ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 1, 2012

MKUTANO WA VIONGOZI WA MAENEO YANAYOLIMA PAMBA ULIOFANYIKA JIJINI MWANZA LEO

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akitoa mchango wake kwenye mkutano wa viongozi wa maeneo yanayolima zao la pamba uliofanyika jijini Mwanza katika ukumbi wa chuo cha benki kuu leo.

Msimu wa kilimo wa 2011/12, utekelezaji wa kilimo cha mkataba katika maeneo yote yanayolima pamba ambapo asilimia 72 ya wakulima wanaokadiriwa kuwa 500,000 walifunga mikataba na wenye viwanda.

Uzalishaji wa pamba kwa msimu huu unatarajiwa kufikia tani 350,000 hadi tarehe 29 octoba 2012, jumla ya pamba tani 339,000 zimekwishanunuliwa na ununuzi unaendelea katika wilaya za Bariadi, Maswa na Meatu. Hili ni ongezeko la asilimia 50 ikilinganishwa na kiwango cha uzalishaji wa tani 225,000 zilizopatikana msimu wa ununuzi wa 2011/12.
Mkuu wa mkoa mpya wa Simiyu akizungumza na wakulima wa zao la pamba.

Pichani mkulima mwezeshaji Bw. Masalu Mazoya kutoka Magu, akichangia kwenye kusanyiko hilo kutetea wakulima kuendelea na kilimo cha mkataba kwani mnamo Tarehe 20 Octoba 2012, TCA na TACOGA waliamua Kilimo cha mkataba kisitishwe kutokana na matatizo mbalimbali yaliyojitokeza msimu unaomalizika.

Uamuzi huo ulistua Bodi ya Pamba na tarehe 25 Octoba 2012 Baraza la Wakurugenzi liliitisha kikao cha dharula na kuamua kuitisha mkutano baina ya Bodi na viongozi wa maeneo yanayolima pamba, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na Vyama vya Ushirika uitishwe haraha ili kujadili kwa undani utaratibu utakaotumika kuwafikishia wakulima wa pamba pembejeo katika msimu huu wa kilimo.
Moja kati ya maazimio ya mkutano huo baina ya viongozi wa serikali, ushirika, wakulima na bodi ya pamba ni kuwa Kilimo cha mkataba ndiyo njia ya kuinua uzalishaji na ubora wa pamba hivyo suala hilo liunganishwe na juhudi za kuimarisha Ushirika.

Meza kuu ikizungumza na kusanyiko hilo lililohusisha wakuu wa mikoa na wilaya mbalimbali kanda ya ziwa walioketi pamoja na wakulima wa zao la pamba

Mmoja kati ya wakulima wa zao la pamba akichangia kwenye kusanyiko hilo.

Bodi ya pamba Tanzania imeanza kusambaza mbegu mpya aina ya UKM 08 kwenye magereza na kwa wakulima wa zao la pamba waanze kuitumia katika msimu wa kilimo mwaka huu baada ya mbegu hiyo kufanyiwa utafiti wa kina na kuthibitishwa kufaa kwenye Chuo cha Utafiti a Kilimo cha Ukiliguru kilichopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania Bw. Marco Mtunga akieleza wajumbe wa kikao cha wadau wa pamba kutoka wilaya zinazolima zao hilo kwenye ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza, amesema kuwa hivi karibuni mbegu hizo mpya za pamba zisizokuwa na manyoya kutoka Ukiriguru zilizofanyiwa utafiti tangu mwaka 2008 na kuthibitishwa kuwa na ubora zitaanza kutumiwa na wakulima katika baadhi ya maeneo yakiwemo Gereza la Malya, Magu na Mahango ili kuongeza uzalishaji wa mbegu hizo kwa nia ya kufikia malengo
Bw. Mtunga amesema kuwa baadhi ya makampuni ambayo yamekuwa hayapeleki kwa wakati pembejeo za kilimo kwa wakulima na kusababisha wakulima kushindwa kuendana na kalenda ya kilimo kwa wakati, Bodi ya Pamba itachukuwa hatua.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.