ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 21, 2013

SERENGETI FIESTA 2013 MUSOMA NI NOWMA SANA

Toka Wanaume halisi Doro

The Crew....Msami, Hamza na James Njuu.

The shabikiz...
Msanii mwingine anaefanya vyema hivi sasa katika anga ya muziki wa Bongofleva,Rich Mavoko akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu,mbele ya wakazi wa mji wa musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Karume mkoani Mara.
 Madansa wa msanii wa muziki wa kizazi kipya,Shilole wakitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya Uwanja wa Karume,ndani ya mji wa Musoma mkoani Mara,ambapo tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea hivi sasa.
 Anajiita tajiri wa Mahaba Cassim Mganga kutoka Manzabay akiwaimbisha jukwaani wakazi wa mji wa Musoma,wakati tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea hivi sasa ndani ya uwanja wa Karume.
 Mashabiki wakijinafasi kwa raha zao.
 Kundi la Wanaume TMK likiongozwa na Chege na Temba wakilishambulia jukwaa la serengeti fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
Temba toka Wanaume TMK akisababisha.


 Mkali mwingine wa muziki wa Reggae kutoka kanda ya Ziwa,Jita Man akiwakumusha mashabiki wa muziki wake enzi hizo,mbele ya wakazi wa mji wa Musoma usiku huu
Anaitwa Godzilla kutoka maskani ya Sala sala,akishusha mistari yake live mbele ya mashabiki wake waliojitokeza kwenye tamasha la serengeti fiesta usiku huu.
Makamuzi yakiendelea jukwaani usiku huu.
 Sehemu ya umati wa watu.
 Msanii wa muziki wa bongofleva ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga hizo,Neylee akiimba jukwaani usiku huu wakati wa tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea usiku huu ndani ya uwanja wa Karume,Musoma mkoani Mara.
 Kundi la Wanaume TMK Halisi likiongoza na msanii nguli Juna Nature wakilishambulia vyema jukwaa usiku huu kwa staili yao mapanga shaa shaa,huku mayowe yakipigwa kutoka mashabiki.
Kila shabiki alikuwa na mzuka wake.
 Mashabiki wa tamasha la serengeti fiesta wakifuatilia yanayojiri ndani ya uwanja wa Karume hivi sasa
 Sehemu ya umati wa watu ndani ya uwanja wa Karume usiku huu.

Mwanadada Shilole akionesha umahiri wake wa kunengua jukwaani mbele ya maelfu ya watazamaji waliojitokeza usiku huu kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2013.
Weusiiiii....

 Anaitwa Linah Sanga,kutoka nyumba ya vipaji THT akiimba jukwaani usiku huu
Linnah...

 Watu kibao,kila mmoja akijaichai kivyake huku jukwaa likiwaka moto vilivyo kwa miondoko ya bandika bandua ya wasanii wanaotumbuiza. 
 Wakali wengine wanaokuja kwa kasi katika anga bongofleva-hip hop,Stamina na Youngkiller wakilishambulia jukwaa kwa kushusha mistari mikavu live.
 Shangwe kila kona za mashabiki zimetawala uwanjani hapa.

Friday, September 20, 2013

KINANA AMPA RUNGU MPINA KUWABANA MAWAZIRI.

Kutoka kushoto ni Katibu Mwenezi wa Siasa CCM Nape Mnauye (mwenye kamera),  Katibu Mkuu CCM Abdarahiman Kinana na Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina (anaye hutubia mkutano wa ziara ya Katibu huyo wa Chama.)
HABARI KAMILI
Simiyu


KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amewataka Wabunge wa chama hicho kuwasukuma mawaziri ili waweze kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia wananchi tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi wao wanafanya kazi kwa mazoea.

Kinana alisema kasi ya kufuatilia utendaji kazi wa mawaziri inayofanywa na Mbunge wa Kisesa(CCM), Luhaga Mpina ni ya kuridhisha na kwamba chama hicho kinaheshimu msimamo wa mbunge huyo katika kuisimamia kikamilifu Serikali ili iweze kutimiza malengo ya kuwaletea maisha bora watanzania.

Alisema Mpina ni mbunge hodari na jasiri aliyemstari wa mbele kuwatetea wananchi na kuhoji uwajibikaji wa Serikali awapo bungeni hivyo chama hicho kitaendelea kuthamini mchango wake kwani kwa kiasi kikubwa unasaidia kuharakisha utendaji wa serikali.

"Mbunge wenu ni hodari, sisi chama tunamuheshimu, ni mchapakazi, mtetezi wenu na tunaamini mtaendelea kumchagua katika uchaguzi mkuu ujao.."alisema Kinana na kushangiliwa na maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wa hadhara katika Kata ya Mwasengela jimbo la Kisesa wilayani Meatu mkoani Simiyu

Alisema matatizo mengi ya wananchi yanashindwa kutatuliwa kutokana na Mawaziri kukaa maofisini bila kufika katika maeneo husika na kwamba ufuatiliaji wa Mbunge huyo kwa kiasi kikubwa utasaidia kuwaamsha ili waweze kuchapa kazi inayotegemewa na wananchi.

Kinana alisema kazi iliyofanywa na Mpina katika utelekeza wa ilani ya CCM katika jimbo hilo ni kubwa kwani amefanikiwa kujenga miundombinu ya barabara, umeme, mawasiliano,maji, madaraja,shule za msingi na sekondari, vituo vya afya hali ambayo inakifanya chama hicho kiendelee kuaminiwa na wananchi.

Pia alisifu uwajibikaji wa Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Rosemary Kirigini katika kufuatilia kero za wananchi na kuwataka viongozi wengine kuacha kusubiri hadi madhara yatokee ndio wakimbilie kwenye maeneo hayo kutafuta suluhu.

Kwa upande wake Mpina alisema mapokezi makubwa aliyopata Katibu Mkuu huyo wa CCM ni ishara tosha kuwa Serikali imekuwa ikiwajibika kwa wananchi hasa katika jimbo hilo kwa kufanikisha kutelekezwa kwa ahadi za Rais Jakaya Kikwete alizotoa kwenye kampeni ikiwa ni pamoja na ujenzi wa daraja la Mongo-obakima ambapo wananchi walipoteza maisha kwa kuliwa na mamba na viboko pamoja na  kusombwa na maji.

Katika mkutano huo wananchi hao walimuomba Katibu Mkuu huyo wa CCM kuwatafutia suluhu ya tatizo la malisho ya mifugo hususan kwa wananchi wanaoishi kando  ya pori la akiba la Maswa kutokana na baadhi ya viongozi kuwabambikia kesi na kuwakamua fedha zao kupitia mgogoro huo wa malisho ya mifugo.

Kufuatia ombi hilo Kinana aliwaagiza Mawaziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kufika katika eneo hilo na kuutafutia ufumbuzi 

MWANAMKE ANUSURIKA KUUAWA KWA KUIBA MTOTO MUSOMA

Hii imetokea mchana wa leo hapa musoma, mwanamke huyu kanusurika kuuawa na wananchi wenye hasira baada ya kudaiwa kuiba mtoto wa siku moja. PICHA kwa hisani ya Shommi Binda
Mtoto aliyenusurika kuibiwa.
 Na Shomari Binda-Musoma


MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jina la Zawadi Hamisi(22) mkazi wa Butimba mkoani Mwanza amenusulika kuuwawa na Wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kuiba mtoto mchanga wa siku moja kwenye hospitali ya mkoa wa Mara.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 8 mchana maeneo ya barabara ya sokoni Manispaa ya Musoma baada ya mwanamke huyo kumdanganya mzazi wa mtoto huyo kuwa anaitwa na mama yake na kutumia mwanya huo kuondoka na mtoto huyo kabla ya kusaidiwa na wasamalia wema kumkamata Mwanamke huyo.

Akizungumza na Habari leo katika kituo kidogo cha polisi cha stedi ya zamani mjini hapa huku akibubujikwa na machozi,mzazi wa mtoto huyo Angelina Singu(22) mkazi wa kijiji cha Masurura Wilayani Butiama alisema mwanamke aliyedaiwa kumuiba mtoto huyo mwenye jinsia ya kiume alimwambia mama yake yupo stend anamsubilia ili waondoke.

Alisema alimfata akiwa hospitali ya mkoa wa Mara akijiandaa kuondoka baada ya kujifungua septemba septemba 19 na kumueleza mama yake anamuita na kumtaka msaidie mtoto ili waweze kumfuata na kuondoka kurudi nyumbani.

Angelina alisema baada ya kutoka nje ya geti la hospitali ya walitembea hadi sted ya zamani na baadae wakiwa umbali kidogo kutokana na mwendo wake kuwa mdogo kutokana na uzazi alimuona mwanamke huyo akipanda pikipiki maarufu kama bodaboda na kuanza kuondoka huku akimuacha.

Alisema baada ya kuona hali hiyo aliamua kupiga kelele ya kuomba msaada ndipo wasamalia wema pamoja na baadhi ya waendesha pikipiki walipoamua kuifukuza pikipiki aliyopanda mwanamke huyo pamoja na mtoto aliyeibwa na kufanikiwa kumkamata barabara ya sokoni.

"Inaonekana huyu mwanamke alinifatilia pale hospitalini tangu nilipojifungua,hakuwa na nia njema ni kweli alitaka kuondoka na mtoto wangu....masikini nimeangaika miei tisa leo mtoto wangu anataka kuchukuliwa kwa kweli nawashukuru walionisaidia ningekuwa kwenye hali gani mimi.

"Wanawake tuoneane huruma hili sio jambo jema hivi karibuni nilisikia kwenye vyombo vya habari mkoa mmoja kuna Mwanamke kaiba mtoto kumbe mambo haya yapo imeniuma sana na namshukuru mungu na walionisaidia jambo hili na vyombo vya sheria vichukue hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizi"alisema Angelina.

Mwanamke anayedaiwa kufanya jaribio la kuiba mtoto huyo alisema alitoka Mwanza kuja Musoma kwa ajili ya kumsalimia kaka yake na alikwenda hospitali ya mkoa wa Mara kuchukua dawa kwa ajili ya matibabu.

Alisema hakuwa na nia mbaya ya kuondoka na mtoto huyo bali alikuwa akimsaidia kumbebea na alipooulizwa kwa nini aliamua kumuacha na kupanda pikipiki peke yake alishindwa kuongea na alipoangaliwa kwenye mkoba wake alikutwa na kadi ya ujauzito ikionyesha anatarajiwa kujifungua septemba 19 mwaka licha ya kwamba alikuwa hana ujauzito.

Mmoja wa mashusuda wa tukio hilo alisema alimuona mwanamke huyo aliyedaiwa kuiba mtoto kwa siku mbili maeneo ya Nyakato Manispaa ya Musoma kama mgeni karibu na nyumba anayoishi.

Kamanda wa polisi mkoani Mara Ferdnand Mtui amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na Mwanamke anayedaiwa kufanya jaribio la kuiba mtoto anaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi na baada ya upelelezi hatua zaidi za kisheria zitafuatwa.

TANZANIA YAINGIZA TIMU MBILI ROBO FAINALI AIRTEL RISING STARS

The Tanzanian Team before their first  match between Ghana. They lost 2-1 at the Onikan Stadium, Lagos.
Tanzania yaingiza timu mbili robo fainali Airtel Rising Stars

Lagos , Septemba 2o , 2013...  Timu zote za wavulana na wasichana zimeingia robo fainali katika michuano ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars yanayofanyika Lagos , nchini Nigeria na mshindi atapata medali , kombe pamoja na dola za marekani 10,000.

Timu ya wasichana imetinga robo fainali baada ya ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Malawi jana  na kumaliza na  pointi nne katika kundi ambapo timu ya Uganda ikishika uskani kwa point sita. Wakicheza kwa kujiami timu ya wasichana ya Tanzania ilipata goli katika dakika ya 17 kupitia kwa mshambuliaji hatari Shelda Boniface , kabla ya Malawi kuzawazisha dakika ya saba katika kipindi cha pili.

Mshambuliaji mwenye uwezo wa hari ya juu  Athanas Mdam alionyesha makeke yake  jana baada ya kufunga magoli matatu (hat-trick) katika mechi dhidi ya Sierra-Leon ambapo Tanzania ilishinda 4-2 na kukata tiketi ya kushiriki hatua inayofata ya michuano ya Mwaka ya kimataifa inayoandaliwa na Airtel.

Mdamu ambaye amedhiliisha kwamba yeye ni liungo muhimu katika michuano hii , alifunga magoli katika dakika ya  6, 48, 56 , Omari Hamisi ndiye aliitimisha goli la nne la Tanzania  katika dakika ya 60. Sierra-Leone walipata magoli yao kupitia kwa Mohamed Mustapha katika dakika ya 8 na Alimamy katika dakika ya 14.

Timu ya wavulana ya Tanzania itacheza mechi ya robo fainali na Madagascar leo wakati wasichana watacheza na Democratic Republic of Congo. Timu ya wavulana itakosa huduma ya mpikaji mabao Athanas Mdamu ambaye yupo majeruhi.

Mshambuliaji hatari Athanas Mdamu ametoa mchango mkubwa sana  katika timu mpka kufikia hatua ya mtoano . Amefunga goli kwa kila mechi , dhidi ya Ghana na Zambia. “ Tutamkosa ila tutapigana mpaka mwisho kuakikisha tuanshinda mechi zote.”Alisema naodha wa timu Thomas Chndeka .

Timu nyingine zilizofanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali kwa upande wa wavulana ni mabingwa watetezi Niger  ,wenyeji Nigeria , Chad, Malawi, Madagascar, Zambia, na Congo. Na kwa upande wa wasichana ni mabingwa watetezi Ghana , Nigeria , Chad, Kenya , Uganda , Malawi and DRC.

Mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars ni mpango wenye lengo la kuchangia maendeleo ya  mpira wa miguu barani Afrika. Pia vijana wanapata fulsa ya kuonyesha uwezo na vipaji vyao katika medani ya soka.

Airtel, Puma, Be Forward, Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, na Baraza la Taifa Usalama Barabarani waungana kuadhimisha wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani 2013

Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akikabithi Tshirt zitakazotumika katika wiki ya nenda kwa usalama kwa mwaka huu kwa Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga ambapo Airtel, Puma pamoja na  Be Forward ni wadhamini wa wiki ya usalama barabarani kwa mwaka huu. akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Puma Bwana Philippe Carsaleti

Mkurugenzi Mkuu wa Puma Bwana Philippe Carsaleti wakwanza kushoto akifatiwa na mwakilishi wa Be Forward bw Kohei Shibata na Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando kwa pamoja wakimkabithi Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga stika za usalama barabarani kwa mwaka huu. Airtel, Puma pamoja na  Be Forward ni wadhamini wa wiki ya usalama barabarani kwa mwaka huu

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga akionyesha stika za usalama barabarani kwa mwaka huu mara baada ya kukabithiwa na wadhamini wa wiki ya usalama kwa mwaka huu ambao ni Airtel, Puma pamoja na  Be Forward wakishuhudia (kutoka kushoto) mwakilishi wa Be Forward bw Kohei Shibata, Mkurugenzi Mkuu wa Puma Bwana Philippe Carsaleti na Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando

"MURrrA! LEO NDIYO FIESTA MUSOMA bHaNA"

"Twenzetu Musoma....!" Ni Young Killer na Stamina.

"Twenzetu Musoma" Hapa ni Nick Wapili.

"Twenzetu Musoma" Our bus...!!!

"Twenzetu"  Jukwaa liko tayari kwaajili ya makamuzi ya leo Serengeti Fiesta 2013  ndani ya Uwanja wa Karume Musoma, jeh wewe Musoma mko tayariiiii....? 

Huduma za maakuli, chomaZz, banikaZz na makunywajiZz haziwezi kukosekana.


Sekta ya ChomaZz na full mafuta..

Udirinki wetu wa Twenzetu ndani ya Uwanja wa Karume Musoma mjini.

Mbuzi....Uskose..

KWA HALI HII ZAO LA PAMBA LITAZIDI KUPOROMOKA KILA KUKICHA.

Meneja wa kiwanda cha Bilchand Oil Mill, Mohamed Gupta akifafanua uchafuzi unaofanywa na baadhi ya wanunuzi na wakulima kwa kuchang’anya pamba, maji, mchanga na mbegu kwa lengo la kuongeza uzito.
Ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba nchini DKT.FESTUS LIMBU katika kiwanda cha kuchambua pamba cha Birchand Oil mill inayomwezesha kujionea uchafuzi wa pamba unaofanywa na baadhi ya wanunuzi na wakulima kwa kuchang’anya pamba, maji, mchanga na mbegu kwa lengo la kuongeza uzito.
Mbegu zilizochanganywa kenye pamba kwa lengo la kuongeza uzito
Ukaguzi ukiendelea kwenye ghala la Pamba.
Meneja wa kiwanda cha Bilchand Oil Mill, Mohamed Gupta akionyesha mchanga uliochanganywa na Pamba za moja wa wakulima waliokiuzia kiwanda chake.
Ukiitizama kwa harakaharaka pamba hii unaweza kuiona kuwa iko salama, ila ukichukuwa jukumu la kuigusa ndipo utagunduwa kuwa kunachembe chembe za mchanga na uchafu mwingine ndani yake.
Hili ni lundo la mchanga wa kilo 60,000 uliopembuliwa wakati wa uchambuzi wa pamba ya msimu huu na uliopita, kwa Kiwanda cha Bilchand Oil Mill ambacho kimepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni 7 kutokana na uchafuzi huo wa kuweka maji na mchanga, hadi sasa Wahasibu wake wanne (hakuwataja) wafikisha polisi kwa tuhuma hizo.  
Meneja wa kiwanda cha Bilchand Oil Mill, Mohamed Gupta akielezea uchafuzi huo ndani ya Pamba.
Kwa ukaribu zaidi mchanga uliopatikana kwenye Pamba baada ya uchambuzi wa awali.

Na Peter Fabian
MWANZA.

TATIZO la kushuka thamani ya Pamba nyeupe ya Tanzania (Dhahabu Nyeupe) kwenye Soko la Dunia na kupelekea kuporomoka kwa bei maradufu kumeishitua seikali na sasa kupitia Bodi ya Pamba nchini (TCB)imeamua kuchukua hatua za kunusuru zao hilo kwa kutangaza kuwa kuanzia msimu ujao wa kilimo utakuwa wa Kilimo cha Mkataba katika Mikoa ya Kanda ya Magharibi.
Hatua hiyo inafuatia tamko la serikali lililotolewa kwa nyakati tofauti na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa Mkutano wa wadau wa kilimo cha pamba kutoka Mikoa kumi hapa nchini kilichofanyika mwezi Mei mwaka huu Jijini humo na lile la Rais Dkt. Jakaya Kikwete alilolitoa wakati wa majumuisho ya kuhitimisha ziara yake ya siku tano Mkoani Mwanza hivi karibuni.
Mwenyekiti Festus Limbu (katikati).
Mwenyekiti wa Baraza la Wakurugenzi Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) Dr.Festus Limbu (Mb) alisema kuwa uamuzi huu umepelekea Bodi hiyo kutoa tamko la Taasisi hiyo Muhimu nchini inayosimamia zao la Pamba hapa nchini kutangaza kuwa kuanzia mwezi Novemba mwaka huu utekelezaji wa Kilimo cha Mkataba utaanza kwa Mikoa kumi ya Kanda ya Magharibi inayojishughulisha na kilimo cha zao.
“Tumezamilia kurejesha ubora wa Pamba Nyeupe zamani ikijulikana ‘Dhahabu Nyeupe’ kwa kuhakikisha msimu huu wa Kilimo wa mwaka 2013/2014 unaoanza mwezi Novemba mwaka huu kila Mwekezaji na mnunuzi wa pamba kuanza kuwekeza kwenye Kilimo cha Mkataba ambacho kimsingi ndiyo kitakuwa suruhisho la Mkulima kunufaika na Mwekezaji huyo hali itakayosaidia pamba kurejea kuwa na thamani na ubora” alisema Dr.Limbu.
Mwanyekiti huyo  alisema kuwa utekelezaji wa Mkataba huo utakuwa ni kati ya Wanunuzi, Wamiliki wa viwanda vya pamba na wakulima ambapo watatakiwa kupeleka kwenye maeneo ya wakulima vijijini Pembejeo za kilimo ikiwa ni Mbegu za Quton, Mbolea na Madawa ya kuulia wadudu na kufunga Mkataba na wakulima huku viongozi wa serikali za vijiji na vyama vya msingi wakiwa mashahidi.
Dr Limbu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Magu Mkoani Mwanza, alisema  tamko la serikali juu ya uamuzi wake wa utekelezaji wa kilimo cha Mkataba katika tasnia ya Pamba pamoja na kuwa na tija ndogo katika uzarishaji ambapo uzarishaji kwa umekuwa wa Hekali moja kutoa kilo 300 ikilinganishwa na lengo la kuzalisha kilo 1,500 kwa Hekali moja ifikapo mwaka 2015 kote nchini.
“Tunazo changamoto nyingi ikiwemo ya uhaba wa viwanda vya kuongeza thamani, matumizi madogo ya pembejeo, kutolewa kwa pembejeo muda ukiwa umepita, kilimo kutegemea mvua za msimu na wanasiasa kutumia mwanya wa kujipenyeza na kuwachezea wakulima jambo ambalo limeonekana kabisa kusababisha ubora hafifu unaosababisha pamba kuuzwe kwa bei punguzo na kumnyonya mkulima” alisema na kuongeza kuwa
Tasnia ya Pamba ni muhimu katika uchangiaji wa pato la taifa na tegemeo la asilimia 40 ya Watanzania, lakini kilimo cha zao hilo kimekuwa kikikabiliwa na matatizo mengi na changamoto mbalimbali hali inayoonekana kudidimia kwa zao hilo kila msimu hivyo kupitishwa kwa mswada wa sheria ya kuanzishwa kilimo cha umwagiliaji kutakuwa mkombozi kwa wakulima. 
“Sekta hiyo binafsi itabidi iwekeze katika kuwapatia wakulima pembejeo na huduma zingine, badala ya kusubiri kwenda kununua pamba kwa wakulima mwishoni mwa msimu, kwa sababu mfumo wa sasa wa mnunuzi kupewa jukumu la kukusanya fedha kutoka kwa mkulima na kuziwasilisha CDTF umeonekana kuwa na matatizo makubwa” alisema Dr. Limbu

Aliitaja Mikoa ya Kanda hiyo itakayo tekeleza kilimo cha mkataba kuwa ni Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera, Tabora, Geita, Singida, Rukwa na Kigoma na kwamba wadau wote walio na nia ya kununua pamba msimu ujao, waanze kusambaza mapema mbegu na pembejeo (Quton) kwa wakulima ili mwakani wanunue pamba kutoka kwao na si kuvamia kununua kiholela kama ilivyo sasa.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa Kampuni ya ununuzi wa pamba na kiwanda kitakachoshindwa kupeleka pembejeo za kilimo kwa wakulima katika utekelezaji wa Kilimo cha Mkataba kuanzaia mwaka huu wa msimu wa kilimo mwezi Novemba, mwakani waklati wa kuanza msimu wa ununuzi wa pamba haitapatiwa Leseni na Bodi ya Pamba na halitaruhusiwa kuvamia kiholela kununua Mikoa yote.

“Leseni za ununuzi wa pamba zitatolewa kwa kuzingatia kigezo cha uwekezaji wa kila mdau katika eneo husika na si vinginevyo na hakutakuwa na ujanja ujanja kwenye kufunga mkataba na wakulima wa zao hilo ieleweke na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya Kampuni husika na wakulima hawataruhusiwa kuuza pamba yao kwa mtu ambaye hakuwapa pembejeo. 

Aidha Dr Limbu alisema kuwa katika kuhakikisha utekelezaji huo unafanikiwa Ofisi za wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zitasimamia kwa karibu utaratibu huo mpya wa kilimo cha mkataba ili malengo ya kuondokana na matatizo yanayoathiri kilimo hicho yafikwe huku wachafuzi wa pamba wakati wa msimu wa kuuza pamba wakiwekewa mwarobaini wa kuwadhibiti.