ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 2, 2018

DALOT AKARIBIA KUFANYA VIPIMO MAN UNITED.


DIOGO Dalot anatarajiwa kufanya vipimo katika kikosi cha Manchester United wiki ijayo, baada ya klabu hiyo kukamilisha malipo yake kwa Porto.

Dalot ameendelea kupata matibabu ya goti wakati United ikiendelea kujadi-liana na Porto juu ya kumnasa kwa chini ya kiwango cha pauni milioni 17.4 (Sh bil 52.5) ambacho anatakiwa kuuzwa.

United inamtaka beki huyo wa kulia ili akampe changamoto Antonio Valencia, ambaye ana umri wa miaka 33 na mara nyingi amekuwa akihitaji matibabu ya goti.

Dalot aliyewahi kung’aa katika timu ya taifa ya Ureno ya vijana chini ya miaka 21, anaweza pia kucheza kama beki wa kushoto. Lakini aliingia kwenye timu kubwa ya taifa hilo Februari, mwaka huu.

Aliisaidia Ureno kubeba ubingwa wa Ulaya (Euro) 2016 kwa vijana chini ya miaka 17, akifunga mabao mawili katika mechi tano likiwemo bao moja kwenye fainali.

Wakati huohuo, United inataka kuachana na beki Matteo Darmian ambaye imepanga kumuuza kwa mabingwa wa Italia, Juventus, kwa dau la pauni milioni 11.5 (Sh bil 34.7).

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.