Meya wa manispaa ya Moshi Zuberi Kidumu akitoa shukrani wa wakazi wa Moshi na viunga vyake waliohudhuria katika uzinduzi katika kampeni ya kutangaza vivutio vilivyopo katika hifadhi ya msitu Rau.
Mgeni Rasmi mkuu wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Kisare Makori akiwa na wageni wengine wakitazama moja ya chemchem za maji zilizo katika msitu huo.
Amesema rais Dkt Samia Suluhu amefungua fursa za Utalii kupitia filamu yake 'Royal Tour', hivyo ni vyema kuendelea kuunga mkono juhudi zake ili kuweza kuongeza idadi ya watalii nchini na ndiyo maana Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi wakishirikiana na Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS) Moshi wamezindua Kampeni ya Kutangaza Utalii ikolojia ndani ya Hifadhi ya Misitu wa Rau ili kuongeza idadi ya watalii.
Aliongeza kuwa mpaka sasa hivi hafurahishwi na idadi ndogo ya watalii wanaofika kutembelea msitu huo, lija ya ukaribu uliopo ambapo ni watalii 1,200 tu kwa mwaka hutembelea msitu huo.
Awali akisoma taarifa kwa niaba Mkuu wa hifadhi ya msitu Rau, Mhifadhi daraja la pili msitu wa Rau Zayana Mrisho, amesema ndani msitu huo kuna chemchem 20 ambazo zinapeleka kuwepo mito mikubwa 3 inayotiririsha maji kipindi chote cha mwaka.
Aidha amesema mito hiyo ni chanzo cha maji inayotumika katika kilimo cha umwagiliaji cha mpunga ambapo hekta takriban 3,000 hutegemea maji kutoka msitu huu.
"Msitu una vivutio vingi ikiwemo mimea pamoja na miti ya asili ambayo haipatikana katika maeneo mengine, ikiwemo Mti wa Mvule ambayo unazaidi ya miaka 200 ni mrefu kuliko yote barani Afrika," amesema.
Aliongeza kuwa utalii mkubwa unaofanyika katika msitu huo ni Utalii wa baiskeli, ibada, tafiti na masomo, picha, nyuki na kuangalia madhari ya misitu ndege na wanyama wanaopatikana ndani ya hifadhi.
Mazoezi ya viungo nayo yalikuwepo katika ya kuingia msituni.Waendesha baskeli nao walinyoosha viungo.
Mhifadhi daraja la pili msitu wa Rau Zayana Mrisho akiwakaribisha wageni.
Meya wa manispaa ya Moshi Zuberi Kidumu akiwasalimia wageni.
Mgeni Rasmi mkuu wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Kisare Makori (kushoto) akiwa pamoja na Meya wa manispaa ya Moshi Zuberi Kidumu (kulia) wakizindua utalii wa baskeli.
"Nawaomba waandaaji kuendelea kuandaa matamasha mengi zaidi yatakayosaidia wananchi wengi ili waweze kutembelea msitu huo na kujifunza mambo mbali mbali," amesema Meya Kidumu.
Hifadhi ya Misitu Rau ulianzishwa ukiwa na ukubwa hekari 3526, ambapo kwa sasa ni hekta 584 zimebaki kutokana uvamizi wa Wananchi na kuanzisha shughuli za kilimo.