ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 23, 2009

FLASH BACK PICTURE WIKI HII

IJUMAA IKO PALE NA ITAENDELEA KUWA PALE NA KAMA KAWAIDA YA BLOGU HII KILA IJUMAA KUANIKA MOJA YA PICHA ZA LONGI.... CHEKISHIA HII NI YA WAJANJA WA MJINI, KUTOKA KUSHOTO NI BLAZA MWITA WA VSS ENTERTAINMENT (chini kakugongea kitu cha zico), DJ SUMMER DANCE (Dj summer dee) NA JACKOB USUNGU (Dj young millionaire, aliyekuwa akiendesha roving dj STAR TV). SWALI NI KWAMBA POZI HILI WANATAFAKARI NINI :-
@ KUNA JAMAA ALITAMBAA NA MKWANJA WAO?
@ JENGO LA DISCO LILIKUWAKWENYE MPANGO WA KUBOMOLEWA?
@ AU WALIPATA TAARIFA ZA MASIKITIKO?
NITUMIENI MASWALI ktk email hii albertgsengo@yahoo.com
HAITOISHIA HAPO NITAWATAFUTA WAO WENYEWE WANAMBIE........ kisha ntakuanikia mzazi.

FIESTA ONE LOVE 2009


NGOMA INAENDELEA KUSONGA NA KILA INAKORINDIMA INAACHA SIMULIZI.
KUWA MAKINI PINDI INAPOZURU MKOA UNAOISHI AU HATA UKIISIKIA MKOA WA JIRANI HIMA ISIKUPITE.

MISS TANZANIA KARIBU ROCK CITY

KONA YA AIR PORT ILEMELA
AIR PORT ILEEEEEEEE
HUYO BI DADA HAPO PEMBENI ALIYE GONGA MSIMBAZI ALIKUWA ANAPIGA SALUTI?


WATU WA MWANZA WAKIKUBALI JAMBO HUWA HAWAFICHI NA WAKIKATAA WAMEKATAA HASWAA!! VODACOM MISS TANZANIA MIRIAM GERLARD NYOTA YAKE IKO SAWA! KWANI AMEPATA MAPOKEZI MAKUBWA HOME KUANZIA AIR PORT (NA HIVI KADOGO NA PARKING KAKISAMJO) HAKUKUWA NA PARKING PALE ILIBIDI WENYE MAGARI YAO WAPAKI MITA KADHAA KUTOKA AIR PORT ILIWAPATE SHUHUDIA HATUA KWA HATUA, POZ KWA POZ.
YOTE TISA MAMBO YOTE LEO IJUMAA (23/10/2009) PALE NYUMBANI HOTEL BURUDANI KUPAMBWA NAYE ISMAIL, MRISHO MPOTO AKA MJOMBA NA PHILBERT KABAGO.FASHION SHOW YA MAVAZI TOKA KWA
WHITNEY FASHION NA FLORA BR. SHOP TIKETI YAKO MKONONI UNCHOMA NDANI.SHUGHULI NZIMA IMEANDALIWA NA VODACOM NA KURATIBIWA NA FLORA TALENT PROMOTION YA JIJINI MWANZA.

Thursday, October 22, 2009

HAPA VODACOM MISS TZ HAPA BSS WINNER



MAPOKEZI MAKUBWA LEO ALHAMIS WANAPOTINGA HOME.
-VODACOM MISS TZ 2009 MARIAM GERALD (MWANZA) NA
-MSHINDI WA BONGO STAR SEACH 2009 PASCAR CASSIAN (MWANZA). BAADA YA HAPO MPANGO MZIMA WA SHEREHE NA BURUDANI ZAIDI IKISHEHENI KILA NAKSHI KUFANYIKA KESHO IJUMAA 23/10/2009 NYUMBANI HOTEL KIINGILIO SH 30,000/= CHAKULA NA VINYWAJI, TIKETI ZINAPATIKANA OFISI ZA CLOUDS FM MWANZA, FLORA SALON, NYUMBANI HOTEL, NA WHITNEY FASHION SHOP. CHUKUWA TIKETI YAKO MAPEMA UKUMBI UNA IDADI MAALUM.

KILIMO KWANZA KWA KASI HII "MBADO SIJAONA"......


KAMA NI ARDHI TENA ILIYONA RUTUBA TUNAYO, ILA SASA WAKULIMA TULIO NAO WENGI NI WALE WANAOLIMA ILI WAPATE MLO WA SIKU(PEASANT) NA SI KWAMBA WANALIMA KWAAJILI YA KUPELEKA MAZAO SOKONI (COMMERCIAL FARMERS).NA WALIO WAKULIMA WA UKWELI NI MASIKINI HIVYO HAWAZIMUDU BEI ZA PEMBEJEO ZA KISASA, NA HATA ZILE ZA MKOPO KUZIPATA ZINAMLOLONGO MREFU WA KUKATISHA TAMAA.
TANZANIA INA ENEO LA EKARI MILIONI 94.4 NA KATI YA HIZO, MILIONI 44.4 NDIZO ZINAZOFAA KWA KILIMO, LAKINI HADI SASA NI EKARI 10.8 TU ZINAZOTUMIKA KWA KILIMO NA KWAMBA ZAIDI YA ASILIMIA 70 YA WAKULIMA WANALIMA KWA JEMBE LA MKONO, ASILIMIA 20 WANATUMIA WANYAMA, NA ASILIMIA 10 TU NDIYO WANATUMIA TREKTA.
"KWA MPANGO HUU KUFIKIA MAPINDUZI YA KILIMO NI NDOTO".

NAZITAMBUA SANA JUHUDI ZA SERIKALI YETU KUHAKIKISHA INATIMIZA KAULI MBIU YAKE YA KILIMO KWANZA. TUMESIKIA MATREKA MADOGO NA PEMBEJEO NYINGINE ZINAVYOGAWIWA. TATIZO NI KWAMBA NCHI HII NI KUBWA NA KASI INAYOTUMIKA HAIRIDHISHI.......itaendelea.

Tuesday, October 20, 2009

BUSTANI YA EDENI NDANI YA JIJI LA MWANZA

NI ENEO LILILOKO PEMPEZONI MWA BARABARA YA MAKONGORO KARIBU NA KITUO CHA DALADALA KINACHOITWA CLINIC, PEMBEZONI MWA ZIWA VICTORIA, NI ENEO AMBALO KILA MWEKEZAJI ALIKUWA AKILITOLEA MACHO AKITAMANI KUMILIKISHWA ILIAPIGE MZIGO. HATIMAYE KUPITIA ZABUNI MWEKEZAJI KAPATIKANA, KWA MUJIBU WA MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA BW. WILSON KABWE AKIONESHA MICHORO SAMBAMBA NA MENGINEYO HAPA KUTASHUSHWA BONGE LA BUSTANI YA KISASA YENYE HUDUMA ZOTE ZA VYAKULA, VINYWAJI NA MABURUDANIZ. HATUA ZINAZOFANYIKA HIVI SASA NI KUSAMBAZA UDONGO NA KUUSHINDILIA TAAAARATIBU ..... KISHA....

Monday, October 19, 2009

KIMOJA ZAIDI KWA MAUNDA ZORO


ANAUJASIRI SANA MBELE YA WANYAMA HASA WAFUGWAO. YUKO FREE KUWALISHA, KUKAANAO KARIBU KWA STYLE NA STYLE HUYU NI MSANII MAARUFU AFRIKA MASHARIKI MAUNDA ZORO.

HATUOGI NA KUNG'AA SISI TU! HATA USAFIRI



HIKI NI KITUO MOJAWAPO MAARUFU MJINI MUSOMA KINACHOTOA HUDUMA ZA GARAGE NA UOSHAJI MAGARI, PEMBENI YAKE KUNA BANDA LA CHIPS+SODA SEHEMU SWAFI KIMTINDO KWA POZI. PICHA YA KWANZA JUU NI GARI LA MATANGAZO YA MOJAKWA MOJA CLOUDS FM LIKIKOSHWA NDANI YA ZIARA YA FIESTA MARA, NALO LILIIFANYA SEHEMU HII KAMA BAFU LAKE.

NI UNYAMA GANI HUU?


ZIARA YA TAMASHA LA FIESTA ONE LOVE 2009 NCHINI TANZANIA SAMBAMBA NA KUTOA BURUDANI KWA WATU WAKE TAMASHA HILI LIMEKUWA KICHOCHEO KATIKA KUSUKUMA MAENDELEO YA JAMII.. KWA KUSAHIHISHA PALE PANAPOKOSEWA NA KUFUKUNYUA UOZO UFANYWAO NA WANAJAMII HATA VIONGOZI WAO KWA MADHUMUNI YA KULETA MABADILIKO.
HILI LINAWEZESHWA KUPITIA WANAHABARI WAKE ZIARANI. AMBAPO WAANDISHI WAKE MBALI NA KUELEZEA MASHAMSHAM YA TAMASHA HILO VILEVILE WAMEKUWA WAKIELEZEA NAMNA WANANCHI WA MAENEO ZIARA HIYO INAPOPITA WANAVYOISHI.
KAMA ULISIKILIZA VIZURI LEO TENA NA DINA MARIOUS CLOUDS FM KIPENGELE CHA HEKAHEKA NA GEA HABIB, HUYU NDIYE MTOTO SIMULA MAGATHI (MIEZI 5) WA MKOANI MARA ALIYEKATWA VIGANJA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA NA MTU ASIYEJULIKANA KISA VINA MICHORO YA MIKUNJO HERUFI M. AKISIMULIA TUKIO HILI BIBI WA MTOTO HUYU NYAPAMBA MAGATHI AMESEMA ILIKUWA NI KTK SHUGHULI ZA MAISHA AMBAPO ALIMWACHA AKIWA AMELALA HUKU MTOTO MWINGINE MKUBWA AKICHUNGA NYUMBA ALIPOREJEA AKAKUTA CHUMBA KIMEJAA DAMU NAKUJIONEA KILICHOTOKEA ASIJUE KIMETENDEKA VIPI, ALIYE FANYA UNYAMA HUU MPAKA SASA HAJAPATIKANA NA HAKUNA JUHUDI ZOZOTE ZINAZOFANYWA NAJESHI LA POLISI KUPELELEZA HATIMAYE MBAYA KUBAINIKA. "INATISHA INAHUZUNISHA" MTOTO SIMULA MAGATHI ANAISHI NA BIBI YAKE KWANI MAMA MZAZI WA MTOTO HUYU NYASATO SIMULA NI MGONJWA WA AKILI AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MKOA WA MARA. PICHANI MTOTO SIMULA MAGATHI AKIWA USINGIZINI NDANI YA HOSPITALI KUU YA MKOA WA MARA AMBAPO ANAPATA MATIBABU. UNYAMAGANI HUU.

EEH MOLA WANGU! WANADAMU NIMEWATENDA NINI?


LAITI KAMA MTOTO HUYU SIMULA MAGATHI (MIEZI 5) ANGEKUWA ANAJUA KUONGEA KAULI NYINGI ZA MACHUNGU ZENYE HUZUNI NA SIMANZI TUNGELIZISIKIA TOKA KWAKE LAKI LAAH...NI MTOTO MCHANGA HAJUI CHOCHOTE MASKINI, ANAUMIA TU ASIJUE KITU GANI KIMEMSIBU KUMBE WABAYA WENYE AKILI ZILIZOZIDI UROHO ZAIDI YA UROHO HATA WAKAPOTEZA UTU WAMEONDOKA NA VIGANJA.

NILISHINDWA KUJIZUIA NAMI MACHOZI YALINIMWAGIKA..


ALIKUWA NA MAZOEA YA KUNYONYA KIDOLE TANGU KUZALIWA KWAKE, NILIPOFIKA HOSPITALI NILISUBIRI MPAKA AAMKE, ALIPOAMKA TU! AKAPELEKA MKONO MDOMONI HIVYO AKAWA ANAFYONZA BANDEJI, ALIVYOENDELEA KUFYONZA KUKISAKA KIDOLE ASIKIONE AKAJITONESHA DAMU IKAWA INAVIA BANDEJINI, MAUMIVU YAKAMZIDIA AKAANZA KULIA......OOOOOHGH....!!!!!
MWANANGU MWENYEZI MUNGU ATAKUPIGANIA.