ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 1, 2024

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KWA MBUNGE KOKA KWA KUFIWA NA BABA YAKE MZAZI



NA VICTOR MASANGU,MOSHI KILIMANJARO 


Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa  Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka kufuatia  kifo cha Baba yake Mzazi Mzee Francis Koka kilichotokea Moshi, Kilimanjaro.


Akitoa salamu za rambi rambi  kwa niaba ya Mhe Rais   Mwakilishi  wake Felister Mndeme alisema ameagizwa na Rais kwenda Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kuungana na familia ya Mbunge Koka  kwa ajili ya kuweza kutoa pole na kuungana katika mazishi.


"Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameniagiza kuja hapa Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kutoa pole kwa Mhe Koka na kwamba yupo pamoja na familia katika kipindi hiki cha maombolezo,"alisema Mdeme kwa niaba ya Rais.


Mdeme alisema kwamba Rais  Dkt. Samia alitamani kujumuika katika Msiba huo lakini ameshindwa kufika kutokana na kuwepo na majukumu mengine. 


Mwakilishi huyo  wa Rais alibainisha kwamba Mhe Rais anatambua Mchango wa Mzee Francis Koka (WW1 Veteran) na kwamba ni vyema kuenzi historia ya kipekee iliyoachwa na Marehemu ambaye ni Baba Mzazi wa Mhe Koka Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini.


Mazishi ya baba yake mzazi   na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka yamefanyika nyumbani kwake katika kijiji cha Mkolowony  Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali,mawaziri wabunge viongozi wa vyama vya siasa,madiwani,taasisi na mashirika  binafsi pamoja na wananchi.

Friday, May 31, 2024

MAELFU YA WANANCHI VIONGOZI,WA SERIKALI NA VYAMA WAJITOKEZA KUMUAGA BABA MZAZI WA MBUNGE KOKA

 

NA VICTOR MASANGU,KILIMANJARO

Maelfu ya  wananchi,viongozi, wa serikali,wakiwemo mawaziri  wakuu wa Wilaya wakuu wa Mikoa, Wabunge  viongozi wa  dini,madiwani na viongozi wa mashirika wamejitokeza kwa kwa ajili ya kumzika aliyekuwa Baba mzazi wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini mzee Francis Koka  katika nyumba yake ya milele.

Mazishi hayo ambayo yamefanyika nyumbani kwa marehemu  katika eneo la kijiji cha Mkolowonyi kata ya Mvienyi  mkoani Kilimanjaro  yameweza pia kuhudhuriwa  na mwakilishi wa Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan Felister Mdeme  pamoja na wawakilishi wa wabunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Akitoa salamu za rambi rambi  kwa niaba ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  mwakilishi  wake Felister Mdeme ametoa pole kwa familia ya Mbunge Koka  kutokana na kufiwa na baba yake.

"Nimeagizwa na Rais Samia kuja hapa Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kuweza kutoa pole kwa familia ya Mh.Mbunge Koka na amesema kwamba yupo pamoja nanyi  katika msiba huu,"alisema Mdeme kwa niaba ya Rais Samia.

Mwakilishi huyo  wa Rais alibainisha kwamba Rais Samia angependa kufika katika shughuli hiyo ya mazishi mkoani Kilimanjaro lakini ameshindwa kufika kutokana na ratiba kuingiliana lakini atayaenzi yote ambayo yameachwa na marehemu mzee Francis.


Akitoa salama za rambi rambi kwa niaba ya Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Ramadhani Mlao amempa pole Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa kuondokewa na baba yake mzazi.

Akizungumza kwa niaba ya wabunge wenzake wa Mkoa wa  Pwani Muharami Mkenge alibainisha kwamba wabunge wote wametoa  salamu za pole kwa  Mbunge Koka kwa kuondokewa na baba yake na kwamba wapo pamoja naye katika kipindi hiki kigumu.

Katika msiba huo pia Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka alitoa pole kwa familia ya Mhe.Mbunge na kuwahimiza kuwa wavumilivu hasa katika kipindi hiki cha majonzi.

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo Taifa  (CHADEMA) Freeman Mbowe alikuwepo katika msiba huo alisema kwamba wameguswa na msiba wa baba yake mzazi na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini na kwamba wapo pamoja katika kipindi hiki cha mahombolezo.

Kwa upande  wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ameshukuru viongozi mbali mbali wa vyama na serikali pamoja na wananchi kwa namna jinsi walivyojitoa kushiriki katika mazishi ya baba yake.

"Kwa kweli marehemu baba yangu amefariki akiwa na umri wa miaka 104 na alishawahi kupigana vita vya pili vya dunia,kwa hivyo kitu kikubwa inabidi tuyaenzi yale yote na ninawashukuru kwa dhati viongozi na wananchi wote kwa ujumla wake ambao wamefia katia msiba huu, "alifafanua Mhe.Koka.

Pia katika msiba huyo ulihudhuliwa na Wakuu wa mikoa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo ambao wametoa salamu zao za pole kwa familia ya Mbunge Koka.

Waziri wa ardhi Jerry Slaa naye alikuwa ni mmoja wa wahombolezaji alitoa salama za pole kwa niaba ya mawaziri wenzake ambao wengine walishimdwa kufika kutoka na bunge la bajeti.

Nao viongozi wa  wa dini ambao walioendesha Ibada ya misa  takatifu  aliwasisitizia wahombolezaji kuhakikisha kwamba kuwa na upendo wakati wa maisha yao na kijifunza na kwamba wayaishi yale yote mazuri ambayo ameyaacha wakati wa uhai wake.

Vingizi huyo hawakusita kumwelezea Mbunge Koka pamoja na marehemu baba yake kwa jinsi walivyokuwa mstari wa mbele katika kushirikiana bega kwa bega na wananchi katika mambo ya maendeleo.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mkolowonyi walisema kwamba familia ya Mbunge Koka imekuwa karibu na jamiii katika kusikiliza kero na changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Marehemu mzee Francis Koka alizaliwa Juni 6/1920 alifariki dunia mnamo Mei 22 mwaka huu wa  2024 akiwa na umri wa miaka 104 na amezikwa leo nyumbani kwake katika kijiji cha Mkolowonyi Kata ya Mvienyi mkoani Kilimanjaro.

SERIKALI YAELEZA NAMNA WALIMU WAPYA WATAKAVYOAJIRIWA

 



Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  Profesa  Adolf Mkenda akizungumza  wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya hali ya ufaulu na ujifunzaji wa wanafunzi ulioshirikisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo maafisa elimu mikoa, Halmashauri,Wakurugenzi na Taasisi uliofanyika Jijini Tanga 
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  Profesa  Adolf Mkenda akizungumza  wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya hali ya ufaulu na ujifunzaji wa wanafunzi ulioshirikisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo maafisa elimu mikoa, Halmashauri,Wakurugenzi na Taasisi uliofanyika Jijini Tanga 
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Caroline Nombo akiungumza  
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA) Dkt Said Mohamed akizungumza 
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akizungumza 
Meza kuu wakifuatilia 


Na Oscar Assenga, TANGA

SERIKALI imetangaza mkakati wa uboreshaji wa elimu nchini huku ikieleza walimu ambao wataajiriwa ni wale wataokuwa wamefanya mitihani yao na kufaulu vizuri tofauti na ilivyokuwa awali ambapo wizara ilikuwa ikijaza nafasi zilizokuwa zikihitajika bila kupitia mchakato huo .

Mkakati huo wa serikali umetangazwa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  Profesa  Adolf Mkenda aliyasema hayo leo Jijini Tanga wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya hali ya ufaulu na ujifunzaji wa wanafunzi ulioshirikisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo maafisa elimu mikoa, Halmashauri,Wakurugenzi na Taasisi

Alisema kwamba wanaoona jambo hilo sio jema kwao lakini wajiulize kwanini madaktari wanapomaliza Shahada ya kwanza wanalazimika kufanya mitihani ndio wanafanya kazi hivyo suala hilo linapelekwa kwa walimu ili kuweza kupata walimu bora.

Waziri Profesa Mkenda alisema kwamba wanaamini kigezo hicho ndio ambacho kitalivusha Taifa na watahakikisha wanachukua walimu waliobora zaidi na watakaofanya mitihani na kufaulu vizuri.

“Kama tunataka tuboresha elimu lazima twende kwa ujasiri tunapojaribu kuajiri walimu tujiulize tunapigania mwanao apata mwalimu bora sasa tutakapo ajiriw lazima wafanye mtihani na watakaofeli hawatapata nafasi”Alisema

Alisema lakini walimu waliopo watalindwa mpaka watakapostaafu na tutaendelea kuwajengea uwezo kwani Rais anatenga fedha nyingi kwenye elimu halafu tujitenge, haiwezekani lazima tathimini tunayoifanya lazima iendelee na hatua nzuri za baraza hatufurahii kufutia mitihani watahaniwa na waliojaribu kuiba mitihani”Alisema .

Aidha alisema kwa sasa wapo kwenye mchakato wa Sheria mpya ambayo itawabana watu watakaobainika kuiba mitihani watakamatwa kushtakiwa kwa kesi za uhujumu uchumi na kwenye hilo niwashukuru Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kwa kufanya kazi nzuri wanayoifanya.

“Katika jambo hilo tuzidi kuwa makini tusijikuta tukazubaa tukaanguka Necta msilegeze kamba nendeni kuhakikisha mnalisimamia na takwimu ni muhimu zitatueleza vizuri tunakwendaje na katika hilo tunataka kuimarisha takwimu za elimu Tanzania na kazi hii imeanza na timu ipo kazini”Alisema Waziri Profesa Mkenda

Awali akizungumza Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Caroline Nombo alilipongeza Baraza la Taifa Mitihani (Necta) kwa taarifa yao ya uwasilishaji wa Taarifa ya Tathimini ya ujifunzaji kwa wanafunzi wa kidato cha pili.

Alisema kwamba taarifa iliyowasilishwa inatoa picha halisi kuhusu na ufundishaji na ujifunzaji kwa shule za Sekondari na msingi nchini na mapendekezoo yaliyotolewa yanaonyesha dira ya nini cha kufanya ili kuhakikisha ufundishaji na ujifunzaji na tathimini katika ngazi ya shule unaimarika.

Alisema Wizara hiyo itaendelea kushirikiana bega kwa bega na wadau wote wa elimu na baraza la mitihani kuhakikisha masuala yote ya ufundishaji na tahimini yanaimarishwa kwa lengo la kukuza umahiri wa wanafunzi katika masomo hayo.

“Vile Wizara kupitia Baraza la mitihani tutaendelea kuhakikisha kuwa tathimini ya ujifunzaji wa wanafunzi wa kidato cha pili awamu ya pili ya mwaka 2025 itafanyika kwa ufanisi mkubwa”Alisema

Naye kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA) Dkt Said Mohamed alisema suala la kufanya tathimini ni muhimu ili kuboresha kiwango cha elimu na wamekuwa wakifanya tathmini na mitihani na kueleza tahimini hiyo katika maeneo mbalimbali ni kutaka kujua maendeleo ya wanafunzi wamesoma na wanataka kufika wapi.

Alisema wamesema wameanza kufanya tathimini na masomo manne ambayo yameyafanya wakianzia na somo la kwanza ni Hisabati,Sayansi huku akieleza kwamba katika somo hilo katika mtihani wa darasa la saba mwaka huu utakuwa hauna maswali ya kuchagua

Aidha alisema pia alisema hali ya ufauli nchini ukiangalia takwimu upimaji darasa la nne kwa miaka 10 uliopo ufaulu wa jumla umekuwa juu ya asilimia 80 itapanda kidogo na kushuka,miaka 10 hiyo utaona namna ya watahiniwa imekuwa ikiongezeka .

“Mfano mwaka 2015 darasa la nne laki tisa sasa kwenye usajili wanafikia mpaka 1,800,000 na ufaulu wameendelea kubakia 80 asilimia na namba ya watahiniwa imeongezeka mwaka hadi mwaka”Alisema

Katibu huyo alisema kwa upande wa Daraja la saba ulikuwa ni asilimia 67 mwaka 2015 na umeendelea kupanda na kufikia asilimia 80 mwaka 2023 kimahesabu huo ni ufaulu unaoafanana na bado wameendelea kufika asilimia 80 huku akieleza kwa upande wa Sekondari kidato cha pili ufaulu 2015 mpaka 2023 umekuwa ukiongezeka kutoka asilimia 67 2015 mpaka kufikia asilimia 89 mwaka jana.


DMI YAJIVUNIA KUTOA WATAALAMU WENYE UWEZO MKUBWA

 

Na Oscar Assenga,Tanga

CHUO cha Baharicha Jijini  Dar es Salaam(DMI) kimeshiriki maonyesho ya Elimu,Ujuzi na Ubunifu Jijini Tanga huku wakijivunia kutoa wataalamu wenye uwezo mkubwa wa kusanifu na kuzikarabati meli kupitia Temesa na hivyo kuondoa uhaba uliokuwepo awali nchini .

Akizungumza leo na waandishi wa habari katika Banda lao lililopo eneo la Shule ya Sekondari Popatlaly kunakofanyika maadhimisho ya elimu,ujuzi na ubunifu Captain Mohamed Kauli alisema wameshirika kwa lengo la kueleza wanachokifanya ikiwemo ufanisi wa meli,usafirisha majini,utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi baharini,usanifu ini na ujenzi wa meli na ubaharia.

Alisema awali chuo hicho kilikuwa kinazalisha mabaharia wakati kilipoanzishwa lakini ili kukabiliana na ombwe la ukosefu wa ajira kutokana na vijana wengi kumaliza vyuo na kukosa ajira na wahitimu haoo wanafaida kubwa mbili wanapohitimu chuo kupata ajiri nchini kwenye sekta ya usafirishaji majini na nje ya nchi kwenye meli.

“Kwa kweli tumekuwa tukizalisha idadi kubwa ya mabaharini wanaofanya kazi nje na ndani ya nchi kuna gepu kwenye utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi baharini lakini pia gepu la upatikanaji wa meli awali zimekuwa zikiagizwa kutoka nje kwa gharama kubwa”Alisema

Alisema lakini sasa Serikali imetengeza wataalamu wanaotoka kwenye chuo hicho ambao wanajenga meli,kuzisanifu ,kuzikarabati kwenye eneo hilo serikali kupitia Temesa wanajenga na kukabarati meli hizo hapa hapa nchini.

Awali akizungumza mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho,Masaka Julias alisema kwamba mafunzo ambayo wanayapata kwenye yamewawezesha kubuni vitu mbalimbali a hivyo kuwawezesha wanapomaliza kuweza kujiajiri kupitia ujuzi walioupata.

Alisema kwamba kwa sasa kupitia mafunzo hayo unawasaidia kutengeneza vitu mbalimbali vya ubunifu huku akieleza wamebuni wazo la kutengeneza mashine ya kutengeneza chilsource na ya kufunga vifuniko kwenye chupa ambayo inasahisisha.

Mwisho.

Thursday, May 30, 2024

JESHI LA POLISI LATOA UFAFANUZI TUHUMA ZA TRAFIKI WAKE KUDAIWA KUCHEPUSHA FEDHA

 

Jeshi la Polisi lingependa kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizoandikwa na kusambazwa kupitia vyombo vya habari zikisema "Wachepusha mfumo wa malipo".

Taarifa hiyo imeenda mbali zaidi ikidai na kutaka kuaminisha umma kuwa askari wa Usalama barabarani wameingilia mfumo wa malipo ya fedha za serikali POS (Point of Sale) na kuchepusha fedha zilizotakiwa kuingia kwenye mfuko mkuu wa serikali. Kilichopo na kilichosahihi ni kwamba Jeshi la Polisi mbali na kuwa na mpango kazi na mikakati ya kutekeleza majukumu yake, hufanya usimamizi na ukaguzi wa namna Askari wanavyotekeleza majukumu yao ili kubaini ufanisi au ukiukwaji wowote ule. Katika ukaguzi uliofanyika hivi karibuni ilibainika baadhi ya Askari walitumia mashine za kupima mwendokasi (,speed radar) kinyume na maelekezo ya Jeshi la Polisi. Baada ya kubainika walichukuliwa hatua za kinidhamu kwa kushtakiwa ambapo nane walishafukuzwa kazi na kufutwa Jeshini na wengine kesi zao zipo katika hatua za mwisho. Hivyo mashine zilizotumiwa kinyume cha utaratibu kwa utashi na kwa manufaa binafsi ya hao askari ni za kupima mwendokasi na si zile zinazotumika kwa ajili ya malipo ya serikali (POS) kwani kuingilia mfumo huo si rahisi kama inavyoelezwa. Mashine aina ya (POS) zinazotumika kwa malipo ya faini za barabarani hadi sasa uchunguzi haujabaini kwamba mfumo wa mashine hizo umeingiliwa na fedha kuchepushwa kama ilivyodaiwa. Jeshi la Polisi linaendelea kusisitiza kwa baadhi ya Waandishi wa Habari wanapoambiwa wasubiri ufuatiliaji unafanyika na taarifa sahihi itatolewa wawe na uelewa na subira kwani wasipofanya hivyo ipo hatari ya kutoa taarifa zenye kuleta taharuki kwa umma bila sababu yeyote ile. Imetolewa na: David A. Misime - DCP Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi Dodoma, Tanzania

Wednesday, May 29, 2024

'HABARI MBOVU MTANDAONI' ATHARI ZAKE NI ZAIDI YA AJALI BARABARANI AU MADHARA YA DAKTARI FEKI - TCRA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA DKT. JABIRI BAKARI AMEWASISITIZA WAANDISHI WA HABARI NA WATOA HUDUMA ZA UTANGAZAJI KUZINGATIA MAADILI, KANUNI NA SHERIA ZA KUTOA HUDUMA KWANI SEKTA HIYO INA MCHANGO MKUBWA KATIKA KUJENGA JAMII BORA NA KULETA MAENDELEO YA JAMII NA TAIFA. DKT. BAKARI AMESEMA HAYO KATIKA WARSHA KWA WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA MWANZA ILIYOANDALIWA NA TCRA LEO TAREHE 29 MEI, 2024 ILI KUWAJENGEA UWEZO NA KUWAKUMBUSHA KANUNI ZA UTANGAZAJI NA MAUDHUI MTANDAONI, KUKUZA UBUNIFU NA KUWAPA FURSA YA MAHALA PA KUANZIA KUFANYA KAZI, VIJANA WASIO NA AJIRA RASMI HAPA NCHINI.

ASILIMIA 90 YA WANAFUNZI WAPO KWENYE HATARI KUBWA YA KUGONGWA BARABARANI

 





Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Dalmia Mikaya akikata utepe kushirikia uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa shule za Msingi Azimio na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini,kushoto ni Kaimu Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga (RTO) Rajab Mhumbi akifuatiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo na kulia ni Mwakilishi wa Balozi wa Uswis nchini Rashid Mbaramula


Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Dalmia Mikaya (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo(Kulia) wakifungua kitambaa ikiwa ni uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini
Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Dalmia Mikaya kulia akiwa amemshika mkono mwanafunzi wa shule ya Msingi Azimio akiashiria uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini,kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo kulia akisisitiza jambo kwa Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Dalmia Mikaya na viongozi wengine wa Halmashauri ya Jiji la Tanga uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini
Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Dalmia Mikaya akizungumza mara baada ya  kuzindua mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini
 Mwakilishi wa Balozi wa Uswis nchini Rashid Mbaramula akizungumza wakati wa wa uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini

Naibu Meya wa Jiji la Tanga Rehema Mhina akizungumza wakati wa wa uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini
 Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Msingi Makorora Jijini Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini


Na Oscar Assenga, Tanga

ASILIMIA zaidi ya 90 ya wanafunzi katika shule za Msingi Makorora na Azimio jijini Tanga wapo kwenye hatari kubwa ya kugongwa na pikipiki,magari na vyombo vyengine vya moto.

Hatua hiyo imelilazimu Shirika la Amend Tanzania kutekeleza mradi wa uwekeji wa miundombinu salama ya barabara katika shule hizo ili kuwaepusha na ajali wanazoweza kukumbana nazo.

Akizungumza leo katika uzinduzi wa mradi wa miundombinu salama ya barabaraani katika Shule ya Msingi Makorora na Azimio jijini Tanga, Meneja Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Saimon Kalolo wakati wa uzinduzi wa Miundombinu salama ya barabarani katika shule za Msingi Makorora na Azimio Jijini Tanga .

Alisema wameamua kutekeleza mradi huo kunatokana na wanafunzi hao kutembea kwenda na kurudi shuleni kila siku hivyo kuwaweka katika hatari kubwa ya kugongwa na pikipiki, magari na vyombo vingine vya moto.

“Takribani wanafunzi wasiopungua 8 katika shule hizi mbili wamejeruhiwa katika ajali za barabarani katika muda wa miezi 12 iliyopita zote zikihusisha pikipiki”Alisema

Alisema baada ya kushauriana na wadau wa shule hizo wakiwemo wanafunzi na walimu, wanajamii, viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa, Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) na Jeshi la Polisi Amend kupitia msaada kutoka kwa Ubalozi wa Uswisi na washirika wake wa serikali.

Alisema baada ya kushauriana wameweka miundombinu salama kwa lengo la kuzuia ajali za barabarani ikiwemo njia za waenda kwa miguu, matuta, vivuko vya pundamilia, alama za barabarani, na elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wote.

“Tumezindua miundombinu mipya ya kuokoa maisha ya watembea kwa miguu hasa watoto katika Shule za Msingi Makorora na Azimio”Alisema

Aliongeza kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), watoto wanaotembea kwa miguu ni miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari kubwa ya kupata majeraha ya barabarani nchini Tanzania.

“Tofauti na watoto katika nchi zilizoendelea wengi wa watoto wa shule katika maeneo ya mijini mkoani Tanga, na Tanzania kwa ujumla, wanatembea kwenda shule bila kusindikizwa na mtu mzima”Alisema

Alisema pia kwa Bara la Afrika watoto wako katika hatari kubwa ya kupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani ikilinganishwa na eneo lingine lolote duniani.

“Kwa bahati nzuri njia za kuzuia ajali hizi zinaeleweka vizuri ikiwa ni pamoja na kuwaepusha watoto na msongamano wa magari na kupunguza mwendo kasi wa magari katika maeneo ambayo watoto wanavuka barabara”Alisema

“Mradi huu unaungwa mkono na Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania na una bajeti ya shilingi za Kitanzania 424,983,396 (takriban Faranga za Uswisi 150,000)”Alisema

Aliongeza mradi huo ulianza Septemba mwaka 2023 ambapo shughuli nyingine za mradi zimejumuisha mafunzo ya waendesha pikipiki (bodaboda) 300 ndani ya Jiji la Tanga, waendesha pikipiki 253 mkoani Dodoma ikiwemo kampeni ya uhamasishaji kuhusu masuala ya usalama wa pikipiki, na kuanzishwa kwa 'Kanuni za Maadili' kwa waendesha pikipiki 200 zaidi watapewa mafunzo jijini Tanga ifikapo Juni 2024.”

MRAMBA KULINDIMA NA MICHUANO YA MBIO ZA SAMIA ONE MARATHON PWANI

 


NA VICTOR MASANGU, PWANI

Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani ndugu David Mramba katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya michezo anatarajia kuanzisha mashindano maalumu ya mbio za miguu zitakazojulikana  kwa jina la Samia One Marathon ambazo zitazishirikisha taasisi mbalimbali zinazofanya shughuli zake ndani ya Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake  kuhusiana na maandalizi hayo Mwenezi alisema kwamba lengo kubwa la kuanzisha mashindano hayo ni kwa ajili ya kuweza kukuza mchezo huo wa riadha, kubadilishana mawazo na wadau mbali mbali  wa Mkoa wa Pwani ili kuweza kuimarisha mahusiano  baina ya chama cha mapinduzi (CCM)  pamoja na  wadau  na taasisi ikiwa sambamba  na kujenga afya zao.

Mramba alisema kwamba katika mashindano  hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika Juni mwaka  2024  yataweza kuwakutanisha wadau mbali mbali wa michezo zikiwemo taasisi  za kiserikali pamoja na taasisi nyigine ambazo sio za kiserikali pamoja na vyamba vingine vya michezo ili kuweza kukutana kwa pamoja na kufanya mambo mbali mbali ikiwemo kukimbia na kubadilishana mawazo.

"Kwanza kabisa nipende kutoka shukrani zangu za kipekee kwa taasisi zisizokuwa za kiserikali katika Mkoa wa Pwani kwani waliweza kunishika mkono na kunipasapoti kubwa hivi karibuni pindi nilipoandaa kikao changu maalumu ambacho kiliweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa na kwamba ninawaomba tushirikiane kwa pamoja  siku ya tukio kubwa la mbio hizo ambalo litakuwa la kihistoria,"alisema Mramba.

Kadhalika Mramba alifafanua kwamba  ana imani kwamba kupitia mashindano hayo ya mbio hizo za Samia One Marathon zitaweza kuleta  matokeo  chanya kwani zitatoa fursa ya wadau  mbali mbali pamoja na taasisi hizo kuonyeha  uwezo na vipaji vyao walivyonavyo katika sekta ya mchezo  huo wa Riadha.

Mwenezi Mramba alibainisha kwamba katika michuano hiyo taasisi hizo na wadau watapa fursa ya kuweza  kukimbia  mbio za kuanzia kilometa zipatazo tano,kumi,hadi kilometa 21 ambapo washindi wote watazawadiwa  zawadi  mbali mbali  kwa ajili  ya kutambua mchango wao katika kufanya vizuri.

Katika hatua nyingine Mwenezi huyo alisema kwamba fomu kwa ajili ya ushiriki wa mashindano hayo zitaanza kutolewa mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu  na kwamba zitapatikana katika ofisi za mwenezi wa CCM  Mkoa wa Pwani na kuwahimiza washiriki wote wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu hizo.

Katika hatua nyingine Mwenezi huyo alitoa wito kwa wadau michezo, wananchi,taasisi mbali mbali za Mkoa wa Pwani kumpa sapoti ya kutosha kwa lengo la kuweza kufanikisha michuano hiyo ya Samia One Marathon ambayo ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa vitendo katika kukuza  sekta ya michezo hususan mchezo wa Riadha.
                                               MWISHO 

Tuesday, May 28, 2024

"RAIS SAMIA YUKO TAYARI KWA KATIBA MPYA LAKINI NASHANGAZWA NA WASAIDIZI WAKE" - WAKILI KIBAMBA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Mjadala kuhusu madai ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umepata msukumo mpya baada ya viongozi wa asasi za kiraia, wanafunzi kutoka vyuo vikuu na wanaharakati kuungana na wadau wa sekta mbalimbali jijini Mwanza kupaza sauti. Mada kuu iliyowasilishwa katika mdahalo huo wa wazi wa siku moja ulofanyika jijini Mwanza ulikuwa ulikuwa umeegemea kwenye kichwa cha habari cha Mjadala wa Wazi Mchakato wa Upatikanaji wa Katiba Mpya. Kutoka Jukwaa la Katiba Wakili Deus Kibamba anasema Rais Samia Suluhu Hassan katika matukio mbalimbali amewahi kutamka waziwazi kwamba yuko tayari kwa mabadiliko ya Katiba lakini wakili Kibamba anashindwa kuwaelewa wasaidizi wake. Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) Ananelia Nkya amezungumza namna jukwaa lake lilivyo jipanga tayari kwa mchakato huo saa yoyote.

Monday, May 27, 2024

MEI 28 HADI TAREHE 1 JUNI 2024 NI WIKI YA MAZIWA KITAIFA MWANZA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Akizungumza leo hii Tarehe 27 MEI 2024 jijini hapa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amewaalika wananchi wa Kanda ya Ziwa, kujitokeza kwa wingi siku ya ufunguzi wa maadhimisho hayo kitaifa katika viwanja vya Furahisha, Kirumba jijini Mwanza, kwaajili ya kujipatia elimu kuanzia umuhimu wa unywaji maziwa, bidhaa zinazozalishwa na maziwa hadi mbinu bora za ufugaji wenye tija. Bodi ya Maziwa Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na wadau mbalimbali wa maziwa kila mwaka imekuwa ikiadhimisha Wiki ya Maziwa Kitaifa ambayo huwa inafanyika kuanzia mwishoni mwa mwezi Mei hadi mwanzoni mwa mwezi Juni na lengo ni kuwataka wadau mbalimbali nchini kuchangamkia fursa ya kufanya uwekezaji katika sekta ya maziwa kwani uzalishaji ni mdogo ukilinganisha na uhitaji. Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa yakiwa na dhana ya kuhamasisha unywaji wa Maziwa yaliyosindikwa na kuboresha soko la maziwa, dhana hiyo imekuwa ikibadilika na maadhimisho hayo kwa sasa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita yanalenga kuboresha wadau wote walioko kwenye mnyororo wa thamani (Value Chain) kuanzia mfugaji mpaka mlaji. Kuelekea wiki maadhimisho haya malengo makuu ni Kuelimisha wananchi na umma matumizi ya maziwa kama chakula bora kwa watu wa rika zote na faida za maziwa katika kujenga afya ya binadamu. Kuwaelimisha wadau kuongeza ubora wa bidhaa za maziwa zinazotengenezwa nchini ,kuwaelimisha wadau umuhimu wa kujiunga na vyama vya Ushirika.

VIDEO:- MAKONDA KUENDELEA KUPIGA SPANA WATUMISHI WAZEMBE NA WALA RUSHWA ASISITIZA KUTOBABAISHWA NA MITANDAO

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli ikiwa ni muendelezo wa ziara yake kutembelea wilaya zote za mkoa wa Arusha aliyoipa jina la SIKU 6 ZA MOTO. Kauli hiyo ya Makonda inakuja kufuatia baadhi ya watu kunukuliwa na vyombo vya habari wakimtaja kama mdhalilishaji wa watumishi wa Umma ndani ya Mkoa wa Arusha, suala ambalo amelitaja kutombabaisha ama kumpunguzia kasi katika kusimamia watendaji wavivu na wazembe wanaoshindwa kutimiza majukumu yao katika kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Arusha.

RC MAKONDA KUENDELEA KUWAPIGA SPANA WATUMISHI WAZEMBE NA WALA RUSHWA, ASISITIZA KUTOBABAISHWA NA MANENO YA MITANDAONI

 


> Asema alidhalilishwa Rais Samia na hakuna kauli yoyote iliyotolewa kumtetea 


"Naomba mnivumilie mtapata watu wengine watakao wasaidia kuwapetipeti lakini kwangu mimi hapana"


"Nasikia sikia kuna watu wanahangaika na mitandao ile ni kama wananipigia..ushawahi kupigiwa lizimu (gitaa) wakati wa kulala...au ushwahi kwenda chumba cha massage halafu ukawekewa kale kamziki...sasa mimi nasikia hiyo hali...wanavyoendelea kutoa kauli zile mimi nasikia hiyo hali ikiniambia nenda Makonda..endelea endelea na leo nipo Monduli kuwapiga spana waviu wote wanyooke..hatuwezi kwenda hivyo (kwa kubembelezana)"


"..Mkuu wa Wilaya (Monduli) jitosheleze chapa kazi kwakuwa kuna utaratibu na kanuni na hata hii miradi ina kikomo chake (muda wa kutakiwa kukamilika) yani mkataba ukisainiwa una mda wake  na ndugu watanzania mfahamu miradi hii usipotekeleza ndani ya muda hata hawa wakandarasi huwa wanaongeza gharama ambayo ni maumivu kwa mwananchi anayelipa kodi..."


"...fikiria katika mkoa wetu shule moja maalum tumepewa upendeleo ya watoto wa kike ili kuondoa mimba za utotoni wasiendelee kubwakwa na kulawitiwa, wasiolewe ndoa za utotoni wakaua ndoto zao...shule hiyo ipo pale Longido , Rais Dkt. Samia amejenga na mabweni na mradi ule ili ukamilike inahitajika pesa ya ziada..inatoka wapi ? Mpango uliokuwepo hela unaambiwa imeisha na mradi haujakamilika na watoto wa kike hawaendi kusoma...aah hiyo haiwezekani"


"Viongozi wetu wa chama (CCM) si mmetupa kazi ya kutekeleza ilani...mtuvumilie tufanye kazi yetu, mmetupa kazi tunatakiwa kuwaletea matokeo ..ile usomaji wa utekelezaji wa ilani kuwa sasa tumefikia wapi ikifika katika hatua hiyo tubaneni lakini kwasasa tufanye kazi ambayo mmetuabidhi ili kuwaletea matokeo ya kukamilika"


"...wale mnaotoa toa kauli muendelee kwakuwa inanisaidia kufanya kazi kwa molari zaidi, siku moja nilisema umoja wa waovu , wala rushwa na wazembe ni mkubwa sana na ukitaka kujua kama upo mguse mvivu mmoja, wavivu wote utaona wanajitokeza , au mguse mla rushwa mmoja utaona wala rushwa wote wanajitokeza...nawaambie tena nitawapiga spana na mnavyojitokeza tunapata nafasi ya kujua kumbe naye huyu yumo"


" Alidharirishwa hapa karibuni Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa Chama (CCM), Mwanadiplomasia namba moja, mama mwenye familia katukanwa asubuhi mpaka asubuhi lakini sikusikia kauli ya mtu yoyote halafu wanaume sisi ndio tulijitokeza kumpigania Mama halafu leo mzembe mmoja , mla rushwa mmoja ndio mnajifanya mnatoa kauli kupiga kelele huko...twendeni tukachape kazi "


 Mhe. Paul Makonda 

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha 


Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli ikiwa ni muendelezo wa ziara yake kutembelea wilaya zote za mkoa wa Arusha aliyoipa jina la SIKU 6 ZA MOTO.


RC Makonda ameyasema hayo kufuatia baadhi ya watu kunukuliwa na vyombo vya habari wakimtaja kama mdhalilishaji wa watumishi wa Umma ndani ya Mkoa wa Arusha, suala ambalo amelitaja kutombabaisha ama kumpunguzia kasi katika kusimamia watendaji wavivu na wazembe wanaoshindwa kutimiza majukumu yao katika kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Arusha.


🗓️27 Mei, 2024

📍Wilayani Monduli - Arusha


#ArushaNaUtalii

#ArushaYaSamia

#Siku6ZaMoto

#KaziIendelee

CRDB KIBAHA YAZIJENGEA UWEZO JUU YA FEDHA TAASISI ZISIZOKUWA ZA KISERIKALI PWANI

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 

Benki ya CRDB katika kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan  imetoa elimu ya fedha kwa taasisi zisizokuwa za kiserikali zipatazo 22 za Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuwajengea uwezo na uelewa zaidi juu ya umuhimu wa kujiunga katika vikundi ili kunufaika na mikopo.

Pia benki hiyo sambamba na hilo imeweza  kuzipa mbinu mbali mbali pamoja na  kuzishauri taasisi hizo kuweka mikakati ya  kufungua akaunti ya NIA MOJA ambayo ni akaunti mahsusi kwa vikundi na haina makato yoyote ya kila mwezi.


Hayo yamebainisha na  Meneja wa biashara wa CRDB tawi la Kibaha mjini Richard Mkakala wakati wa kikao kazi maalumu ambacho kilizikutanisha taasisi zizosokuwa za kiserikali kwa ajili ya kujadili mambo mbali mbali yanayohusiana na uchukuaji wa fedha na utunzaji wake kupitia mfumo wa kufungua akaunti.
Meneja huyo Mkakala alisema kwamba kwa sasa benki ya CRDB wameanzisha akauniti ya   NIA MOJA ambayo ni maalumu kwa ajili ya kuweka  fedha za taasisi ili ziwe katika hali ya usalama  katika kipindi chote bila wasiwasi.

Kadhali Meneja huyo alifafanua kwamba  wanachama hasa kwa upande wa  wanawake wanashauriwa kufungua akaunti ya iMBEJU ili wazitumie katika kuweka  akiba zao na kupitisha mapato ya biashara zao mbali mbali kwa urahisi zaidi.

" Ninyi wanachama mkiwa na akaunti za CRDB, mnayo fursa kubwa zaidi  kupitia katika hizi  taasisi zenu kuweza  kunufaika na mpango wa uwezeshaji unaowalenga wanawake kuwapa mitaji midogogo kwa ajili ya kuendeleza biashara zenu ili ziweze kukua na kuwa kubwa,"alifafanua Meneja huyo.

Kadhalika aliongeza kuwa lengo lao kubwa ni kuziwezesha taasisi hizo ili ziweze kujikwamua kiuchumi kwa masharti nafuu ambayo wanaweza kuyamudu lengo ikiwa waweze kutimiza malengo yao waliyojiwekea.
 "Kwa kweli sisi kama benki ya CRDB kwa sasa tuna  uwezeshaji huu wa kuziwezesha taasisi mbali mbali mbali zisizokuwa za kiserikaki na kiukweli  unatolewa kwa masharti nafuu sana na benki yetu,"aliongeza Meneja huyo.

Katika hatua nyingine alizishauri na kuzihimiza taasisi zote ambazo zimesajiliwa rasmi  hiyo nazishauri  kuhakikisha zinafungua akaunti ya CRDB  ili kuwa na uhakika zaidi juu ya   usalama wa fedha zao.

 Pia aliongeza kuwa wananchi wanapaswa kuhakikisha wanajiunga katika vikundi mbali mbali na kuvisajili ili viweze kutambulika na  kupata fursa ya  mikopo katika benki hiyo  kwa  masharti nafuu zaidi.

 
Benki ya CRDB imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu mbali mbali kwa taasisi zisizokuwa za kiserikali pamoja na wanachi juu ya umuhimu wa kufungua akaunti ili kuweza kutunza fedha zao zikiwa katika hali ya usalama.