ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 22, 2024

MARCO WA ZABRON SINGERS AFARIKI DUNIA

 
 
TAARIFA ya huzuni asubuhi hii...

Mwimbaji wa kundi la Zabron Singers, Marco Joseph amefariki dunia kwa ugonjwa wa Moyo usiku wa tarehe 21 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.


BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJI LAMLILIA RAIS DKT. SAMIA KUPATIWA ARDHI YA SHIRIKA LA ELIMU ILI KUIENDELEZA


 NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 

Baraza la madiwani katika  Halmashauri ya mji Kibaha limemuomba Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwapatia baadhi ya eneo la ardhi ambayo inamilikiwa na shirika la elimu Kibaha ili waweze kuiendeleza katika shughuli mbali mbali za kiuchumi na kimaendeleo.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Kibaha Mussa Ndomba  wakati wa  kikao cha baraza la madiwani cha robo ya nne ya mwaka wa fedha kwa kipindi cha mwaka 2023/2024.

Ndomba akizungumza kwa niaba ya madiwani wenzake amesema kwamba kwa kipindi kirefu eneo kubwa la ardhi limekuwa likimilikiwa  na shirika la Elimu Kibaha limeshindwa kuendelezwa na kusababisha kuwa sehemu kubwa ya vichaka na  pori hali ambayo inahatarisha usalama.

Alibainisha kwamba lengo lao kubwa la Halmashauri ya Kibaha mji ni kuwa Manispaa hivyo wakipata  eneo hilo la ardhi  wataweza kuliendeleza katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo kuliko lilivyo kwa sasa halitumiki katika shughuli yoyote ile.


"Kwa kweli sisi kama baraza la madiwani ombi letu kubwa kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kupata baadhi ya  eneo la ardhi ambalo linamilikiwa na Shirika la elimu Kibaha na nia yetu ni nzuri ya kuweka mipango ya kuendesha shughuli mbali mbali za maendeleo,"alisema Ndomba.

Aidha Ndomba alitumia kikao hicho kukumbushia ahadi ya Waziri wa Maji Juma Aweso ya kupeleka mradi wa maji kwa baadhi ya kata ikiwemo kata ya Pangani na viziwaziwa.

 Alibainisha kwamba kuna baadhi ya kata bado zinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama hivyo ana imani ahadi ya Waziri ikitekelezwa kutaweza kusaidia wananchi kupata huduma ya maji safi na salama.

Katika hatua nyingine Ndomba alimpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha kwa ajili ya kuweza kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule mpya.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Tangini Mfaume Kabuga hakusita kuunga mkono hoja ya kupewa baadhi ya  eneo la Shirika la elimu Kibaha kutokana na kugeuka kuwa mashamba pori na sehemu ya kujificha waharifu.

Pia baraza hilo limeiomba serikali kuweka mipango madhubuti ya kufanya upanuzi katika barabara kuu ya morogoro  road kwa lengo kwa lengo la kuweza kupunguza foleni na ajali.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji Kibaha Dkt.Rogers Shemweleka amesema lengo lake kubwa ni kuhakikisha analinda na kuzitunza rasilimali zote kwa maslahi.

Kadhalika Mkurugenzi huyo aliwaomba madiwani na wataalamu kuwa na ubunifu na kuwa na vyanzo vipya vya mapato ambavyo ni vikubwa kuliko kutegemea vyanzo vile vile.

"Lengo langu ni kuwahudumia wananchi wote na mimi kiukweli tangu nianze kazi hii nimejitahidi kwa hali mali kushirikiana na timu yangu ya wataalamu na tumefanikiwa kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato,"alisema Dkt Rogers.

Pia katika baraza hilo pia kulienda sambamba na  kufanyika uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji.


Katika uchaguzi huo Diwani wa kata ya picha ya ndege Karim  Mtambo ameweza kuibuka kidedea baada ya kuibuka na ushindi kwa kuweza kupata kura 18 za ndio.

Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi ya  Makamu Mwenyeki alisema aliwataka madiwani kuwa.na umoja na mshikamano ili kuwaletea wananchi maendeleo.



Nao baadhi ya madiwani akiwemo diwani wa viti maalumu  Aziza Mruma amehimiza suala la kuwa na uwazi katika utekezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ili kuondokana na sintofahamu baina ya watendaji,wananchi na madiwani.


Kikao cha baraza la madiwani Halmashauri ya mji kibaha robo ya nne imeweza kujadili mambo mbali mbali ya kimaendeleo,kufanya uchaguzi wa kamati tofauti na kupanga mipango ya kimaendeleo.

Wednesday, August 21, 2024

RC KUNENGE AUNGURUMA AWAONYA WAKANDARASI WANAOKWEPA MIKATABA YAO YA KAZI

HABARI NA VICTOR MASANGU, PWANI SAUTI NA G.SENGO

 
SERIKALI  mkoani Pwani imesema kwamba haitowafumbia macho hata kidogo  wakandarasi ambao watakwenda kinyume na miongozo ya mikataba yao na kuwaagiza wahakikishe kwamba wanatekeleza miradi ya miundombinu ya barabara kwa kiwango ambacho kinatakiwa ikiwemo suala la kuwashirikisha wananchi  ili waweze kufahamu miradi inayotekelezwa.

Kunenge ametoa kauli hiyo wakati  wa halfa fupi  ya utiani wa saini wa mikataba  ya kazi za barabara kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2024/2025 inayotekelezwa na Wakala wa barabara za vijiijini na mjinini (TARURA) Mkoa wa Pwani na kuongeza kuwa fedha zinazotolewa ziende kutekeleza  miradi hiyo na imalizike kwa wakati.

WAFANYABISHARA TANGA WATOA USHAURI KWA BENKI YA NMB WALIOCHUKUA MIKOPO NA KUSHINDWA KUIREJESHA

 

 

Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Tanga (JWT) Ismail Masoud akizungumza wakati wa mkutano huo 
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka Ladislaus akizungumza wakati wa mkutano huo

Tuesday, August 20, 2024

NAIBU KATIBU MKUU MAENDELEO YA JAMII AVUTIWA NA KAMATI YA ULINZI WA MTOTO STENDI YA NYEGEZI MWANZA.

 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu amekagua shughuli za kamati ya ulinzi wa watoto wanaoishi mazingira magumu/ mitaani iliyopo stendi Kuu ya Mabasi Nyegezi jijini Mwanza.

Mdemu amekagua shughuli za kamati hiyo Jumanne Agosti 20,2024 akiwa kwenye mwendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii mkoani Mwanza.

"Nimevutiwa sana na kamati hii, sote tukiungana na kuwajibika pamoja, tutafanikiwa kuwalinda watoto na vitendo vya ukatili wa kijinsia lakini pia kuwaondoa katika maeneo ya stendi" amesema Mdemu huku akipongeza wazo la uanzishaji wa kamati hiyo akisema linaweza kusaidia kuwa na kamati za aina hiyo katika stendi mbalimbali nchini.

Awali akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Kamati hiyo, Afisa Ustawi wa Jamii Kata ya Ngegezi, Edith Ngowi amesema tangu mwaka 2021 kamati hiyo imewaokoa watoto 297 katika stendi ya mabasi Nyegezi.

"Kwa kushirikiana na shirika la Railway children Africa na Jeshi la Uhamiaji, watoto 230 wameunganishwa na familia zao ingawa tumepata changamoto ya watoto 30 ambao wamerejea tena mitaani baada ya kuumganishwa na familia zao huku wengine wakitoa taarifa ambazo si sahihi na hivyo kushindwa kuwapata ndugu zao" amesema Ngowi.

Aidha Ngowi amebainisha kuwa watoto hao wamekuwa wakifika stendi kwa njia mbalimbali ikiwemo kudandia malori na mabasi kutoka mikoani huku wengine wakitumikishwa kazi za usafi wa kuosha magari hayo kwa ujira mdogo wa hadi shilingi 500.

"Hali hiyo inawashawishi kuvutiwa kubakia stendi hivyo tunaendelea kutoa elimu kwa makondakta kuacha kuwatumia watoto hasa wa kiume kwenye kazi za kuosha magari" amesema Ngowi akibainisha kuwa wengi wana umri kati ya miaka saba hadi 14.

Kamati hiyo inaundwa na viongozi mbalimbali wakiwemo maafisa maendeleo ya jamii, wenyeviti wa Serikali za mitaa, polisi, uongozi wa stendi ya Nyegezi, wafanyakazi kwenye mabasi na shirika la kutetea haki za watoto wanaoishi mazingira magumu la Railway Children Africa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa afua za Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu akizungumza na kamati ya ulinzi wa mtoto stendi ya Nyegezi jijini Mwanza.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu akizungumza na kamati ya ulinzi wa mtoto stendi ya Nyegezi jijini Mwanza.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu akizungumza na kamati ya ulinzi wa mtoto stendi ya Nyegezi jijini Mwanza.
Afisa Ustawi wa Jamii Kata ya Ngegezi, Edith Ngowi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kamati ya ulinzi wa mtoto Stendi ya mabasi Nyegezi jijini Mwanza.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi wa mtoto Stendi ya mabasi Nyegezi jijini Mwanza.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi wa mtoto Stendi ya mabasi Nyegezi jijini Mwanza.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu (katikati) akiwasili Ngudu wilayani Kwimba kuendelea na ziara ya kukagua afya mbalimbali zinazotekelezwa na Wizara hiyo.

HII HAPA SHOW KALI YA FALLY IPUPA KWA MWAKA 2024

 


 -  Les Ardentes 2024

Monday, August 19, 2024

WAFANYAKAZI WA BARICK WASHIRIKI CRDB MARATHON 2024

 


Wafanyakazi wa Barrick wakifurahi baada ya kumaliza kushiriki mbio hizo


Wafanyakazi wa Barrick wakishiriki kukimbia mbio za CRDB Bank Marathon 2024




Wafanyakazi wa Barrick wakishiriki kukimbia mbio za CRDB Bank Marathon 2024

Na Mwandishi Wetu.

Wafanyakazi wa kampuni ya Barrick nchini kupitia klabu zao za mchezo wa marathon wameshiriki katika mbio za msimu wa tano wa mbio za CRDB Bank Marathon, zilizofanyika jijini Dar es salaam.

Mbio hizo zililenga kuchangisha fedha kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watoto,huduma za afya kwa akina mama na vijana.

Wakimbiaji kutoka Barrick Runners clubs wamekuwa wakishiriki marathon mbalimbali zinazofanyika nchini na nje ya nchi hususani zinazolenga kuchangia kupambana na changamoto mbalimbali za kijamii.

Kampuni pia imekuwa na program za mazoezi kwa ajili ya wafanyakazi wake kwa ajili ya kuhakikisha wanakuwa na nguvu na afya bora pia imewekeza katika miundombinu ya michezo na mazoezi kwa ajili ya kuwawezesha wafanyakazi wake kushiriki michezo na mazoezi katika mazingira rafiki.

Dkt. BITEKO APONGEZA JITIHADA ZA CRDB Bank MARATHON KUSAIDIA WATOTO WAKINAMAMA NA VIJANA.

 

 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko (katikati), akiwa ameongozana na Waziri wa Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro (watatu kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila (wapili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (watatu kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB Bank Foundation, Martin Warioba (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wanne kushoto) pamoja na viongozi wengine wakianza mbio za kilometa tano katika kilele cha msimu wa tano wa CRDB Bank Marathon zilizofanyika viwanja vya farasi 'The Green Grounds' jijini Dar es salaam Agosti 18, 2024 na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 8,000.
Tanzania 18 Agosti 2024 – Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko ameipongeza taasisi ya CRDB Bank Foundation kwa kuendelea kuandaa mbio za CRDB Bank Marathon ambazo zimejielekeza katika kusaidia jitihada za serikali kuboresha sekta ya afya, kusaidia wenye uhitaji, pamoja na kukuza ustawi wa jamii.

Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo wakati wa kilele cha msimu wa tano wa CRDB Bank Marathon ambapo Shilingi Milioni 350 zimekusanywa kwa ajili ya kusaidia watoto wenye uhitaji wa upasuaji wa moyo Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI), huduma za afya kwa wakinamama wenye ujauzito hatarishi hospitali ya CCBRT, na uwezeshaji wa vijana.
“Niwapongeze kwa kuendelea kusaidia matibabu ya wakinamama na watoto wetu. Wakinamama ndio wamebeba uchumi wa Taifa letu. Lakini pia wakinama ndio waangalizi wa familia zetu hususani watoto. Hivyo ukiimarisha afya ya mama na watoto umeimarisha afya ya Taifa,” amesema Dkt. Biteko huku akisema Serikali na Watanzania wanaona jitihada hizo zinazofanywa na Benki ya CRDB kupitia CRDB Bank Foundation.
Akizungumza Waziri wa Sanaa, Utamaduni, na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema CRDB Bank Marathon imesaidia kwa kiasi kikubwa kuchochea ari ya michezo nchini. Dkt. Ndumbaro amesema mbio hizo zimekuwa jukwaa muhimu kwa wanariadha nchini kuonyesha vipaji vyao katika jukwaa la kimataifa kwani mbio hizo zimesajiliwa kimataifa na Shirikisho la Upimaji Mbio Kimataifa (AIMS) na Shirikisho la Riadha Duniani (World Athletic).

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema katika kiasi cha fedha kilichokusanywa; shilingi milioni 100 zitakwenda kusaidia watoto wenye uhitaji wa upasuaji wa moyo Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI), Shilingi Milioni 100 kusaidia huduma za afya kwa wakinamama wenye ujauzito hatarishi hospitali ya CCBRT, na Shilingi Milioni 150 uwezeshaji wa vijana.
Katika mbio hizo zawadi za jumla ya Shilingi Milioni 98.7 zimetolewa kwa washindi 60 wa mbio za kilometa 42, 21, 10, 5, pamoja na mbio za baiskeli za kilometa 65. Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB Bank Foundation, Martin Warioba amesema jumla ya washiriki waliojiandikisha mwaka huu ni 8,000 huku akisema lengo la mwaka kesho ni kupata washiriki 10,000 Tanzania, huku malengo ya washiriki Burundi na DRC wakiwa ni 3,000 kila nchi.

Mbio hizi zilizofanyika Dar es Salaam ni za tatu baada ya zile zilizofanyika nchini DRC, na Burundi. Nchini DRC mbio hizo zilifanyika tarehe 4 Agosti ambapo Dola za Marekani 50,000 zilikusanywa kusaidia kuboresha huduma za afya kwa watoto hospitali ya Jason Sendwe jijini Lubumbashi. Kwa upande wa nchini Burundi, mbio hizo zilifanyika tarehe 11 Agosti ambapo Faranga za Burundi Milioni 120 zilikusanywa kusaidia wahanga wa mafuriko mkoa wa Gatumba jijini Bujumbura.

Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya mbio hizo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa amewapongeza washindi wa mbio hizo, na kuwashukuru washirika wa mbio hizo wakiwemo kampuni za bima Sanlam na Alliance Life ambao ni washirika wakuu wa mbio hizo. “Tunawashukuru sana washirika wetu na wakimbiaji wote kwa kuungana nasi katika juhudi za kusambaza tabasamu kwa watoto walioathirika,” amesema Mwambapa.

Washindi wa mbio hizo Kilometa 42 upande wa wanawake ni Joyloyce Kemuma kutoka Kenya, upande wa wanaume mshindi ni Moses Nengichi kutoka Kenya. Kilometa 21 upande wa wanawake ni Sara Makera kutoka Tanzania, na upande wa wanaume ni Joseph Panga kutoka Tanzania. Kilometa 10 upande wa wanawake ni Hamida Nasor kutoka Tanzania, na upande wa wanaume ni Mao Hindo Ako kutoka Tanzania.
Sara Makera mshindi wa mbio za Kilometa 21 upande wa wanawake ameeleza furaha yake kushiriki katika mbio hizo na kusema kuwa ushindi wake ni sehemu ya kusaida matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo na  matibabu ya wakinamama wenye ujauzito hatarishi hospitali ya CCBRT.

 “Mimi kama mwanamke ninajisikia faraja kubwa kushiriki kusambaza tabasamu kwa watoto na wakinamama. Watu wanapaswa kufahamu kuwa afya bora ni haki ya kila mtoro na wakinamama pia hawastahili kupoteza maisha wakati wa kujifungua. Tunawashukuru CRDB Bank Foundation kwa kutuunganisha pamoja katika juhudi hizi,” amesema.








MBUNGE KOKA APANIA KUWAKOMBOA KIUCHUMI UVCCM KATA YA TANGINI

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 


Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwakomboa vijana katika kujikwamua kiuchumi ameahidi kuwasaidia vijana wa kata ya Tangini kuanzisha miradi mbali mbali ikiwemo kuwapatia pikipiki.

Koka ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na vijana wa UVCCM kata ya Tangini wakati  kufunga rasmi kikao cha baraza la vijana lenye lengo la kuweza kujadili mambo mbali mbali ikiwemo kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

"Kikubwa vijana wa kata ya Tangini mimi Mbunge wenu nipo pamoja nanyi lakini kitu kikubwa inabidi muungane kwa pamoja na mkiwa tayari mimi nitawasaidia katika miradi mbali mbali ikiwemo kuwapatia pikipiki ambayo itawasaidia kuwaingizia kipato,"alisema Koka.
Koka alisema kwamba ataendelea kuwa bega kwa bega na vijana hao wa kata ya Tangini katika kuwasaidia katika nyanja mbali mbali kwa lengo la kuweza kuleta chachu ya kimaendeleo.


Aidha Mbunge huyo  amewataka Vijana wa chama Cha mapinduzi UVCCM kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kwamba   atakuwa tayari kutoa ushirikiano Kwa kijana ambaye atajitokeza kugombe. 



Amesema kwamna atajisikia furaha kubwa kuona vijana nao wanajitokeza kwa wingi kugombea na kuongoza serikali  za kitaa na pia kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika mitaa yote.

Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa vijana Wilaya ya Kibaha mjini(UVCCM))  Ramadhani Kazembe  amewataka Vijana kukaa na kuangalia ni kijana gani wanayeweza  kumteua ili kugombea nafasi hizo na yeye atakuwa nao bega Kwa bega.