Timu ya toto ya jijini Mwanza leo tena imeendeleza wimbi lake la ushindi kwenye mechi zake za Pre' season ya Tz Premium League mara baada ya kutandaza kichapo kingine cha mabao 5-0 kwa timu ya TSC ya jijini Mwanza.
Magoli ya Toto Africans yamefungwa na Chika Chukwu, Salum Kamana na Ariwodo Darlington aliyepiga 3.
Baadhi ya wafanyakazi wa Villa park wakishiriki futari iliyoandaliwa maalum kwao na wadau wao wa karibu. Blogu hii inawatakia kheri na fanaka waislamu wote katika kipindi chote hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe (kulia) akishikana mikono na motto yatima, Zena Mohamekatika hafla ambayo Airtel ilikanodhi msaada wa vyerahani 10 kwa vikundi vitatu vya wanawake vya kulelea watoto yatima vya Msasani, Kawe na Kinondoni, Jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe (kushoto) akikabidhi moja ya mashine za kushonea, cherahani, kwa mwakilishi wa kikundi cha wanawake cha kulelea watoto yatima cha Kawe Huruma Group , Hilda Rwebangira.
Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe (kushoto) akikabidhi moja ya mashine za kushonea, cherahani, kwa mwakilishi wa kikundi cha wanawake cha kulelea watoto yatima cha Msasani Womens and Orphans Centre, Yonnes Kihiyo katika hafla hiyo.
KAMPUNI ya simu za mikononi ya AIRTEL imetoa msaada wa vyerehani kumi kwa vikundi vitatu vya wanawake vinavyolea watoto yatima jijini Dar Es Salaam ili kuviongezea uwezo wa kulea watoto wanaolelewa katika vituo hivyo. Msaada huo umekabidhiwa na meneja huduma za jamii wa airtel Tunu kavishe kwa vikundi hivyo. Vikundi vilivyofaidika na msaada huo ni kikundi cha wanawake cha kulea watoto yatima cha Msasani, kikundi cha Huruma cha Kawe pamoja na kile cha kulea watoto yatima cha Kinondoni.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Bi.Kavishe alisema "AIRTEL itaendelea kugawa misaada kwa vikundi vya wasiojiweza ikiwa ni sehemu ya kampeni yake ya kusaidia jamii katika kutatua baadhi ya matatizo ambayo inayakabili hususani katika sekta ya elimu". Akipokea msaada huo wa mashine za kushonea, mwakilishi wa kikundi cha wanawake cha kulelea watoto yatima cha Msasani Womens and Orphans Centre, Prudencia Kibatara alisema " Msaada huu utatusaidia katika kuboresha utoaji wa huduma kwa watoto hawa ambao tunawahudumia katika vituo vyetu. Tunachangamoto nyingi ikiwemo idadi kubwa ya watoto na kipato kidogo cha uendeshaji vikundi hivi, hivyo tunawapongeza sana Airtel kwa kushirikiana nasi katika kusaidia jamii. Kupitia cherehani hizi tutaanzisha madarasa ya ushonaji na ada zitakazolipwa zitatumika kusaidia watoto hawa, vilevile chereharani hizi zitatumika kushona vitambaa na mashuka ambayo yataleta pato katika vikundi na tutaweza hata kuendelea kuwasomesha watoto hawa vizuri" aliendelea kusema Bi Kibatara
Aidha Afisa mtendaji wa kata ya msasani .. Swai aliiipongeza kampuni ya simu ya Airtel kwa kujitokeza na kusaidia vikundi hivyo na kutoa angalizo kwa walezi wa vikundi hivyo kutumia msaada huo kwa manufaa ya watoto na si yao binafsi.
"Jamani wakina mama naomba huruma zetu za dhati ziendelee hakikisheni mnaendelea kutumia msaada huu mlioupata kama nyenzo ya kuendelea kuwatunza na kusaidia watoto hawa na sio kujifaidisha sisi wenyewe" alisema Afisa mtendaji wa Msasani .
..Leo Airtel wameonyesha jinsi wanavyojali jamii wanayoihudumia hivyo naomba tuwaunge mkono ili dhamira yao itimie" alimaliza kwa kusema afisa mtendaji...
Vituo vilivyopata msaada huo viko jijini Dar es salaam ambavyo kwa ujumla vyote vinalea watoto wasiopungua 40 kila kimoja. Watoto wanaolelewa katika vituo hivyo bado wanamahitaji mengi japo kampuni ya simu za mkononi airtel imeweza kujitolea msaada huo wa vyerehani bado pia wanahitaji vifaa vya shule, vifaa vya kujifunzia, chakula pamoja na malazi ya kila siku.
Airtel imekuwa mstari katika kusaidia uboreshaji wa maisha ya jamii kwa kutoa misaada ya aina mbalimbali na kudhamini shughuli za miradi ya maendeleo.bado Airtel inampango wa kutoa msaada wa cherehani pia katika mikoa ya mwezi huu kwa dhumuni la kuendelea kupunguza tatizo la kipato kwa vituo vya wananchi wanaoishi katika mazingira magumu.
Mwisho
Wednesday, August 03, 2011
HABARI
Aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak amekana mashtaka ya rushwa na kuamuru kuuliwa kwa waandamanaji, siku ya mwanzo ya kesi yake iliyofanyika mjini Cairo.Bw Hosni Mubarak
Waandishi walisema, alipelekwa akiwa kwenye kitanda cha hospitali na kuwekwa ndani ya kizimba mahakamani humo, jambo lililowashtusha wengi waliokuwa nje.
Bw Mubarak mwenye umri wa miaka 83 anashtakiwa na watoto wake wawili wa kiume, ambao pia walikana mashtaka yanayowakabili, na pia aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Habib al-Adly na waliokuwa maafisa wengine sita.
Hukumu ya kuamuru mauaji ya waandamanaji ni adhabu ya kifo.
Takriban askari na polisi 3,000 wamezambazwa kuhakikisha kuna utulivu katika chuo cha mafunzo cha polisi ambapo kesi hiyo inasikilizwa.
Awali ilikuwa isikilizwe kwenye kituo cha mkutano cha Cairo lakini mamlaka husika zikahamisha eneo na kuunda mahakama ya muda ndani ya chuo hicho kutokana na suala la usalama.
Inakadiriwa watu 600 walitazama kesi hiyo ndani na nje ya mahakama, na mamilioni ya wengine wengi wakitazama kupitia televisheni.
URBAN PULSE CREATIVE ikishirikiana na True Talk Records Company inapenda kuwaletea program mpya ya tv inayoitwa Friday Night Freestyle special. Hii ni Reality Programme yenye mchanganyiko wa ucheshi, ubunifu wa kushika Mic mtaani mbele ya kamera na kuonesha vipaji kutoka kwa wasanii waliopo hapa UK. Programme hii itarushwa kwenye TV Hapa UK na baadhi ya Nchi jirani za Ulaya. Vilevile kutakuwepo na zawadi mbalimbali kwa washindi na recording deal mwishoni mwa series
Asanteni
URBAN PULSE CREATIVE
Monday, August 01, 2011
AFYA
PICHA ZOTE KWA HISANI YA AHMAD MICHUZI WA JIACHIE BLOG NA CUTHBERT ANGELO WA HABARI NA MATUKIO BLOG
IMETENGENEZWA NA
FREDY TONY NJEJE-MBEYA YETU BLOG