ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 14, 2014

HIVI NDIVYO VUNJA JUNGU LA MWANZA LITAKAVYO KUWA...!!

Vunja jungu 2014 safari hii Villa Park inakuletea Mkali Nani kati ya Bendi mbili za kisasa Bodaboda Band ya mwanamuziki Kidumu toka nchini Kenya na Malaika Band yake Cristian Bella toka nchini Tanzania.
Ni Ijumaa 27/06/2014.
 ....Unakosaje??....!!!

MAENDELEO YA KWIMBA YATALETWA NA WANAKWIMBA WENYEWE: ASEMA HAMISI MZEE.

Mkuu wa wilaya ya kwimba ambaye vilevile ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo Hamisi Mzee akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa idara, viongozi wa dini toka madhehebu mbalimbali na baadhi ya wakulima mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kwanza cha mwaka huu kujadili maendeleo ya wilaya, chakula, ulinzi na  usalama.
PICHA NA ZEPHANIA MANDIA 
Katika kikao hicho Mkuu wa wilaya ya Kwimba Bw. Hamisi Mzee amesisitiza kuimarisha ulinzi shirikishi ndani ya jamii, akiwaasa viongozi wa dini kuweka msisitizo katika ibada zao na kukazia elimu ya kuepuka masuala ya imani potofu inayo chochea mauaji na ukatili kwenye jamii pamoja na kuasa vijana kuepukana na madawa ya kulevya.

Ili kuwa na jamii yenye afya, amani na maendeleo  amewasisitiza wananchi wa wilaya ya hiyo kuzingatia kanuni bora za kilimo kinachozingatia hali ya hewa na jiografia ya maeneo kwa wakulima hao kulima mazao yanayo stahimili ukame kama mtama kwa chakula, alizeti na pamba kama zao la biashara.

COCACOLA YAPATA WASHINDI WENGINE 7 WA LUNINGA ZA KISASA KUSHUHUDIA KOMBE LA DUNIA.

Marco Masaka akiongea na waandishi wa Habari katika viwanja vya Cocacola jijini Mwanza wakati wa kutangaza washindi wa Tv bapa za shindano la Jionee mwenyewe Kombe la Dunia 2014 Brazil.
Kubebeka Japhet ambaye ni Training Manager wa Cocacola Mwanza akimkabidhi zawadi ya Tv Bapa aina ya Sony mshindi toka Sengerema Bi. Jacquline C Ngaiza.
Kubebeka Japhet ambaye ni Training Manager wa Cocacola Mwanza akimkabidhi zawadi ya Tv Bapa aina ya Sony mshindi toka Tabora Nzega johnson Kubakulija.
Kushoto ni Kelvin Matindiko ambaye ni Even Coordinator akimkabidhi Mussa Inano Chacha kutoka Mabatini.
Kushoto ni Kelvin Matindiko ambaye ni Even Coordinator akimkabidhi zawadi ya Tv Pambano Joseph magembe kutoka Sapiwi Bariadi. 
Kulia Meneja Masoko Kanda ya ziwa Marco Masaka akikabidhi zawadi kwaRevocatus Mwinamila kutoka Runzewe Bukombe mkoa wa Geita.
Kushoto ni Kelvin Matindiko ambaye ni Even Coordinator akimkabidhi zawadi ya Tv kwa Limbu Nghugulu Ilekebu kutoka Mkula Busega.
Marco Masaka akimtunukisha zawadi Bahame Erasto kutoka Chinfunfu wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza.
 Ni picha ya washindi wa Tv Bapa pamoja na viongozi wa Nyanza Botling Co.Ltd
 
PICHA ZOTE  NA ZEPHANIA MANDIA.

UHOLANZI YAIFUNZA SOKA UHISPANIA

Uholanzi iliinyeshea Uhispania mabao 5-1.
Mabingwa watetezi wa kombe la dunia Uhispania wameambulia kichapo cha mabao 5-1 mikononi mwa timu walioishinda katika fainali ya kombe la dunia huko Afrika Kusini miaka minne iliyopita.
Kabla ya leo Uhispania ilikuwa haijashindwa katika dakika 476 ya mechi za kombe la dunia.
Mabao hayo ni zaidi ya mabao yote waliofungwa katika mchuano wa Euro na kombe la dunia la mwaka wa 2010 huko Afrika Kusini.
Uholanzi ilitoka nyuma baada ya Xavi Alonso kuiweka Uhispania mbele kwa mkwaju wa penalti baada ya Diego Costa kuangushwa katika eneo la hatari.
Hata hivyo Robin van Persie aliisawazishia Uholanzi kwa mkwaju wa kipekee wa kichwa dakika moja tu kabla kipindi cha kwanza hakijakamilika.
Casillas alisababisha bao la Nne
Na hapo ndipo mkoko ulialika maua .
Mabingwa hao wa dunia hawakuwa na majibu ya wimbi baada ya wimbi ya mashambulizi kutoka Uholanzi Arjen Robben Robin van Persie na Wesley Sneijder waliposhirikiana kwa karibu na juhudi zao zikazaa matunda .
Arjen Robben aliiweka Uholanzi mbele kunako dakika ya 53.
Hata hivyo masihara ya kipa Iker Cassillas yalipelekea RVP kufunga bao lake la pili na hivyo kumhakikishia kocha Van gal alama tatu muhimu katika mechi yao ya kwanza ya kundi lao.
Robben kwa upande wake aliidhalilisha safu ya ulinzi ya Uhispania na kufuma bao lake la pili na la tano kwa kocha Van Gaal.

Kufuatia kichapo hicho Mabingwa hao watetezi walishuka hadi nafasi ya mwisho kwenye kundi B wakiwa wametinga idadi kubwa ya mabao ikilinganishwa na Australia na Chile .
KWA HISANI YA BBC SWAHILI.

Friday, June 13, 2014

UZINDUZI WA KOMBE LA DUNIA 2014 BRAZIL 3 Croatia 1.


Brazil iliyotoka nyuma kwa bao la kujifunga toka kwa Marcelo ilitulia na kusawazisha makosa hatimaye kuilaza Croatia 3-1, katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la dunia 2014, inayofanyika mwaka huu nchini Brazil.
Wenyeji wa kombe la dunia Brazil walitoka nyuma na kuilaza Croatia mabao 3-1 katika mechi ya kufungua fainali ya dimba la mwaka huu iliyochezwa katika uwanja wa Sao Paolo (Arena de Sao Paulo).
Mechi hiyo ilikuwa ikitizamwa na mashabiki 65,000 uwanjani humo baada ya kushuhudia tafrija ya ufunguzi iliyotizamwa na watazamaji zaidi ya bilioni moja kupitia kwa runinga
Wenyeji Brazil walitazamiwa kufunga bao la kwanza mapema katika mechi hiyo lakini uwanjani mambo yalikuwa tofauti ,Marcelo alijifunga mwenyewe na kuiweka Croatia mbele baada ya dakika 11 pekee ya kipindi cha kwanza .
Wenyeji waliotamaushwa na bao hilo walikuwa na matumaini kuwa kiungo machachari anayechezea Barcelona ya Uhispania Neymar atawaongoza ''the samba boys'' kutwaa taji lao la sita la dunia nyumbani.
Na nyota huyo hakuboronga alitumia kila mbinu ikiwemo kumbo iliyompelekea kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano na refarii kutoka Japan Yuichi Nishimura.
Hata hivyo dakika chache tu baada ya kuonyeshwa kadi hiyo ya njano Neyma alijifurukuta na kuisawazishia Brazil katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza.
Mchezaji huyo wa mwenye umri wa miaka 22 aliiweka Brazil Mbele zikiwa zimesalia dakika 19 mechi hiyo kukamilika baada ya refarii kutoka Japan
Nishimura kupiga kipenga na kuashiria penalti baada ya Dejan Lovren kuonekana kama aliyemtega Fred katika eneo la lango.
hata hivyo picha za runinga zilizorejelea mara kadhaa hazikuonesha kama Lovren alimgusa Fred.
Wachezaji wa Croatia walijaribu kumshawishi mjapan huyo kuwa haikuwa kweli fred alikuwa amejiangusha lakini maoni yao hayakusikika.
Cameroon kukabiliana na Mexico hapo kesho..
Neymar kwa mara ya kwanza katika mechi hiyo aliiweka Brazil mbele kufuatia mkwaju huo wa penalti.
Vijana wa Luiz Scolari hawakuwachia hapo waliendelea kushambulia lango la Croatia na juhudi zao zilizaa matunda katika kipindi cha ziada Oscar alipompata kipa wa croatia ameduwaa na kufutamatisha kichapo hicho kunako dakika ya 91 .
Kufuatia ushindi huo wenyeji hao sasa wamejikita katika nafasi ya kwanza katika kundi A wakiwa na alama tatu.
Cameroon na Mexico zinashikilia nafasi ya pili na tatu katika kundi hilo .

Timu hizo zitakabiliana hapo Kesho.
Maandishi hisani ya BBC Swahili.

MASHINDANO YA NGUMI YA MEYA CUP KUANZA IJUMAA CCM KATA 15 TEMEKE

Kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli akifafanua jambo wakati wa upimaji uzito kwa mabondia.
Bondia Amir Shekhe akipima uzito kabla ya kushiliki mashindano ya meya cup yatakayoanza ijumaa katika ukumbi wa ccm kata 15 temeke kulia ni Lemmy Ngabo.
Bondia Titas kanje wa amana ilala akipima uzito kwa asjili ya kushiriki mashindano ya meya cup yanayoanza kesho katika umkumbi wa ccm kata ya 15 temeke jijini Dar es salaam. 
Mambondia wakipanga foleni kwa ajili ya kuonana na dokta kabla ya mpambano wa meya cup utakaoanza ijumaa katika ukumbi wa ccm kata ya 15 temeke dar es salaaam. picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com

AFLEWO KUFANYA MKESHA KWA AJILI YA KUIOMBEA TANZANIA NA AFRIKA


Mchungaji Abel Orgenes (wa kwanza kulia) wa Kanisa la International Evangelism akiongea machache na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza mkesha utakaofanywa na Huduma ya AFLEWO ambao utakuwa wa kusifu na kuabudu na maombi kwa ajili ya Afrika na Tanzania. Anayefuatia ni Mchungaji Fred Okello wa Kanisa la Upper Room Ministries Tz, Mchungaji Deo Lubala wa Kanisa la Word Alive pamoja na mwenyeji wao Mchugaji Paul Safari wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste.
Mchungaji Abel Orgenes (wa kwanza kulia) wa Kanisa la International Evangelism akiendelea kufafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza mkesha utakaofanywa na Huduma ya AFLEWO ambao utakuwa wa kusifu na kuabudu na maombi kwa ajili ya Afrika na Tanzania. 
Mchungaji Deo Lubala (katikati) wa Kanisa la Word Alive akiongea machache na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza mkesha utakaofanywa na Huduma ya AFLEWO ambao utakuwa wa kusifu na kuabudu na maombi kwa ajili ya Afrika na Tanzania. Anayefuatia kulia ni Mchungaji Fred Okello wa Kanisa la Upper Room Ministries Tz na mwenyeji wao Mchugaji Paul Safari wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste.
Huduma ya AFLEWO imeandaa mkesha wa kusifu na kuabudu na maombi kwa ajili ya Afrika na Tanzania. Waimbaji zaidi ya hamsini kutoka makanisa mbali mbali watakuwa kwenye jukwaa moja wakisifu Mungu. Waumini na Wachungaji na maaskofu watakusanyika kumsifu na kumuomba Mngu kwa ajili ya taifa la Tanzania hasa kwa ajili ya mchakato wa katiba na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani 2015.
Mkesha huu maalum utafanyika kesho Ijumaa Juni 13, 2014 katika kanisa la City Christian Center, Upanga jijini Dar es Salaam (CCC) lililoko karibu na Chuo Kikuu cha Mzumbe. Kutakuwa hakuna kiingilio, watu wote mnakaribishwa kusifu na kuabudu.

Thursday, June 12, 2014

Wednesday, June 11, 2014

HABARI MBAYA POLISI AUAWA NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA UVAMIZI WA KITUO CHA POLISI KIMANZICHANA MKOANI PWANI

**TAHADHARI**
.!!!...TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI ZA KUTISHA...!!!

Mnamo 11/06/14 majira ya 0100hrs huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani, watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema walivamia kituo kidogo cha Polisi Kimanzi Chana huku wakikimbia wakiwa na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada. 
Cha kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye amefahamika kwa jina la JOSEPH NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha SMG ikiwa na risasi 30. Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana. Askari Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali wilaya ya Mkuranga. 

Askari mwingine aitwaye VENANCE amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la mguu wa kulia. Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni. 

Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye VERONICA MUSIME, anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu ya kina. 

TAHADHARI; Vituoni tuwe makini sana na stahili hii ya ujambazi; HESHIMA PEKEE kwa marehemu na majeruhi hawa ni kuwapata watuhumiwa wote na silaha walizoiba bila kuchelewa. Bila kujali mkoa ulipo, taarifa za haraka tunatarajia kupata toka kwako kuhusiana na wahusika wa tukio hili. AMEN

VURUGU ZA WAMACHINGA MWANZA MABOMU YA MACHOZI YARINDIMA ZAIDI YA SAA 3, BIASHARA ZAFUNGWA KABISA.

Jeshi la wananchi lilitoa askari wake wa kijeshi “MP” kuimarisha ulinzi kwenye vitengo vya mabenki, ofisi za serikali na maeneo nyeti ili kutokwaza shughuli za kila siku kuendelea.
KATIKATI ya jiji la Mwanza leo paligeuka kuwa pachungu baada ya mabomu zaidi ya 120 kulindima toka saa 3:58 asubuhi hadi 8:45 na kulifanya eneo hilo lisikalike.
Mabomu hayo yalilindima maeneo mbalimbali ya mji ikiwemo eneo  maarufu la Makoroboi  kufuatia kuvunjwa kwa vibanda vya machinga jana asubuhi hali iliyowafanya wacharuke na kuanza mapambano na askari polisi na mgambo wa Jiji huku wakishinikiza wenzao walio kwenye maeneo halali nao waondolewe ili wote waikose makoroboi.

Katika sekeseke hilo wamachinga  zaidi ya 40 wamekamatwa kwa kukiuka sheria za mipango miji.

Hatua hiyo inafuatia maamuzi ya baraza la halimashauri ya Jiji la Mwanza kusafisha biashara “chafu” ya wamachinga kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria.
Vijana waandamanaji wakifunga barabara, ingawa kuna walakini je hawa nao ni machinga? Abdukadri Salim anasema kuwa vijana wanatumiwa kufanya vurugu na siyowamachinga. (MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY)

Jeshi la polisi katika doria mtaa kwa mtaa.
Hapakukalika.
Hakuna biashara kila mtaa uligeuka kuwa mchungu.
Askari zimamoto washiriki zoezi la kuzima moto uliowashwa na wamachinga na kuhatarisha usalama wa msikiti wa Hindu wanaosali masinga singa. 
Eneo hili la kutoka barabara ya Lumumba linaloingia Makoroboi hadi kupitia msikiti wa Hindu (ukuta wa mahala panapo zimwa moto) na kuingia barabara ya Nyerere linatakiwa kuwa wazi bila kuwa na wafanyabiashara wanaotandaza bidhaa zao chini au kuegesha kunye kuta, na tukio la leo ni la zaidi ya mara mbili kutokea kwa wamachinga  kulikalia kwa nguvu.
Oparesheni ofisa wa zima moto, Sajenti meja Gadafi Masoud  amesema msikiti wa Hindu wanaosali masinga singa umenusurika kuchomwa moto na machinga hao baada ya magari makubwa mawili kikosi chake kuuzima moto uliowashwa na wamachinga kwa lengo la kuuteketeza msikiti huo ulio katika eneo waliloondolewa.(MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY)

Mbali ya milindimo ya mabomu ili kudhibiti vyema vurugu hizo ilibidi jeshi la polisi mkoani hapa lifanye msako mtaa baada ya mtaa kuwasaka waanzisha fujo sanjari na kulinda usalamawa mali za wafanyabiashara kwani vurugu hizo zilizmbatana na uporaji.
Katika mitaa ya Makoroboi hata kwa wale wawamachinga walioruhusiwa kufanya biashara kutokana na kuwa katika maeneo sahihi ya ramani walishindwa kuendelea kutokana na vurugu hizo. 
Milindimo ya mabomu na moshi wake uliwapa wakati mgumu pia wanahabari.
Jeshi la polisi mkoani Mwanza lilitoa tahadhari ya watu kutosimama kwa makundi.
Mikakati ikifanyika kusuia maafa.
Hakika ni hasara kubwa kwa huduma na maduka ya biashara kufungwa kwa muda mwingi hali ambayo imewapa usumbufu mkubwa wateja kutoka katika mikoa ya jirani ya Mara, Shinyanga, Kagera, Simiyu na Geita waliohitaji bidhaa katika maduka ya jumla.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Valentino Mlowola hakuweza kupatikana kwa kuwa yuko safari kikazi na msaidizi wake Christopher Fuime alidaiwa kuwa katika oparesheni hiyo huku baadhi ya askari ambao hawakutaka  kutajwa majina yao wakisema zaidi ya wamachinga 40 wamekamatwa  kuhusiana na vurugu hizo.

Airtel YAWEZESHA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA AFYA KIJIJI CHA MBOLA TABORA.

Mfanyakazi wa huduma za afya bi Amina Wakasuvi akitoa huduma kwa moja ya familia katika kijiji cha mbola mkoani Tabora  ambapo Airtel chini ya mradi wa millennium village imewawezesha wafanyakazi hao kutumia mtandao wa mawasiliano kutoa huduma za Afya.
Akitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa huduma za afya katika kijiji cha Mbola mkoani Tabora namna ya kutumia huduma ya mawasiliao ya simu kutoa huduma za kiafya Ambapo Airtel imewapatia wafanyakazi hao huduma ya internet , message na simu bure na kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kufikia maeneo mengi zaidi.
Wafanyakazi wa huduma za afya katika kijiji cha Mbola mkoani Tabora wakijaribu namna ya kutumia simu zao mara baada ya mafunzo ambapo Airtel inawawezesha kutumia simu zao kutoa huduma za Afya chini ya mradi wa millennium village
Wafanyakazi wa huduma za afya katika kijiji cha Mbola mkoani Tabora wakijaribu namna ya kutumia simu zao mara baada ya mafunzo ambapo Airtel inawawezesha kutumia simu zao kutoa huduma za Afya chini ya mradi wa millennium village

Airtel yawezesha mafunzo kwa wafanyakazi wa Afya kijiji cha Mbola Tabora
·         Airtel yajikita kuboresha mazingara ya jamii  vijijini
Tabora Junanne 10 Juni 2014, wafanyakazi wa afya wa kijiji cha mbola mkoni Tabora wametoa shukrani zao kwa Airtel kufatia technologia ya huduma ya mawasiliano inayoyowawezesha kutoa huduma za afya kwa wigo mpana na kuwafikia wakazi wengi zaidi.

Wafanyakazi hao wa afya walipata mafunzo ya namna ya kutumia technologia ya huduma ya afya kupitia simu iitwayo COMCARE, iliyoanzisha kwa msaada wa Dagiba  inapatikana kupitia simu za smart phone zenye application maalumu inayowawezesha wafanyakazi wa afya kukusanya takwimu za wagonjwa na kutuma repoti kwenye vituo vya afya.

Akiongea wakati wa mafunzo mmoja wa wafanyakazi wa afya Ms Amina Wakasuvi alisema” Tekinologia hii mpya  ya kisasa itatuwezesha kufatilia kazi zinazofanywa na wafanyakazi wa afya wakiwa katika maeneo mbalimbali na wafanyakazi hao wataweza kutuma repoti zao kwa wakati kila siku kupitia mtandao wa Airtel. Hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa ubunifu huu na huduma ya vifurushi vya internet vya bure vinavyotuwezesha kufanya kazi zetu kwa wakati.

Akionge wakati wa tukio hilo Meneja huduma kwa jamii bi Hawa Bayumi alisema” kwa miaka mitatu sasa Airtel imewekeza katika kuleta mapinduzi ya kupatikana kwa  huduma kwa jamii husasani katika maeno ya vijiji vya Tabora  kwa kushiriki katika mradi wa  Millennium village kama mtowaji mkuu wa huduma za mawasiliano.

Katika mradi huu Airtel inatoa njia ya mawasiliano kwa kuwezesha jamii inayoishi katika maeneo ya pembezoni kupata huduma za Afya. Wafanyakazi wa afya katika maeneo hayo wameunganishwa na mtandao wa kisasa unaowapatia huduma ya internet na simu na kurahisisha kazi zao pindi wakiwa kazini. 

Sasa wafanyakazi hawa wanaweza kukusanya takwimu kwa kutumia simu na pia kuwawezesha wagonjwa walioko vijijini kuongea na madakitari specialist walioko mjini na kupata huduma za afya kupitia simu za mkononi” Bayumi aliongeza mpaka sasa tumeiwezesha miradi mitatu kupata huduma ya kupiga simu, ujumbe mfupi na vifurushi vya internet bure, Airtel inaendelea na dhamira yake ya kuwaleta watanzania karibu na huduma muhimu za jamii kupitia technologia ya mawasiliano.

Akiongea kuhusu mradi huo, Mkurugnzi wa mradi wa Millennium Village Dr. Gerson Nyadzi alisema “ Mtandao wa 3G wa Airtel umetuwezesha kwa kiasi kikubwa  kufikia maeneo ya vijijini  ambapo huduma ni duni na haba. Kuanzia mradi huu uanzishwe  kumekuwa na ongezeko la 85% la  upatikanaji wa huduma muhimu za afya hapa Mbola.

Kwa kuongeza mradi wa Child count katika techonologia ya huduma za afya ya CommCare kutawezesha zaidi ya wakazia 97% kupata huduma za afya kupitia watoa huduma wetu wa afya wenye vyenzo hizi muhimu za kutendea kazi.

Tuesday, June 10, 2014

MUONEKANO WA LEO KITUO CHA MWENGE JIJINI DAR KUPISHA UPANUZI WA BARABARA.

Tofauti na awali hapa zilikuwa zikionekana sura za mabasi yaelekeayo pande mbalimbali jijini Dar yakiwa katika mistari.
Chini palikuwa na sakafu ya vitofa lakini kwa sasa vimeenjuliwa na kukusanywa kama vifusi mafungu kwa mafungu. 
Ni taabu kwa abiria walikuwa na mazoea ya kupata huduma kupitia kituo hiki ambapo kwa sasa huduma zote zimehamishiwa kituo cha Makumbusho umbali wa mita kama1,000 toka kituoni hapa.
Eneo hili mbali na kuwa kituo cha daladala pia lili sheheni mishemishe mbalimbali za biashara likiwawezesha na kuwarahisishia wajasiliamali mbalimbali mamia kwa maelfu kukutana kirahisi na wateja wao kukuza vipato vyao kwa kufanya biashara na utoaji huduma mbalimbali za tija kwa wananchi wa kawaida la kini kwa sasa kweupeeeee kutoka hapa mpaka kuleee!!
Hapa kulikuwa na huduma za vyoo na kuoga!!
Majengo yaliyo salia.
Tutegemee mabadiliko gani katika muonekano wa eneo hili?
Majibu yatapatikana hapa hapa.