ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 17, 2011

MAONYESHO YA AJIRA SEKTA YA AFYA KWA HALMASHAURI YA MKOA WA MWANZA

Maonyesho ya ajira sekta ya Afya kwa halmashauri ya mkoa wa Mwanza na nyinginezo yamefanyika wilayani sengerema mkoani Mwanza. Lengo ni kuwatambulisha wanafunzi wa sekta ya Afya kuhusu nafasi za kazi zilizopo katika Halmashauri ya mkoa wa Mwanza ambapo maafisa ajira toka Halmashauri zote walikusanyika wilayani hapa na kuziainisha nafasi zilizopo kwenye wilaya zao. mfano Wataalam wa maabara, wauguzi, katibu afya na nyinginezo.

Katibu Tawala Msaidizi - Utawala na Utumishi Crecensia Joseph akitoa hotuba ya ufunguzi.

Field Zonal Cordinator wa Benjamin Mkapa HIV AIDS Foundation Remmy Moshi akitoa maelezo kuhusiana na kusudio la Taasisi hiyo kuziainisha nafasi za ajira sekta ya Afya.

Katibu wa Afya Wilaya ya Misungwi
Wadau hao wa Sekta ya Afya walipata fursa ya kuandika majina yao kwa wilaya walizotaka kufanya kazi pamoja na anuwani, mawasiliano ili pindi mchakato utakapo kamilika waitwe kwaajili ya kufanya kazi.

Katibu wa Afya Wilaya ya Geita Maganga H. Mwita akitoa maelezo na vivutio vilivyopo toka wilaya yake.

Ongezeko la ajira katika sekta ya afya inaonekana kukuwa toka 7,634 katika mwaka wa fedha 20007/2008 hadi 9391 kwa mwaka 2010/2011.

Hii inatokana na mkakati huu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamiii wa kupeleka moja kwa moja wahitimu kutoka vyuoni kwenda vituo vya kazi.

Toka wilayani Sengerema kuna nafasi nyingi za ajira kama vile Asst.Env.Health Officer ii(4), Asst. Medical Officer ii (3), Nursing Officer ii (1), Asst. Technologist ii (18), Clinical Asst (6), Health Secretary ii (1), Technologist ii (4), Medical Attendant (8), Nurse ii (16), Nutrition Officer ii (1), Pharmacist ii (1), Phsiotherapist ii (114), Technologist ii (1).

Katibu wa Ukerewe Ester Marick akitoa maelezo ya nafasi za ajira na vivutio vilivyopo katika halmashauri hiyo.

Vile vile Wizara inatekeleza mpango wa kukuza taaluma kwa njia ya masafa (Distance Learning); Tabibu Msaidizi kuwa Tabibu na Muuguzi kuwa Afisa Muuguzi Msaidizi.

Yote haya yanafanyika kama sehemu ya maboresho katika sekta ya Afya na ajira.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Niliomba ajira mlipokuja pale Sengerema my email address is deomk07@yahoo.co.uk my name is Deogratias Mkemangwa A CLINICAL OFFICER graduated 2004.Niliomba Morogoro

    Regard

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.