ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 2, 2018

DALOT AKARIBIA KUFANYA VIPIMO MAN UNITED.


DIOGO Dalot anatarajiwa kufanya vipimo katika kikosi cha Manchester United wiki ijayo, baada ya klabu hiyo kukamilisha malipo yake kwa Porto.

Dalot ameendelea kupata matibabu ya goti wakati United ikiendelea kujadi-liana na Porto juu ya kumnasa kwa chini ya kiwango cha pauni milioni 17.4 (Sh bil 52.5) ambacho anatakiwa kuuzwa.

United inamtaka beki huyo wa kulia ili akampe changamoto Antonio Valencia, ambaye ana umri wa miaka 33 na mara nyingi amekuwa akihitaji matibabu ya goti.

Dalot aliyewahi kung’aa katika timu ya taifa ya Ureno ya vijana chini ya miaka 21, anaweza pia kucheza kama beki wa kushoto. Lakini aliingia kwenye timu kubwa ya taifa hilo Februari, mwaka huu.

Aliisaidia Ureno kubeba ubingwa wa Ulaya (Euro) 2016 kwa vijana chini ya miaka 17, akifunga mabao mawili katika mechi tano likiwemo bao moja kwenye fainali.

Wakati huohuo, United inataka kuachana na beki Matteo Darmian ambaye imepanga kumuuza kwa mabingwa wa Italia, Juventus, kwa dau la pauni milioni 11.5 (Sh bil 34.7).

WAARABU WATIBUA MIPANGO YA CHIRWA KUTUA SIMBA.

Huku taarifa za chini kwa chini zikielezwa kuwa Simba inamuwinda kwa udi na uvumba mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa, imeelezwa waarabu wameingilia kati mpango huo.

Klabu ya Ismailia ya Misri imeingilia rada za Simba kuhusiana na usajili wa Mzambia huyo ambapo taarifa zinasema imeanza mazungumzo ya kuweza kumnyaka mchezaji huyo tegemeo kwa Yanga.

Chirwa ameshindwa kujumuika na kikosi cha Yanga kuelekea Kenya kwa ajili ya michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza kesho.

Waarabu hao wameanza kuifanyia umafia Simba ambapo inaelezwa wameandaa dau nono zaidi ya Simba hivyo kuweka ugumu wa kujiunga na wekundu hao wa Msimbazi ambao wanatajwa kupigania saini yake hivi sasa.

Mzambia huyo amekuwa akiwindwa na Simba ingawa mwenyewe amekuwa akieleza kuwa anatamani kucheza soka la kimataifa hivyo kuna hatihati kama anaweza akasalia Tanzania msimu ujao.

Uwezekano mkubwa wa Chirwa kuondoka Yanga unawezekana kutokana na mchezaji huyo kugoma mara kadhaa kusafiri na timu pale inapotoka kwenda nje ya nchi kushiriki mashindano ya Kimataifa, ikielezwa kuwa anaidai stahiki zake ikiwemo mishahara.

Friday, June 1, 2018

RC MONGELLA AZINDUA TAWI JIPYA LA KAMPUNI YA RESOLUTION INSUARANCE MWANZA


GSENGO tV
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongella leo amezindua Tawi jipya la Kampuni ya Bima RESOLUTION INSURANCE Mwanza ambalo litakuwa Tawi la kanda ya ziwa.

HIKI HAPA KICHUPA KINACHOTIKISA CHA DIAMOND PLATNUMZ FT RAYVANNY - IYENA (Official Music Video)


Ndani ya kipindi kifupi tu mkali kutoka East Africa anayetikisa kwa level zisizo na kifani Diamond Platnumz kachafua anga la burudani, hapa ninamaanisha kuwa kimenuka. 

Hatimaye Diamond Platnumz kaachia mkwaju wake mpya wenye mahadhi ya pwani 'Iyena' ambapo humo ndani akimshirikisha mkali mwingine kutoka Wasafi, Rayvanny na katika kichupa hicho mkali huyo katoa bonge la fumbo ambalo kwalo limewaacha watu wengi kwenye kiza cha tafakari.

Dumbukia You Tube kisha utaniambia kama kweli hutotoka na maswali.....

HII NDIYO NGOMA YA KALA JEREMIAH INAYOSUMBUA MJINI KWA SASAKala Jeremiah Ft Walter Chilambo - NATABIRI (Official Video)

Thursday, May 31, 2018

ZIDANE AACHIA NGAZI REAL MADRID, WENGER ATAJWA KUMRITHI.

KOCHA Mfaransa, Zinedine Zidane amejiuzulu ukocha wa Real Madrid baada ya kuiongoza timu kutwaa mataji matatu ya kihistoria ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu hiyo, aliitisha mkutano na Waandishi wa Habari leo ghafla akisema kwamba ataondoka baada ya miaka miwili na nusu kazini.

Zidane mwenye umri wa miaka 45 na gwiji wa klabu kama mchezaji na kocha amesema anafikiri huu ni wakati mwafaka kuondoka.

Makocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger, kocha wa sasa wa Chelsea, Antonio Conte na wa Tottenham, Mauricio Pochettino wapo mstari wa mbele katika kuwania nafasi hiyo.

Akiwa ameongozana na Rais wa Real, Florentino Perez, Zidane alisema: "Nimechukua uamuzi wa kutoendelea msimu ujao. Kwangu mimi na kwa mtu yeyote, nafikiri wakati wa mabadiliko umefika. Haukuwa uamuzi mwepesi,".

Zidane alimuambia Perez mpango wake huo Jumatano. "Naipenda hii klabu, nampenda rais,"amesema. "Alinipa nafasi ya kuja kama mchezaji na sasa kocha na ninajivunia. Lakini tunatakiwa kubadilika.

"Nitakuwa karibu na hii klabu kwa maisha yangu yote yaliyobaki. Ninataka kuwashukuru mashabiki, ambao wakati wote wamenisapoti nikiwa kama mchezaji na kocha. Kulikuwa kuna wakati mgumu katika msimu na pia kuna wakati nilikubaliana na hali halisi, ninataka kuwashukuru mashabiki,".

Zidane, kiungo wa zamani wa Real, Juventus na Bordeaux inafahamika alikuwa ana mkataba Madrid hadi mwaka 2020.

Baada ya kujiuzulu ukocha wa kikosi cha vijana cha Real Madrid, kijulikanacho kama Castilla B, akaenda kuchukua nafasi ya Rafa Benitez kikosi cha kwanza Januari mwaka 2016 na mwishoni mwa msimu Real ikamaliza nafasi ya pili nyuma ya Barcelona katika La Liga.

Akatwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa penalti 5–3 baada ya sare ya 1–1 mjini Milan.

Zidane akaongeza taji la La Liga Juni 2017 kabla ya kutetea taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuifunga 4-1 Juventus mjini Cardiff. 

HIII HAPA NAMBA NYINGINE KATIKA USAJILI LIVERPOOL, ILIYOPACHIKWA JINA COUTINHO MPYA.


Nabil Fekir - Welcome To Liverpool - "The Next Coutinho" - Insane Goals, Dribbling and Skills 2018

POLISI YA RWANDA YAWATAKA RAIA KUACHA KUINGIA HIFADHI ZA TANZANIA KINYEMELA ILI KUEPUKA MATATIZO.


CHANZO/PARStoday
Katika juhudi za kudumisha ujirani mwema kati ya Rwanda na Tanzania, serikali ya Kigali imewaonya raia wa taifa hilo hususan wale wanaoisho maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo karibu na mpaka wa Tanzania kujiepusha na vitendo vya kuvuka mpaka kuingia nchi hiyo jirani.
Hii ni kwa kuwa raia hao wamekuwa wakivuka mpaka wa Rwanda na kuingia Tanzania kwa ajili ya kuwinda na kushenya kuni, kitendo ambacho kimekuwa na matokeo mabaya.

Askari wa kulinda hifadhi Tanzania wakiwapiga vikali watu wanaowakamata katika operesheni zao

Kwa mujibu wa maafisa wa polisi wa Rwanda, aghlabu ya Wanyarwanda wanaokamatwa na maafisa wa wanyamapori wa Watanzania huwa wanapigwa vibaya huku wengine wakipoteza maisha kabisa.

AIRTEL NA ITEL WAZINDUA SMARTPHONE MPYA YA A32 F NA BANDO NA AILTEL BURE MIEZI SITA.

 Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchuda akionyesha simu mpya ya A32 F ya smartphone baada ya kuzindua kwa kushirikiana na itel pamoja na Airtel Tanzania. Simu hiyo inakuja na GB 12, dakika 300, na sms 300 BURE kwa miezi sita kutoka Airtel. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mauzo itel Dar es Salaam Loalla Xu  na Meneja Uhusiano Itel Erick Mkomoya.
 Mkuu wa Masoko na Mauzo itel Dar es Salaam Loalla Xu- kulia Nchuda akionyesha simu mpya ya A32 F ya smartphone baada ya kuzindua kwa kushirikiana na itel pamoja na Airtel Tanzania. Simu hiyo inakuja na GB 12, dakika 300, na sms 300 BURE kwa miezi sita kutoka Airtel. Kati ni  Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mauzo  na Meneja Uhusiano Itel Erick Mkomoya
Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchuda akisalimiana na Mkuu wa Masoko na Mauzo itel Dar es Salaam Loalla Xu  baada ya kuzindua simu mpya ya A32 F ya smartphone kwa kushirikiana na itel pamoja na Airtel Tanzania.   Simu hiyo inakuja na GB 12, dakika 300, na sms 300 BURE kwa miezi sita kutoka Airtel. Kulia ni na Meneja Uhusiano Itel Erick Mkomoya.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Airtel na itel wazindua SMARTPHONE mpya ya A32 F na Bando la Airtel BURE miezi sita
·         Wateja wa Airtel kuunganishwa na GB 12, dakika 300, na sms 300 BURE kwa miezi sita wakinunua simu ya Airtel katika maduka ya Airtel na itel  popote
·         Airtel na itel yazindua smartphone nafuu inayotumia alama za vidole yenye AndroidTM  Oreo
Dar-es-Salaam, Jumatano 30, Mei 2018: Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania na kampuni ya kutengeneza simu ya itel leo kwa pamoja wamezindua simu mpya ya itel A32 F iliyoambatanishwa na offer ya bando ya intaneti yenye kifurushi cha BURE cha GB 12, dakika 300 pamoja na sms 300 kwa muda wa miezi 6 mfululizo.

Ushirikiano wa Airtel na itel unawahakikishia Watanzania uwezo wa kupata simu za kisasa za smartphone zenye ubora wa juu kwa gharama nafuu zaidi. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa simu hiyo ya kisasa kabisa yenye ofa kabambe, Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania Isack Nchuda alisema “Tunajivunia ushirikiano wa Airtel  na itel kwa kuzindua simu mpya na ya kisasa ya A32F. 

Wenzetu wa itel wanalenga kuhudumia  wateja wa kipato cha kati na cha chini kwa bidhaa zenye ubora na unafuuu, Hivyo basi Airtel ikiwa moja ya makampuni yanayotoa huduma za smartphone za kisasa na  uhakika, tukaona tuwafikishie ofa hii kabambe watanzania wote ili kuwawezesha kuendana na ulimwengu wa kidigitali kwa kutumia mtandao wetu ulio bora na ulioenea kote nchini na simu ya itel.  

Simu ya A32 F itakuwa inapatikana kwenye maduka yote ya Airtel na itel kote nchini ikiwa  na ofa ya kifurushi cha bando ya intaneti ya 12GB chenye muda wa miezi sita ambapo kila mwezi ni 2GB pamoja na nyongeza ya sms 300 na dakika 300 zote kutoka Airtel Tanzania.

Kwa upande wake, Mkuu wa Masoko Mkoa wa Dar es salaam kutoka itel Mobile Mr. Walle XU, alisema kuwa ni furaha kubwa sana kushirikiana na Airtel kuzindua simu mpya ya kisasa ya itel A32 F ambayo ni smartphone ya kwanza kutumia alama za vidole (finger print) yenye AndroidTM  Oreo™ ambayo ni toleo la kisasa na inapatikana kwa bei nafuu kabisa Tanzania nzima. Simu ya A32 F ni nyepesi sana na inatoa suluhisho bora kwa watumiaji wa huduma za kidigitali kwa uhakika na haraka kabisa itapatikana kwa gharama nafuu, alisema Khosla.

Bwana Walle aliongeza kuwa itel A32 F ina usalama na uhakika kwa kuwa inauwezo wa kutambua vidole vya mwenye simu na iweza kuweka programu nane ambazo zinatumika kwa matumizi mbalimbali kama kupiga picha, kupiga video, kupokea simu, stop alarm pamoja kusajili vidole vitano ambavyo kila kidole kinakuwa na kazi yake maalum.

Alisema vifaa vingine ni ukumbwa wake wa inch 5.0 pamoja na kamera ya kisasa ya 5mp kwa nyuma na mbele 2mp na inaweza kupiga picha kwa mazingira yeyote yale. Pia simu hiyo ina memory ya 8GB+1GB ambazo zinaweza kuzidi mpaka 32GB.
Mwisho

TBL GROUP YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUPANDA MITI MKOANI KILIMANJARO

 Wafanyakazi wakijiandaa kuanza zoezi la kupanda miti wilayani Siha, Kilimanjaro.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL waliopo katika mafunzo ya kukuza vipaji wakishiriki zoezi la kupanda mito wilayani Siha, Kilimanjaro.
Wafanyakazi wakipanda miti wilayani Siha, Kilimanjaro.
Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group, George Kavishe akiongea wakati wa tukio la upandaji miti Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba wakati wa hafla hiyo

Na Mwandishi Wetu.

*Kushirikiana na Kilimanjaro Project kupanda miti 100,000 mkoani humo.

Kampuni ya TBL Group  imeshiriki zoezi la kupanda miti wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, ukiwa ni mwendelezo wa mkakati wake wa pamoja na taasisi ya Kilimanjaro Project na wadau wengine, kupanda miti 100,000 mkoani Kilimanjaro, katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani

Zoezi la upandaji miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani limeongozwa na Mkuu wa wilaya ya Siha, Mheshimiwa Onesmo Buswelu, ambaye alisema kuwa jukumu la kutunza mazingira ni la kila mmoja na kupongeza kampuni ya TBL Group na wadau wake kwa jitihada wanazofanya kulipa kipaumbele suala la kutunza mazingira.

Alisema katika miaka ya karibuni  Tanzania imekuwa ikikabiliwa na mabadiliko ya tabia nchi, ambayo yametokana na athari za uharibifu  mbalimbali wa mazingira kama vile, kukata miti ovyo,shughuli za kilimo kisicho na mpangilio.Moja ya eneo lililoathirika na uharibifu wa mazingira alilitaja kuwa ni maeneo yanayozunguka mlima Kilimanjaro.

Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano wa TBL Group, Zena Tenga, alisema ili kukabiliana na changamoto ya kudhibiti uharifu wa mazingira mkoani Kilimanjaro,  kampuni ya TBL kwa  kushirikiana na taasisi ya  Kilimanjaro Project imejiwekea malengo ya kuunga mkono jitihada za serikali za kudhibiti uharifu kwa mazingira kwa kujiwekea malengo ya kupanda  miti 100,000 katika mkoa wa Kilimanjaro katika kipindi cha miaka 10 ambao imeanza kuutekeleza

Tenga alisema, idadi ya mamilioni ya miti inakatwa kila mwaka mkoani Kilimanjaro pia hekari zipatazo 300,000 za ardhi zinakatwa miti kwa ajili ya mkaa na kuni na shughuli nyinginezo za kilimo,takwimu hizi zinatoa tahadhari kuwa hatua za kulinda mazingira zinapaswa kuchukuliwa “Katika kipindi cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka huu tunaanza hatua ya awali ya kupanda miti milioni moja”,alisistiza.

Mwasisi na Kiongozi wa mradi huu, Sarah Scottt, kutoka taasisi ya Kilimanjaro Project amesema “Maandalizi ya kufanikisha mpango huu  yanaendelea vizuri,hatua za awali za kuotesha mbegu za miti na kuainisha maeneo ya kupanda miti na mikakati ya kuitunza ili isitawi yanaendelea vizuri. Tunaamini tukiungaisha nguvu kukabiliana na changamoto hii tunaweza na kurejesha  hali nzuri ya hewa mkoani Kilimanjaro ilivyokuwa hapo awali na mvua za uhakika kupitia kupanda miti kwa wingi”

Mradi huu kwa upande wa TBL Group utatekelezwa na chapa yake ya Bia maarufu ya Kilimanjaro Lager. Meneja Masoko na Udhamini  wa TBL Group, George Kavishe amesema “Kupitia bia ya Kilimanjaro tutaelimisha  jamii juu na elimu hiyo  itahusu uhamasishaji wa kupanda miti kwa wingi,kutunza mazingira ya asili na kuhamasisha kila mmoja kuwajibika na  utunzaji wa dunia yetu tunayoishi”,alisema Kikuli.

Ili kufanikisha lengo ya upandaji miti milioni moja,TBL Group na taasisi ya Kilimanjaro Project zinakaribisha mashirika na kampuni nyingine za biashara ikiwemo na watu binafsi kushiriki katika kampeni hii na kupanda miti Kilimanjaro. TUJE PAMOJA!  Tushirikiane kwa kuonyesha vitendo ili kufanikisha kuleta mabadiliko change!

Mbali na kupanda miti mkoani Kilimanjaro, TBL Group chini ya kampuni mama ya ABInBev imekuwa mstari wa mbele kutekeleza sera ya kulinda mazingira kwa kuhakikisha inatumia uzalishaji kwa kutumia  mifumi isiyoharibu mazingira sambamba na kushiriki kutoa elimu ya kulinda mazingira na vyanzo vya maji.Vilevile wafanyakazi wake wamekuwa mstari wa mbele kushiriki katika miradi mbalimbali ya utunzaji wa mazingira.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi Ahmed Msangi.

Wednesday, May 30, 2018

MARUFUKU YATOLEWA:- KUHUSU MAROLI YABEBAYO WATU KWENYE MISIBA.

Jeshi la polisi mkoani Mbeya limepiga marufuku matumizi ya malori kwenye misiba na minadani kwa madai kuwa ni chanzo cha ajali.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Mussa Taib ametoa kauli hiyo Jijini Mbeya wakati akizungumza na madereva wa bodaboda na bajaj.

MWANZA YAJIUNGA NA LIGI YA MIJI INAYOPATA HUDUMA YA USAFIRI KIDIJITALI BAADA YA TAXIFY KUINGIA RASMI JIJINI HUMO.

 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Ms. Mary Tesha ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Taxify iliyozinduliwa hivi karibuni jijini humo. Jiji la Mwanza sasa limeingia kwenye ligi ya miji ya kisasa duniani baada ya kuingia rasmi kwa Kampuni ya Taxify inayotoa huduma ya usafiri kidijitali.
 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Ms. Mary Tesha ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Taxify iliyozinduliwa hivi karibuni jijini humo. Jiji la Mwanza sasa limeingia kwenye ligi ya miji ya kisasa duniani baada ya kuingia rasmi kwa Kampuni ya Taxify inayotoa huduma ya usafiri kidijitali. 
 Msanii wa muziki wa hiphop, Fareed Kubanda a.k.a Fid Q akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya Taxify iliyofanyika hivi karibuni jijini Mwanza.
 Meneja wa Taxify Kanda ya Ziwa, Milumbilwa Kipimo akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hafla ya uzinduzi ya huduma ya Taxify hivi karibuni jijini Mwanza. Jiji hilo limeingia kwenye ligi ya miji ya kisasa duniani baada ya kuingia rasmi kwa Taxify, Kampuni inayotoa huduma ya usafiri kidijitali.
 Meneja Uendeshaji wa Taxify nchini Tanzania, Remmy Eseka akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Taxify hivi karibuni jijini Mwanza. Jiji hilo limeingia kwenye ligi ya miji ya kisasa duniani baada ya kuingia rasmi kwa Taxify, Kampuni inayotoa huduma ya usafiri kidijitali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taxify, Kanda ya Afrika Mashariki, Shivachi Muleji (kushoto) akikabidhi fulana kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Ms. Mary Tesha ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Taxify iliyofanyika hivi karibuni jijini Mwanza. Jiji hilo sasa limeingia kwenye ligi ya miji ya kisasa duniani baada ya kuingia rasmi kwa Kampuni ya Taxify inayotoa huduma ya usafiri kidijitali.

MWANZA YAJIUNGA NA LIGI YA MIJI INAYOPATA HUDUMA YA USAFIRI KIDIJITALI BAADA YA TAXIFY KUINGIA RASMI JIJINI HUMO.
  • Mwanza, ‘The Rock City’ kama inavyofahamika kwa wengi nchini Tanzania, leo imeingia kwenye ligi ya miji ya kisasa duniani baada ya kuingia rasmi kwa huduma ya usafiri kidijitali jijini humo.
Mwanza, Taxify, ambayo ni miongoni mwa Kampuni kubwa zinazotoa huduma ya usafiri kidijitali barani Ulaya na Afrika imezindua rasmi huduma zake jijini Mwanza huku mamia ya madereva wakiwa tayari wamesajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma katika maeneo yote ya jiji.
Katika kusherekea uzinduzi wa huduma hiyo, Taxify inatoa punguzo la asilimia 50 kwa abiria kuanzia tarehe 28 Mei, 2018 mpaka mwisho wa mwezi wa sita mwaka huu. Gharama za usafiri kwa kipindi hiki ni:- Kuanza safari ni TZS 700, Kwa kilometa ni TZS 460, Kwa dakika ni TZS 70 huku gharama ya chini kabisa ya safari ikiwa ni TZS 2,000.
Mwanza ni jiji lenye watu zaidi ya milioni 3.5, barabara nzuri zenye ubora, Huduma bora ya mitandao inayopatikana kirahisi na maelfu ya magari. Tulifanikiwa kupokea maombi mengi kutoka kwa wakazi wa jiji hili waliokuwa na shauku ya kutumia huduma yetu lakini huduma yetu ilikuwa bado haijafika jijini hapa, jambo hili limetusukuma kuzindua rasmi huduma yetu leo jijini hapa. Mamia ya madereva wameshasajiliwa kwenye jukwaa letu na tayari tumeshaona mamia ya safari ambazo zimefanyika hata kabla ya uzinduzi rasmi. Mwanza ipo tayari kwa huduma ya usafiri kwa njia ya mtandao na tunaimani kuwa huduma hii itafanya vizuri katika jiji la ‘Rock City’ alisema Remmy Eseka, Mkuu wa Operesheni, Taxify Tanzania.
Mary Tesha, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati wa uzinduzi wa Taxify Mwanza, alisema "Kama Serikali tumejenga miundombinu na kupitisha kanuni ambazo zinaunda mazingira wezeshi ya biashara na wawekezaji kuja kutoa fursa kwa Watanzania. Huduma hii ya usafiri kwa njia ya mtandao imeonekana kuboresha maisha katika miji/majiji kwa kutoa fursa za kuongeza kipato kwa madereva, usafiri wa uhakika, na nafuu kwa wakazi. Mwanza sasa ipo tayari kujiunga na ligi ya miji ya kisasa duniani na tunaanza kwa kusherekea na ujio wa Taxify”.
Furaha ya madereva humaanisha huduma nzuri na bora kwa abiria. Taxify inaamini katika maelewano mazuri na madereva wake, kuhakikisha kuwa wanapata kipato zaidi ya wanachopata kutoka kwa washindani huku ikiwapa aina mbalimbali za ulinzi na vipengele vinavyowasaidia kufanya kazi kwa njia inayofaa kwao. Pia Taxify inaamini katika utoaji wa huduma iliyotukuka kwa abiria wake, huku ikiwa na timu ya huduma kwa wateja ya hapa hapa nchini na chaguo la kulipa kwa fedha taslimu.
Taxify imekuwa ikifanya kazi katika jiji la Dar es Salaam tokea Desemba 2017 na tayari ina maelfu ya madereva wanaojipatia kipato kutokana na kutumia program yake. Programu hiyo inaruhusu madereva kutumia muda mwingi barabarani na muda mchache sana katika maegesho kusubiria wateja.
***
Kuhusu Taxify
Taxify ni miongoni mwa kampuni barani Ulaya inayoongoza katika utoaji wa huduma ya usafiri kwa njia ya mtandao, ikiunganisha mamilioni ya watumiaji usafiri na madereva ulimwenguni katika kurahisisha huduma ya usafiri, kwa haraka na ufanisi zaidi. Ufanisi wa Taxify na teknolojia ya biashara yake inawanufaisha wote madereva ambao wanalipa kamisheni ndogo sambamba na abiria ambao wanalipa nauli ya gharama nafuu.
Taxify ambayo iliasisiwa na Markus Villig ilizunduliwa mwaka 2013. Ni kampuni ya utoaji wa huduma kwa njia ya mtandao inayokuwa kwa kasi ulimwenguni ikijikita zaidi Ulaya na Afrika.
Nchini Tanzania, Taxify inafanya kazi jijini Dar es Salaam. Taxify ina wateja zaidi ya milioni 10 katika nchi 20 ulimwenguni. www.taxify.eu
Taxify ina wateja zaidi ya milioni 10 katika nchi zaidi ya 20 duniani kote. Programu ya Taxify inapatikana kwenye mifumo ya iOS na Android.
Kwa taarifa zaidi tembelea www.taxify.eu

MBUNGE RITTA KABATI ATOA SADAKA YA TENDE KWA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM MANISPAA YA IRINGA


 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiongea na viongozi wa misikiti yote ya manispaa ya Iringa wakati wa utoaji sadaka ya tende kwa waumini wa dini ya kiislamu wa manispaa ya Iringa kwa ajili ya kuadhimisha mfungo wa ramadhan kwa waislamu wa wote wa manispaa ya Iringa. 


 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amemshukuru mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa kutoa sadaka ya tunda la tende kwa waiislamu katika  kipindi hiki cha mfungo wa ramadhan.
 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akikabidhi tende alizokabidhiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa kutoa sadaka  kwa waiislamu katika  kipindi hiki cha mfungo wa ramadhan.
Mkuu wa walimu na msimamizi wa misikiti ya Dhinureyn Tanzania Abdul Salam Ahmad Ayub akimshukuru mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa sadaka aliyoitoa kwa waislam katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan.
Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) na viongozi wa misiki ya manispaa ya Iringa walipohudhulia zoezi la utoaji wa sadaka ya tende ilitolewa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ametoa sadaka ya tende kwa waumini wa dini ya kiislamu wa manispaa ya Iringa kwa ajili ya kuadhimisha mfungo wa ramadhan kwa waislamu wa wote wa manispaa ya Iringa

Akizungumza wakati wa kukabidhi sadaka hiyo katika msikiti wa Dhinureyn Gangilonga Kabati alisema kuwa kila mwaka amekuwa akifutulisha katika maeneo mbalimbali hivyo mwaka huu ameamua kununua tende na kugawa kwenye misikiti yote ya manispaa ya Iringa.

“Unajua mwaka huu tende ni tunda ambalo linahitajika katika kipindi hiki cha mfungo na kuna watu ambao hawana uwezo wa kununua tende hizi na ukiangalia mwaka huu tende zimepanda bei sana hivyo kwa kiasa ambacho nakipata nimeamua kutoa sadaka hii kwa waumini wa kiislam” alisema Kabati

Kabati aliwataka wananchi wengine kuendelea kumuabudu mwenyezi mungu pale ambapo tunapata nafasi ili kupunguza maovu ambayo tumekuwa tukiyatenda kwa kukusudia au bila kukusudia na kufanya hivyo basi mwenyezi mungu atatuongezea pale ambapo tumepunguza kwa ajili ya kumtumiaka mungu.

“Katika kipindi hiki nawaomba wazazi,walezi na viongozi wetu naomba tutoe elimu kwa vijana wetu kwa kuwapa elimu ya dini pamoja maadili ya nchi yetu kwa lengo la kuwajenga vijana wawe wanamcha mungu hasa kipindi hiki cha mfungo wa ramadhan” alisema Kabati

Kabati alisema kuwa ametoa sadaka ya tende tani mbili ambayo ipo katika halmashauri ya manispaa ya Iringa kwa ajili ya misikiti yote na vituo vya watoto yatima ambavyo vinawatoto wa kiislam ambao wanafunga katika kipindi hiki cha mfungo.

“Mimi nimeleta tani mbili ili kuongezea nguvu wafungaji wa kipindi hiki lakini kutoa sadaka kwa mwenyezi mungu katika kipindi ambacho waislamu wapo kwenye mfungo wa ramadhan nakuwasidia wale ambao hawana uwezo wa kununua tunda hili la tende” alisema Kabati

Kwa upande wake mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amemshukuru mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa kutoa sadaka ya tunda la tende kwa waiislamu katika  kipindi hiki cha mfungo wa ramadhan.

“Tunashukuru sana kwa sadaka hii ambayo umetusaidia kwa waislam wa manispaa ya Iringa kwa msaada wako ambao utasiadia kwa wale ambao wanamahitaji maalumu na mungu atakuongezea aple ulipopunguza na mungu akubariki” alisema Masenza

Masenza aliwaomba maimamu kuwagawia tende hizo waislam ambao hawana uwezo wa kununua tende tukani ili nao wapate hiki chakula cha kwanza pindi unapofungua na wale wenye uwezo wa kununua tende dukani basi waendelee kununua

Naye mkuu wa walimu na msimamizi wa misikiti ya Dhinureyn Tanzania Abdul Salam Ahmad Ayub alisema kuwa msaada aliotoa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati utawasaidia waislam waliofunga.

“Sadaka hii aliyoitua huyu mbunge Kabati umekuja wakati muafaka na umamanufaa makubwa sana kwa waislam kwa kuwa tumehimizwa kufuturu kwanza tende hivyo kwa muislam kula tende ni fadhila kubwa sana”alisema Ayub

Ayub alisema kuwa katika kipindi hiki cha mfungo waislam tunatakiwa kupeana vyakula ili kila mtu ambaye hana kitu aweze kupata chakula na ndio alivyofanya huyu mbunge Ritta Kabati kwa waislam wa manispaa ya Iringa.

“Zamani watu walikuwa wanatandika jamvi nje wakati wa kufutulu ili waweze kufutulu na waislam ambao hawana uwezo na ndio uzalendo wenyewe huo,hivyo tunamuombea mbunge huyu aendelee na moyo huo huo” alisema Ayub

CHAMA TAWALA DRC CHAMUANDALIA KABILA MAZINGIRA YA KUGOMBEA MUHULA WA TATU.

Chama tawala katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kimemuandalia Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo mazingira ya kugombea urais kwa muhula wa tatu, licha ya lalama na makelele kutoka vyama vya upinzani.
 Ingawaje Rais Kabila amekuwa akikwepa kujibu swali kuhusu iwapo atawania muhula wa tatu au la, lakini chama tawala cha People’s Party for Reconstruction and Democracy (PPRD) kimebandika mabango yenye picha za kiongozi wao huyo kuanzia mijini hadi vijijini,miezi miwili kabla ya uchaguzi wenyewe.
Aidha chama hicho tawala kimetengeneza fulana zenye picha za Kabila na kuzigawa kwa watu katika kila kona ya nchi, na haswa ngome za kisiasa za rais huyo. 
Wapinzani wanasema Kabila ambaye mwezi huu aliwapiga kalamu nyekundu baadhi ya majaji wa Mahakama ya Katiba na kuteua wengine wapya, hapaswi kugombea urais wa muhula wa tatu.
Hii ni katika hali ambayo, utafiti wa shirika la Congo Research Group CRG likishirikiana na Kituo cha Utafiri wa Maoni cha BERCI,  unaonyesha kuwa kwa kila raia kumi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wanane hawamungi mkono Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo.
Wananchi wakiandamana dhidi ya Kabila
Utafiti huo unaonesha kuwa, akthari ya Wakongomani wamechoshwa na uongozi wa miaka 17 wa Rais Kabila na wanataka kumuona akiachia ngazi.
Joseph Kabila alikataa kuachia madaraka baada ya kumalizika muhula wake wa utawala kikatiba mwaka 2016, na mpaka sasa hajajitokeza hadharani kusema iwapo atagombea au ataachia ngazi baada ya uchaguzi wa rais unaotazamiwa kufanyika Disemba 23 mwaka huu au la.

FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY WATOA SOMO KUELEKEA UCHAGUZI NCHINI

a
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga akitoa ufafanuzi mbele ya wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es salaam wakati akifungua  mkutano wa kujadili nafasi ya Asasi za kiraia katika chaguzi zijazo hapa nchini.

Asasi za kiraia nchini zimetakiwa kujitoa katika kuhakikisha wananchi wanashiriki kwa wingi katika chaguzi mbalimbali ikiwemo ya serikali za mitaa na wa serikali kuu wa mwaka 2020.

Hayo yamesemwa mapema leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi, wenye lengo la kujadili hali ilivyo kabla ya kufikia uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hapo mwakani.

Mzee Gallus Abeid kutoka Mwalimu Nyerere Foundation akichangia mjadala mapema leo jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Uchaguzi ulioandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Foundation for Civil Society.

Katika Mkutano uliowakutanisha wadau kutoka Asasi mbalimbali za Kiraia, Taasisi za elimu ya juu, vyama vya wafanyakazi, vyama vya dini mashirika yanayoshughulikia amani nchini  kujadili nafasi na wajibu wao kama azaki kuelekea chaguzi zijazo hapa nchini.
Bwana Kiwanga amesema kuwa ushiriki wa wananchi katika kupiga kura umekuwa ni mdogo sana kwani 2010 wamepiga asilimia 43 peke yake na kwa mwaka 2015 ni asilimia 67 ya wananchi wote wenye sifa za kupiga kura.

Baadhi ya washiriki kutoka asasi mbalimbali za kiraia wakifuatilia kwa umakini mkutano.

Ameeleza kuwa  hii inatokana na wananchi kutokuwa na imani na viongozi wanaochaguliwa kwani wanaamini hata usipopiga kura basi mgombea wa chama fulani atapita kwa njia yeyote ile, hivyo taasisi zinazohusika ikiwemo wizara ya tamisemi na NEC pamoja na ZEC kuboresha utendaji wao wa kazi ili kurejesha imani hiyo kwa wananchi.


Amesema  kuwa asasi za kiraia zina jukumu kubwa la kushirika katika mchakato kabla, kipindi chenyewe cha uchaguzi na baada ya uchaguzi kwa kuwapa hamasa wananchi lakini pia kuomba nafasi za uangalizi katika kipindi hicho.

Wageni waalikwa wakifuatilia mkutano kwa umakini.

Amesistiza uhalali wa kuwapata viongozi ambao ni matwakwa ya wananchi kwani hii inaweza kuleta kitu kizuri kwa kuwa atakuwa kapewa Baraka zote na wananchi na pia watashirikiana nae kwa hali na mali kwa kuwa wanajua ndio chaguo lao sahihi.
Kwa upande wake Mzee Gallus Abeid kutoka Mwalimu Nyerere Foundation amesisitiza uwepo wa amani katika kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi kwani amani ndio msingi wa mambo yote.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa uchaguzi ulioandaliwa na shirika la Foundation for Civil Society wakiwa katika picha ya pamoja mapema leo jijini Dar es salaam.

Amesema  kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa hivyo inapotokea watu wanamchagua mgombea Fulani alafu matokeo yanabadilishwa na kupewa mtu mwingine hii sio sawa na inaweza kutowesha amani ya nchi

Lakini pia hali ya mtu anatumia muda mwingi kwenye foleni ya kujiandikisha na mwisho wa siku anaenda kupiga kura anaambiwa jina lako halipo kwenye daftari hali hii inasababisha watu wengi kuacha kujiandikisha kupiga kura na kupoteza haki yao ya msingi.

Tuesday, May 29, 2018

MKANDARASI WA KITUO CHA AFYA GAIRO ATAKIWA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI


 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (aliyeshika tofali na mwiko) na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Rachel Nyangasi (wa kwanza kulia) wakishirikiana kujenga ukuta wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (aliyebeba tofali) kumsaidia fundi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe kujenga ukuta wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akikagua ujenzi kwa ajili ya kupanua eneo la kulaza, na sehemu ya kuhifadhia maiti wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akishiriki katika ujenzi wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (wa kwanza kushoto) wakati akikagua upanuzi wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Dennis Ngaromba (wa kwanza kulia) wakati akitoa maelezo juu ya upanuzi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakiangalia mchanganyo wa saruji na mchanga.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) akipima ukuta kuona kama wamefikia viwango vinavyotakiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Dennis Ngaromba (wa kwanza kulia) wakati akitoa maelezo juu ya ujenzi wa jengo ya kuhifadhi maiti.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakiwa mbele ya jengo jipya la kuhifadhi maiti.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakikagua kijengo kidogo kilichokuwa kikitumika miaka ya nyuma kuhifadhia maiti.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakiwa mbele ya jengo la zamani la kuhifadhi maiti.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameutaka uongozi wa wilaya ya Gairo unamsimamia mkandarasi na kuhakikisha upanuzi wa kituo cha afya na unakwisha kwa wakati.

Akizungumza na uongozi na mkandarasi wakati wa ziara yake mwishoni mwa wiki iliyopita ya kukagua maendeleo ya Wilaya ya Gairo, Mhe. Kebwe amesema kuwa hajaridhishwa na kasi wanayokwenda nayo katika upanuzi wa kituo cha afya unaofanyika hivi sasa licha ya kuwa fedha za kituo hizo zote zimeshatolewa.

"Ni nini kinakwamisha ujenzi kuisha wakati fedha mmeshapewa???? amemuuliza Mkandarasi na Uongozi unaosimamia jengo hilo ... nawaomba sana, hebu fanyeni haraka maana kuna baadhi ya huduma wananchi wanakwenda kuzipatia mbali," amesema.

Amesema kuwa ipo haja ya kila mtu kutimiza majukumu yake bila ya kusukumwa sukumwa maana hali ya sasa ni kazi tu.

Awali akitoa maelezo ya ujenzi, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Dennis Ngaromba amesema kuwa ujenzi huo umeshagharimu zaidi ya milioni 139 na baada ya kukamilika jumla ya wananchi wapatao 218,000 wataweza kupatiwa huduma huku vipimo vyote vikipatikana.

"Kituo hiki cha afya kitakuwa ni cha kisasa na kitakuwa na vipimo vyote huku huduma zote zikipatikana maana kimekaa pembezoni mwa barabara ya Gairo-Dodoma," amesema.

Upande wake Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe kwa kuweza kutembelea wilaya yao na kuhamasisha wananchi kuendelea kujitoa katika shughuli za maendeleo.

Mhe. Mchembe amewashukuru wananchi kwa kuendelea kujitolea katika shughuli za maendeleo ya wilaya yao na kuwaomba kuwa bega kwa bega kuwafichua wale wote wanaokwamisha shughuli za maendeleo.