ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 27, 2024

RC MAKONDA KUENDELEA KUWAPIGA SPANA WATUMISHI WAZEMBE NA WALA RUSHWA, ASISITIZA KUTOBABAISHWA NA MANENO YA MITANDAONI

 


> Asema alidhalilishwa Rais Samia na hakuna kauli yoyote iliyotolewa kumtetea 


"Naomba mnivumilie mtapata watu wengine watakao wasaidia kuwapetipeti lakini kwangu mimi hapana"


"Nasikia sikia kuna watu wanahangaika na mitandao ile ni kama wananipigia..ushawahi kupigiwa lizimu (gitaa) wakati wa kulala...au ushwahi kwenda chumba cha massage halafu ukawekewa kale kamziki...sasa mimi nasikia hiyo hali...wanavyoendelea kutoa kauli zile mimi nasikia hiyo hali ikiniambia nenda Makonda..endelea endelea na leo nipo Monduli kuwapiga spana waviu wote wanyooke..hatuwezi kwenda hivyo (kwa kubembelezana)"


"..Mkuu wa Wilaya (Monduli) jitosheleze chapa kazi kwakuwa kuna utaratibu na kanuni na hata hii miradi ina kikomo chake (muda wa kutakiwa kukamilika) yani mkataba ukisainiwa una mda wake  na ndugu watanzania mfahamu miradi hii usipotekeleza ndani ya muda hata hawa wakandarasi huwa wanaongeza gharama ambayo ni maumivu kwa mwananchi anayelipa kodi..."


"...fikiria katika mkoa wetu shule moja maalum tumepewa upendeleo ya watoto wa kike ili kuondoa mimba za utotoni wasiendelee kubwakwa na kulawitiwa, wasiolewe ndoa za utotoni wakaua ndoto zao...shule hiyo ipo pale Longido , Rais Dkt. Samia amejenga na mabweni na mradi ule ili ukamilike inahitajika pesa ya ziada..inatoka wapi ? Mpango uliokuwepo hela unaambiwa imeisha na mradi haujakamilika na watoto wa kike hawaendi kusoma...aah hiyo haiwezekani"


"Viongozi wetu wa chama (CCM) si mmetupa kazi ya kutekeleza ilani...mtuvumilie tufanye kazi yetu, mmetupa kazi tunatakiwa kuwaletea matokeo ..ile usomaji wa utekelezaji wa ilani kuwa sasa tumefikia wapi ikifika katika hatua hiyo tubaneni lakini kwasasa tufanye kazi ambayo mmetuabidhi ili kuwaletea matokeo ya kukamilika"


"...wale mnaotoa toa kauli muendelee kwakuwa inanisaidia kufanya kazi kwa molari zaidi, siku moja nilisema umoja wa waovu , wala rushwa na wazembe ni mkubwa sana na ukitaka kujua kama upo mguse mvivu mmoja, wavivu wote utaona wanajitokeza , au mguse mla rushwa mmoja utaona wala rushwa wote wanajitokeza...nawaambie tena nitawapiga spana na mnavyojitokeza tunapata nafasi ya kujua kumbe naye huyu yumo"


" Alidharirishwa hapa karibuni Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa Chama (CCM), Mwanadiplomasia namba moja, mama mwenye familia katukanwa asubuhi mpaka asubuhi lakini sikusikia kauli ya mtu yoyote halafu wanaume sisi ndio tulijitokeza kumpigania Mama halafu leo mzembe mmoja , mla rushwa mmoja ndio mnajifanya mnatoa kauli kupiga kelele huko...twendeni tukachape kazi "


 Mhe. Paul Makonda 

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha 


Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli ikiwa ni muendelezo wa ziara yake kutembelea wilaya zote za mkoa wa Arusha aliyoipa jina la SIKU 6 ZA MOTO.


RC Makonda ameyasema hayo kufuatia baadhi ya watu kunukuliwa na vyombo vya habari wakimtaja kama mdhalilishaji wa watumishi wa Umma ndani ya Mkoa wa Arusha, suala ambalo amelitaja kutombabaisha ama kumpunguzia kasi katika kusimamia watendaji wavivu na wazembe wanaoshindwa kutimiza majukumu yao katika kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Arusha.


🗓️27 Mei, 2024

📍Wilayani Monduli - Arusha


#ArushaNaUtalii

#ArushaYaSamia

#Siku6ZaMoto

#KaziIendelee

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.