Saturday, December 17, 2011
AFYA
Maonyesho ya ajira sekta ya Afya kwa halmashauri ya mkoa wa Mwanza na nyinginezo yamefanyika wilayani sengerema mkoani Mwanza. Lengo ni kuwatambulisha wanafunzi wa sekta ya Afya kuhusu nafasi za kazi zilizopo katika Halmashauri ya mkoa wa Mwanza ambapo maafisa ajira toka Halmashauri zote walikusanyika wilayani hapa na kuziainisha nafasi zilizopo kwenye wilaya zao. mfano Wataalam wa maabara, wauguzi, katibu afya na nyinginezo.
Katibu Tawala Msaidizi - Utawala na Utumishi Crecensia Joseph akitoa hotuba ya ufunguzi.
Field Zonal Cordinator wa Benjamin Mkapa HIV AIDS Foundation Remmy Moshi akitoa maelezo kuhusiana na kusudio la Taasisi hiyo kuziainisha nafasi za ajira sekta ya Afya.
Katibu wa Afya Wilaya ya Misungwi
Wadau hao wa Sekta ya Afya walipata fursa ya kuandika majina yao kwa wilaya walizotaka kufanya kazi pamoja na anuwani, mawasiliano ili pindi mchakato utakapo kamilika waitwe kwaajili ya kufanya kazi.
Katibu wa Afya Wilaya ya Geita Maganga H. Mwita akitoa maelezo na vivutio vilivyopo toka wilaya yake.
Ongezeko la ajira katika sekta ya afya inaonekana kukuwa toka 7,634 katika mwaka wa fedha 20007/2008 hadi 9391 kwa mwaka 2010/2011.
Hii inatokana na mkakati huu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamiii wa kupeleka moja kwa moja wahitimu kutoka vyuoni kwenda vituo vya kazi.
Toka wilayani Sengerema kuna nafasi nyingi za ajira kama vile Asst.Env.Health Officer ii(4), Asst. Medical Officer ii (3), Nursing Officer ii (1), Asst. Technologist ii (18), Clinical Asst (6), Health Secretary ii (1), Technologist ii (4), Medical Attendant (8), Nurse ii (16), Nutrition Officer ii (1), Pharmacist ii (1), Phsiotherapist ii (114), Technologist ii (1).
Katibu wa Ukerewe Ester Marick akitoa maelezo ya nafasi za ajira na vivutio vilivyopo katika halmashauri hiyo.
Vile vile Wizara inatekeleza mpango wa kukuza taaluma kwa njia ya masafa (Distance Learning); Tabibu Msaidizi kuwa Tabibu na Muuguzi kuwa Afisa Muuguzi Msaidizi.
Yote haya yanafanyika kama sehemu ya maboresho katika sekta ya Afya na ajira.
Thursday, December 15, 2011
MICHEZO
Wadau wa mwanza timu ya mpira wa kikapu mkoa wa mwanza (rocky city team) ipo katika mashindano ya Taifa cup jijini dar. Mpaka sasa timu hiyo imeshacheza mechi 2, mechi ya kwanza ilikuwa dhidi ya Zanzibar ambapo Zanzibar walishinda vikapu 56 vs Mwanza 55,game ya pili Mwanza iliigagadua Tanga kwa jumla ya vikapu 71 vs 40, Leo Mwanza imeshuka uwanjani kupepetana na timu ya mkoa wa Rukwa iwapo itashinda basi itakuwa ni tiketi kuingia hatua ya robo fainali.
Robo fainali itaendelea kesho sambamba na nusu fainali na fainali itakuwa jumamosi.Uongozi wa basketball wa mkoa wa Mwanza unatoa wito kwa wana mwanza wote popote walipo hasa waliopo jijini Dar wajitokeze kwa wingi kuipa support timu yao ya mkoa iwe kwa hali na mali ukizingatia inakabiliwa na ukata kwani wadhamini TBL kupitia Castle lite wametoa shilingi laki 9 tu kwa kila timu hivyo gharama zingine ni juu ya mkoa wenyewe.
Hima hima mwenye maji ya kunywa ayaa, chakula ayaa, nauli ayaa na kulala pia. Timu inaishi Topland hotel Magomeni Mapipa na viwanja vya mashindano ni Don Bosco Upanga na Leaders Club.
Ni chini ya coach Robert Mwita, Timu ya mkoa wa Mwanza inaundwa na wachezaji Bundala Charles, Enock Charles, Ahmed Said, Vincent Shinda, Francis Shilinde, Wilson Sajigwa Masanja, Adam Jegame, Juma Kissoky, Mahamed Ally Dibo, Amri Mohamed, Amon Diba Semberya, Chacha Mukolo Tubert na Kizito Sosho Bahati.
Thursday, December 15, 2011
ELIMU
Wakati wa kuadhimisha Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara Ubalozi wetu nchini Uingereza ukishirikiana na Chuo Kikuu cha mji Coventry wanapenda kuwatangazia wadau wote wa elimu kuwepo kwa Scholarship sita maalum za masomo kwa watanzania ambazo zimetolewa kutoka katika Chuo kikuu cha Coventry katika nyanja zifuatazo:
1. MSc Oil & Gas Management
Coventry Campus
Kuanzia Septemba 2012
2. MBA Oil & Gas Management
London Campus
Kuanzia April, July, Septemba 2012
3. MSc Finance & Investment
IAA Dar Campus
Kuanzia Septemba 2012
4. MBA Logistics
IAA Dar Campus
Kuanzia Septemba
5. MSc Finance & Investment
IAA Arusha Campus
Kuanzia Septemba 2012
6. MBA Logistics
IAA Arusha Campus
Kuanzia Septemba 2012
Jinsi ya kujiandikisha, tembelea tovuti ifuatayo:
http://www.coventry.ac.uk/tanzania2012scholarship
ZAIDI ya hayo Ubalozi wetu ukiwakilishwa na Balozi Mh Peter kallaghe, Chabaka Kilumanga na Allen Kuzilwa, ulipata fursa pekee ya kukutana na kumpongeza afisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ndg. Semu Mwakyanjala ambaye pia ni mwanafunzi wa shahada ya Pili( Masters Degree in Communication, culture & Media) katika chuo kikuu cha Coventry alieshinda tuzo ya kuandika insha kuelezea jinsi gani nchi ya Ujerumani itakavyokua mwaka 2051.
Aidha Mh. Balozi Kallaghe alimpongeza sana Afisa Semu kwa juhudi zake kwa kufanikiwa kushinda tuzo hii na kuiletea heshima Tanzania Ughaibuni na kuwahamisisha watanzania wote kusoma na kufanya kazi kwa bidii zaidi. Wakati akiongea na waandishi wa Habari afisa Semu alianza kwa kutoa shukrani kwa familia yake, wafanyakazi wenzake kutoka TCRA na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa kumwezesha kufikia hatua aliyopiga leo.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na ubalozi wetu hapa London 00 44 20 7569 1470
Tafadhalini watanzania wote chukueni hii nafasi mapema iwezekanavyo kwa wale wote mnaopenda kujiendeleza kimasomo.
Tuesday, December 13, 2011
HABARI
Tuesday, December 13, 2011
BANGO
Picha namba Moko'Picha namba Bee yenye kwesicheni'Hebu tunyetishe nani Kapatiwaaa!!
Tuesday, December 13, 2011
BANGO
Tuesday, December 13, 2011
HABARI
Zaidi ya watu 5,000 wanaaminika kuuawa katika maandamano ya nchini Syria, afisa wa ngazi za juu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa amesema.Pillay amewaambia wajumbe wa Baraza la Usalama kuwa watu 14,000 wanaaminika kukamatwa na wengine 12,400 wamekimbia hadi katika nchi jirani.
Takriban watu 20 waliuawa katika makabiliano ya siku ya Jumatatu. Licha ya fujo, uchaguzi ulifanyika, lakini idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura inasemekana kuwa ndogo.
Serikali inasema kuwa uchaguzi umekuwa huru zaidi kuliko miaka iliopita, lakini upinzani ulitoa wito wa kususia uchaguzi na kuanzisha mgomo.
Shirika la habari la serikali nchini Syria linasema watu wengi wamejitokeza katika vituo vya kupiga kura, Lakini katika ngome za upinzani wanaharakati wanasema hakuna dalili kama uchaguzi unafanyika, na hata pengine hakuna hata mmoja anayepiga kura, mwandishi wa BBC Jonathan Head aliye nchi jirani ya Uturuki anasema.
Navi Pillay anaelezea hali nchini Syria kama "isiyoweza kuvumiliwa" na kusema kuwa mateso dhidi ya binaadamu huenda yalifanyika.
Bi Pillay anasema makadirio yake ya mauaji ya watu zaidi ya 5,000 hayajumuishi maafisa wa usalama. Serikali ya Syria inasema kuwa zaidi ya maafisa 1,000 wa polisi na jeshi wameuawa.
Chanzo bbc swahili
Monday, December 12, 2011
BANGO
Waungwana leo ni BorzDEi ya mtangazaji wa Star Tv FATMA SHAMWETA kama mna namba yake mpigieni mumpongezezZ!! Au kama vipi tupa makomenti... Kwani siku yake muhimu maishani.... Blogu hii na wadau wake wa ukweli inakutakia kila la kheri katika harakati za maisha yako Inshahlah Mwenyezi Mungu akujazie kheri kwa kila jema ulipangalo.