Saturday, February 12, 2011
HABARI
Washiriki miss utalii Tanzania wakiwa katika daraja lililoko katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti jana.
Meneja mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti Paulo Ningelera akiwaonyesha washiriki miss utalii Ramani ya kutembelea Hifadhi.
Saturday, February 12, 2011
HABARI
Hosni Mubarak ameamua kujiuzulu urais wa Misri.HOSNI MUBARAK AJIUZULU
Katika tangazo kupitia televisheni ya taifa, makamu wa rais Omar Suleiman amesema Bw Mubarak amekabidhi madaraka kwa jeshi. Hatua hii imekuja baada ya maelfu ya watu kukusanyika mjini Cairo pamoja na miji mingine mikuu katika siku ya 18 ya maandamano ya kudai Bw Mubarak ajiuzulu.
Waandamanaji walipokea taarifa hizo kwa kushangilia, kupeperusha bendera, kukumbatiana na kupiga honi za magari. "Watu wameuangusha utawala," wamekuwa wakiimba.
MUBARAK NA OMAR SULEIMAN.
"Kwa jina na Mungu mwenye neema, mwenye rehema, raia, katika wakati huu mgumu, Misri inapopitia, Rais Hosni Mubarak ameamua kuachia madaraka kutoka ofisi ya rais ya jamhuri na ametoa jukumu la kuendesha nchi kwa baraza kuu la jeshi," amesema.
"Mungu awasaidie wote," amesema Omar Suleiman.
Bw Mubarak tayari ameondoka Cairo na yupo katika mji wa Sharm el-Sheikh, ambapo ana makazi mengine huko, maafisa wamesema.
Mjini Cairo, maelfu ya watu wamekusanyika nje ya Ikulu, katika eneo la wazi la Tahrir na katika kituo cha taifa cha televisheni. Waandamanaji hao walikuwa na hasira kufuatia hotuba ya Bw Mubarak siku ya Alhamisi. Alikuwa akitarajiwa kutangaza kujizulu, lakini hakufanya hivyo na badala yake kupunguza madaraka yake kwa makamu wa rais.
KWA HISANI YA BBC SWAHILI
Ni mambo ya tekinolojia tu! So huna haja ya kuhofia eti-"oh uzee", ajali za kuvunjia kiuno wala kujisumbua na matumizi ya mkwanja mrefu kwa manunuzi ya SUPER SHAFTI na VIAGRA.
Friday, February 11, 2011
HABARI
Rais wa Misri, Hosni Mubarak amesema atasalia madarakani na kukabidhi madaraka yote baada ya uchaguzi wa urais mwezi Septemba.RAIS MUBARAK AKIHUTUBIA KUPITIA TV.
Matamshi yake katika hotuba kupitia televisheni ya taifa, yamepishana na taarifa za awali kuwa alikuwa akijitayarisha kujiuzulu. Bw Mubarak amesema atakabidhi baadhi ya majukumu kwa makamu wa rais Omar Suleiman, lakini taarifa kamili ya jambo hili haifahamiki vyema.
Maelfu ya waandamanaji katika eneo la wazi la Tahriri wamepokea kwa hasira tangazo lake hilo. Walikuwa wakipiga kelele za "tumechoka na Mubarak", huku waandamanaji wengine 'wakipeperusha' viatu vyao kwa ghadhabu. Maelfu wameripotiwa kutembea kuelekea katika ikulu ya rais ambayo iko umbali mrefu.
WAANDAMANAJI TAHRIR.
Bw Mubarak alikwisha sema mapema kuwa hatogombea urais mwezi Septemba, na kusema atasalia kusimamia mchakato wa mabadiliko ya katiba.
"Natangaza nia yangu ya kuendelea na kuitetea katiba na kuwalinda wananchi na pia mabadiliko kwa yeyote atakayechaguliwa mwezi Septemba katika uchaguzi huru na wa wazi," amesema Mubarak. Akiwahutubia moja kwa moja waandamanaji "waliopo Tahrir na kwingineko" katika kile alichoita "hotuba kutoka moyoni mwake", bw Mubarak,82, amesema: "Sioni aibu kusikiliza vijana wa nchi yangu na kuchukua hatua."
Ameomba radhi kwa familia za waandamanaji waliokufa katika mapigano na majeshi ya usalama katika wiki za hivi karibuni, na kusema waliohusika na vifo hivyo watachukuliwa hatua.
MUBARAK ALIINGIA MADARAKANI BAADA YA ANWAR SADAT KUUAWA.
Bw Mubarak ameongeza kuwa sheria za hali ya dharura nchi humo zitaondolewa pale tu hali itakapokuwa sawa, na kusema atawapuuza "madikteta kutoka nje ya nchi". "Misri imepitia nyakati ngumu na hatuwezi kuruhusu hali hii kuendelea," amesema. "Hasara kwa uchumi wetu itasababisha hao vijana wanaotaka mabadiliko kuwa wa kwanza kuathirika."
OBAMA AMEKUTANA NA MAAFISA WA USALAMA.
Rais wa Marekani Barack Obama amekutana na maafisa wake wa usalama wa taifa katika ikulu ya Marekani, baada ya hotuba ya Rais Mubarak. Serikali ya Marekani katika siku za hivi karibuni, imezidisha wito wake kwa sauti za waandamanaji kusikilizwa.
Mapema, katibu mkuu wa chama kinachotawala cha Bw Mubarak - National Democratic Party - Hossam Badrawi alisema, jambo sahihi kwa rais kufanya ni kuondoka madarakani, na kuwa hakuwa akitarajia Bw Mubarak kuwa bado rais siku ya Ijumaa.
Wakati huohuo, jeshi la Misri limetangaza kuwa liko tayari "kulilinda taifa". Shirika la habari la Misri Mena, limeripoti kuwa baraza kuu la jeshi lipo katika hali ya "kulilinda taifa, na matakwa ya watu".
KWA HISANI YA BBC swahili.
*Kwa wanaotizama runinga hapa Bongo watakubaliana nami kwamba hawa jamaa wanaojulikana kama FUTUHI wa Rock City, Mwanza wanatisha! Jamaa walianza kwa tabu sana huku na kule wasieleweke! Tukiwaponda na 'kukomenti' kwa mabango ile mbaya! SIJUI NAMI NILIKUWA MMOJA WAPO? Ene weiz nitacheki mafaili yangu.
*Lakini mdogomdogo hatimaye WAKASOMEKA na swaga zao toka lugha za makabila ya asilia Afrika. Pamoja na kutuvunja mbavu ila pia wamekuwa wakituletea picha halisi ya matatizo tunayokumbana nayo kila siku hapa Bongoland. Sasa MAJAMAA ile Yanaanza kunoga na kushika ETI naskiaaaaaaaaaaAAA....
'WATU 7 MUHIMU WAMEPIGWA STOPU'
*KISA
ETI-Kushiriki show za nje bila kibali cha meneja wao!
*HATUA no.1
ETI-Hawaruhusiwi kuingia hata mjengoni kwa ofice!
*VIPI WIKI HII? (LEO ALHAMISI)
ETI-Timu mpyaaaaa kuonekana hewani (star tv)!
CHUNGUZA MJOMBA UTABAINI.
Thursday, February 10, 2011
MICHEZO
NDOTO za kocha Jan Poulsen kupata ushindi wa kwanza katika mechi ya kimataifa imetimia baada ya jana timu yake, Taifa Stars kuilaza Palestina kwa bao 1-0 la Mrisho Ngassa, dakika ya 62 kutokana na kazi nzuri ya Mohammed Banka aliyetokea akitokea benchi kipindi cha pili.
MSHAMBULIAJI wa stars Mrisho Ngasa (kulia), akiwania mpira na beki wa Palestina Samer Mahmoud Amin.
Ngassa alifunga bao hilo kwa kumchambua kipa Abdallah Alsidawi kutokana na mpira wa Banka, ambaye alikuwa ameingia uwanjani dakika tatu kabla ya bao hilo.
Stars walikaribia kupata bao la pili dakika ya 88, lakini Bonny alikosa umakini na kushindwa kutumia pasi ya Mrope ambaye alikuwa amewapiga chenga mabeki lukuki wa Palestina.
TAREHE 14 FEBRUARY YA KILA MWAKA NI SIKU YA WAPENDANAO DUNIANI TWAITA ‘VALENTINE’S DAY’. ASKWAMBIE MTU WATU WA MWANZA WANAKITU KIZURI KULIKO VYOTE DUNIANI KITAKACHO FANYIKA NDANI YA UKUMBI WA NYUMBANI HOTEL.
USIKU HUO UTAKAUKUWA NA RANGI TOFAUTI KABISAAA - KUTANA NA MICHEZO MBALIMBALI KWA WAPENDANAO ITAKAYO KUTUNUKISHA ZAWADI ZA KUPENDEZA.
BIBI NA BWANA WATAKAOPENDEZA YAANI BEST COUPLE KUTOKA NA BONGE LA ZAWADI TOKA FLORA SALON, MWANADADA ATAKAYE NG’ARA NA KUPENDEZA ILE MWAAAAA!.. ANAZAWADI YAKE.
ALBUM MBILI ZITAZINDULIWA UTABEMBELEZWA NA BARNABA…. NA KULIWAZWA NA AMINI … DISCO TAAAMU LA WAPENDANAO KUTOKA KWA MABINGWA WA BURUDANI NCHINI USPITWE NA UHONDO HUO! KWANI WATANGAZAJI WA LEO TENA WATAKUWA NDANI DINA MARIOUS, GEA HABIB, ZAMARADI WATATINGA KATIKATI YA SHEREHE WAKIWA NA WATU MASHUHURI USIOWATARAJIA.Amini.
VAZI MAALUM KWA SIKU HIYO WANAWAKE WATATUPIA RED, WANAUME WAKITINGA WHITE.
WATU 200 WA KWANZA KUPATA KINYWAJI CHA REDS, UA JEKUNDU NA COCACOLA - MLANGONI.
UTAJUMUIKA NASI KWA KIINGILIO CHA SH. 10,000 TU! NDANI YA UKUMBI WA NYUMBANI HOTEL (NSSF BUILDING) TRH 14/2/2011 VALANTINE’S DAY.
USIKU WA WAPENDANAO NI CHINI YA UDHAMINI WA REDS PREMIUM COLD, NYANZA BOTLING CO.LTD, VICTORIA ISTITUTE OF TOURISM &HOTEL MANAGEMENT, ZAI FASHION, WHITNEY FASHION, FLORA SALON, MARYAM MAGONGO SHOPING CENTRE, BEAUTY BEST SALON, CLOUDS FM NA CLOUDS TV. !!!!WAHI TIKETI YAKO SASA!!!!
Wednesday, February 09, 2011
AFYA
Save money and trips to the market with these tips and tricks from Rebecca DiLiberto’s Penny Saving Household Helper. You’ll be surprised how simple it is to keep food at its best.
1. Line the bottom of your refrigerator’s crisper drawer with paper towels. They’ll absorb the excess moisture that causes vegetables to rot.
2. To keep herbs tasting fresh for up to a month, store whole bunches, washed and sealed in plastic bags, in the freezer. When you need them, they’ll be easier to chop, and they’ll defrost the minute they hit a hot pan.
3. A bay leaf slipped into a container of flour, pasta, or rice will help repel bugs.
4. Stop cheese from drying out by spreading butter or margarine on the cut sides to seal in moisture. This is most effective with hard cheeses sealed in wax.
Plus: Browse our favorite cheese recipes and learn how cheese is made!
5. When radishes, celery, or carrots have lost their crunch, simply pop them in a bowl of iced water along with a slice of raw potato and watch the limp vegetables freshen up right before your eyes.
6. Avoid separating bananas until you plan to eat them – they spoil less quickly in a bunch.
7. Put rice in your saltshaker to stop the salt from hardening. The rice absorbs condensation that can cause clumps.
8. Stock up on butter when it’s on sale – you can store it in the freezer for up to six months. Pack the butter in an airtight container, so it doesn’t take on the flavor of whatever else you’re freezing.
9. In order to make cottage cheese or sour cream last longer, place the container upside down in the fridge. Inverting the tub creates a vacuum that inhibits the growth of bacteria that causes food to spoil.
10. Believe it or not, honey is the only nonperishable food substance, so don’t get rid of the stuff if it crystallizes or becomes cloudy. Microwave on medium heat, in 30-second increments, to make honey clear again.
Bonus: We narrow down America's best local honey.
11. Prevent extra cooked pasta from hardening by stashing it in a sealed plastic bag and refrigerating. When you’re ready to serve, throw the pasta in boiling water for a few seconds to heat and restore moisture.
12. Keeping brown sugar in the freezer will stop it from hardening. But if you already have hardened sugar on your shelf, soften it by sealing in a bag with a slice of bread – or by microwaving on high for 30 seconds.
13. If you only need a few drops of lemon juice, avoid cutting the lemon in half – it will dry out quickly. Instead, puncture the fruit with a metal skewer and squeeze out exactly what you require.
14. If you’re unsure of an egg’s freshness, see how it behaves in a cup of water: Fresh eggs sink; bad ones float.
Tuesday, February 08, 2011
HABARI
Taarifa Rasmi ya Serikali kwa Vyombo Vya Habari.
SERIKALI imeamua kuwa kuanzia sasa walimu nchini, kama ilivyo kwa madaktari, wataajiriwa na kupangiwa moja kwa moja vituo vya kazi bila kufanya usaili ama kucheleweshwa na michakato na taratibu nyingine za kirasimu, ili mradi wawe wameshinda mitihani yao.
Ili kutekeleza uamuzi huo wa Serikali, imeamuliwa kuwa walimu watapangiwa vituo vya kazi katika miezi ya mwisho ya mafunzo yao ili kuwawesha kuripoti moja kwa moja kwenye vituo vyao baada ya kumaliza masomo na mafunzo yao.
Uamuzi huo wa Serikali ulifikiwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika wiki iliyopita, Alhamisi, Februari 3, 2011, mjini Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Baraza limefikia uamuzi huo kwa kutilia maanani uhaba wa walimu, kama walivyo madaktari nchini na, kwa nia ya kupanua na kuboresha kiwango cha huduma elimu.
(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU WA BARAZA LA MAWAZIRI
07 FEBRUARI, 2011
Tuesday, February 08, 2011
BANGO
Award winning soul singer Maya Azucena and percussionist/rapper Okai,
join local star Mzungu Kichaa for a live jam!
WEDS FEB 9TH
@ Triniti
FREE OF CHARGE
9-Midnight
Featuring:
Mzungu Kichaa (TZ)
Maya Azucena (NYC)
Okai (NYC)
Mama C (Arusha)
Bongo Beat (TZ)
Mkufunzi wa Bendi ya Jeshi la Polisi, Damas Mpepo akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuhusu Mchango wa Majeshi Katika Kuthamini Ajira za Sanaa. Kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego, Afisa wa Bendi ya Polisi Bw. Mayalla na Mratibu wa Jukwaa hilo, Ruyembe C.Mulimba.(picha na Sufiani Michuzi)
Na Mwandishi Wetu
Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeombwa kuliingiza rasmi somo la Sanaa kwenye mitaala ya elimu kutoka ngazi ya awali ili kujenga vipaji vya vijana katika tasnia hii na baadaye kuweza kujiajiri.
Ombi hilo limetolewa Jumatatu ya wiki hii na wadau wa sanaa wakati wakichangia mada kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) iliyohusu Mchango wa Majeshi Katika Kukuza Ajira za Sanaa nchini iliyowasilishwa na Mkufunzi wa Bendi ya Polisi Damas Mpepo ambapo wengi walikunwa na jinsi majeshi yetu yanavyoenzi sanaa na kuwa mstari wa mbele kuiimarisha tasnia hii.
“Majeshi yetu yamekuwa yakifanya vizuri katika tasnia ya Sanaa kwa kuwa kuna elimu wanayoipata katika tasnia hii. Ni lazima Wizara ya Elimu iamke sasa na itambue kwamba tasnia ya sanaa ni kimbilio la vijana wengi kwa sasa hivyo lazima uwekwe utaratibu wa kujenga vipaji vya sanaa toka ngazi ya awali ili kukuza tasnia hii inayoajiri vijana wengi kwa sasa” alichangia mdau.
Hoja hii iliungwa mkono na Mkufunzi Mpepo wa Bendi ya Polisi ambapo aliweka wazi kwamba, wizara haina jinsi kwa sasa zaidi ya kuliingiza somo la sanaa kwenye mitaala ya elimu badala ya ilivyo sasa ambapo limekuwa halitahiniwi na vijana wengi mashuleni wamekuwa wanalikuta mitaani baada ya kumaliza shule.
“Sanaa inaajiri watu wengi sana, hata Jeshi la Polisi limeajiri wasanii karibu 500, tatizo lililopo sasa ni kwamba somo la Sanaa halifundishwi na hivyo ujuzi katika tasnia hii ni tatizo kubwa. Wizara ya Elimu lazima sasa ione haja ya kuliingiza somo la sanaa kwenye mitaala ya elimu toka ngazi ya awali na litahiniwe kwenye mitihani ya shule na taifa” alisisitiza Mpepo.
Kwa upande wake, Mratibu wa Jukwaa la Sanaa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mfuko na Uwezeshaji BASATA Ruyembe Mulimba alisema kwamba, hoja ya somo la sanaa kufundishwa toka ngazi ya awali ya elimu ilichukua muda mwingi kwenye Kikao cha Nane cha Sekta ya Utamaduni kilichomalizika hivi karibuni jijini Mwanza ambapo wadau walitoka na azimio la kushawishi somo hili kuanza kufundishwa na kutahiniwa kama masomo mengine.
“Kauli mbiu ya kikao cha nane cha sekta ya utamaduni ilikuwa ni Sanaa ni Ajira Tuithamini lakini wadau wengi walisikitishwa na somo la sanaa kutokufundishwa toka ngazi ya awali na walitaka wizara ya elimu kusikia kilio hicho kwani tasnia hii kwa sasa inaajiri vijana wengi sana wanaokadiliwa kufika milioni sita.
Katika kikao hicho cha Jukwaa la Sanaa, Jeshi la Polisi kupitia Bendi yake lilitoa taratibu za kuajiri wasanii na sifa zinazohitajika ambapo jumla ya wadau 157 waliohudhuria walipata wasaa wa kuelimishwa kazi mbalimbali za Bendi ya Jeshi la Polisi.
Monday, February 07, 2011
MWANZA
Ni kule Maryland nchini Marekani. Jamaa kavunja na kuingia ndani ya nyumba ili "kuchaji" simu yake. Simu hiyo haikuwa na chaji kwa sababu katika mtaa wake hakukuwa na umeme kutokana na barafu nyingi iliyokuwa imeanguka katika eneo hilo. Basi baada ya kuichomeka simu yake kwenye umeme ili ipate chaja, wenye nyumba wakarejea. Huyoo akakurupuka na kuiacha simu. Polisi wakaitwa na walipopiga baadhi ya namba zilizokuwa kwenye simu hiyo, jamaa akakamatwa kwa ulaini tu!!..
Baadaye imegundulika kwamba kumbe jamaa ni mwizi sugu ambaye ameshawaliza watu kibao katika maeneo hayo na polisi walipokwenda kupiga sachi nyumbani kwake waligundua vitu vingi tu vya wizi. Jamaa anashikiliwa umwelani na dhamana yake imeamriwa iwe 1,100,000.
Chelsea imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani na pia wachezaji wake wapya iliyowasajili, kwa kufungwa bao 1-0 na Liverpool.RAUL MEIRELES.
Fernando Torres wa Chelsea ambaye ndiye alikuwa gumzo kabla ya kuanza kwa mchezo, hakuweza kuwika na kupata goli dhidi ya timu yake ya zamani.
Timu zote zililikuwa zikicheza mchezo wa kutegeana kwa karibu muda wote.
Bao pekee na la ushindi kwa 'LIVA' lilipatikana katika dakika ya 69 baada ya krosi ya Steven Gerrard kumkuta Raul Meireles aliyepachika bao hilo kwa utamu na huku akisindikizwa na mlipuko wa shangwe utadhani LIVA walikuwa wakicheza dimba la HOME.
Chelsea inaendelea kusalia katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 44, sawa na Tottenham, huku Liverpool ikijikita katika nafasi ya sita ikiwa na pointi 38.
Monday, February 07, 2011
BANGO
Leo ni siku ya kuzaliwa mtangazaji mahiri hapa nchini Tanzania anaitwa Gerald Hando. Akifanya kazi ndani ya Clouds fm kwenye kipindi 'SUPER' cha Power Breakfast kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 3:00,
.............:hEpI bAZdEi bRO:
Monday, February 07, 2011
BANGO
Wimbo mpya kutoka kwa CRISS WAMARYA waja hewani. Wimbo waitwa "NAJUA" umefanyika kwa MJ Record,pia Video itakuwa soon tayari upate kuiona kwenye luninga yako.