ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 5, 2009

SHINYANGA IMESAHAULIKA AU WAKAZI WAKE WAMEJISAHAU?


WIKI HII NIMESAFIRI HADI SHY TOWN NIA NA MADHUMUNI JUST KUBADILISHA MAZINGIRA, PAMOJA NA KUBADILISHA MAZINGIRA HALI YA HAPA KITUONI HAILIPI..... PICHANI KITUO CHA MABASI YA MIKOANI MJINI SHINYANGA TAKATAKA ZIKIWA ZIMEZAGAA KILA SEHEMU VUMBI KIANGAZI, TOPE MASIKA.


NA HAWA JAMAA HIVI BADO WAPO KWELI DUNIA? NA HII PROGRAM YAO ILIISHIA WAPI? MAANA JAMAA WALIKUWA WABISHI KWELI! NA OF COZ PROGRAM YAO IMESAIDIA SANA,LAKINI PAMOJA NA HAYO BANGO HILI LILILOKO KATIKATI YA MJI WA SHINYANGA STAND KUU YA MABASI TOKA LISIMIKWE MPAKA LEO HALIJAFANYIWA UKARABATI, BANGO LENYEWE LA KIZAMANI, RANGI NA MAANDISHI YAKIFUTIKA NA KUTU IKICHUKUWA NAFASI, NASHAURI KAULI KATIKA BANGO HILI IBADILISHWE TUANDIKE KWA CHAKI "FUATA NYOTA YA KUTU!"

KITUO HAKINA SEHEMU ZA KUKAA ABIRIA SEHEMU ZILIZOPO NIKAMA UNAKALIA MATOFALI NA UTACHOMWA JUA MPAKA UTAJUTA.

HUYU NI MAMA PEKEE ANAYE TAMBULIKA NA MANISPAL, ANAYETEGEMEWA KATIKA SHUGHULI ZA USAFI KITUONI HAPO, VITENDEA KAZI DUNI, HUKU AKIHATARISHA AFYA YAKE KWA KUTOKUVAA NYENZO MADHUBUTI. NYUMA YAKE NDIYO SEHEMU ZA KUKAA ABIRIA.

DALADALA ZA SHY TAYARI KWA ABIRIA WASHUKAO
EPUKA MIKWARUZANO "BAGEIN KABLA YA SAFARI

Thursday, December 3, 2009

Monday, November 30, 2009

KIPITA SHOTO KIPYA CHA FISH


TOFAUTI NA SANAMU ZILIZO PITA IKIWEMO ILE YA BABA WA TAIFA AMBAYO MCHONGAJI HAKUMCHONGA MZEE MCHONGA IPASAVYO HATA MCHONGO WAKE (SANAMU) KUFANANISHWA NA TASWIRA YA MZEE MMOJA JIJINI MZ. SAFARI HII WADAU HAWAJATUMIX! TENA WALIKUWA WAJANJA KWANI SIKU KADHAA KABLA YA KUIZINDUA SANAMU HII TUME ILIKUSANYA WADAU KUFANYA TATHMINI JE IKO SAWA? BAADA YA KUKUBALIKA WATU WAKARAMBA BIA KUSHEREHEKEA.


PAMOJA NA KWAMBA ENEO KUBWA LA JIJI LA MWANZA KUZUNGUKWA NA ZIWA VICTORIA LENYE SAMAKI WATAMU MFANOWE HAKUNA HUKU WAKAZI WAKE WAKIZOEA SIYO KUWAONA TU SAMAKI AINA KWA AINA MPAKA KUWAKARIRI NA KUWEZA KUWATOFAUTISHA BALI HATA KULA MPAKA KUKINAI WAKAZI HAO KILA KUKICHA WAMEONEKANA WAKIMIMINIKA KWA WINGI KUISHANGAA SANAMU YA SAMAKI AINA YA SATO ILIYOSIMIKWA KATIKA KIPITASHOTO CHA BARABARA YA KENYATA MWANZA. SANAMU HII ILIYO NAMWONEKANO WA SAMAKI WA UKWELI ANAYETEMA MAJI IMEHISANIWA NA KIWANDA CHA KUSINDIKA MINOFU YA SAMAKI VIC FISH... MZEE WA VIVA AFRIKA KIPITASHOTO ULICHOKUWA UKIULIZA NDICHO HIKI.