Jeshi la wananchi lilitoa askari wake wa kijeshi “MP” kuimarisha ulinzi kwenye vitengo vya mabenki, ofisi za serikali na maeneo nyeti ili kutokwaza shughuli za kila siku kuendelea. |
KATIKATI ya jiji la Mwanza leo paligeuka kuwa pachungu baada ya mabomu zaidi ya 120 kulindima toka saa 3:58 asubuhi hadi 8:45 na kulifanya eneo hilo lisikalike.
Mabomu hayo yalilindima maeneo mbalimbali ya mji ikiwemo eneo maarufu la Makoroboi kufuatia kuvunjwa kwa vibanda vya machinga jana asubuhi hali iliyowafanya wacharuke na kuanza mapambano na askari polisi na mgambo wa Jiji huku wakishinikiza wenzao walio kwenye maeneo halali nao waondolewe ili wote waikose makoroboi.
Katika sekeseke hilo wamachinga zaidi ya 40 wamekamatwa kwa kukiuka sheria za mipango miji.
Hatua hiyo inafuatia maamuzi ya baraza la halimashauri ya Jiji la Mwanza kusafisha biashara “chafu” ya wamachinga kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria.
Vijana waandamanaji wakifunga barabara, ingawa kuna walakini je hawa nao ni machinga? Abdukadri Salim anasema kuwa vijana wanatumiwa kufanya vurugu na siyowamachinga. (MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY) |
Jeshi la polisi katika doria mtaa kwa mtaa. |
Hapakukalika. |
Hakuna biashara kila mtaa uligeuka kuwa mchungu. |
Askari zimamoto washiriki zoezi la kuzima moto uliowashwa na wamachinga na kuhatarisha usalama wa msikiti wa Hindu wanaosali masinga singa. |
Katika mitaa ya Makoroboi hata kwa wale wawamachinga walioruhusiwa kufanya biashara kutokana na kuwa katika maeneo sahihi ya ramani walishindwa kuendelea kutokana na vurugu hizo. |
Milindimo ya mabomu na moshi wake uliwapa wakati mgumu pia wanahabari. |
Jeshi la polisi mkoani Mwanza lilitoa tahadhari ya watu kutosimama kwa makundi. |
Mikakati ikifanyika kusuia maafa. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.