mwenge ambazo kitaifa zimefanyika Jijini Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba tarehe 14 Oktoba, 2024. |
"Nimehitimisha Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru pamoja na Wiki ya Vijana hapa mkoani Mwanza. Ninawashukuru wote waliojitokeza kushiriki tukio hili la kihistoria ambapo Mbio za Mwenge wa Uhuru zimefikisha miaka 60."
"Pongezi kwa wote walioshiriki kuukimbiza kwa mwaka huu na kazi nzuri waliyofanya ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo"
"Nimepokea taarifa ya miradi yote iliyotembelewa katika mbio hizi ambayo inakwenda kunufaisha wananchi kwenye kila kona ya nchi yetu. Nimepokea mapendekezo na salamu za wananchi wa maeneo yote ulikopita Mwenge wa Uhuru, na kwa umakini na uharaka tutayafanyia kazi yale yote yaliyoainishwa kwa manufaa ya Taifa letu"
RAIS wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 14, 2024 amewaongoza Viongozi na Wananchi mbalimbali kwenye kilele cha mbio za Mwenge zilizoambatana na Wiki ya Vijana na Nyerere Day katika uwanja CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Rais Samia akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kiongozi wa mbio hizo Ndugu Godfrey Eliakim Mzava kwenye Kilele cha Maadhimisho Mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. |
Matukio mbalimbali katika kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. |