Mkurugenzi wa Vigimark Hotel Mjini Shinyanga Abel Majige amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Alhamisi Agosti 24,2023 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan Nairobi nchini Kenya.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika familia, kesho jioni mwili utawasili uwanja wa ndege Mwanza na kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Kanda ya Bugando, Jumatatu mwili utafuatwa Bugando na kulala nyumbani Lubaga Shinyanga.
Jumanne Ibada katika kanisa la A.I.C.T na mwili kusafirishwa kwenda Salawe kwa ajili ya mazishi siku ya Jumatano.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.