ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 26, 2017

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA ASHIRIKI UZINDUZI WA JENGO LA HUDUMA ZA MATIBABU YA BIMA YA AFYA BUGANDO

 Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula leo ameshiriki Uzinduzi wa Jengo la Huduma za Matibabu ya Bima ya Afya lililojengwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando Jijini Mwanza zoezi mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela

Akizungumza katika Uzinduzi huo Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kusifu uongozi wa hospitali ya Bugando kwa hatua kubwa ya maendeleo waliyoyafikia kwa haraka na muda mfupi  amewaasa watumishi wa hospitali hiyo kuongeza uadilifu na uwajibikaji huku akiwahakikishia utayari wa Serikali katika kuunga mkono na  kuisaidia hospitali hiyo.‘… Bugando ya sasa si ile ambayo tulikuwa tumeizoea huduma nyingi na bora zinapatikana hapa kama tunavyoona  tiba ya saratani inafanyika, magonjwa ya moyo inafanyika,  upasuaji unafanyika na hata yale ya ubongo kwa hiyo hakuna kitachobaki au kupungua, Mimi kama mwakilishi na kama msaidizi wa Mhe Rais nitakuwa shuhuda wakuyasemea na kushawishi namna bora ya kuiona Bugando kwa jicho la pili ili huduma zinazoihelemea hospitali yetu ya Muhimbili na Ocean Road  zianze pia kutolewa hapa hospitali ya Bugando …’ Alisema

Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula ametumia hadhara hiyo kuwasilisha salamu za Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula aliyeshindwa kuhudhuria uzinduzi huo kutoka na vikao vya kamati za bunge vinavyoendelea

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Mhe Raymond Mwamgalwa  amesema kuwa kilichofanyika ni utekelezaji wa  Ilani ya chama chake kinachounda Serikali hivyo anaridhishwa na utekelezaji huo wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kunakoenda  sambamba na ile sera ya HAPA KAZI TU

Nae mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya Bugando na baba askofu mkuu wa jimbo katoliki  Mwanza Thadei Rwai’ chi amemuhakikishia mgeni rasmi utayari wa kanisa katika kuhakikisha linasaidia wananchi kwa utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kijamii

Uzinduzi huo wa la huduma za matibabu ya bima ya afya hospitali ya kanda Bugando ulihudhuriwa na wabunge mbalimbali wa mikoa ya kanda ya ziwa, wawakilishi wa wakuu wa mikoa, wawakilishi wa wakuu wa wilaya, wataalamu wa wizara ya afya na viongozi wa dini

‘Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ’

MARUFUKU YA MIFUKO YA PLASTIKI KUTEKELEZWA KENYA KUANZIA AGOSTI 28.


Serikali ya Kenya imetanagaza kwamba marufuku ya mifuko ya plastiki itaanza kutekelezwa Jumatatu Agosti 28 kama ilivyopangwa.
Katibu katika wizara ya mazingira, Charles Sunkuli amesema makataa ya marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki hayatabadilishwa licha ya malalamiko ya watengenezaji bidhaa hiyo. Katibu huyo alisema marufuku hiyo inafanyika kwa mujibu wa katiba ambayo inampa kila Mkenya haki ya kuishi katika mazingira safi.
Sunkuli alisema tayari serikali imechukua hatua za kupunguza utengenezaji au uagizaji wa mifuko ya plastiki na inashirikiana na serikali za kaunti kubuni sera kuhusu kupunguzwa kwa matumizi ya mifuko hiyo. Aidha amesema serikali za kaunti kuhakikisha zimebuni sheria za kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki. 

Alisema Wakenya hawana budi ila kutafuta njia mbadala za kubeba bidhaa kwa lengo la kuhifadhi mazingira. 

Watengenezaji bidhaa wamedai kwamba marufuku dhidi ya mifuko ya plastiki itaathiri moja kwa moja takriban nafasi elfu 60 za ajira na nyingine laki 4 zisizokuwa za moja kwa moja. Hata hivyo serikali imekanusha ikisema mikakati kabambe imewekwa ili kuwalinda.

Harakati ya kuunga mkono marufuku ya mifuko ya Plastiki Kenya.
Kulingana na waziri wa mazingira nchini Kenya, Prof Judy Wakhungu mazungumzo kuhusiana na karatasi hizo yalianza miaka 15 iliyopita licha ya kwamba shirikisho la muungano wa watengenezaji wa bidhaa Kenya linaomba kupewa muda zaidi kutafuta njia mbadala.
Kwa mujibu wa sheria mpya, atakayekiuka marufuku ya mifuko ya plastiki hiyo anawezwa kutozwa faini ya kati ya shilingi milioni mbili na milioni nne pesa za Kenya (Dola 20,000-40,000 za Marekani) ama kifungo cha kati ya mwaka mmoja na miaka minne gerezani, au adhabu zote mbili.

POLISI YAFANYA UCHUNGUZI MLIPUKO OFISI ZA WANASHERIA.

Muonekano wa mbele wa ofisi hizo huku moto ukiendelea kuwaka muda ulipita.

Ofisi za IMMMA Advocates zinazomilikiwa na  wanasheria Fatuma Karume na Lawrence Masha zilizopo Upanga jijini Dar es Salaam, zimewaka moto leo asubuhi huku chanzo kikiwa bado hakijafahamika. Chanzo cha moto huo na hasara iliyosababishwa, bado havijafahamika na habari zaidi zitaendelea kukujia.
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya 

Dar es Salaam. Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya amethibitisha kushambuliwa ofisi za wanasheria za IMMMA saa 8 usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Agosti 26.

Mkondya amesema polisi wanafanya uchunguzi kujua ni nini kilihusika katika tukio hilo la mlipuko.


“Tupo hapa eneo la tukio, uchunguzi unaendelea na ukikamilika tutawapa taarifa zaidi, ila hatujajua kama bomu limehusika,” amesema Mkondya.


Ameeleza hadi sasa hakuna watu wanaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo.

Mmoja wa viongozi wa Kampuni ya IMMMA, Sadock Magai amesema hakuna wizi ambao umefanyika katika mali zilizokuwa ndani.


“Tuwaachie Jeshi la Polisi wafanye kazi yao,” amesema Magai.

 

Ofisi za wanasheria wa kampuni hiyo zipo Barabara ya Umoja wa Mataifa eneo la Upanga jijini hapa.


Miongoni mwa wamiliki wa kampuni hiyo ni Fatma Karume, ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume. 


Friday, August 25, 2017

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLY IDD AFUNGA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR

MWANAUME MTEKAJI AKAMATWA.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, DCP Ahmed Msangi.

Mwanaume mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumteka mtoto wakike aitwaye Khailati Bashiri (8) ambaye ni mwanafunzi wa darasa pili katika Shule ya msingi ya Iloganzala mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, DCP Ahmed Msangi amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Emmanuel Kirumbas (25) mkazi wa Malampaka mkoani Shinyanga ambapo majira ya 6:00 mchana ya tarehe 21.08.2017 alimchukua mwanafunzi huyo na kumpeleka kusikojulikana na baadae kutuma taarifa kwa njia ya simu kwamba apatiwe fedha kiasi cha Milioni 3 ili aweze aweze kumrudisha mtoto huyo.

Inasemekana kuwa baada ya mtoto huyo kutoka shuleni alikwenda nyumbani kwao mtaa wa Iloganzala anapoishi na wazazi wake kubadilisha nguo kisha aliondoka na kuelekea kusikojulikana, na kusababisha wazazi wake kuhangaika kumtafuta bila ya mafanikio ndipo walipoamua kutoa taarifa kituo cha Polisi.

DCP Msangi amesema baada ya kupokea taarifa hizo jeshi la polisi lilifanya upelelezi ambao ulipelekea kuwakamata watu watano na baadae kufanikiwa kumkamata mtekaji nyara ambae alikuwa akihitaji kulipwa fedha.

Jeshi la Polisi lipo katika mahojiano na mtuhumiwa na pindi uchunguzi utakapokamilika mtuhumiwa aliyehusika na utekaji atafikishwa Mahakamani.

JANUARY MAKAMBA AFUNGUA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

Na Mathias Canal, Zanzibar

Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) limefunguliwa jana tarehe 4 Agosti 2017 kwa kuwashirikisha washiriki wapatao 350, ambapo miongoni mwao wanadiaspora wamehudhuria zaidi ya 200 na watendaji kutoka taasisi za Serikali zote mbili wakiwa ni 150.

Diaspora wametakiwa kutumia fursa mbalimbali za uwekezaji nchini katika sekta ya kuimarisha na kuanzisha viwanda ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa dhamira yake ya kuifanyaTanzania kuwa nchi ya viwanda.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba (MB)  alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi litakalodumu kwa siku mbili Agosti 23 na 24, 2017 katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel uliopo katika kijiji cha Kama Wilaya ya Magharibi A.

Mhe Makamba alisema kuwa kwa sasa Demokrasia imeimarika nchini kutokana na serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kukubaliana kwa kauli moja kuimarisha usalama wa wananchi ili kurahisisha uimara wa uwajibikaji wa ujenzi wa Taifa.

Alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kuwa kuna changamoto nyingi zinazowakabili Diaspora ikiwemo ucheleweshwaji wa uwekezaji sambamba na kutokuwepo sera ya utambuzi dhidi yao lakini changamoto hizo zinaendelea kutatuliwa na hatimaye kumalizika kabisa.

Changamoto zingine ilikuwa ni pamoja na kuwepo kwa uraia wa nchi mbili ambapo Mhe Makamba alisema kuwa serikali inalifanyia kazi jambo hilo kwani halipo katika uhalisia kwa sasa kwa kutokuwepo kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili Diaspora waweze kutumia fursa ya uwekezaji nchini kwa urahisi huku akiwasihi kutumia fursa muhimu za uwekezaji katika Nyanja zote kwani faida itakuwa kwa Diaspora wenyewe, watanzania waishio nchini na Taifa kwa ujumla wake.

Alisema kuwa Diaspora ni kiungo muhimu katika kuchangia sehemu kubwa ya maendeleo endelevu katika nchi zao za asili kwa kuchangia katika uhamishaji wa rasilimali, ujuzi na mawazo na hatimaye kupelekea nchi yao kunufaika na uchumi wa kidunia unaoonekana kukua siku hadi siku.

Alisema kuwa fedha zinazotumiwa na Diaspora katika nchi wanazoishi ni miongoni mwa vyanzo vinavyosababisha ukuaji wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, fedha hizo zitakapotumika vizuri kwa uwekezaji katika biashara na vitega uchumi ndio huwa chanzo na kichocheo cha ukuaji jadidifu wa pato na uchumi wa nchi zinazopokea fedha hizo.

Aidha, Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imeweka msisitizo na juhudi za kukusanya mapato ili kukuza uchumi wa Tanzania na uwezo wa serikali kujiendesha.
Mhe Mkamba aliwasihi Diaspora kufuata kanuni,taratibu na sheria katika nchi wanazoishi ili kuendelea kuiweka Tanzania katika sifa nzuri ya kuwa na wananchi wenye kufuata sheria na taratibu.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeratibu Kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi Ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) kwa minajili ya kuwaweka pamoja watanzania hao ili kujadili kwa pamoja namna ya kutumia fursa za uwekezaji.
Kongamano hilo ni mwendelezo wa makongamano matatu ya awali yaliyofanyika mwaka 2014 na 2015 Jijini Dar es Salam na mwaka 2016 lililofanyika Mjini Zanzibar.

Lengo kuu la makongamano hayo ni kwa Serikali na wanadiaspora kukutana, kubadilishana mawazo na kuwashajihisha wanadiaspora kuwekeza nchini kwao kwa maslahi yao na kwa ustawi wa uchumi wa taifa lao.

Kongamano hili la nne la Diaspora limebebwa na dhamira ya “Uzalendo kwa Maendeleo” chini ya kauli mbiu isemayo “Mtu Kwao, Ndio Ngao”

Katika hatua nyingine washiriki wote wamepata fursa ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuboresha umoja huo wa watanzania waishio nje ya nchi sambamba na kutoa maoni yao kwa serikali kwa dhamira ya kuwa na Umoja na ushirikiano bora kati yao na serikali.

Pia walitembelea shamba la BIG BODY SPICE linalolima mazao mbalimbali ya
viungo ikiwemo mazao ya Pilipilimanga, Mdalasini, Kahawa, Hiliki, Vanila,
Mdoriani, Kakao, Karafuu, Tangawizi, Mrangirangi na Mkungumanga.

Baadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Mkurugenzi Mpya wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Ndg Geofrey Mwambe akizungumza wakati wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni linalofanyika Sea Cleaf Hotel Mjini Zanzibar
Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo

Dkt Hamed Hikmany (Katikati) akiongoza mada kuhusu Ushauri wa uwekezaji kwa siku zijazo mara baada ya ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

Mhe Hassan Khamis (Katikati) akiongoza mada kuhusu Jukumu la jumuiya ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi katika uwekezaji sambamba na Diaspora na nchi yao katika maendeleo endelevu mara baada ya ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar


Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni wakimsikiliza kwa makini Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

Baadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni wakifatilia kwa makini Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar
Baadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Baadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Baadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni wakimsikiliza kwa makini Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar.

Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) wakitembelea shamba la BIG BODY SPICE kujionea kilimo cha mazao ya viuongo

Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu kilimo cha mazao ya viuongo mara baada ya kutembelea shamba la BIG BODY SPICE

Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu kilimo cha mazao ya viuongo mara baada ya kutembelea shamba la BIG BODY SPICE


Mkwezi akionyesha umahiri wa kukwea mnazi mbele ya Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) walipotembelea shamba la BIG BODY SPICEWashiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Kisasa Fumba Town Development mara baada ya kutembelea katika eneo hilo.