Tupe maoni yako
Serikali yazindua vitabu vya kiada kwa Elimu ya Ualimu
-
Leo tarehe 25/11/2024 Serikali imezindua zoezi la ugawaji wa vitabu vya
kiada kwa vyuo vya ualimu chini ambavyo vitataumika kwa walimu tarajali
nchi nzima....
25 minutes ago
sawa tunatambua umuhimu wa matunda na mboga mboga, lakini mboga zinazolimwa na kuvunwa pembezoni mwa ziwa victoria hususan kata ya Kirumba kuanzia daraja la mto Mirongo hadi njia panda ya Mwaloni Kirumba, na eneo la Iloganzala kata ya Pasiansi ni hatari sana ! Mboga hizo zipo pembezoni mwa barabara ambapo magari na vyombo vya moto vinatoa moshi ikiwa ni mchakato wa kuunguza mafuta ambayo yana madini ya risasi (lead - Pb) ni hatari kwa afya za binadamu. Tunakufa pole pole kutokana na kula mboga zilizozalishwa katika maeneo ambayo si salama kimazingira. Aidha, wakati mwingine walzalishaji hao wa mboga hutumia madawa ya kuulia wadudu kwenye mimea hata siku chini ya 14 kabla ya kuvuna. Dawa hizi hubaki katika majani na hivyo kuwa sumu kwa mlaji.
ReplyDeleteNi ujasilia mali kwa anayelima na kuuza. Lakini kwa mlaji mboga mboga hizo hazifanyi kazi inayostahili kama wewe mtangazaji unavyojaribu kutushawishi kuwa twajua umuhimu wa matunda na mboga mboga. Badala yake wakulima wanawaua walaji pole pole. Ndiyo maana baada ya muda matatizo ya figo, maini, shinikizo la damu na magonjwa mengine mengi hatari yanajitokeza. Tabia yetu ya kutopima afya mara kwa mara husababisha mtu kugundua tatizo wakati limekwisha komaa. Aidha, elimu ndogo ya afya ya walaji wengi, matatizo ya namna hii yanapojitokeza, badala ya kwenda hospitali unawakuta kwa sangoma wakifikiri wamelogwa. Kumbe wachawi ni wakulima wa mboga mboga pembezoni mwa barabara.
CHUKUENI TAHADHARI, ACHENI KUNUNUA MBOGA ZILIZOLIMWA PEMBEZONI MWA BARABARA MADHARA YAKE NI MAKUBWA MNO KWA WATUMIAJI WA MUDA MREFU WA MBOGA HIZO.Pia mnaponunua mnawahamasisha waendelee kuharibu mazingira ya ziwa ! kaombwe
Aaaaaa KAOMBWEeeee!!! umetisha kaka aksante kwa elimu.
ReplyDelete