ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 19, 2024

MBUNGE KOKA APANIA KUWAKOMBOA KIUCHUMI UVCCM KATA YA TANGINI

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 


Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwakomboa vijana katika kujikwamua kiuchumi ameahidi kuwasaidia vijana wa kata ya Tangini kuanzisha miradi mbali mbali ikiwemo kuwapatia pikipiki.

Koka ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na vijana wa UVCCM kata ya Tangini wakati  kufunga rasmi kikao cha baraza la vijana lenye lengo la kuweza kujadili mambo mbali mbali ikiwemo kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

"Kikubwa vijana wa kata ya Tangini mimi Mbunge wenu nipo pamoja nanyi lakini kitu kikubwa inabidi muungane kwa pamoja na mkiwa tayari mimi nitawasaidia katika miradi mbali mbali ikiwemo kuwapatia pikipiki ambayo itawasaidia kuwaingizia kipato,"alisema Koka.
Koka alisema kwamba ataendelea kuwa bega kwa bega na vijana hao wa kata ya Tangini katika kuwasaidia katika nyanja mbali mbali kwa lengo la kuweza kuleta chachu ya kimaendeleo.


Aidha Mbunge huyo  amewataka Vijana wa chama Cha mapinduzi UVCCM kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kwamba   atakuwa tayari kutoa ushirikiano Kwa kijana ambaye atajitokeza kugombe. 



Amesema kwamna atajisikia furaha kubwa kuona vijana nao wanajitokeza kwa wingi kugombea na kuongoza serikali  za kitaa na pia kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika mitaa yote.

Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa vijana Wilaya ya Kibaha mjini(UVCCM))  Ramadhani Kazembe  amewataka Vijana kukaa na kuangalia ni kijana gani wanayeweza  kumteua ili kugombea nafasi hizo na yeye atakuwa nao bega Kwa bega.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.