ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 27, 2024

DOZI MOJA INATOSHA KUFANIKISHA KUZUIA SARATANI SHINGO YA KIZAZI.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

NI maadhimisho ya ‘dozi ya chanjo ya HPV’, inayomkinga mtoto wa kike asipate ugonjwa wa saratani ya mlango wa shingo ya uzazi.

Chanjo hiyo ya HPV inawalenga watoto wenye umri kati ya miaka tisa na 14, ambayo Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, anasema kuwa dozi moja inatosha kumkinga msichana kupata ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi. 

Waziri Ummy anayaongea hayo kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya Dozi moja ya chanjo ya HPV kwa wasichana, akinena ni jukumu la wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto kupata chanjo hiyo. 

Ni hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Furahisha Wilayani Ilemela, Mwanza akiwa na ufafanuzi: “Wataalamu wetu ambao wanatoka kwenye Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). 

“Wametuhakikishia kuwa dozi moja ya chanjo ya HPV inatosha kumkinga msichana kupata saratani ya mlango wa kizazi.” 

Anasema awali dozi zilitolewa mbili, ya pili ikiwa ni miezi sita akipelekewa binti, hata hivyo wengi hawakurudi kumalizia. 

Lakini anaeleza mbadala uliopo ni kwamba, hivi sasa anasema wanatoa dozi moja, inayotosha kuwakinga wasichana dhidi ya maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi.  

Waziri anaeleza saratani inayoongoza kuwatesa Watanzania ni ‘Mlango wa Kizazi’ anayosema katika kila wagonjwa100, wako 23 wagonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi.  

Anaorodhesha saratani zinazofuatia kwa ukubwa ni inayohusu: Mfumo wa Chakula, asilimia 11; matiti asilimia 10.4; tezi dume asilimia 8.9. 

Pia, Waziri anatoa wito kwa wazazi na walezi nchini, kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo zote wanazopaswa, ili wanufaike na kinga dhidi ya maradhi yaliyotajwa, ikiwamo lengo kubwa la kuwakinga na magonjwa, yakiwamo haya ya saratani pamoja na kuwakinga na vifo vinavyoweza kuzuilika na chanjo.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi.

  

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Saidi Mtanda atahakikisha watoto wote wenye umri wa kuanzia miaka tisa hadi 14, wanapata chanjo hiyo ili kufikia malengo.  

“Kwa mwaka 2022/23 Mkoa wa Mwanza ulifanikiwa kuchanja watoto zaidi ya laki Mbili sawa na asilimia 107 kati ya walengwa waliotarajiwa kuchanjwa ni laki 191,440 wenye umri chini ya mwaka mmoja, tumefikia malengo na kuyavuka,” anasema. 

Mkazi wa Jiji la Mwanza Amina Said, anasema kutolewa kwa chanjo hiyo ni moja ya mapambano ya kumkinga mtoto wa kike asipate saratani ya mlango wa kizazi. 

Anasema elimu juu ya chanjo hiyo inatakiwa kutolewa mara kwa mara ili jamii iendelee kuelewa umuhimu wa chanjo hiyo. 

"Mimi nina mtoto wa kike ana umri wa miaka name,lakini sina  elimu yoyote, kuwa anapofikisha miaka tisa anatakiwa kupatiwa chanjo hiyo," anasema. 

Anaongeza kuwa, serikali inapambana kuwahakikishia wananchi wake wawe na afya njema, hivyo ana rai elimu iendelee kutolewa kwa jamii, ijue umuhimu wa chanjo. 

Aziza Jumanne, mkazi wa Mwanza anaitaja chanjo hiyo kuwa mkombozi kwa wasichana wenye sifa ya kupata chanjo hiyo, akiishauri jamii izingatie jinsi ya kuwasaidia watoto wa kike wasipate ugonjwa huo. 

"Kila mzazi ambaye ana mtoto wa kike aliye na sifa za kupata chanjo, awapeleke kupata chanjo hiyo," anasema, kuwa watoto wanapopatiwa chanjo, wananudhurika kwa maradhi hayo.

 Anthony Andrew, mkazi wa Maduka Tisa, jijini Mwanza anasema ni wakati wa wazazi na walezi kuachana na mila potofu dhidi ya kuwapo chanjo hizo na kinachotakiwa ni kuisaidia serikali, ili watoto wapate waelewe.

 Andrew anakumbusha chanjo inatolewa bure na inabaki  jukumu la walezi na wazazi kujitokeza na watoto wao waweze kupatiwa chanjo hiyo. 

"Tumekuwa tunasikia kutoka kwa wataalamu wetu wa afya, magonjwa sugu yanayo changia vifo kwa jamii. Katika magonjwa hayo, saratani nayo ipo," anasema, akiwa na ufafanuzi.

 Anaongeza kuwa, saratani zote zina changamoto zake, kama mtu atachelewa kupata matibabu kwa wakati anayonafasi kubwa ya kupoteza maisha.













Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza, wakiwa katika maadhimisho ya chanjo ya HPV, katika viwanja vya Furahisha.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza, wakiwa katika maadhimisho ya chanjo ya HPV, katika viwanja vya Furahisha.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza, wakiwa katika maadhimisho ya chanjo ya HPV, katika viwanja vya Furahisha.
Sehemu ya baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za Jiji la Mwanza, wakiwa katika maadhimisho ya chanjo ya HPV, katika viwanja vya Furahisha.
Sehemu ya waandishi wa habari wakichukuwa matukio na taarifa katika maadhimisho ya chanjo ya HPV,  viwanja vya Furahisha Mwanza.
Binti aliyetia fora katika uwasilishaji wa shairi lenye kutia hamasa kwa wazazi kushiriki vyema kuhakikisha watoto wanapatiwa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi, wakiwa katika Uzinduzi wa maadhimisho ya chanjo ya HPV, katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
Sehemu ya baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za Jiji la Mwanza, wakiwa katika maadhimisho ya chanjo ya HPV, katika viwanja vya Furahisha.
Sehemu ya baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za Jiji la Mwanza, wakiwa katika maadhimisho ya chanjo ya HPV, katika viwanja vya Furahisha.
Kutoka Bujora ni kundi la ngoma likinogesha shughuli katika maadhimisho ya chanjo ya HPV, viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
 

Wednesday, April 24, 2024

MSIFANYE KAMPENI KINYEMELA KABLA YA MUDA WAKE -KATIBU CCM KIBAHA MJI


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 


Katibu wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Issack Kalleiya amekemea vikali tabia ya baadhi ya wanachama kuanza kufanya kampeni za chini chini na kutangaza nia kwa ajili ya kuwania nafasi mbali mbali za uongozi kabla ya muda kitu ambacho ni kinyume kabisa na taratibu za chama.

Katibu huyo ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi kata ya kongowe yenye lengo la kuweza kuzungumza na wanachama wa CCM ikiwa pamoja na kuimarisha uhai wa chama kuanzia ngazi za matawi,mashina pamoja na Kata husika.

Kalleiya ambaye katika ziara yake aliambatana na viongozi mbali mbali wa chama alisema kuwa lengo kubwa ni kuweka misingi imara ya kukijenga chama kuanzia katika ngazi za chini hadi ngazi za juu.

Aliongeza kuwa anashangazwa kuona baadhi ya wanachama kwenda kinyume na taratibu zilizowekwa kwa kuanza kutangaza nia kinyemela ya kuwania katika nafasi mbali mbali za uongozi.
"Nipo katika ziara yangu yemye lengo la kuona namna ya kusimamia mwenendo mzima kwa wanachama ili waweze kuimarisha uhai mzuri kuanzia katika ngazi za matawi,mashina na ngazi nyingine,"

"Kitu kingine ambacho nakemea vikali ni hili suala la baadhi ya wanachama kuanza kufanya kampeni za chini chini za kutaka kuwania nafasi mbali mbali za chama kwa kweli hii sio sahii kwani muda wake ni bado,"alisisitiza Katibu Kalleiya.

Aliongeza katika chama cha mapinduzi kuna miongozo ambayo ipo wazi katika mambo ya uchaguzi hivyo ni lazima kila mwanachama anapaswa kuwaacha viongozi waliopo madarakani wamalize muda wao bila kuvunjiwa heshima.

Katibu huyo pia alliwahimiza wanachama wote wa ccm kuhakikisha kwamba wanajisajili kwa mfumo mpya wa njia ua kieletroniki ili waweze kutambulika kwa urahisi.

Alisema kwamba kwa sasa chama kinaendelea kuwahimiza wanachama wake kufanya uchaguzi mbali mbali ili kuweza kujaza nafasi nafasi ambazo bado zimeachwa wazi.
Katika aliongeza kuwa chama cha mapinduzi kikiimarisha kuanzia katika ngazi za chini kitaweza kuleta matokeo chanya na kuibuka na ushindi katika uchaguzi  wa serikali za 
 mitaa ambao unatarajiwa kufanyika mwaka huu pamoja na uchaguzi mkuu mwaka 2025.