Pambano lingine la kitaa

Kocha wa ngumi za kulipwa Christopher Mzazi kutoka katika gym ya "no talking" ya Mabibo ya jijini Dar es salaam ameamua kuwapoza machungu wale mabondia chipukizi waliopiganishwa na promota kaike na kutolipwa kwa kuwaandalia pambano litakalopigwa tarehe 18/11/2012 hukohuko mabibo katika ukumbi wa D.I.D pambano litakuwa ni kati ya Mwaite juma na Baina Mazola. Ni pambano la kiupinzani na kwani wawili hao walikuwa wanatafutana baada ya kukosana kupigana kavu.

Akilizungumzia pambano hilo kocha mzazi alisema 'issa omar na mwaite juma ni mabondia wanaofundishwa na kocha mzuri mwenye uwezo mkubwa pia ni mabondia wazuri na ni tegemeo zuri la baadae,sijui kwanini kaike kaamua kuwafanyia uhuni wa kuwadhulumu,hivyo mimi nikiwa kama mzazi kama jina langu nikaona ni vema nikawapoza machungu kwa kuwapa pambano na mabondia wangu na kuwalipa zaidi ya pesa walizodhulumiwa kwa kuwa ninaelewa machungu na ugumu wa mchezo wenyewe 
ulivyo.
Hivyo basi Mwaite juma kutoka Big Right boxing gym atacheza na Baina Mazola wa No talking gym katika pambano la raundi nane.yakisindikizwa na karim Ramadhan(mdogo wake nasibu Ramadhani-bondia bora wa mwaka) atakaecheza na martin Richard.
Siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mengi ya kiushindani ya kuwekana sawa nani zaidi ya mwingine kati ya mabondia wa mabibo na Mwananyamala