ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 15, 2009

BADO NIKO SHY TOWN MWANAWANE.


USIJE UKAHAMAKI PINDI UTAKAPO ULIZA VITUO VYA DALADALA UKAELEKEZWA MAHALA AMBAPO KUNA BAISKELI TUPU! AU VIJANA WA BAISKELI WAKIKUGOMBANIA KUKUHUDUMIA USAFIRI. UKITUA SHY TOWN BAISKELI NDIYO TWAITA DALADALA.. SITI ZINA SOFA KULIKARIMU KALIO LA MTEJA.. TEHE!!!

HII NDO CHAI.KWA WALE WASAFIRI TUNAO NGOJA USAFIRI KAMA NI ASUBUHI EH BANA KUNA MAMA MMOJA ANAYEZINGATIA KANUNI ZOTE ZA AFYA NA USAFI KATIKA KITORORI CHAKE AMBACHO NI FUUL NYENZO KUNA CHAI YA UKWELI "NZITO", VITAFUNWA VYA UHAKIKA. BABAKO NILIJICHUKULIA VITUMBUA NA CHAI YA MAZIWA (acha zile zetu za chai ya maziwa kutiwa maji hapa ni ziwachukuchuku imin lile shata shata)
HUDUMA ZA USWAFI KWA BUTI ZANGU NILIKUWA NIKIZIPATA HAPA MSHIKAJI ALINIPA JINA LAKE LAKINI DAH! LIKAWA GUMU KUTAMKIKA SEMBUSE KUANDIKIKA? TEH TEH NILIMWITA NYOKA LIKAWA JINA LAKE
NI MAMBO YA SHY BUS STAND PILIKAPILIKA HAZIISHI KITUO HIKI KINGEPATA WASEMAJI NA WATENDAJI WA KWELI KINGEKUWA TISHIO KWANI KIKO ENEO ZURI KATIKATI YA MJI.

Thursday, August 13, 2009

KITU CHA MALOVEE HEWANI"

KAA MKAO WA KUONA NA KUSIKIA HEWANI KAZI MPYA YA KOLABO LA MTU BEE TARSIS MASELA WA AKUDO IMPACKT MAVIJANA YA MASAUTI NAYE MSANII KUTOKA JIJINI MWANZA NURJAN KWA PAMOJA kupitia 88.1 WAMETAMKA RASMI KUITAMBULISHA KAZI YAO KATIKA SHOW YA JIJINI MWANZA IJUMAA HII na JUMAPILI NA KWA WALE WAPENZI WA MWONEKANO PLIZ KWA WAKATI WAKO CHUNGULIA LUNINGA YAKO.... KWANI VYOTE VITATOKA PAMOKO.

TUMEKOSA NINI?


PICHANI JUU NI BARABARA IINGIAYO KITUO KIKUU CHA MABASI MKOANI SHINYANGA. HEBU Tafakari mjomba:- WILAYA ZAKE ZIKIWA TEGEMEO LA PATO KWA TAIFA KUPITIA ZAO LA PAMBA, MKOA UKIWA WAZALISHJI WAKUU WA MADINI YA ALMASI NA DHAHABU PAMOJA NA RASLIMALI ZOTE HIZO HAPA KATIKA KITUO CHAKE KIKUU NI KULA VUMBI MWANZO MWISHO.
KWA MKOA WA MWANZA AJALI ZA PIKIPIKI NDIZO ZINAZOONGOZA KATIKA KUSABABISHA VIFO LAKINI MKOANI HAPA (SHY) AJALI ZA BAISKELI NDIZO NYINGI KWNI NDIYO USAFIRI MKUU WANAITA DALADALA.

KUNA MTU KANYOSHA MKONO ANATAKA KUJIBU... ENHEE!

HIVI ILE MIKWARA YA MADEREVA WA MABASI YA MIKOANI WAINGIAPO STAND INA MAANISHA NINI? KUONESHA KUWA MTU MZIMA ANAINGIA? PENGINE DEREVA ANATAKA KUONESHA UHODARI WAKE AU PENGINE KUDHIHIRISHA MBELE YA UMMA WA WALOSTENDI KUWA GARI NI ZIMA? SASA DHAHMA NI PALE KWENYE VITUO VISIVYO NA LAMI,, VUMBI LAKE......

NI USALAMA BARABARANI "UNASHANGA"

JAMAA ALISIMAMISHWA BAADA YA KUONEKANA ANA PEPA ZOTE ZA KUMRUHUSU KUWA BARABARANI SIKIO LANGU LIKANASA KILICHOKUWA KIKISIKIKA TOKA KWA AFANDE "WASHA ENDIKETA! WASHA FULL LIGHT! PIGA HONI! NENDA MBELE PIGA BREKI! WEIPER MBONA MOJA AICHEZI! TEH TEH.....

KILIMO KWANZA

PICHANI NI BWANA EMANUEL MASALU AMBAYE NI MKULIMA NA KWA MKULIMA HII NI MOJA KATI YA NYENZO ZA USAFIRI KUBEBEA MAZAO HUSUSANI PAMBA TOKA SHAMBANI KWENDA EITHER GHALANI AU SOKONI.