ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 2, 2016

RATIBA YA EPL JUMAMOSI HII NA JUMAPILI.

Jumamosi 2 Aprili (Saa za Afrika Mashariki).
  • Aston Villa v Chelsea 14:45
  • Arsenal v Watford 17:00
  • Bournemouth v Man City 17:00
  • Norwich v Newcastle 17:00
  • Stoke v Swansea 17:00
  • Sunderland v West Brom 17:00
  • West Ham v Crystal Palace 17:00
  • Liverpool v Tottenham 19:30
Jumapili 3 Aprili
  • Leicester v Southampton 15:30
  • Man Utd v Everton 18:00

NAIBU WAZIRI WA AFYA, DK KIGWANGALLA AZINDUA RASMI JENGO JIPYA LA T-MARC TANZANIA

Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa: 
Taasisi isiyo ya kiserikali T-MARC Tanzania imezindua rasmi jengo lake jipya pamoja na ghala maalum la kisasa litakalotumika kuhifadhia bidhaa zao ikiwemo zile za mipira ya kiume na kike kupitia bidhaa zao za DUME.

Tukio hilo limefanyika rasmi mapema jana Aprili 1.2016, ambapo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla alikuwa mgeni rasmi akiwakilisha Serikali katika tukio hilo kubwa na la kihistoria.

Akizungumza na wanahabari, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, Serikali inapongeza juhudi za Taasisi za watu binafi ikiwemo T-MARC Tanzania wanavyofanya juhudi kubwa hapa nchini katika kuwafikia wananchi kupitia bidhaa zao hizo za kinga.

Dk. Kigwangalla amewapongeza kwa hatua hiyo tokea walipoanza hapa nchini kuanzia mradi hadi taasisi ambapo kwa hatua yao hiyo pia imesaidia na mapambano ya virusi vya UKIMWI kwani kupitia bidhaa zao hizo za kondomu kupitia kondomu za DUME zimekuwa msaada mkubwa sana kazi hizo wanazofanya wanaisaidia Serikali kwa kiwango kikubwa sana.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania, Bi.Diana Kisaka alishukuru Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na taassi hiyo kwani imeweza kutimiza malengo yake hapa nchini na itaendelea kushirikiana na Serikali bega kwa bega kwa kipindi chote.

Aidha, aliongeza kuwa, wataendelea kutoa huduma bora hiyo ya kinga kupitia bidhaa zao za mipira ya kinga yaani kondomu za DUME ilikuzuia mapambano ya virusi vya UKIMWI hapa nchini.

Awali Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kukagua mabanda ya maonyesho ya miradi mbalimbali ya taasisi hiyo na kupata maelezo ya kwa kina kisha alipata wasaha wa kufungua rasmi jengo hilo la kisasa ambalo ni la ofisi za taasisi hiyo pamoja na kuzindua ghala maalum la kuhifadhia bidhaa hizo za DUME Condom.
DSC_8863
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akisalimiana na Mjumbe wa bodi ya T-MARC Tanzania, Bi Joyce Mhavile wakati wa kuwasili katika eneo la tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la kisasa la makao makuu ya T-MARC Tanzania yaliyopo Jijini Dar es Salaam.
DSC_8871
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akimsikiliza Meneja Mradi wa T-MARC Tanzania, Bi. Halima Mwinyi wakati wa kutembelea miradi ya kwenye mabanda ya maonyesho kwenye tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la kisasa la makao makuu ya T-MARC Tanzania yaliyopo Jijini Dar es Salaam.
DSC_8881
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akimsikiliza afisa wa T-MARC Tanzania, Bi. Sophia Komba wakati wa kutembelea miradi ya kwenye mabanda ya maonyesho kwenye tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la kisasa la makao makuu ya T-MARC Tanzania yaliyopo Jijini Dar es Salaam.
DSC_8930Jengo jipya la T-MARC Tanzania kabla ya uzinduzi huo linavyoonekana
DSC_8933Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akikata utepe kuashiria kulifungua rasmi jengo hilo la kisasa la makao makuu ya T-MARC Tanzania yaliyopo Jijini Dar es Salaam.
DSC_8949
Jiwe la msingi la ufunguzi wa jengo hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea 
DSC_8963
..Dk. Kigwangalla akitembezwa katika maeneo mbalimbali ya jengo hilo..
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea 
DSC_9035
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akifungua kitambaa kuashiria ufunguzi wa jengo la kuhifadhia bidhaa ya taasisi hiyo ghala maalum

DSC_9046
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akiangalia ghala hilo kwa ndani namna lilivyojengwa .
DSC_9019
Dk.Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa taasisi hiyo ya T-MARC Tanzania.
DSC_9026
Dk.Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na wadau na wadhamini wa taasisi hiyo ya T-MARC Tanzania.
DSC_9052
Dk.Kigwangalla akiwasili katika eneo maalum la kutolea hotuba ya tukio hilo.
DSC_9060
Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania, Bi.Diana Kisaka akitoa hotuba fupi ya ufunguzi huo
DSC_9063
Mwanamuziki Barnaba akitoa burudani katika tukio hilo..DSC_9064DSC_9085
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa hutuba katika tukio hilo
DSC_9086
DSC_9098
mjumbe wa bodi, Bw.Alex Mgongolwa akitoa shukrani zake
DSC_9104
Uongozi wa T-MARC Tanzania wakitoa zawadi maalum ya picha ambayo yenye kuonyesha mwanamke akiwa na mtoto katika malezi bora iliyoelezewa kwa njia ya sanaa
DSC_9130
Wadau wakifuatilia tukio hilo
DSC_9110 DSC_9141
Dk. Kigwangalla akipata picha ya pamoja na wadau katika tukio hilo
DSC_9157
Baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya T-MARC Tanzania wakifurahia katika tukio hilo
DSC_9128Bi. Teddy Mapunda akijadiliana jambo na Katibu wa Naibu Waziri wa Afya Bw. Kulwa.DSC_9168Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akiagana na Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania, Bi.Diana Kisaka wakati akiondoka katika eneo la tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la kisasa la makao makuu ya T-MARC Tanzania yaliyopo Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

MAGAZETI LEO> MAGUFULI AJINYIMA MSHAHARA WA JK, AJILIPA MILIONI 9.5 BADALA YA MILIONI 34, BEI YA UMEME YASHUKA, CUF KUMREJESHA LIPUMBA.


Magufuli ajinyima mshahara wa JK, ajilipa milioni 9.5 badala ya mil.34. Kitilya, wenzake wawili kortini. Bei ya umeme yashuka.

 Kamishna mkuu TRA mahakamani akidaiwa kutakatisha trilioni 1.3. CUF kumrejesha profesa Lipumba. Bunge lazidi kuchafuka.

Friday, April 1, 2016

HII NDIYO KALI YA KISPORT ILIYOVUNJA REKODI SIKUKUU YA WAJINGA.

Renewed hope for Nigeria, Tanzania as Chad rescind decision to withdraw from Afcon qualifiers

Goal.com 10 hours ago 

KUHUSISHWA UBADHILIFU WA ZAIDI YA MILIONI 300 WAMSIMAMISHA KAZI MHANDISI WA JIJI LA MWANZA.


NA PETER FABIAN, MWANZA.

HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza kupitia Kamati yake ya Uongozi na Fedha imemsimamisha kazi Mhandisi wa jiji hilo, Ezekiel Kunyalanyala, kwa tuhuma za kushindwa kusimamia vyema matumizi ya zaidi ya sh ml 300 fedha za miradi ya maendeleo zilizotolewa kwa matengenezo ya dharula.

Miradi hiyo ni ya kukarabatiwa jengo la machinjio ya jiji yaliyopo eneo la Nyakato Kata ya Mhandu, daraja la Mwananchi lililopo Kata ya Mahina, mitaro ya barabara za Kata za Mhandu, Mkuyuni na ukarabati wa Kituo cha kulelea watoto waisho katika mazingira magumu cha zamani kijulikanacho kama Kuleana katika Kata ya Nyamagana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Meya wa jiji la Mwanza, James Bwire, alisema kwamba tayari agizo la Kunyalanyala kusimamishwa kazi limetekelezwa na ameisha kabidhiwa barua yake kutokana na kushindwa kusimamia matumizi ya fedha za miradi hiyo ambayo inaonekana kutekelezwa chini ya kiwango kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa.

Meya huyo alieleza kuwa, Kuleana kilitakiwa kukarabatiwa kwa sh ml 19 kwa ajili ya kutumiwa na Idara ya Ustawi wa Jamii, lakini badala ya ukarabati ulioelekezwa, kimepakwa rangi na kuwekwa milango miwili tu na vitasa.

“Mhandisi huyo ndiye aliyependekeza na kuomba fedha hizo kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho, haiwezekani sh ml 19 ziishie kupaka rangi, chokaa na kutengeneza milango miwili tu, badala ya kukarabati sehemu zilizoelekezwa, huo ni wizi tusioweza kuuvumilia,” alichachamaa Bwire.

Alieleza kuwa, baada ya Kamati ya Fedha na Uongozi chini ya uenyekiti wake mbali na kutembelea kituo hicho pia walitembelea miradi ya Machinjio ya jiji yaliyopo Nyakato, Daraja la Mwananchi na ujenzi wa mitaro ya barabara ya Mhandu, walibaini ujenzi kuwa chini ya kiwango kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa baada ya wataalamu wa  Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuja na kutembelea kabla ya kuidhinisha kwa matengenezo hayo.

“Halmashauri iliomba kujengewa machinjio mpya ya kisasa kupitia mradi wa mazingira wa LVMP II kwa thamani ya sh bl 1.7 kwa sharti la kukarabati jengo moja la stoo ya ngozi katika machinjio hayo ili litumike kama machinjio ya mda, jiji likakubali na kutoa sh ml 150 lakini ukarabati huo pia hauendi vizuri,” alidai.

Alieleza miradi mingine aliyodai na Kamati yake kutoridhishwa na usimamizi wake katika ujenzi wa daraja la Mwananchi (sh ml 110) na ujenzi wa mitaro ya Mhandu (ml 26) hivyo kumuagiza Mkurugenzi wa jiji, Adam Mgoyi amwandikie baraua ya kumsimaisha kazi Mhandisi Kunyalanyala na tayari ameisha kabidhiwa barua ya kusimishwa.

Meya Bwire ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mahina (CCM) wilayani Nyamagana, alimtaja mtumishi mwingine aliyesimaishwa kuwa ni Mwanasheria wa jiji hilo, Maksudi Bwabo kutokana na kulalamikiwa na  wadau (wafanyabiashara) wa jiji hilo wakati wa kukusanya mapato kuwatishia kuwapeleka mahakamani bila kuwapatia nafasi ya kujitetea.

“Mwanasheria huyo anadaiwa kutembea na kutoa Samansi mfukoni kutishia wadau hali ambayo tumeomba akae pembeni “naye kusimamishwa” ili kupisha uchunguzi wa malalamiko ya tuhuma hizo , pia kuwataka watumishi wa Halmashauri hiyo wabadilike na kuacha kufanya kazi kwa mazoea ukizingatia kasi ya serikali ya Dk John Magufuli haina mchezo katika kuwatumikia wananchi.


HIZI HAPA NAFASI ZA MASOMO MWANZA

CHUO KIMESAJILIWA NA   NACTE; NO: ANE/026

SCHOOL OF HOSPITALITY,TOURISM AND AIRLINE MANAGEMENT
 
 





TANGAZO LA KOZI.
(BADO TUNAENDELEA KUPOKEA MAOMBI INTAKE YA MARCH)
MKUU WA CHUO – CHINI YA IDARA YA UONGOZI WA HOTEL, UTALII NA SHUGHULI ZA NDEGE ANATANGAZA NAFASI ZA MASOMO KAMA IFUATAVYO:-

NGAZI YA KOZI:                  BASIC TECHNICIAN CERTIFICATE( NTA- LEVEL 4)
SIFA ZA MWOMBAJI:         WAHITIMU WOTE WA KIDATO CHA 4 (FORM FOUR).
ADA KWA MWAKA:            TSHS. 900,000/= KWA MWAKA (DAY)
HOSTEL:                                TSHS.45, 000/= KWA MWEZI
                                        
UNIFORM:                              TSHS.45, 000/= (ONE PAIR AND LOGO T-SHIRT)
REGISTRATION FORM:     TSHS. 15,000/=
MUDA WA MASOMO:          KUANZIA SAA 2:00 ASUBUHI – 8:00 MCHANA
MUDA WA KOZI:                  MWAKA MMOJA. (MIEZI 9-CLASS.MIEZI 3-PRACTICAL).
ANGALIZO:                            WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE LAZIMA WAANZIE NA NTA LEVEL 4
                                                   ILI WAKUBALIKE KUENDELEA NA DIPLOMA CHUO CHOCHOTE.
                                                      

           KOZI ZINAZOTOLEWA NI:
                  .  HOTEL MANAGEMENT (HOSPITALITY MANAGEMENT)
                  .  FOOD & BEVERAGE SERVICE & SALES
                  .  FOOD PRODUCTION (TOURIST CUISINE)
                  .  HOTEL FRONT OFFICE & RECEPTION OPERATION
                  .  HOTEL ACCOMMODATION OPERATIONS
                  .  INTERNATIONAL TOURISM & TRAVEL SERVICES
                  .  AIRLINE MANAGEMENT (AIRFARE, RESERVATION & TICKETING)
                  .  TOUR OPERATIONS & WILDLIFE GUIDING MANAGEMENT
                  .  INTERNATIONAL CAR RENTAL MANAGEMENT
                  .  INFORMATION COMPUTER TECHNOLOGY (ICT)
                  .  HERITAGE CULTURAL ANTHROPOLOGY MANAGEMENT & TOUR GUIDENCE.
                  .  BUSINESS ADMINISTRATION
                  .   MARKETING & SALES MANAGEMENT
                  .  PROCUREMENT & SUPPLY MANAGEMENT
                  .  BANKING & FINANCIAL SERVICES.

           APPLICATION FORMS ZINAPATIKANA;
           MWANZA        -     CCM MKOA – GHOROFA YA 3 CHUMBA No. 77.
                                             SIMU  No. 0754 301962 AU  0753 – 006367

           BUKOBA         - ELCT – BUKOBA HOTEL.

           N .B:            PIA ZIPO NAFASI ZA KAZI YA KUFUNDISHA. TUMA MAOMBI    HARAKA.

WAHI NAFASI NI CHACHE


KENYA AIRWAYS KUWAFUKUZA KAZI WAFANYAKAZI 600

Wafanyikazi 600 wa Shirika la Ndege la Kenya, Kenya Airways watapoteza kazi zao katika juhudi za kulichepua shirika hilo. Kenya Airways ilitangaza hasara ya dola milioni 270 mwaka uliopita, ikiwa ndio hasara kubwa zaidi kuripotiwa na kampuni nchini Kenya.

Likijulikana kama Fahari ya Afrika, hakuna cha kufurahia tena katika shirika la Ndege la Kenya.
Makali ya hasara yalioripotiwa na kampuni hiyo sasa yameanza kuwalenga wafanyikazi wake ambapo mamia wanatarajiwa kupigwa kalamu.

Kenya Airways pia imesema hatua hiyo ni katika juhudi za kurejesha mabawa yake tena katika safari za ndege barani Afrika.

Watakaoponea kutemwa nje huenda wakajipata katika kazi nyingine ambazo hawakuzoea.
Mamlaka za shirika hilo zinakabiliwa na changamoto ya kurejesha imani kwa wawekezaji na wenye hisa ambao wamelalamikia kwamba huenda shirika la Ndege la Kenya linatumbukia kwenye kaburi la sahau.

Mpango mpya wa kufufua Kenya Airways maarufu kama 'operation pride' unaolenga kuokoa kima cha dola milioni 200, pamoja na kupunguza gharama za kufanyia kazi.

Aidha kampuni niyo itauza baadhi ya ndege zake ambapo imeafikiana mkataba na kampuni ya ndege kutoka Marekani Omni Air International kuuza ndege mbili aina ya Boeing.

JESHI LA POLISI LAONGEZA MUDA WA KUHAKIKI SILAHA SASA ITAKUWA NI MIEZI MITATU KWA NCHI NZIMA

 Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mchakato wa kuhakiki silaha ambapo jeshi hilo limeongeza muda wa miezi mitatu kwa nchi nzima kuanzia leo.
 Msemaji wa Jeshi Nchini, Advera Bukumbi (kulia), akizungumza na wanahabari wakati akimkaribisha  Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya kuzungumza na waandishi.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.



Na Dotto Mwaibale 
JESHI la Polisi nchini limeongeza muda wa miezi mitatu kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi kuhakiki silaha zao kote nchini. 

Hayo yalibainishwa na Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa taarifa kuhusu kufanyika kwa amani uchaguzi wa marudio wa Urais Zanzibar na uhalifu mbalimbali hasa wa makundi ambao unaonesha umeanza kushamiri.

 Kamishna Mssanzya alisema mchakato wa kuhakiki silaha na kuzisajili na kufanya malipo katika mkoa wa Dar es Salaam unaendelea vizuri.

 Akizungumzia vitendo vya uhalifu Mssanzya kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana navyo hasa uhalifu unaofanywa na mtu mmoja mmoja kwani ule wa makundi wamefanikiwa kuudhibiti kwa kiasi kikubwa "Hivi karibuni tumefanikiwa kuwakamata watu katika maeneo mbalimbali wanaojihusisha na uhalifu wa kimakundi ambao bado tunaendelea kuwahoji na kufanyiwa uchunguzi" alisema Mssanzya.

 Alisema watu hao wamewakamata Mafia na kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwafanyia uchunguzi ili waweze kupata taarifa mbalimbali ambazo zitasaidia kuweza kuwatia nguvuni watu wengine.

Alisema pamoja na kuwakamata watu hao jeshi hilo linaendelea kufanya msako katika maeneo yote nchini kuhakikisha vikundi hivyo vinadhibitiwa na kutoa rai kwa wananchi kuongeza ushirikiano ili kuwakamata watu hao. "Jeshi kama jeshi pekeake aliwezi likakakamata wahalifu bila kupata ushirikiano wa wananchi kwani wengi wao wapo miongoni mwao hivyo wananafasi kubwa ya kuwaona na kutoa taarifa ili waweze kukamatwa," alisema.

AIRTEL YAZINDUA DUKA MBAGALA.

  • Airtel yazindua duka Mbagala, Yatangaza kuzindua maduka mengine 10 kwa mwezi
  • Airtel kufungua maduka mapya Babati, Sumbawanga, Tegeta, Mpanda, Kigoma, Shinyanga, Singida, Musoma, Songea, na Lindi
    Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua duka jipya la kisasa jijini Dar es salaam Mbagala ikiwa ni muendelezo wa kukamilisha mkakati wake wa kutoa huduma na bidhaa bora za mawasiliano kila mahali nchini.
    Uzinduzi wa duka jipya la Airtel Mbagala uko katika mkakati waliojiwekea Airtel ambapo hadi sasa wamefanikiwa kujenga maduka mapya 6 katika mikoa ya Tanga, Moshi, Kariakoo, Kahama, Mwanza ndani ya Rock City Mall pamoja na duka la Airtel Expo lililopo makao makuu ya Airtel Moroko jijini DSM. Sambamba na hilo Airtel imekarabati maduka yake yote nchini ili kutoa huduma zinazoendana na karne ya sasa katika sekta ya mawasiliano
    Akizindua hilo Mbagala jijini Dar es salaam Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi Sophia Mjema aliipongeza Airtel na kuwataka wakazi wa Mbagala na maeneo ya jirani kulitumia vyema duka hilo katika kupata huduma za mawasiliano kwa kuwa mawasiliano sasa yanachangia sana katika maendeleo ya jamii
    “Ninawapongeza sana Airtel kwa ha kufungua duka hapa MBAGALA, ninatambua huduma ya mawasiliano ni chachu ya maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla, tunajionea jinsi baadhi ya huduma za kimtandao kama Airtel Money zilivyo na usalama kwa jinsi zinavyowawezesha watumiaji hata kutunza pesa zao, kulipia ankara mbalimbali, kutuma na kupokea pesa pamoja na kujipatia mikopo kama ilivyo huduma ya kipekee ya mikopo isiyo na masharti ijulikanayo kama Airtel TIMIZA sasa”.
  • “Nitoe wito sasa kwa wakazi wa MBAGALA, sasa tumieni duka lenu hili la karibu kujipatia huduma mbalimbali, kusajili namba za simu pamoja na kuzihakiki ili kutimiza maagizo ya serikali ya kwamba kila anaetumia namba ya simu iwe imesajliliwa kwa jina lake ili kupunguza uhalifu”.
Nae  Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba alisema “ huduma zitakazotolewa ni pamoja na kukusanya Ankara, kurudisha namba zilizopotea, mauzo ya simu za kisasa na ORIGINAL, Airtel money-kutoa na kuweka fedha, kuunganisha wateja na Intaneti ya Airtel pamoja na huduma zote za kimtandao .

“katika muendelezo wa dhamira yetu ya kutoa huduma karibu zaidi na wateja wetu baada ya uzinduzi wa Duka hili hapa Mbagala Airtel tumeijipanga kufungua  maduka mengine  zaidi ya 10 yajulikanayo kama Airtel Xpress Shop  katika katika maeneo ya Tegeta,   Babati, Sumbawanga, Mpanda, Kigoma, Shinyanga, Singida, Musoma, Songea, na Lindi” alieleza Bi, Lyamba

Duka la Airtel Mbagala litakuwa likitoa huduma kuanzia saa 3 asubuhi  hadi saa 11 na dakika 30 jioni kwa siku za Jumatatu hadi Ijumaa na pia siku ya Jumamosi kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6 za mchana.

1) Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba wakikata utepe kuzindua Duka jipya la Airtel, lililopo Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana.

2) Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba (wa pili kushoto), baada ya kuzindua Duka jipya la Airtel, lililopo Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana.

3) Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba (kulia), akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kushoto), baada ya mkuu huyo kuzindua  Duka jipya la Airtel, lililopo Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja wa Duka hilo, Lulu Mashiba.

4) Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba (kulia), baada ya kuzindua Duka jipya la Airtel, lililopo Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana.


5) Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (wa pili kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba (kulia), Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa tatu kulia), baada ya kuzindua  Duka jipya la Airtel, lililopo Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana.

HAKUNA ATHARI KUBWA USITISHWAJI MISAADA YA MCC.

Mkurugenzi mkuu  REA Lutengano Mwakasefya  aeleza kusitishwa kwa misaada ya MCC haitaathiri miradi ya mfuko huo.

Thursday, March 31, 2016

POLISI MWANZA YAFUKUA MWILI WA MAREHEMU.

Jeshi la polisi wilayani Nyamagana mkoani Mwanza limelazimika kuufukua mwili wa marehemu uliochukuliwa kimakosa na kuzikwa na watu wengine. 

WABUNGE WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA.

Wabunge Kangi Lugola, Sadiq Murad na Victor Mwambalaswa wafikishwa mahakamani na Takukuru kwa tuhuma za kuomba rushwa ya milioni 30. 

WANAFUNZI WALAZIMIKA KUSOMA MADARASA MA3 CHUMBA KIMOJA MKOANI SIMIYU.


Wanafunzi wa shule ya msingi ya Zawa wilaya ya  Maswa mkoani Simiyu wanalazamika kusoma madarasa matatu katika chumba kimoja kwa kupeana migongo na kutumia mbao mbili tofauti wakati walimu wakifundisha  kutokana na changamoto ya vyumba vya madarasa ambapo shule hiyo  ina vyumba vitatu yenye wanafunzi 513.


Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mashimba Ndaki  ameshuhudia vyumba hivyo na idadi ya wanafunzi kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu Wiliam Timothy kufuatia ziara yake na kujionea changamoto kupitia wajumbe wa Serikali za vijiji na mikutano ya  hadhara ikiwa ni mara yake ya pili kufika shuleni hapo  na kuweza kuahidi saruji ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu.

Aidha Mbunge huyo amewapongeza wananchi kwa nguvu kazi ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa vilivyofikia hatua ya Renta ,ufiatuaji wa matofali na mchanga wa ujenzi wa nyumba ya mwalimu hali ambayo itapunguza tatizo la watoto kusoma wakiwa wamebanana na walimu watano kuishi katika nyumba moja na kuahidi mabati 160 kwaajili ya kuezeka  jengo hilo na saruji mifuko 50,huku akisisitza dhana ya ushirikishwaji wananchi katika shughuli za maendeleo.

MAGAZETI YA LEO> WAKUU WA WILAYA WAPIGANA VIKUMBO. UAMUZI WA MAREKANI WAWAGAWA WATANZANIA. KITI ALICHOKALIA MAGUFULI CHA WA DILI.


Wakuu wa wilaya wapigana vikumbo. Uamuzi wa Marekani wawagawa Watanzania. Kiti alichokalia Magufuli mgahawani chawa dili; 

JPM azitikisa taasis 200 zenye sh22 trilioni. DC awasweka rumande wananchi 17,diwani. Mrema akwaa tena kisiki kesi dhidi ya Mbatia.

WAZIRI MKUU WA ZAMANI RWANDA AFIA JELA.

Waziri wa zamani wa Rwanda afia jela Burundi


Waziri wa zamani w Rwanda, Jacques Bihozagara ameaga dunia akiwa katika jela ya Burundi yapata miezi minne baada ya kutiwa nguvuni kwa tuhuma za kufanya ujasusi.


Jacques Bihozagara ambaye aliwahi kuwa waziri wa vijana wa Rwanda na balozi wa nchi yake katika nchi za Ubelgiji na Ufaransa alitiwa nguvuni December 4, 2015 na Shirika la Upelelezi la Taifa la Burundi (National Intelligence Service (SNR)) linalodhibitiwa moja kwa moja na Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi. Bihozagara ambaye amefariki dunia katika jela ya Mpimba mjini Bujumbura, alikuwa akikabiliwa na tuhuma za kufanya ujasusi kwa maslahi ya shirika la ujasusi la Rwanda.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda imetangaza kuwa imeshtushwa na habari ya kifo cha mwanadiplomasia huyo wa zamani na kusisitiza kuwa, serikali ya Burundi inapaswa kutoa majibu kuhusu mazingira na sababu za kifo chake.

Uhusiano wa Rwanda na Burundi ulivurugika baada ya Rais Nkurunziza kuituhumu Rwanda kwamba inawasaidia waasi wanaotaka kuiondoa madarakani serikali yake. Rwanda inakanusha madai hayo.

WAKALI KUTOKA MWANZA WAANZA KUFYATUA TRAXX MAALUM KWA JEMBEKA FESTIVAL.

Ikiwa imesalia miezi miwili tu kwa wasanii mbalimbali na wapenzi wa burudani nchini Tanzania wapate kushuhudia Tamasha kubwa la burudani linalofanyika kwa mwaka wa pili jijini Mwanza nazungumzia Jembeka Festival 2016 Tamasha linalotarajiwa kufanyika mnamo mwezi Mei tarehe 22 mwaka huu.

Tayari baadhi ya wasanii kutoka Mwanza wameshaanza kuonyesha moto wao jinsi ya namna vipi watakavyokwenda kulipamba tamasha hilo ambalo ndani ya kipindi kifupi limeweza kuteka hisia za wengi kutokana na either vihusishi vinavyotajwa kuwako tamashani mwaka hadi mwaka ima mahusiano mazuri ya kampuni husika JEMBE NI JEMBE na MASHABIKI WAKE kwamba kwa kila wanacho ahidiwa ndicho ambacho huwa kinafanyika tena kwa ubora.

Kupiti mstakabar huo wasanii kutoka mji wa waasisi wa Tamasha hilo  unaotambulika zaidi kama Rock City, tayari msanii mmoja mmoja na wengine kwa makundi wameanza kuachia ngoma zao za uhamasishaji wa burudani kwa tamasha hilo, ukijikita kwenye maaudhui, amshaamsha zake pamoja na kauli mbiu ya mwaka wa tamasha husika.

Biznea na Coyo Mc ni wasanii wa Hip-hop toka Mwanza waliojizolea heshima sasa kutokana na kuwa na kazi nzuri zinazo bang kwa hewa anga za radio stesheni mbalimbali Kanda ya Ziwa na kote nchini, nao wametinga studio za Update Record chini ya mtayarishaji Dee Classic na kufyatua mpini uliokwenda skuli walioubatiza jina la Gusa Nikuguse Tugusane.

Najua unahamu ya kuonja ladha ya mpini huo (BOFYA PLAY) 

Msanii maarufu wa muziki wa R&B kutoka nchini marekani Neyo na Diamond Platnumz kutoka nchini Tanzania ni moja kati ya wakali watakao ungana na wengine wakali kutoka pande mbalimbali wenye uwezo watakao tosha kukisanukisha siku hiyo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr. Sebastian Ndege amesema kuwa yuko kwenye mazungumzo ya mwishoni na Makampuni mbalimbali ambayo yameonyesha nia ya kuwa sehemu ya wadhamini wa tamasha hilo na hadi sasa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi Vodacom Tanzania tayari imeweka miguu yote miwili na kuwa mdamini mkuu wa JEMBEKA FESTIVAL 2016 KAZI NI KWAKO.

Wednesday, March 30, 2016

TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 116.4 KUTOKA JAPAN

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini hati mbili za makubaliano na Serikali ya Japan itakayoiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.


Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile alisema mkataba wa kwanza utasaidia katika kukamilisha bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17.

Dkt. Likwelile alisema kuwa msaada huo unalenga kuweka mazingira rafiki ya kwa wafanyabiashara, kuboresha masoko na kuwezesha mazingira ya ushindani katika utengenezaji wa ajira nchini.

Mkataba wa pili  unahusu masuala ya kiufundi  yatakayotumika katika kufanya marekebisho ya mkataba uliosainiwa  Octoba 20, 1966, kwa kuzingatia sheria nyingi zimebadilika, kusainiwa kwa hati hiyo ya makubaliano itasaidia kutabadilisha baadhi ya vifungu vyenye jina Tanzania na kuweka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kujumuisha pande zote mbili za Muungano katika kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.

Aidha, makubaliano hayo yatasaidia kubadilisha baadhi ya vipengele vya mkataba uliopita ikiwemo kipengele cha usambazaji wa madawa ili kuweza kukidhi mahitaji ya sasa ya wataalamu kutoka nchini Japan kuweza kuja kufanya kazi za kujitolea hapa nchini Tanzania.

Katibu Mkuu Dkt. Likwelile ameishukuru Serikali ya Japan na kusisitiza kuwa fedha hizo zitatumika kama ilivyopangwa ili kuweza kuwa na tija na kuwaletea maendeleo Watanzania.

Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japan ina imani kuwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili utasaidia kukuza maendeleo ya uchumi na kijamii.

Balozi Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japani inaunga mkono juhudi za Serikali inayo ongozwa na Rais Dkt. John Magufuli katika masuala ya viwanda na mazingira mazuri yanayovutia wawekezaji  kuwekeza nchini Tanzania.

Adha Balozi Yoshida amesema kuwa Japan itaendelea kuwaleta vijana wanaojitolea katika sekta ya uchumii na ya kijamii jambo limekuwa likitekelezwa tangu mwaka 1969 ambapo hadi sasa idadi ya vijana hao wa kujitolea imefikia zaidi ya 1500.

TAASISI YA TIBA YA MIFUPA, UPASUAJI WA UBONGO NA MISHIPA YA FAHAMU (MOI) YAPOKEA MILIONI 20

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk. Othman Kiloloma akizungumza wakati alipokua akipokea msaada kutoka, Taasisi ya GSM ya Dar es Salaam baada ya kumkabidhi hundi ya mfano ya Milioni 20 kwa ajili ya kununulia vifaa tiba na matibabu kwa watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi ambao unajulikana kama Hydrocephalus & Spinal Bifida. Jijini, Dar es Salaam leo (PICHA NA KHAMISI MUSSA)

NA KHAMISI MUSSA 

Taasisi ya GSM ya Dar es Salaam, imekabidhi msaada wa fedha taslimu shilingi milioni 20, kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) kwa ajili ya kununulia vifaa tiba na matibabu kwa watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi ambao unajulikana kama Hydrocephalus & Spinal Bifida.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mfano wa hundi, mwakilishi wa Kampuni ya GSM, Shannon Kiwamba, alisema wameguswa na changamoto zinazowakabili Watanzania ndiyo maana imeamua kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli ya kuboresha huduma za afya hapa nchini.


Shannon alisema, pamoja na msaada wa fedha ambazo GSM imeipa Moi, vilevile watafadhili kambi za upasuaji (Surgical camps) kwa watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na mgongo wazi katika mikoa mitano ya Kanda ya Ziwa.


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Moi, Dkt Othman Kiloloma, alisema anaishukuru GSM kwa kuguswa na hali za Watanzania hususan watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na mgongo wazi ambao kimsingi wanahitaji kufarijiwa.


Dkt kiloloma aliongeza, GSM imefanya uamuzi sahihi wa kuunga mkono jitihada za Serikali kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za afya kwa wakati mwafaka.


Alisema, fedha zilizotolewa na GSM zitatumika kama ilivyoelekezwa, vilevile Moi ipo tayari kutoa wataalamu kwenda mikoani kuwafanyia upasuaji watoto katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kuwapunguzia wagonjwa adha ya kusafiri kwenda Dar es Salaam.


Taasisi ya Moi imekuwa ikichukuwa jitihada madhubuti za kuhakikisha Watanzania hususan watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wanapata huduma bora pale walipo, ambapo imekuwa ikipeleka wataalam mikoani kwa ufadhili wa wadau mbalimbali na kuwafanyia upasuaji.


Takwimu zinaonesha hapa Tanzania watoto zaidi ya 5,000 kwa mwaka wanazaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi ambapo watoto 400 mpaka 500 pekee ndiyo wanapokelewa Moi.