ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 7, 2023

UBISHI WAMALIZWA FEISAL SALUM BADO NI MALI YA YANGA.

Feisal Salum bado ni Mali Ya Yanga TFF Yaamua

 Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu wa Tanzania (TFF) imeamua kuwa Feisal Salum bado ni mchezaji wa Yanga, kwa mujibu wa mkataba.

 

Uamuzi kamili kwa pande zote mbili zilizokuwa zinahusika katika shauri hilo utatolewa Jumatatu, Januari 9 2023.

Klabu ya Yanga iliwasilisha malalamiko mbele ya kamati hiyo ikipinga hatua ya mchezaji wao kuvunja mkataba kati yao bila kuwashirikisha.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ilisikiliza malalamiko hayo jana ambapo apnde zote mbili Yanga na kiungo huo ziliwakilishwa na wanasheria wao.

YANGA OUT MAPINDUZI.

 

MWENDO wa Yanga kwenye Kombe la Mapinduzi 2023 umegota mwisho baada ya kuambulia sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Singida Big Stars.

Yanga ambayo ipo kundi B la Mapinduzi 2023 ilikuwa inahitaji ushindi ili kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali lakini haikuwa hivyo kwani hata Singida Big Stars nao walikuwa wanahitaji ushindi.

Mabao yote mawili yalipatikana katika dakika 45 za mwanzo kutokana na mapigo huru huku ukipigwa mpira wa ushindani kwa miamba hao wawili.

Ni Francis Kazadi alianza kuipa bao Singida Big Stars dakika ya 22 akimalizia pigo la kona ambalo lilitemwa na kipa Johora Eric kisha Yanga walisubiri mpaka dakika ya 31.

Beki wao David Bryson ambaye alikuwa sababu pia ya kupata ushindi kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya KMKM alipiga pigo la faulo iliyoleta bao katika mchezo huo.

Ikumbukwe kwamba mbele ya KMKM Bryson alipiga faulo dakika ya 90 iliyokuwa chonganishi kwa wapinzani wao na ilifanikiwa kuleta bao la ushindi lililofungwa na Dickson Ambundo.

Kwa matokeo hayo ya Yanga kuvuna pointi moja kwenye kundi B inafikisha pointi nne sawa na Singida Big Stars kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungana.

Sasa Singida Big Stars itamenyana na Azam FC hatua ya nusu fainali na nusu fainali nyingine itawahusisha waliowavua ubingwa Simba, Mlandege dhidi ya Namungo iliyokuwa kundi D.

Shukrani kwa kipa wa Singida Big Stars, Benjamin Haule ambaye aliokoa hatari nyingi langoni mwake na kuifanya timu hiyo kupata pointi moja katika mchezo huo.

Sasa Yanga inaungana na watani zao wa jadi Simba kuwa watazamaji wa kombe hilo ambalo limekuwa na ushindani mkubwa mwaka huu 2023.

UTEKELEZAJI WA MAELEKEZO YA RAIS. DKT SAMIA SULUHU HASSAN MRADI WA MAJI MUSOMA VIJIJINI

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (wa pili kushoto) akikagua Mradi wa Maji wa Mugango-Kiabakari-Butiama. Wa pili kulia ni Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (wa pili kushoto) alipotembelea eneo la Mradi wa Maji wa Mugango-Kiabakari-Butiama. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Khalfan Haule akifuatiwa na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo.
Mkurugenzi wa Mamalaka ya Maji ya Mugango/Kiabakari, Mhandisi Cosmas Sanda akizungumza wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) kwenye mradi. Wengine kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Khalfan Haule akifuatiwa na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) Akijadiliana jambo na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo baada ya kutembelea Mradi wa Maji wa Mugango-Kiabakari-Butiama.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mugango wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (hayupo pichani)

Zaidi ya Bilioni 4 kusambaza maji Kata za Tegeruka na Mugango

 

Na Mohamed Saif

 

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga ameelekeza ifikapo Februari, 2023 utekelezaji wa mradi wa kufikisha maji kwenye Kata za Mugango na Tegeruka Wilaya ya Musoma Vijijini uwe umeanza ili ifikapo Mwezi Juni, 2023 wananchi wawe wanapata maji. 

 

Ametoa maelekezo kwa nyakati tofauti Januari 5, 2023 mbele ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo kwenye mikutano ya hadhara na wananchi wa Kata hizo kwa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maji Mkoani Mara ambazo ni Mamlaka ya Maji Musoma (MUWASA), Mamlaka ya Maji Mugango-Kiabakari-Butiama na RUWASA Mkoa wa Mara.

 

Amesema utekelezwaji wa mradi ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa Mugango-Kiabakari-Butiama tarehe 6 Februari, 2022.

 

“Mtakumbuka Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dokta. Samia Suluhu Hassan alifika hapa na kutuwekea jiwe la msingi la mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 70.5.  Katika mradi huo palikuwa na awamu mbili za utekelezaji lakini maelekezo yake yalikuwa ni kwamba mradi uwe na awamu moja badala ya kuwa na awamu mbili,” amesema Mhandisi Sanga.

 

Amebainisha kuwa ziara yake wilayani humo imelenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Mugango-Kiabakari-Butiama lakini pia kutoa maelekezo mbalimbali kuhusiana na maendeleo ya mradi sambamba na kuzungumza na wananchi wa Kata za Mugango na Tegeruka ili kuwafahamisha kuhusiana na neema inayokuja ya kufikishiwa huduma ya maji.

 

“Nimefika hapa kuzungumza na wananchi wa vijiji vyote vya Kata za Mugango na Tegeruka kuwafahamisha kuwa Mheshimiwa Rais Dokta. Samia Suluhu Hassan ametuongezea shilingi bilioni 4.775 kwaajili ya kuhakikisha mnapata huduma ya maji kupitia mradi huu mkubwa wa Mugango-Kiabakari-Butiama,” anabainisha Mhandisi Sanga.

 

Mhandisi Sanga ameelekeza wataalam watakaosimamia utekelezaji wa mradi kuhakikisha ndani ya mwezi huu wa Januari, 2023 watafute wakandarasi wengine tofauti na huyo anayetekeleza mradi mkubwa ili ikifika mwezi Februari wasaini mikataba na kuanza utekelezaji lengo likiwa ni kwamba pindi mradi mkubwa unavyokamilika mwezi Juni, 2023 nao uwe umekamilika na wananchi wanapata huduma.

 

Amewaasa wananchi wa kata hizo kuepuka kusikiliza maneno ya mitaani yanayotolewa na wasiopenda maendeleo ya kwamba hawatopata maji. “Kumekuwa na wapotoshaji ambao wanakuelezeni kwamba mnadanganywa, niwahakikishie ndugu zangu Serikali hii ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Mheshimiwa Dokta Samia Suluhu Hassan imejipambanua vyema katika kukabiliana na kero zinazowatatiza wananchi wake,” amebainisha Mhandisi Sanga.

 

Aidha, alimpongeza Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo kwa ufuatiliaji wake wa mara kwa mara wa miradi ya maji na aliwaomba radhi wananchi wa Kata hizo kwa kuchelewa kuanza utekelezaji kwakuwa walikuwa wakisubiri ujenzi wa mradi mkubwa usogee ambao ndio chanzo cha maji cha mradi husika ili yote ikamilike kwa pamoja.

 

“Tulichelewa kuanza utekelezaji kwakuwa utatoa maji kwenye mradi mkubwa sasa endapo tungelaza tu mabomba yangelikuwa hayana maji lakini kwa sasa ni wakati muafaka tuanze ili mradi mkubwa unapokamilika hapo Juni na hapa tunakuwa tumekamilisha,” anafafanua Mhandisi Sanga.

 

Akizungumzia mradi wa Mugango-Kiabakari-Butiama, Mhandisi Sanga amesema maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee alipofanya ziara kwenye mradi Desemba, 2022 ndiyo maelekezo ya Wizara ya Maji.

 

“Mtakumbuka hivi karibuni Mkuu wa Mkoa alitembelea hapa na alitoa maelekeozo kwa wakandarasi na wasimamizi kwamba ifikapo tarehe 30 Juni, 2023 mradi uwe umekamilika na hakuna muda wa nyongeza nasi tunaungana na maelekezo yake na tunasisitiza aliyoyaelekeza yabaki vilevile ifikapo tarehe 30 mradi uwe umekamilika,” amesisitiza Mhandisi Sanga.

 

Kwa upande wake Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo amesema ameshuhudia jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Maji za kumtua mama ndoo ya maji kichwani ambapo amebainisha kuwa vijiji vingi vilivyoko pembezoni mwa Ziwa Victoria tayari vinahuduma ya maji.

 

Amebainisha kuwa baadhi ya Kata jimboni mwake zikiwemo Kata ya Etaro, Nyegina, Ifulifu, Nyakatende watatumia maji kutoka Musoma mjini na jukumu hilo tayari Wizara ya Maji imelitolea maelekezo kwa MUWSA ya kuhakikisha vinafikishiwa huduma.

 

“Ninaendelea kuwathibitishia namna ambavyo Serikali yetu ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan inavyopenda jimbo la Musoma Vijijini, mwaka huu tunaouanza Serikali inazidi kuwekeza fedha nyingi ndani ya jimbo letu mbali na mradi wa mugango tumeletewa miradi mingine,” amesema Profesa Muhongo.

 

Amebainisha kuwa kwa Kata ya Mugango tayari kuna miradi miwili mmoja ikiwa ni huo aliyouzungumzia Mhandisi Sanga na kwamba kabla ya mradi huo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwapatia fedha kiasi cha shilingi Milioni 600 ambazo walizigawana na Butiama na kwamba zimewezesha maeneo mengi kupata huduma ya maji yakiwemo maeneo ya Kaburabura, Bugoji, Kanderema, Saragana, Nyambono na Mikuyu kufikishiwa huduma ya maji.


 


CCM IRINGA YAMPONGEZA RAIS DKT.SAMIA KURUHUSU MIKUTANO YA HADHARA

 

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Daud Yassin akizungumza na waandishi wa habari Iringa kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kurusu mikutano ya hadhara kwa vyama vyote

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Daud Yassin akizungumza na waandishi wa habari Iringa kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kurusu mikutano ya hadhara kwa vyama vyote. 

Na Fredy Mgunda, Iringa.

CHAMA cha mapinduzi (CCM),mkoani Iringa kimepongeza hatua ya Rais wa jamuhuri ya Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa ruhusa ya kufanyika kwa mikutano ya kisiasa yenye ustaarabu kwa maslahi ya taifa

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa Daudi Yassin amesema kuwa wanampongeza Rais Samia kwa ruhusa mikutano hiyo huku wakitarajia siasa safi na zisizo na uvunjifu w amani

“Sisi kama chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa tunampongeza dkt. Samia Suluhu Hassan kwa tamko alilolitoa ya kuruhusu vyama vya kisiasa na tufanye siasa za kistaarabu na zenye kujenga" alisema Yassin

Alisema kuwa wamejipanga vizuri kutoka matawi,kata ,wilaya hadi mkoa katika kufanya siasa safi na hawatarajii kuona uvunjifu wa amani ukifanyika kutokana na mikutno ya kisiasa .

Kwa upande wao wenyeviti wa CCM katika wilaya zote mkoani Iringa walisema kuwa pamoja na kuwepo kwa tetesi za mikutano yenye uwazi hawana wasiwasi badala yake wanatarajia mabadiliko makubwa na utenda kazi mzuri katika kipindi hiki

“Mheshimiwa mwenyekiti katika wilaya zetu hakuna wasiwasi wala mitetmo tupo vizuri na tupo tayari kufny siasa safi pamoja na kuwepo kwa baadhi ya maneno yanayotaka kututia wasiwasi nataka nikudhihirishie ya kwamba tupo vizuri”

Kwa upande wake chifu wa wahehe Mkoa wa Iringa Adam Sapi alisema kuwa yupo tayari kushirikiana na vyama vyote vya kisiasa hivyo ni vyema zikafanyika siasa safi zenye kuleta tija katika jamii .

“Kutokana na kauli aliyoitoa mama samia kuhusu ruhusa ya kufanya mikutano hapa nchini tupo tayari na tutashikana mikono na vyama vyot ili tuu tulete amani katika nchi yetu asante”

Nao wananchi wa manispaa ya Iringa wammpongeza Rais Dkt.Samia ambapo wamesema kuwa ruhusa hiyo itaonyesha ukomavu wa kisiasa pamoja na kusaidia kuibuliwa kwa changamoto nyingine zilizojificha kupitia vyama vya kisiasa .

HUU NDIO WIMBO UNAOSUMBUA YOU TUBE Harmonize - Wote (Official Music Video)

 Wow........   Harmonize - Wote (Official Music Video)

Friday, January 6, 2023

'TULIMISS SANA MIKUTANO YA HADHARA' CCM MKOA WA MWANZA YATOA TAMKO KUMPONGEZA RAIS SAMIA.

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

1. Hatua hii Jeh! inatija yoyote kwa CCM au inakuja mkiipokea kwa shingo upande? 2. Unataka kutuambia kwamba nanyi pia wakati wa katazo kwa namna moja au nyingine mlikuwa mnaathirika na hiyo hatua? 3. Vyama vingine vya siasa vilikuwa vikiamini kuwa Chama Cha Mapinduzi pamoja na katazo kilikuwa kikiendelea na mikutano hili limekaa vipi? 4. Vipi hali ya utekelezaji wa Ilani mkoa umefikia mahala gani?

Mwenyekit wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza Reuben Sixbert, amezungumza mapema hii leo.

UTEKELEZAJI MRADI WA BILIONI 24.6 KUPELEKA MAJI TINDE NA SHELUI WAMKOSHA MHANDISI SANGA AMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA

  1. Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akiwa katika Tenki la Maji wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa kutoa Maji kutoka Ziwa Victoria kupeleka Miji ya Tinde na Shelui
    Muonekano wa Tenki la maji Tinde lililojengwa kupitia Mradi wa kutoa Maji kutoka Ziwa Victoria kupeleka Miji ya Tinde na Shelui.

    Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa ziara yake kwenye Mradi wa kutoa Maji kutoka Ziwa Victoria kupeleka Miji ya Tinde na Shelui. Kulia ni Mtaalam Mshauri kutoka Kampuni ya WAPCOS Ltd, Arnab Saha

    Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kulia) akijadiliana jambo na watendaji wanaosimamia Mradi wa kutoa Maji kutoka Ziwa Victoria kupeleka Miji ya Tinde na Shelui


    Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akiwa Tinde kwenye eneo la Mradi wa kutoa Maji kutoka Ziwa Victoria kupeleka Miji ya Tinde na Shelui.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa mradi wa shilingi Bilioni 24.6 wa kutoa maji Ziwa Victoria kupeleka kwenye Miji ya Tinde Mkoani Shinyanga na Shelui Mkoani Singida.

 

Mhandisi Sanga amedhihirisha hayo kwa nyakati tofauti alipofanya ziara ya kukagua utekelezwaji wa mradi kwenye miji hiyo Januari 4, 2023.

 

Amesema Serikali inaendelea kutekeleza dhamira yake ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kuhakikisha fedha za utekelezaji wa miradi ya majisafi na salama zinapatikana kwa wakati na hivyo kuwawezesha wakandarasi kutekeleza miradi hiyo kwa mujibu wa mikataba yao.  

 

“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Dokta Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhakikisha fedha za utekelezaji wa mradi huu zinapatikana kwa ajili ya wananchi wa Tinde na Shelui,” amesema Mhandisi Sanga.

 

Akizungumzia hali ya utekelezaji wa mradi kwa ujumla wake baada ya ziara yake kwenye miji yote miwili, Mhandisi Sanga amebainisha kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi imekamilika kwa asilimia 99 kwa maeneo yote mawili kwani tayari maji yamefika kwenye matenki.

 

Amesema hatua inayofuata ni ujenzi wa mtandao wa kilomita 32 wa kusambaza maji kwenye miji yote miwili huku kila mji ukijengewa kilomita 16 za mtandao.  

 

Hata hivyo, amebainisha kwamba kwa upande wa Shelui tayari wananchi wameanza kutumia maji kutoka Ziwa Victoria kwakuwa wameunganisha kwenye mfumo wa usambazaji uliokuwepo tangu zamani na kwamba kinachofuata kwa Mji wa Tinde ni kuhakikisha maji yanasambazwa kwa watumiaji.

 

“Nimeridhishwa na hatua iliyofikiwa, ninampongeza Mkandarasi Kampuni ya Megha Engineering and Infrastructure Ltd pamoja na Mtaalam Mshauri Kampuni ya WAPCOS Ltd kwa kukamilisha mradi huu,” amesema Mhandisi Sanga.

 

Amefafanua kwamba mradi wa kupeleka maji kwenye miji ya Tinde na Shelui unatoa maji kutoka katika mradi mkubwa wa Kahama-Shinyanga ambao pia umepeleka maji kwenye Miji ya Tabora, Igunga na Nzega.

 

Aidha, Mhandisi Sanga amewapongeza wasimamizi wa mradi ambao ni Mamlaka za Maji za Shinyanga na Igunga kwa kushirikiana na Jumuiya za Watumia Maji Shelui pamoja na watendaji wa Wizara ya Maji wanaosimamia mradi huo moja kwa moja.

 

Vilevile amewasihi watumishi wa Wizara ya Maji na Mamlaka za maji kuhakikisha miundombinu inalindwa na pia mazingira yanatunzwa ili kuwa na mradi endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

 

IHEFU FC BINGWA WA MISITU SPORTS BONANZA MSIMU WA NANE 2022

 

Nahodha wa timu ya Ihefu fc akikabidhiwa kombe la mashindano ya misitu sports Bonanza lilioandaliwa na uongozi wa shamba la miti la Sao Hill mkoni Iringa.
Mchezaji wa timu ya sawala akipokea medani baada ya kuibuka mshindi wa pili katika Bonanza lilioandaliwa na uongozi wa shamba la miti la Sao Hill wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Na Fredy Mgunda, Iringa.


TIMU ya Ihefu FC imefanikiwa kutwaa kombe la mashindano ya misitu sports bonanza baada ya kuifunga timu ya Sawala FC kwa mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika viwanja vya Makao makuu ya shamba la Sao Hill wilayani Mufindi.

Akizungumza Mara baada ya fainali hiyo mratibu wa mashindano ya misitu sports bonanza, Frank Milanzi alisema kuwa bonaza hilo lilizikutanisha Tarafa nne zinazolinguka shamba la miti la Sao Hill kwa kuwa na jumla ya timu 32 ambazo zilipambana ambapo Ihefu FC inaibuka kuwa bingwa.

Milanzi alisema kuwa mshindi wa kwanza wa bonanza kwa upande wa mpira wa miguu amepata kiasi cha shilingi laki tano, mshindi wa pili Laki tatu, mshindi wa tatu amepata kiasi cha shilingi laki mbili na mshindi wa nne amepata mpira hiyo yote kwa ajili ya kujenga ujirani mwema katika ya wananchi na shamba la miti la Sao Hill Mufindi.

Alisema kuwa mashindano ya misitu sports bonanza mwaka huu yamekuwa na msisimko tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma hiyo inatokana na maboresho ambayo yamekuwa yakifanyika mara kwa mara na kuongeza kwa ubunifu wa waandaaji wa bonanza hilo kila mwaka.

Milanzi alimazia kwa kusema kuwa mashindano ya misitu sports bonanza limesaidia kuongeza ujirani mwema katika kuhakikisha wananchi wanalinda shamba la miti la Sao Hill dhidi ya majanga ya moto pamoja wananchi kuhamasika kuendelea kupata miti kila wakati.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mpira Wilaya ya Mufindi Festo Kilipamwambu amewapongeza  Uongozi wa TFS kwa kuendelea kuandaa Bonanza hili kila mwaka kwani linasaidia katika kujenga na kuimarisha umoja kati ya shamba na vijiji hivyo.

"Mashindano haya ya Misitu Sports Bonanza  yamekua yakileta tija sana katika wilaya yetu ya Mufindi hususani katika timu zetu zinazozunguka wilaya na yamekua ni mashindano ya muhimu sana kwani yanasaidia katika kuibua vipaji na kuendeleza ujirani mwema baina ya watu mbalimbali" Alisema Festo

Kilipamwambu alisema kuwa anazipongeza timu zote zilizoweza kushiriki katika mashindano hayo na kuwapongeza mabingwa Ihefu FC kwa kutwaa kombe pamoja na washindi wa michezo mingine.
 
Alisema kuwa lengo mashindano hayo ni kuwambusha jinsi ya kuweza kuhifadhi rasilimali za misitu ikiwemo kupanda miti hasa katika kipindi hiki cha mvua na kuitunza  pia kwa kushirikiana na jamii inayotuzunguka tunaweza kulinda na kuitunza misitu yetu.

michezo mbalimbali imechezwa na washindi kupewa zawadi zao ambapo IHEFU FC wakiibuka mabingwa wa mwaka huu na kutwaa kombe. 

Thursday, January 5, 2023

BINTI WA MIAKA 15 APANDISHWA KIZIMBANI AKIDAIWA KUMWUA BOSI WAKE.


Msichana mwenye umri wa miaka 15, Sarah Mwendesha amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Ilemela na kusomewa shtaka la mauaji ya aliyekuwa mhadhiri wa Kitivo cha Uhandisi cha Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (Saut) mkoani Mwanza, Hamida Mussa maarufu “Mama Mwakitosi”.

 

Mshtakiwa huyo katika kesi ya mauaji (Juvenile) namba 1/2022, anadaiwa kumuua mhadhiri huyo Novemba 29, 2022 kwa kumnyonga kwa kutumia mtandio akiwa nyumbani kwake Mtaa wa Buzuruga Mashariki.

 

Inadaiwa kwamba Sarah ambaye alikuwa msaidizi wa kazi za ndani wa mhadhiri huyo baada ya kutekeleza mauaji hayo alitoroka na kukimbilia wilayani Misungwi kabla ya kutiwa mbaroni na maofisa wa polisi siku tatu baadae kisha kufunguliwa shtaka hilo.

 

Amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilemela, Fortunatus Kubaja kwa ajili ya kesi yake kutajwa kisha kuahirishwa hadi Januari 19, 2023 itakapoitwa kwa ajili kutajwa tena.

SOMALIA: WATU 26 WAKIWEMO 9 WA FAMILIA MOJA WAUAWA KWA BOMU


Tukio limehusisha milipuko katika Magari mawili kwenye Jimbo la Hiraan huku Kundi la Al-Shabaab likidaiwa kuhusika


Milipuko hiyo iliambatana na milipuko mingine katika eneo la Soko ambapo Watu wengi wamejeruhiwa


Al-Shabaab wamekuwa wakitajwa kuhusika katika matukio mengi ya aina hiyo hivi karibuni baada ya Rais wa #Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, kutangaza vita dhidi ya kikundi hicho


KENYA: "KINOTI HAKUJIUZULU KUTOKA DCI NILIMFUTA KAZI" RAIS RUTO


Baada ya taarifa za Septemba 27, 2022 za Kujiuzulu kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), George Kinoti, Rais #WilliamRuto amesema alimfuta kazi kutokana na kuongezeka kwa Mauaji na kutoweka kwa Raia kulikohusishwa na Polisi


Rais Ruto alielezea masikitiko yake kuhusu kupatikana kwa zaidi ya miili 200 ya Wakenya katika Mito na vichaka vya maeneo mbalimbali huku sababu za vifo zikiwa ni kitendawili, ambapo aliiagiza Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (Ipoa) kuchunguza na kuwakamata waliohusika na mauaji hayo


Amesema, "Miili 30 huko #Yala, 17 #Garissa, kulikuwa na kontena hapa #Nairobi ambapo Watu walikuwa wakichinjwa katika Kituo cha Polisi, tulifikaje hapo? Ilikuwa ni Taasisi gani ya kihuni? Na ndio maana nilimfukuza huyo Kinoti, kwa sababu sio sawa"

SIRI YAGUNDULIKA DRONE ZA URUSI ZATUMIKA KUISHAMBULIA UKRANE


SHIRIKA
la habari CNN limeripoti kuwa ndege zisizo na rubani za Kamikaze za Irani ambazo jeshi la Urusi limekuwa likitumia kuishambulia Ukraine katika miezi ya hivi karibuni zimetengenezwa na kampuni ya Marekani.

 

Wakati huo huo, Adrienne Watson, msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Marekani, aliiambia CNN kwamba utawala wa nchi hiyo unatathmini uwezekano wa kuanzisha vikwazo vipya na vikwazo vya kuuza nje dhidi ya makampuni yanayosambaza sehemu kwa Iran zinazotumika katika utengenezaji wa ndege zisizo na rubani.

 

"Tunaangalia hatua zaidi tunazoweza kuchukua katika suala la vikwazo vya usafirishaji ili kukata ufikiaji wa Iran kwa teknolojia ya droni," alisema Watson.

 

Jeshi la Urusi lilianza kutumia ndege zisizo na rubani za Kamikaze dhidi ya Ukraine mwaka uliopita. Katika miji mikuu ya Kyiv na Magharibi wanasema kwamba hizi ni hasa ndege za anga zisizo na rubani zilizotengenezwa na Iran za aina ya Shahed. Iran hapo awali ilikanusha kuwa ilikuwa imekabidhi ndege zisizo na rubani kwa Urusi, lakini ikakubali kwamba kundi la ndege kama hizo zilitumwa Moscow (wakati Tehran inadai kwamba hii ilitokea hata kabla ya vita na Ukraine).

'HIZO LIST HAZINA HESHIMA HIVYO SIZIHESHIMU' MENEJA WA HARMONIZE JEMBE NI JEMBE

 NA ALBERT G. SENGO/ MWANZA

Meneja wa mwanamuziki mkubwa nchini Tanzania Harmonize, Jembe ni Jembe ameulizwa na mtangazaji Natty E, wa Jembe Fm kupitia kipindi cha Hit Zone, "Umeziona List?" akimaanisha Orodha za wasanii waliotajwa kuwa ni ya 'Wasanii bora wa Bongo Fleva 2022'

Wednesday, January 4, 2023

WENGI WALITEGEMEA HARMONIZE ANGETAMBULISHA MENEJA WAKE USIKU ULE NINI KILITOKEA?

 

NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Kwa siku za hivi karibuni bila shaka ulizisikia taarifa zilizozagaa zikisema baada ya kuachana na aliyekuwa Meneja wake lakini pia mpenzi wake Kajala Frida , Msanii wa Bongofleva Harmonize alitangaza kumtambulisha meneja wake mpya kama Suprise kwenye usiku wa Harmo-Night , show yake ya kufungia mwaka iliyofanyika siku usiku wa Christmas ya Disemba 2022. Pia kupitia insta story, Harmonize amefunguka kuutumia usiku huo pia kutambulisha wasanii wengine wapya kwenye lebo ya Konde Gang. Akaenda mbali zaidi kwa kudai kuwa ataitumia show yake ya Harmo Night 2022, kupima upendo na unafiki wa wasanii wenzie haswa aliofanya nao kazi ya pamoja na kuzalisha Hit songs. Meneja wa Harmonize ambaye pia ni CEO wa Jembe Media Limited inayomiliki kituo cha Jembe Fm, Dr. Sebastian Ndege al maarufu Jembe ni Jembe, amezungumza leo na Natty E wa kipindi cha Hit Zone kinachochapa mangoma ya kileo kinachoruka mchana majira ya saa 13:00 hadi 16:00

UWT YAMPONGEZA RAIS DKT SAMIA SULUHU KWA KUIMARISHA DEMOKRASIA NCHINI

 

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT Taifa Mary Chatanda akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kuhusu kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuimarisha Demokrasia nchini

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT Taifa Mary Chatanda akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga ambao hawapo pichani kuhusu kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuimarisha Demokrasia nchini
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT Taifa Mary Chatanda akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kuhusu kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuimarisha Demokrasia nchini


 

Na Oscar Assenga,TANGA


MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT Taifa Mary Chatanda amesema UWT imekoshwa na uamuzi wa kihistoria wa Rais Dkt Samia Suluhu  kuondoa zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa nchini maamuzi ambayo yameleta faraja kwa vyama hivyo na hivyo kufungua ukurasa mpya wa demokrasia nchini

Chatanda aliyasema hayo leo kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Tanga wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu kuondoa zuio la mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa nchini ambapo

Alisema kwamba UWT imekoshwa na hatua ya kihistoria kuondoa zuio la mkutano ya hadhara vyama vya siasa ikiwemo kukwamua mchakato wa kupata Katiba mpya ambapo alisema  kwamba wao wanaunga mkono uamuzi wa Kukwamua mchakato wa marekebisho ya Katiba  ya Tanzania  na hivyo tunahimiza amani na utulivu wakati wote wa kusubiri Serikali kukamilisha taratibu zote za kuanza mchakato huu kama alivyoeleza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake jana tarehe 3 Januari 2023.

Alisema pamoja na kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali ili kupanua wigo wa demokrasia nchini ambapo alisema maamuzi ya Rais Dkt Samia yameleta faraja kwa vyama mbalimbali vya siasa nchini na kuwezesha kufikia hatu kubwa ya kidemokrasia nchini.

Aidha alisema Rais Dkt Samia ameendelea kuonyesha udhabiti wa kauli zake kwa matendo ambapo hata alipohutubia Taifa mara baada ya kuapishwa Maci 19,2022 alisema wakati huo sio wa kutazama mbele kwa mashaka bali ni kwa kutazama kwa matumaini mwisho wa kumnukuu.

Mwenyekiti Chatanda alisema maamuzi aliyoyafikia Rais Dkt Samia kupitia mchakato wa maridhiano kuanzia kuundwa Kikosi cha kazi pia mazungumzo kati ya Vyama vya Siasa na Vyama vya CCM na Chadema yameleta matumaini mapya katika kujenga demokrasia ya kuaminiana baina ya vyama vyote vya siasa nchini ambayo ni chachu katika ujenzi wa Taifa lenye umoja Amani a Utulivu.

“Lakini niwaambie kwanza falsafaya Rais Samia Suluhu ni kujenga upya nchi yenye umoja katika ujenzi wa Taifa inayoongozwa falsafa ya 4R maridhiano ustahimilivu,mabadiliko na kujenga upya nchi hadi sasa falsafa hiyo imefanikiwa kwa asilimia 100” Alisema Chatanda

Hata hivyo alisema sio tu kwa kuleta mafanikio makubwa ya kisekta aliyotekeleza Rais kwa muda mfupi wa chini ya miaka miwili madarakani licha kuipokea nchini ikiwa na hali tete ya kutokana majanga ya Corona ,vita ya Ukraine na kufiwa na mtangulizi wake mwaka 2021

“Kwa kweli sisi UWT tunasema Rais Dkt Samia amefanya jambo kubwa sana hivyo tunampongeza na hizo zinazotokana na matokeo  ya mkutano baina ya  Rais Samia na vyama vya siasa kwenye usajili wa kudumisha nchini,uwt wanampjgeza  Rais Samia kwa kufanya maamuzi yalitileta furaha isiyo na kifani kwa wananchi wa Tanzania na wapenda Amani dunia kote kwa kutoa majawabu ya vikwazo vya demokrasia nchini wao na  majanga ya korona,vita ya Ukraine na kufiwa na mtangulizi wake Mwaka 2021" Alisema Chatanda 
 
Aliongeza kwamba bali falsafsa hìzo zinahimiza siasa za kustaarabu zenye kuweka watu pamoja,kujenga hoja za ushawishi kupitia majadiliano mazungumzo kuhusisha vyama vya siasa katika kuendesha nchi hivyo kutokana na hilo UWT wanampongeza Rais huku wakieleza kwamba hakika wanawake wanaweza.

Hata hivyo alisema kwamba Jumuiya hiyo ya UWT inawahimiza viongozi wanawake wa vyama mbalimbali kuandaa mikutano mingi ya hadhara ili kuweza kupokea changamoto mbalimbali zinazowagusa wanawake wa Tanzania wanakabiliwa na changamoto zinazofanana bila kujali itikadi zao na pia katika mikutano wanapendeleza hatua mahususi za kuchukua kwa Serikali ili kumkomboa mwanamke kiuchumi,kijamii na kisiasa.

Mwenyekiti Chatanda alisema kwamba pia wamefurahishwa na uamuzi wa Serikali ya awamu ya sita ya kuridhia mapendekezo ya kikosi kazi cha kufanya marekebisho ya sheria kadhaa ndani ya nchi kwa nia ya kuimarisha demokrasia zaidi ambayo yatahusisha wananchi.

Alisema wanaamini marekebisho hayo pia yatazingatia masuala ya usawa wa kijinsia katika kuongeza uwakilishi wa wanawake kwenye siasa na uongozi kuanzia kwenye vyama vya siasa kama ambayo wameshuhudia namna Rais Samia Suluhu alivyojitahidi kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye uongozi ndani ya Serikali yake na chama cha Mapinduzi


Mwenyekiti Chatanda aliwahimiza viongozi wake wa Jumuiya ya UWT kuanzia ngazi za Tawi ,Kata/Wadi ,Jimbo, wilaya , Mkoa mpaka Taifa pamoja na Madiwani,wawakilishi na Wabunge Wanawake kufanya mikutano ya hadhara kwa kufuata taratibu zote ,mikutano hiyo ilenge kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 , kusikiliza kero za wananchi na kujibu hoja mbalimbali zitakazopotoshwa kwa lugha ya kistaarabu na kwa kutumia takwimu sahihi , sisi Viongozi wa UWT Taifa tutaonyesha mfano kwa kutumia fursa hii iliyotolewa na Mhe Dk Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . 
 
Hata hivyo pia alitumia nafasi hiyo kuitaka Jumuiya ya UWT kuendelea kuwaomba Watanzania kuendelea kumuamini Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kumuunga mkono kwani ana dhamira njema ya kujenga Taifa linaloongea lugha moja , na ambalo kila mmoja anashiriki katika ujenzi wa Taifa lake .

'WATAPATA HASARA SISI TUKIONGEA' MENEJA WA HARMONIZE JEMBE NI JEMBE

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Amefunguka juu ya kuondoka kwa wasanii kwenye Lebo ya Konde Gang ikiwa ni pamoja na "machawa' Meneja wa Harmonize ambaye pia ni CEO wa Jembe Media Limited inayomiliki kituo cha Jembe Fm, Dr. Sebastian Ndege al maarufu Jembe ni Jembe, amezungumza leo na Natty E wa kipindi cha Hit Zone kinachochapa mangoma ya kileo kinachoruka mchana majira ya saa 13:00 hadi 16:00

DC MOYO MARUFUKU KAMPUNI ZA ULINZI KUAJIRI WASIOPITIA MAFUNZO YA KIJESHI

 


Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wahitimu wa mafunzo ya mgambo juu ya serikali ya wilaya ya Iringa kuwapambania kupata ajira kwenye kampuni za Ulinzi zizopo katika wilaya hiyo
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akikagua gwaride la askari mgambo ambao wamemaliza mafunzo ya awali ya kijeshi tayari kwa ajili ya kufanya kazi za Ulinzi kwenye makampuni mbalimbali ya ulinzi

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akikagua gwaride la askari mgambo ambao wamemaliza mafunzo ya awali ya kijeshi tayari kwa ajili ya kufanya kazi za Ulinzi kwenye makampuni mbalimbali ya ulinzi



Na Fredy Mgunda, Iringa.


SERIKALI ya wilaya ya Iringa imezitaka kampuni za Ulinzi kuajiri wafanyakazi waliopitia mafunzo ya kijeshi ili kuboresha ufanisi wa kazi katika sekta ya ulinzi wa mali za UMMA, serikali,watu binafsi na mashirika binafsi.

 

Akifunga mafunzo ya Jeshi la akiba katika kata ya Masaka mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa kitendo cha makampuni ya ulinzi yaliyopo wilaya ya Iringa kuajiri walinzi wasio na mafunzo kinakinzana na taratibu na sheria zilizopo, huku kikiwanyima fursa askari waliopitia mafunzo ya kijeshi.

 

Moyo aliliagiza Jeshi la Polisi kuanzisha ukaguzi maalum dhidi Makampuni ya ulinzi Wilayani Iringa ili kujiridhisha endapo walioajiriwa Kwa kazi ya Ulinzi wamekidhi vigezo vinavyotambuliwa kwa mujibu wa sheria.


Alizitaka kampuni za Ulinzi zizopo wilaya ya Iringa kuwaondosha kazini wafanyakazi wasiopitia mafunzo ya Jeshi,Kabla ya Serikali kuchukua hatua ya kuyafutia leseni makampuni hayo.


Kiongozi huyo ameeleza mpango wa Serikali ya wilaya katika kusaidia kundi kubwa la vijana waliohitimu mafunzo hayo..

 

Moyo alimazia kwa kusema kuwa Serikali haiwezi kuvumilia kuona makampuni hayo yakikiuka sheria kwa makusudi akibainisha kuwa kitendo cha kuajiri watu wasiopitia mafunzo kuwa ni chanzo cha uhalifu katika maeneo mbalimbali


Kwa upande wao wahitibu wa mafunzo haya ya jeshi la akiba katika risala yao wameeleza miongoni mwa changamoto kuu ni kukosa ajira katika makampuni ya ulinzi kwani makampuni yaliyo mengi yanaajiri watu wasiopitia mafunzo ya jeshi

 

Naye Diwani wa kata ya masaka Methew Nganyagwa akimualika Mgeni wa heshima katika hafla hiyo amesema mafunzo hayo yamekuwa na tuija kubwa ya kimaendeleo katika kata hiyo

 

Tuesday, January 3, 2023

RAIS SAMIA ALIVYOIGUSA MWANZA 2022 - 2023

 NA ALBERT G.SENGO / MWANZA

Kwa ufupi haya ni yale yaliyofanyika mwaka 2022 na Serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo pia utawasikia wadau kadhaa, wakiwemo viongozi na wananchi wa mkoa wa Mwanza wakizungumza jinsi walivyokoshwa na utekelezaji huo.

Sunday, January 1, 2023

KUTOKA KUNYWA TOPE SASA NI MWAKA MPYA WA MAJI SAFI NA SALAMA.

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Wakazi wa kijiji cha Mahina Kati wilayani Nyamagana mkoani hapa wameanza kuondokana na kadhia ya muda mrefu ya kupata maji baada ya kukabidhiwa kisima cha maji safi na salama. Akikabidhi mradi huo mbele ya wananchi na viongozi wa kijiji, Mwakilishi wa Shirika la “The desk & chair foundation” tawi la Mwanza Sibtain Meghjee amesema kuwa shirika lake liko kwenye mkakati wa kuchimba visima vingine vinne (4) kwenye maeneo tofauti ii kupunguza msongamano kwenye kisima hicho kipya cha kwanza.