ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 5, 2023

BINTI WA MIAKA 15 APANDISHWA KIZIMBANI AKIDAIWA KUMWUA BOSI WAKE.


Msichana mwenye umri wa miaka 15, Sarah Mwendesha amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Ilemela na kusomewa shtaka la mauaji ya aliyekuwa mhadhiri wa Kitivo cha Uhandisi cha Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (Saut) mkoani Mwanza, Hamida Mussa maarufu “Mama Mwakitosi”.

 

Mshtakiwa huyo katika kesi ya mauaji (Juvenile) namba 1/2022, anadaiwa kumuua mhadhiri huyo Novemba 29, 2022 kwa kumnyonga kwa kutumia mtandio akiwa nyumbani kwake Mtaa wa Buzuruga Mashariki.

 

Inadaiwa kwamba Sarah ambaye alikuwa msaidizi wa kazi za ndani wa mhadhiri huyo baada ya kutekeleza mauaji hayo alitoroka na kukimbilia wilayani Misungwi kabla ya kutiwa mbaroni na maofisa wa polisi siku tatu baadae kisha kufunguliwa shtaka hilo.

 

Amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilemela, Fortunatus Kubaja kwa ajili ya kesi yake kutajwa kisha kuahirishwa hadi Januari 19, 2023 itakapoitwa kwa ajili kutajwa tena.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.