WATU 36 wamepoteza maisha huku wawili wakijeruhiwa vibaya kwenye ajali
iliyohusisha gari namba T 871 BYS Toyota costa lililokuwa linasafirisha
wanafunzi wa shule ya Luck vicent waliokuwa wanatokea jijini Arusha
kwenda shule ya msingi Tumaini Iliyoko wilayani Karatu kwa ajili ya
masomo.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoani Arusha
Charles Mkumbo Amesema kuwa wanafunzi 33 wakiwemo walimu 2 pamoja na
Dereva aliyekuwa anaendesha gari hilo.
Kamanda MKUMBO amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya SAA tatu
asubuhi wakati mvua inanyesha ambapo mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo
hakijajulikana.
Amesema kuwa baada ya ajali hiyo miili yote 36 imepelekwa katika
hospital ya Lutheran karatu kwa ajili ya kufanya utaratibu wa kuipeleka
Mount Meru Arusha kwa ajili ya ndugu zao kuitambua na taratibu za
mazishi ziendelee ambapo uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea.
Mkurugenz wa Jiji la ARUSHA Athumani Kihamia amewasihi wazazi pamoja na
wana Arusha kuwa wavumilivu kwenye kipindi hiki kigumu cha msiba mzito
uliotokea katika Jiji la Arusha
Naye Mwalimu wa shule ya msingi Luck vicent ambaye ndiye mlezi wa
wanafunzi hao Bwana Efrem Jackson amesema kuwa watoto hao walikuwa
wanaenda Karatu kwa ajili ya ujirani mwema na shule ya msingi ya Tumaini
iliyoko Karatu kwa ajili ya masuala ya kimasomo.
Jumla ya watu waliokuwemo Ndani ya Gari hilo ni 38 waliopoteza maisha ni 36 wawili ni majeruhi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.