ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 6, 2017

LOWASA NA LEMA WATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA WAFIWA | AJALI YA WANAFUNZI KARATU.


WATU 36 wamepoteza maisha huku wawili wakijeruhiwa vibaya kwenye ajali iliyohusisha gari namba T 871 BYS Toyota costa lililokuwa linasafirisha wanafunzi wa shule ya Luck vicent waliokuwa wanatokea jijini Arusha kwenda shule ya msingi Tumaini Iliyoko wilayani Karatu kwa ajili ya masomo.



Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo Amesema kuwa wanafunzi 33 wakiwemo walimu 2 pamoja na Dereva aliyekuwa anaendesha gari hilo.



Kamanda MKUMBO amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya SAA tatu asubuhi wakati mvua inanyesha ambapo mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana.



Amesema kuwa baada ya ajali hiyo miili yote 36 imepelekwa katika hospital ya Lutheran karatu kwa ajili ya kufanya utaratibu wa kuipeleka Mount Meru Arusha kwa ajili ya ndugu zao kuitambua na taratibu za mazishi ziendelee ambapo uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea.



Mkurugenz wa Jiji la ARUSHA Athumani Kihamia amewasihi wazazi pamoja na wana Arusha kuwa wavumilivu kwenye kipindi hiki kigumu cha msiba mzito uliotokea katika Jiji la Arusha



Naye Mwalimu wa shule ya msingi Luck vicent ambaye ndiye mlezi wa wanafunzi hao Bwana Efrem Jackson amesema kuwa watoto hao walikuwa wanaenda Karatu kwa ajili ya ujirani mwema na shule ya msingi ya Tumaini iliyoko Karatu kwa ajili ya masuala ya kimasomo.



Jumla ya watu waliokuwemo Ndani ya Gari hilo ni 38 waliopoteza maisha ni 36 wawili  ni majeruhi.

WANAFUNZI 31 WATHIBITISHWA KUFARIKI KATIKA AJALI ARUSHA.

Arusha. Kamanda wa Polisi, mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema wanafunzi 31 na walimu wao wamefariki katika ajali iliyotokea wilayani Karatu, ulipo mto Mlera.

Mkumbo ambaye yupo njiani akielekea wilayani Karatu amesema wanafunzi waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni wa shule ya mchepuo wa Kiingereza, iitwayo LackVicent ya mjini Arusha.

Taarifa zaidi kuhusu tukuio hili zitaendelea kuwekwa hapa katika chumba cha habari cha kidijital.

Friday, May 5, 2017

SUGU AMVAA TENA 'Bashite' BUNGENI SASA AMTAKA MWAKYEMBE AJE NA MAJIBU YA RIPOTI YA NAPE.


MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amemshambulia Bashite huku akisema kuwa mtu huyo alipaswa awe mahakamani na sio ofisini kwa madai kuwa amefoji vyeti vya elimu ya sekondari jambo ambalo ni kosa kisheria.
Hayo ameyasema leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akichangia hoja kuhusu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Aidha Sugu amemtaka Rapa ROMA Mkatoliki ajitokeze hadharani aeleze wazi kuhusu alivyotekwa na nani alihusika ili jamii ielewe na mamlaka husika iweze kuchukua hatua ikiwemo kuwabaini waliyotekeleza tukio hilo ambalo si la kibinadamu.
Sugu aliwageukia wasanii wa Filamu Bongo ambao hivi karibuni waliandama wakipinga uingizwaji holela wa filamu za nje ambazo wanadai zinaporomosha soko la filamu za ndani. Sugu amewataka wasanii hao waache kutumika kisiasa na badala yake wafate misingi ya kazi zao.

ANTONIO GUTERRES AITAKA BOKO HARAM IKOMESHE UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO.


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelitaka kundi la kigaidi la Boko Haram la nchini Nigeria kuhitimisha ukiukaji wake wa haki za watoto.
António Guterres amesema hayo katika ripoti yake kuhusiana na hatima ya watoto katika machafuko yanayoendelea kaskazini mashariki mwa Nigeria kutokana na mashambulio ya kundi la kigaidi la Boko Haram.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema katika ripoti yake hiyo kwamba,  kuna watoto wengi ambao wamekuwa wahanga wa ngono ambao wamechukuliwa mateka na Boko Haram na kutumikishwa kama watumwa wa ngono na kundi hilo.
 

António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
António Guterres ameeleza kuwa, hali wanayokabiliwa nayo watoto katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi la kigaidi la Boko Harama inasikitisha mno na kwamba, kuna haja ya kuchuliwa hatua zinazokazolifanya kundi hilo la kigaidi lihitimishe ukiukaji wake wa haki za watoto.

Inaelezwa kuwa, kwa uchache watoto 3900 wameuawa katika hujuma na mashambulio ya kundi la kigaidi la Boko Haram kuanzia Januari mwaka 2013 hadi 2016 huko nchini Nigeria na kwamba, kuna watoto wengine 7200 ambao wameuawa kinyama na wanamgambo hao.
Kundi la Boko Haram lilianzisha mashambulizi dhidi ya maeneo ya umma na taasisi za serikali huko kaskazkini mwa Nigeria mwaka 2009 na baadaye mwaka 2015 likapanua mashambulizi hayo hadi katika nchi za Chad, Cameroon na Niger.

Zaidi ya watu elfu 20 wameuwa hadi sasa katika mashambulizi hayo na mamilioni ya wengine wamelazimika kuwa wakimbizi.

TANZANIA YAPOKEA TUZO UMEME VIJIJINI,

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akipokea Tuzo kutoka kwa Meneja Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ensol, Hamis Mikate akizungumza wakati wa makabidhiano ya Tuzo. Kulia ni Meneja Miradi wa kampuni hiyo, Prosper Magali na Afisa wa Ensol, Magdalena Ally.
 Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini waliohudhuria tukio la upokeaji wa Tuzo. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara na Taasisi zake na wawakilishi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol baada ya kukabidhiwa Tuzo.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa nne kutoka kulia) katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara na Taasisi zake na wawakilishi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol baada ya kukabidhiwa Tuzo.
 Meneja Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali (kushoto) akipokea Tuzo ya Uwezeshaji wa Mazingira Bora ya Upatikanaji wa Umeme Vijijini kwa Nchi zinazoendelea kwa niaba ya Serikali kutoka kwa Mwenyekiti wa Sera ya Mtandao wa Kimataifa wa Nishati Mbadala (REN21) yenye makao makuu yake nchini Ufaransa, Profesa Arthouros Zervos.

Meneja Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali pamoja na washiriki kutoka nchi mbalimbali wakionesha Tuzo walizopokea kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Alliance for Rural Electrification katika hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika Lisbon, Ureno

TANZANIA YAPOKEA TUZO UMEME VIJIJINI
Jitihada za Wizara ya Nishati na Madini za kuhakikisha umeme unafika na kusambaa maeneo ya vijijini zimetambuliwa kimataifa hali iliyopelekea Serikali kupokea Tuzo ya Uwezeshaji wa Mazingira Bora ya Upatikanaji wa Umeme Vijijini kwa Nchi zinazoendelea.

Serikali imetunukiwa Tuzo hiyo mwezi Machi, 22 na Taasisi ya Kimataifa ya Alliance for Rural Electrification yenye Makao Makuu yake nchini Ubelgiji ambayo ilipokelewa na Meneja Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali kwa niaba ya Serikali katika hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika Lisbon, Ureno. Magali pia ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA).

Akikabidhi Tuzo hiyo Jijini Dar es Salaam, kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo; Magali alisema Tuzo hiyo imetolewa kwa kutambua mchango wa Serikali ya Tanzania wa kufikisha huduma ya umeme maeneo ya vijijini pamoja na uwezeshaji wa mazingira bora na rafiki kwa wawekezaji wanaosambaza umeme katika maeneo ya vijijini.

“Kwa mwaka huu, Serikali yetu imetambuliwa kwa kufikisha umeme vijijini na juhudi zake za kuhakikisha kunakuwa na mzingira rafiki kwa watoaji na wasambazaji wa huduma ya umeme vijijini,” alisema Magali.

Kwa upande wake Dkt.Mhandisi Pallangyo aliipongeza kampuni ya Ensol kwa kupokea tuzo kwa niaba ya Serikali na kuahidi kuendeleza ushirikiano na kampuni zote zinazojihusisha na usambazaji wa umeme maeneo ya vijijini.

Alisema Serikali itaendelea kuandaa mazingira rafiki kwa wawekezaji ili kutimiza azma ya kuhakikisha vijiji vyote vinafikiwa na huduma ya Nishati ya Umeme.
Aidha, Dkt. Mhandisi Pallangyo alizitaka kampuni nyingine zinazoshughulika na uzalishaji na usambazaji wa umeme vijijini kujiunga na Taasisi za Kimataifa ikiwemo ya Alliance for Rural Electrification ili kunufaika na fursa zinazopatikana kwenye Taasisi hizo.

Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na watendaji wa Wizara na Taasisi zake wakiongozwa na Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ensol, Hamis Mikate.

SWALI LA MBUNGE ZITTO KABWE LEO BUNGENI DODOMA.

Fahamu  swali la mbunge Mhe. Zitto Kabwe kuhusu taarifa ya utafiti wa mafuta na gesi kusini mwa ziwa Tanganyika. 

MJADALA MKALI WAIBUKA BUNGENI FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO.

Mvutano mkali umeibuka kuhusu suala la fedha za mfuko wa jimbo ambapo wabunge viti maalum wakitaka hizi fedha.

KESI YA MAUAJI YA KAMANDA BARLOW



Moja ya vielelezo vilivyobaki kama vithibitisho ni Radio call hii iliyo patikana katika shimo la maji taka ambayo ilikuwa ikitumiwa na marehemu kamanda Barlow, kabla haijafanyiwa usafi mnamo tarehe 9 October 2012...
NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza

MAHAKAMA kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza imetupilia mbali pingamizi  la shauri dogo kwenye kesi ya msingi ya mauaji ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa mwanza, Liberatus Barlow, lililokuwa likipinga kupokelewa kwa kielelezo namba 24 cha maelezo ya onyo kama ushahidi mahakamani hapo.

Pingamizi hilo liliwasilishwa jana  na wakili wa mshitakiwa wa sita, Maduhu Ngassa baada ya shahidi wa 16 Vedastus Pius ambapo upande wa mashitaka uliomba  kupokelewa kwa kielelezo hicho kama ushahidi.

Pingamizi hilo lilikuwa limejikita katika hoja mbili ambapo upande wa mshitakiwa ulidai kulikuwa na ukiukwaji wa sheria ya mashitaka kwa sababu maelezo yaliyotolewa siyo ya mshitakiwa hivyo sheria haikuzingatiwa na kulikuwa na ukiukwaji wa sheria ya ushahidi kwa sababu mshitakiwa hakupewa nafasi ya kufanya masahihisho kwenye maelezo yake na kwamba ilitumika nguvu.

Akitoa maamuzi ya pingamizi hilo, Jaji anayesikiliza kesi hiyo, Sirilius Matupa, amesema kifungu kilichotumika na upande wa utetezi hakiusiki na utoaji wa maelezo bali kinahusika wakati wa ukamataji ambapo hutoa haki ya mtu anayekamatwa na kwamba kifungu sahihi kinavchohusika na utoaji maelezo ni cha 50 (2) b (1) kinachomruhusu muandika maelezo kumpa fursa anayehojiwa kuita mtu atakayeshuhudia wakati wa utoaji maelezo.

“Sijaridhika na ushahidi uliotolewa kwamba kulikuwa na mazingira ya kutumia nguvu katika kutoa maelezo ingeonekana tofauti kama hakusomewa maelezo yake au kulikuwa na ubishi.

“Baada ya kupitia hoja zote na kwa ajili ya kutoathiri mtiririko wa ushahidi wa kesi ya msingi, baada ya kupima maelezo yote hayo sijapata shaka ya msingi kwamba kulikuwa na nguvu katika kutoa maelezo hivyo nimeamua niipokee hii statement (kielelezo) kiwe sehemu ya ushahidi na pingamizi hili linatupiliwa mbali,” alisema Jaji Matupa.

Maamuzi hayo ya Jaji Matupa yalitoa fursa kwa kesi ya msingi kuendelea kusikilizwa kwa shahidi wa 16 wa upande wa jamhuri kuendelea na ushahidi wake ambapo aliruhusiwa kuyasoma maelezo ya onyo ya mshitakiwa wa sita Abdalla Petro yenye kurasa 24 yakielezea namna ambavyo mshitakiwa huyo alivyoshiriki katika tukio la mauaji ya marehemu Barlow na mengine ya uhalifu wa kutumia silaha jijini Mwanza.

Shahidi huyo alifunga ushahidi wake na Jaji Matupa kuhairisha kesi hiyo ambapo itaendelea kesho  kwa ajili ya kusikilizwa na shahidi wa 17 upande wa mashitaka atatoa ushahidi wake mahakamani hapo.

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2017 AMOUR HAMADI AMOUR AKATAA KUZINDUA MRADI WA BWALO LA CHAKULA SHULE YA MSINGI LILONDO

Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru 2017 Amour Hamadi Amour amekataa kuzindua mradi wa Bwalo la chakula la shule ya msingi Lilondo iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma.

Taarifa iliyosomwa na Mwalimu mkuu wa shule hiyo Agnes Amlike inaonyesha kuwa kuwa jingo hilo lilianza kujengwa mwaka 2015 ,hali

Thursday, May 4, 2017

UEFA YADHAMIRIA KUBADILI UTARATIBU WA PENALTI.

Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA limesema linatathmini utaratibu wa kupigwa kwa mikwaju ya penalty baada ya mechi kuufanya uwe wa haki zaidi.

Shirikisho hilo tayari limeanza kufanyia majaribio utaratibu mpya.

Badala ya klabu kubadilishana mmoja baada ya mwingine, UEFA inatafakari uwezekano wa kufuata utaratibu sawa na unaofuatwa katika mchezo wa tenisi.

Utaratibu huo unafanyiwa majaribio katika michuano ya ubingwa wa Ulaya kwa wachezaji wa chini ya miaka 17 ambayo ilianza Croatia Jumatano.

Kwa sasa, baada ya atakayeanza kupiga penalti kuamuliwa kwa kurushwa kwa sarafu juu, baadaye huwa ni kupishana.

Mfano mchezaji wa timu A akianza, anafuata wa timu B kisha anarudi mchezaji wa timu A.

Utaratibu mpya unaitwa ABBA ambapo mchezaji wa timu A akianza, atafuatwa na wawili wa B kabla ya mchezaji wa A kupiga.

Sarafu bado itarushwa kuamua atakayeanza.

Pendekezo hilo linatokana na ugunduzi kwamba timu inayofuata kwa kupiga penalti wachezaji wake hukabiliwa na shinikizo zaidi, kwani kila mara huwafuata wapinzani.

Utafiti unaonesha kwenye matuta, klabu inayotangulia kupiga mkwaju imekuwa ikishindwa katika asilimia 60 ya michuano yote. CHANZO BBC SWAHILI.

JPM AFANYA UTEUZI TBS, PROFESA ALA SHAVU.

Rais Dr John Pombe Magufuli amemteua Profesa Egid Mubofu kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la viwango nchini TBS. 

MWENGE WA UHURU WAMULIKA CHANGAMOTO ZA VIFO VYA UZAZI.



Ili kupunguza vifo vinavyosababishwa na akina mama kujifungulia majumbani kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Amour Hemed Hemed amewataka watu wote wenye utamaduni huo kuachana nao ili kunusuru vifo vitokanavyo na uzazi.

Kiongozi huyo ametoa rai huyo Wilayani Ludewa kwa wakazi wa kijiji cha Madope mara baada ya kuzindua jengo la hospitali ya mama na mtoto lililogharimu zaidi ya shilingi Milioni 37 na kuwataka wanawake wa kijiji hicho wenye utamaduni huo kuelimishana juu ya madhara ya kitendo hicho.

Nao Wakazi wa kijiji cha Madope Wilayani Ludewa Mkoani Njombe ambao wamefanikiwa kujenga zahanati kwa ajili ya kurahisisha huduma za afya kwa kina mama na watoto wamesema wamekuwa wakitembea umbali wa zaidi ya kilomita 20 kupata huduma za afya hali ambayo iliwawia vigumu wajawazito.

Mwenge wa Uhuru umemaliza mbio zake Mkoani Njombe na kukabidhiwa Mkoani Ruvuma ambapo ukiwa mkoani Njombe umekagua, umezindua na kutembelea miradi 55 yenye thamani ya zaidi ya shilingi ya BILIONI 8 na milioni 674.

FIBA YARUHUSU MABINTI WA KIIRANI KUSHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA WAKIWA NA VAZI LA HIJABU


Shirikisho la Mpira wa Kikapu Duniani (FIBA) limetangaza kuafiki pendekezo la Iran la kutaka wanawake wa Kiislamu na mabinti wenye Hijabu wa Kiirani kushiriki katika michezo ya kimataifa ya mpira wa kikapu (basketiboli). 
Mahmoud Mashhoon Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  ametangaza kuwa, hatimaye Shirikisho la Mpira wa Kikapu Duniani (FIBA) limekubaliana na matakwa ya Iran ya wachezaji wake wa kike kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya mpira wa kikapu wakiwa wamejistiri kwa vazi tukufu la Hijabu. 
Ameongeza kuwa, uamuzi huo wa FIBA umetangazwa katika kikao cha shirikisho hilo kilichofanyika huko Hong Kong. Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kufuatia uamuzi huo, kuanzia Oktoba mwaka huu mabinti wa Kiirani sasa wataweza kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya mchezo huo wakiwa wamejistiri kwa vazi la Hijabu.

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Kikapu ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran
Ikumbukwe kuwa, Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Kikapu ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran kwa muda sasa haikuwa ikishiriiki katika mashindano ya kimataifa ya mpira wa kikapu kutokana na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Duniani (FIBA) kupiga marufuku wanawake wanaovaa Hijabu kushiriki katika mashindano yanayoandaliwa na shirikisho hilo. 
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Duniani (FIBA) lililazimika kuanzisha mchakato wa kuangalia uwezekano wa kuruhusiwa vazi la Hijabu baada ya shirikisho hilo kupokea malalamiko kutoka nchi kadhaa kufuatia marufuku yake ya Hijabu katika mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na shirikisho hilo.

ZAIDI YA ASILIMIA 70 YA WAPIGA KURA WANATARAJIWA KUSHIRIKI KATIKA UCHAGUZI WA RAIS IRAN


Uchunguzi wa maoni unaonesha kuwa, takriban asilimia 70.6 ya wananchi wa Iran waliotimiza masharti ya kupiga kura wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi wa 12 wa Rais humu nchini.
Asilimia takriban 63.5 ya walioshiriki kwenye uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na Kituo cha Utafiti cha Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB wameamua kuwa watashiriki katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 mwezi huu wa Mei na asilimia 7.1 wengine wamesema huenda wakashiriki kwenye uchaguzi huo.
Wagombea urais nchini Iran
Uchunguzi huo wa maoni umefanyika kwa kuwauliza maswali watu 38,000 walio na umri wa zaidi ya miaka 18 katika mji mkuu Tehran na katika miji mikuu ya mikoa ya Iran na pia katika miji mingine miwili yenye watu wengi pamoja na vijiji 10 kutoka katika kila mkoa wa Iran. Uchunguzi huo ulianza siku ya Jumapili na kumalizika juzi Jumanne (kuanzia Aprili 30 hadi Mei 2).
Asilimia takriban 23.6 ya waliojibu maswali waliyoulizwa wameamua hawatoshiriki na asilimia 1.2 wengine wamesema huenda wasishiriki. Asilmia 4.6 wengine wamesema hawajaamua iwapo watashiriki katika kupiga kura au la.


Grafu nayoonesha matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na IRIB kuhusu uchaguzi wa 12 wa rais wa Iran
Uchunguzi huo wa maoni umefanyika baada ya mjadala uliorushwa hewani mubashara kati ya wagombea sita wa urais, Ijumaa iliyopita na unaonesha kuongezeka idadi ya watu walioamua kushiriki kwenye uchaguzi baada ya mjadala huo.
Uchunguzi mwingine wa maoni uliofanywa na shirika la IRIB kabla ya mjadala huo ulikuwa umeonesha kuwa, asilmia 56.1 tu ya wapiga kura ndio waliokuwa na nia ya kushiriki kwenye uchaguzi huo.

WAVUVI WA 5 WAFA MAJI ZIWA RUKWA.


Sumbawanga. Watu watano wamekufa  maji katika Ziwa Rukwa lililopo mkoani Rukwa wakati wakiwa katika shughuli za uvuvi ziwani humo.

Tukio hilo lilitokea juzi wakati watu hao wakiwa katika shughuli zao za uvuvi katika ziwa hilo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Polycarp Urio akizungumza leo amesema kuwa watu hao walikuwa wakifanya shughuli za uvuvi katika ziwa hilo.

Urio amesema kuwa wavuvi walio kufa  maji ni wakazi wa Kijiji cha Ilanga, Kata ya Muze, tarafa ya Mtowisa, wilaya ya Sumbawanga mkoani humo.

Aliwataja wavuvi hao kuwa ni Paschal Kipeza(30), Peter William(45), Edward Emily(40), Frank Kadima(36) pamoja na Saliboko Damasi(28) wote hao wanasadikika kufa  maji baada ya boti walilokuwa wakifanyia uvuvi kuzama.

UTATA WAZUKA USHAHIDI KESI YA MAUAJI YA BARLOW.

NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza
USHAHIDI wa shahidi wa 16 Vedastus Pius, kesi ya mauji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow umeibua shauri dogo katika kesi kubwa mahakamani hapo.

Kesi hiyo imeibuliwa jana katika Mahakama kuu kanda ya Mwanza mbele ya jaji Sirilius Matupa na wakili wa kujitegemea Maduhu Ngasa baada ya kuonekan kweny baadhi ya nyaraka za ushahidi kufutika kwa tarehe husika jambo ambalo lilizua utata na kusababisha kuwepo kwa kesi ndogo.

Baada ya wakili  huyo kutoa hoja zake mtuhumiwa namba  sita Abdalla Petro Amos Abdalla Ndayi (22) alisimama kizimbani kwa ajili ya kutoa ushahidi wake.

Abdalla ameiambia Mahakama kuwa amefikishwa mahakamani kwa kosa la mauji kesi namba 192/2014   ambapo alikamatwa mnamo Novemba 2 mwaka 2012 saa 12 alfajiri na kwamba anahusika na mauji ya askari.

"Wakati nakamatwa sikuelezwa kosa langu na kupelekwa kituo kidogo cha polisi cha Pamba na nilipofika Pamba niliambiwa kuwa nimekuja kupanga biashara sehemu ambayo hairuhusiwi nikawekwa ndani siku mbili" amesema Abdalla.

Amesema mnamo Novemba 4 mwaka 2012 akatolewa na kupelekwa kituo kikubwa cha Nyamagana  na kuwekwa ndani  na baada ya hapo walifika askari watatu ambao hakuwafahamu na kumuita na kwamba hakuitika.

Amesema hakuitika kwa sababu hayakuwa majina yake na kwamba anaitwa Abdalla Petro  ndipo alitolewa kwa ajili ya kuchukuliwa maelezo.

" Kutokana na shahidi wa 16 hauwahi kuniohoji maelezo aliyokuwa akiyaandika ni ya kwake na baada ya hapo nilisaini kwa shinikizo ili nisiuwawe mnamo Novemba 5 mwaka 2012 na sio Novemba 3 mwaka 2012 kama shahidi alivyoeleza" amesema Abdalla.

Aidha baada ya mtuhumiwa kumaliza ushahidi wake  Jaji matupa aliwaruhusu mawakili wa pande zote mbili kutoa hoja zao kuhusiana na shauri hilo na Jaji aliihairisha kesi hiyo ambapo uamuzi utatolewa asubuhi hii kabla ya kuendelea na kesi kubwa ya mauji.

WANAOKATA RUFAA VYETI FEKI WAONYWA, SERIKALI YAMWAGA AJIRA 15000, MAGUFULI AMSAMEHE MBOWE.

Wanaokata rufaa vyeti feki waonywa, serikali  yamwaga ajira 15000, Sakata la vyeti feki: Ngoma bado mbichi, Magufuli amsamehe Mbowe, Maalim Seif : Kukaa na Lipumba! No way. 
 
Wizara kupunguza rufaa ya matibabu nje, Maalim Seif: Heri CCM kuliko Lipumba msaliti, serikali yashusha presha vyeti feki, mafuta yashuka bei, CCM yatoa tani 1000 za chakula cha msaada. Pata uchambuzi wa magazeti ya leo hapa.

Wednesday, May 3, 2017

DK. MWAKYEMBE: TELEVISHENI, REDIO KUSOMA VICHWA VYA HABARI TU KWENYE MAGAZETI KUANZIA KESHO.


MWANZA. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amezitaka Televisheni na Redio kuanzia kesho kusoma vichwa vya habari vya magazeti tu ili kuwavutia wasomaji kununua magazeti kwa habari kamili.

Dk Mwakyembe amesema hayo leo jijini Mwanza katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini ambapo pia amesema ataendelea kutetea na kulinda haki za waandishi wa habari huku akiwahakikishia ulinzi waandishi wa habari za uchunguzi.

Pamoja na mambo mengine Dk Mwakyembe amehakikisha kuwepo kwa ushirikiano wa kutosha kwa wamiliki wa vyombo vya habari  na kwamba ameagiza idara ya mawasiliano kutengeneza mawasiliano ya kudumu na wawe wanakutana angalau mara moja kwa mwezi kujadili udhaifu unaoweza kujitokeza na kuchukua hatua lengo ni kuwekana  sawa. 

Kuhusu kuzorota kwa hali ya uchumi kupitia mauzo ya magazeti amesema kuwa mchawi wa anguko hilo ni vyombo vya habari hususani radio na magazeti ambapo amevionya vyombo hivyo kuacha kusoma taarifa kwa undani kiasi cha kupoteza umuhimu wa mwananchi kununua magazeti. BOFYA PLAY KUSIKILIZA











RIPOTI YA HUMAN RIGHTS WATCH: MAKUMI YA RAIA WAMEUAWA KATIKA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI.


Makumi ya raia wameuawa katika Jamhuri ya Afrika Kati kufuatia kuzuka mapigano yanayoendelea kushuhudiwa nchini humo kati ya makundi ya wabeba silaha.
Hayo yamo katika ripoti ya Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch ambayo imefichua kuwa, raia wapatao 45 wameawa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kutokana na machafuko yanayoendelea kuikumba nchi hiyo.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa,  mapigano hayo yameyakumba zaidi maeneo ya miji ya Bambari, Ouaka, mkoa wa katikati na Makoum, kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Inaelezwa kuwa, mbali na mapigano hayo kusababisha mauaji makubwa yamepelekea pia wakazi wengi wa maeneo hayo kuwa wakimbizi.
Kikosi cha kusimamia amani cha UN katika Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika mgogoro, mwaka 2013 baada ya kuzuka mapigano ya kikaumu yaliyopelekea kuondolewa madarakani serikali ya rais François Bozizé. 
 
Hivi karibuni Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitaka kukomeshwa haraka iwezekanavyo, mapigano na vitendo vya utumiaji mabavu vya makundi ya wabeba silaha, Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Taarifa iliyotolewa na baraza hilo la usalama la Umoja wa Mataifa mbali na kuonyesha wasiwasi wake juu ya mapigano hayo nchini CAR, liliyataka makundi ya wabeba silaha hususan 'Harakati ya Kitaifa kwa Ajili ya kufufua nchi FPRC' na kundi la 'Umoja kwa ajili ya Amani ya Afrika ya Kati UPC' kukomesha uhasama na mapigano yao nchini humo.

TAASISI YA KILIMANJARO DIALOGUE YATAKA WANAHABARI KUTUMIA KALAMU ZAO KUDUMISHA AMANI NCHINI

 Mdhamini wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue, Habib Miradji (katikati) akiongoza mjadala jijini Dar es Salaam leo, kuhusu umuhimu wa wanahabari kuandika habari za kudumisha amani nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi hiyo. 9PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
  Mdhamini wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue, Habib Miradji (katikati) akiongoza mjadala jijini Dar es Salaam leo, kuhusu umuhimu wa wanahabari kuandika habari za kudumisha amani nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi hiyo. Kutoka kulia ni Rais wa taasisi hiyo, Ali Akkiz na Mshauri wa masuala ya Habari, Felix Kaiza.
 Mshauri wa Masula ya Habari, Felix Kaiza akielezea umuhimu wa wamiliki wa vyombo vya habari kuweka utaratibu wa mafunzo ya ndani (In House Training) kwa waandishi wa habari ili kuinua weledi pia alishauri kuwepo na Exchange Program kati ya vyombo vya habari nchini na nje ya nchini jambo ambalo huwaongezea uwezo wanahabari.
 Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten, Esther Zaramula akielezea kwenye mjadala huo jinsi alivyonufaika na mpango wa kubadilishana uzoefu
 Habib Miradji akisisitiza jambo wakati wa mjadala huo ambapo alifafanua zaidi umuhimu wa wanahabari kuandika habari kwa kufuata maadili na kusimamia kwenye ukweli.

Pia katika kongamano hilo waliwaasa wanahabari kutojiingiza katika mkumbo wa kuingizwa mifukoni mwa wanasiasa na matajiri kwa kuandika habari za kuwasifia wao badala ya maslahi ya wananchi.
 Mwandishi wa habari, Ezekiel Kamwaga  akielezea umuhimu wa wanahabari kujiendeleza kielimu pamoja na vyombo vya habari kubadilika kwa kwendana na kasi ya mabadiliko ya kizazi hiki cha maendeleo ya teknolojia ya habari.
Rais wa taasisi ya Kilimanjaro Dialogue, Ali Akkiz aktoa shukrani kwa wanahabari walioshiriki kwenye mjadala huo uliofanikiwa.