SERIKALI mkoani Mwanza, imewataka wananchi kuchukua tahadhali kuhusiana na tishio la ugonjwa wa Ebola ambao umeripotiwa kuuwa watu kadhaa nchi jirani ya Uganda.
Tahadhali hiyo ilitolewa jana na
Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Mhandisi Evarist Ndikilo, alipozungumza waandishi wa habari kuhusuiana na ugonjwa huo.
Alisema serikali ya mkoa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepanga mikakati ya kukabiliana na tishio la ugonjwa huo hatari unaouwa kwa haraka.
“Ukiangalia jiji letu la Mwanza lina mwingiliano mkubwa kutokana na kuwa kitovu cha biashara kwa nchi za Maziwa Makuu, hivyo wananchi wanapaswa kuchukua tahadhali kwa kujikinga na kutoa taarifa pindi wanapomwona mtu mwenye dalili za ugonjwa huo,”alisema Ndikilo
Alisema shirika la Afya Duniani (WHO) tayari limethibitisha kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda, katika Wilaya ya Kibule, Magharibi mwa nchi hiyo ambapo watu 26 wameriptiwa kuambukizwa na kati yao 14 wamefariki dunia kwa kuambukizwa ugonjwa huo tangu Julai 28, mwaka huu.
Mhandisi Ndikilo, alieleza kuwa ugonjwa huo huambukiza kwa kugusana na mtu mwenye kuathiriwa na virusi vya Ebola ambavyo hutokana na sokwe pamoja na jamii ya wanyama aina hiyo, ambapo kwa mara ya kwanza ulibainika kuwapo 1976.
Dalili za ugonjwa huo ni homa kali ya ghafla,vidonda vya koo, upele katika ngozi na kutokwa damu sehemu mbalimbali za mwili na katika kukabiliana na maambukizi Ebola, wataalamu wa wizara ya Afya ambao tayari wapo jijini hapa, watafanya ukaguzi kwa wageni waingiao nchni kupitia njia ya anga, majini na nchi kavu bila usumbufu.
“Hatua za kuchukua ni kuongeza kasi ya ufuatiliaji, kufanya ukaguzi bila usumbufu kwa wageni wanaosafiri kwa ndege, meli na mabasi kuingia nchini, kutoa elimu kwa wananchi na watumishi wa afya na upatikanaji wa vifaa vya kinga;”alisema
Alisema ili kuwalinda wananchi, vipeperushi na vijarida vinavyohusu ugonjwa huo wa Ebola vitasambazwa ili wananchi wapate ufahamu wa dalili zake lakini pia wawe tayari kutoa taarifa pndi wanapomhisi mtu mwenye dalili za gonjwa huo.
“Pamoja na juhudi za serikali, kupitia vyombo vya habari eneo la mikoa ya Kanda ya Ziwa tuchukue tahadhali kuhakikisha wananchi wanafahamu tatizo hili kwa kusoma vipeperushi na kupashana habari,”alisema Mkuu huyo wa mkoa
Tayari watu 14 wamefariki dunia katka wilaya ya Kibule Magharibi mwa nchi ya Uganda tangu kuzuka kwa ugonjwa huo Julai 28 mwaka huu.
Mwaka jana mtu mmoja aliliripotiwa kufa nchini humo kutokana na kuambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ebola.
Mbali na Uganda, miaka kadhaa iliyopita Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) iliwahi kukumbwa na ugonjwa huo na watu kadhaa kuripotiwa kufa.
TASAF YAJENGA STENDI YA MABASI LUNDUSI KUMALIZA CHANGAMOTO YA USAFIRI KWA
WANANCHI
-
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Songea
MRADI wa Ujenzi wa Stendi ya mabasi unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii(TASAF) katika Kijiji cha Lundusi wil...
57 minutes ago