JANA Dk Mwakyebe alipiga marufuku
suala la kuchimba dawa safarini na hasa wale wasafirio na mabasi yaendayo
mikoani ambapo mabasi husimama pori na kuwaruhusu watu kwenda kujisaidi
maarufu kwajina la kuchimba dawa.
Utamaduni huo umeota mizizi katika
barabara zote kuu iwe Dar Lindi Mtwara, Dar Iringa Mbeya Tunduma, Dar Iringa
Songea, Dar Mwanza na kwingineko nchini.
Akiongea wakati akijibu hoja za
wabunge wakati wa kuhitimisha mjadala kwa wizara yake Dk Mwakyembe amesema basi
lolote litakalokamatwa limesimama porini kwa ajili ya kuchimba dawa, kosa la
kwanza atapewa onyo, la pili atapigwa faini kubwa na la tatu atafungiwa
akatafute/ akafanye biashara nyingine.
Kauli hi imekuja wakati tukijua kwamba
njia zote kuu za barabara ziendazo mikoni hakuna vituo maalum vya kupumzika abiria
na kuchimba dawa na hata kama vipo hakuna vyoo na au vyoo havitoshi au havina
usafi wa kutosha ukiacha vile vilivyopo kwenye mahoteli ya njiani.
Wadau hii imekaje... kipi
kingeanza kupiga marufuku kusimamisha mabasi njiani au kungeanza mradi wa
kujenga vyoo kwenye maeneo yale maarufu kwa kuchimba dawa?
Mwalimu Msungu
Majibu :-
@Mwezi uliopita nimesafiri kwa basi kutoka Dar hadi Tanga, Tanga hadi Arusha, Arusha hadi Dar, Dar hadi Songea, na Songea hadi Dar. Haiwezekani kufanya safari yoyote ya aina hiyo bila kuchimba dawa, na sisi wengine tunahitaji hata mara mbili au zaidi.
Napinga kabisa, na kwa nguvu zote uamuzi huu wa Mheshimiwa Mwakyembe. Nitakubaliana naye tu iwapo sehemu za kuhudumia wasafiri zitakuwa tayari zimejengwa, kama ilivyo sehemu kama Marekani. Mheshimiwa Mwakyembe ashinikizwe kutengua amri yake hiyo leo hii.
Joseph L. Mbele
@Nini vipaumbele vya wizara yake Mwakyembe? Suala la uchimbaji dawa kwangu mimi binafsi ni la baadae sana na angeliongelea mara tu baada ya kuweka miundo mbinu safi vikiwemo vyoo kwenye vituo kadhaa. Atachanganya mambo!! Suala la kuchimba dawa ni minor sana.
Sent from my BlackBerry
@Mweshimiwa inaonekana dhahiri siku nyingi zaidi ya miaka mingi hajapanda usafiri wa basi zaidi ya hivi majuzi kuakti (kutengeneza picha) picha la mweshimiwa kupanda treni naye akiwa stering wa lile muvi.
Muheshimiwa kazoea kupanda gari binafsi lenye hewa safi na kiyoyozi akijichagulia vyakula vya kula safarini tena hii ni kwa mara moja moja kwa safari ndefu, mara zote yeye ni juu kwa juu na pipa aka ndege,,, sasa sie akina kajamba nani kwenye basi lenye watu zaidi ya 60 kila mtu na tumbo lake na maji yake huyu yamechemshwa yule hayajachemshwa kisha vyakula vya njiani vya bana matumizi, karanga na makande makavu (ngararuu) wafanya mchezo.
Alipaswa kufanya utafiti kwanza na kujua umbali wa kituo na kituo kwani maeneo mengi ni pori na hata ukikuta vijiji vyoo ni vya kaya havikidhi mahitaji ya nyomi ya wasafiri.
Serikali kupitia wizara yake ingetengeneza kwanza utaratibu wa kujenga vyoo kwa utaratibu ule ule wa utafiti kupitia madereva kugundua ni maeneo gani korofi kwa maana kwamba maeneo ambayo abiria wengi husumbua kuchimba dawa kisha katazo likafuata.
Mie mwenyewe huwa nainjoi kuchimba dawa yaaani hata nisipochimba dawa basi nita piga picha basi tulilopanda, miti ya porini nini na nini na nini ...daaaah hakika kwa hili nitamisi sana hako kazoezi. Kwa mpango huu tutajinyea sana safarini.
Mwakyembe kachemka.
Jipange.
g to tha s.
@Interesting discussion. Wasioona adha ya kuchimba dawa ni sisi "wahuni" ambao tomezoea popote tu unasimama unatoa maungo yako na kukojoa au kunanii peupe. Mtu yeyote mstaarabu hawezi kushabikia kukojoa au kupata haja kubwa vichakani!!!! Mwakyembe kwa jinsi nilivyomuelwa hajakataza mabasi kusimama njiani abiria wapate kukojoa, alichosema yeye ni kuwa hayaruhusiwi kusimama porini ambapo kina mama, wazee na watoto wote wanalazimika kupata haja zao mithili ya wanyama. Mnaotetea kuchimba dawa porini naombe mtangaze maslahi yenu kwenye hili isije ikawa ni wapiga nanii!!!!
Du Veda.
@Ni akili kidogo tu inahitajika kwa wenye mabasi. Leo hii Ndenjela Bus inasimama
stendi ya Makambako na kutoa dakika 10 abiria kujisaidia na kunywa chai
wakati wengine wakifukuzana kuwahi pale porini!!!
Felix.
Felix.
@Hapa dokta naye kaenda mbali, sasa kuchimba dawa na wizara yake wapi na wapi?
Nilidhani hoja hii angeitoa daktali mwenzake Telezia wa Makamu wa Rais!!
Labda angesema mabasi yawe na vyoo ndani kwani ni jambo lisilowezekana mtu
kupanda basi Dar kwenda Mtwara ujisaidie Nangurukuru ndiyo kwenye vyoo urefu
wa kilomita zaidi ya 200!!!
Wa Simbeye. |
Tupe maoni yako
swali langu moja tu ,je atakaeshikwa na tumbo la kuharisha itakuaje ?
ReplyDelete